Namba za Magari: Kwanini herufi “O” imerukwa!?

Kwenye mfumo wa plate number za magari naona kama herufi O imerukwa.
Yaani hii namba mpya D.
Baada ya kumalizika kwa namba DN....
Nilitarajia kuona T 111 DOA
lakini badala yake imekua DP...
Ni mimi tu ndo nimeona na nyie wenzangu mmegundua hii kitu
 
Kuna uzi umezungumzia hilo, walisema 0 na O huwezi kutofautisha ndio maana zero imezuia O isiwepo vile vile 1 imeizuia I isiwepo kwenye plate number.

Barafu la moto
 
Hizo herufi huwa hazitumiki, zinafanana na tarakimu 1 na 0. nakumbuka hata TZO ilirukwa miaka hiyo.
 
Hizo herufi huwa hazitumiki, zinafanana na tarakimu 1 na 0. nakumbuka hata TZO ilirukwa miaka hiyo.
Kwenye mfumo wa plate number za magari naona kama herufi O imerukwa.
Yaani hii namba mpya D.
Baada ya kumalizika kwa namba DN....
Nilitarajia kuona T 111 DOA
lakini badala yake imekua DP...
Ni mimi tu ndo nimeona na nyie wenzangu mmegundua hii kitu


Nasikia kuna watu wameanza kuilalamikia S na 5 very soon nazo huenda zikachunguzwa
 
Lakini kwa mfumo wetu wa sasa wa numbering zingeweza tu kutumika kwasababu kuna vipande vitatu
Kitambulisho cha nchi ambacho ni T
Kipande cha namba T 789 ---
Kipande cha herufi T --- OIO
Hapo akili ya msomaji lazima ijiongeze kutambua huo mtenganisho wa kipande cha namba na herufi kwamba lazima zianze namba tatu zifuatiwe na herufi tatu
Kwenye utaratibu wa zamani ndiko mkanganyiko ulikuwa dhahiri kwa mfano
TZ1234
TZI234
 
Wajuzi wa mambo na vijambo, heri ya mwaka mpya ulioanza na mabadiliko kiduchu kwenye baraza la wandugu mawaziri!!!!

Naona ni vyema kujulishana nimeshangaa sijaona herufi O katika mtiririko wa namba za magari.

Nilitegemea kabla ya herufi “P” ilipaswa kuanza “O” lakini sijaona gari zenye plate number za T 123 DOA nk ina nimeona zimerukia kwenye T123 DPA.

Mwenye kufahamu hayo mambo atujuze na sisi wengie tujue zaidi kama wao!!!!

Asentini!!!!!
Mkuu hata herufi I ilirukwa
 
Back
Top Bottom