stable-negro
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 509
- 347
Kwa jina naitwa 'Surprise', ni msichana niliyechumbiwa na nilitegemea kufunga ndoa mnamo Mei 2013.
Kwa bahati mbaya au nzuri last week nimegundua ni mjamzito wa siku kadhaa ilhali mhusika akiwa si mchumba wangu bali ni rafiki yangu tunayefanya kazi ofisi jirani hapa mjini, kiukweli huyu alikuwa 'JUST A FRIEND' ila tukawa na mazoea ya karibu mno ikafikia siku ya siku tukiwa wawili (hata sijui kilichoendelea) tukajikuta tupo dunia nyingine iliyosababisha huu ujauzito.
Bahati nzuri huyu rafiki amesema yupo tayari kwa lolote na anaomba nimpe nafasi aweze kumlea mwanae akiwa na mimi as mke wake, nimemwambia naenda nyumbani kwanza kuwapa taarifa kisha nikirudi nimwambie yaliyojiri ili aanze michakato ya ndoa, na kishawaambia hadi kwao kuwa ataoa karibuni; anasubiri ruksa yangu.
Ki ukweli, mimi nilijua ni bahati mbaya kumbe kwake ilikuwa planned na ameniomba msamaha sababu alikuwa anatamani kufunga ndoa nami sema nilikuwa nimewahiwa na alinipenda muda mrefu ila alikuwa hajui aanzie wapi. Kwa kipindi nilichoishi naye kama rafiki amenipenda, amenijali sana labda awe amejivika ngozi ya kondoo.
Nilikuwa sina mipango wala mawazo ya kumsaliti mchumba wangu ila baada ya kugundua ni mjamzito nikawa na fikra mbili zilizonisababisha kuja kuomba ushauri:
1. As soon as possible bila kupoteza muda nimtafute mchumba wangu niweze kumtegeshea then after two weeks nimwambie mjamzito (of which he will be so happy) lakini nawaza what about LON GRUN? Ni kweli ataamini mimba ya mwezi mmoja kumwambia ni ya wiki 2? Tufanye hakuweza ng'amua hadi tukafunga ndoa na mtoto akazaliwa hafanani na yeyote, wapambe wamshauri DNA, si nitaumbuka mimi jamani!
2. Nianze mipango ya ndoa na baba mtoto halali then nivunje uchumba wa sasa. Hapa nawaza upande wa wazazi wangu, hiyo aibu wataibebaje? Naanzaje kuwaambia home wanielewe mie jamani wakati ukoo mzima unajua ni mchumba wa mtu, na wakinielewa hiyo mahari inarudishwaje? Nawaza upande wa wakwe watanionaje jamani?
Kiukweli tangu nipate hizi taarifa nimekwama, siwezi fanya lolote nahisi ntapata na magonjwa ya presha mwaka huu, nimepanga safari ya kwenda nyumbani lakini naogopa kwenda nahofia ntapokelewaje?
NSHAURINI JAMANI MWENZENU, nimekubali kosa siwakatazi kunilaumu ila naomba way forward ndio kitachonisaidia kwa mda huu.
N.B.
Nitafurahi kama hamtamshauri 'Surprise' bali kilichomo ndani ya ujumbe wangu maana ukimshauri 'Surprise' you might be biased
ucache kile ulichotaka maishan ghafla 2 kw kufata kile ulichotaman