Nakushauri kocha wangu Robertinho yule Yao Yao wa Yanga mwekee Kibu Dennis au Saido upande wake na sio Chama, utanishukuru

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Semaji la Simba kaongea maneno ya mpira, Yanga wako vizuri sana sasa hivi na sio ajabu uwezo wao dimbani wakiongezea na mambo yao ya nje ukifanya masihara lazima ukae.

Namshauri sana kocha wangu Robertinho yule beki wa kulia wa Yanga aitwae Yao Yao ni beki aliyekamilika, kwanza ana nguvu, ana akili, ana control, anapanda yaani kama uliwahi kumuona marehemu Raphael Paul Rp au marehemu Yussuf Ismail Bana basi hana tofauti na huyo Yao Yao.

Kwa namna anavyocheza na spidi yake kocha hapaswi kumweka Chama upande wa kushoto, Chama ameshuka sana kiwango kucheza upande wa kushoto, Chama acheze kiungo wa kati au namba 10 kama Yanga wanavyofanya kwa Aziz Ki, Chama hatomweza Yao Yao kwa sababu anaulinda mguu wake, Yao Yao sio mtu wa kawaida, Chama ataonekana amehongwa tu na watu wa Yanga, katika cku za hv karibuni upande anaowekwa Chama hauna impact kabisa, mzambia huyo akae kati mtaona hao akina Bacca au Mwamnyeto kama hawakujamba siku hiyo.

Upande wa Yao Yao akae mgeni rasmi Kibu Dennis au Micquisone au Saido kwa sababu hao wana nguvu, akili na uwezo mkubwa dimbani, asije akamweka Chama au Onana upande wa Yao Yao, tutashambuliwa mwanzo mwisho.

Pia namuona Ngoma ni mzuri sana lakin wale vijana akina Max Mzengeli, Pacome, Aucho, na Aziz Ki bila mganga wale watatusumbua sana, wale wanahitaji viungo wababe kama Mzamiru, Sadio Kanoute, chama akae kati naamini hawataonekana, Ngoma akicheza uchezaji wake uko slow wakat Pacome na Max wanateleza sana wajinga wale.

Tuombe mungu tu Derby iishe salama lakini jamaa hawa wameshazifunga timu zote, wamejipanga mno kuhakikisha wanatufunga ili tukose cha kusema.Kila la heri nguvu moja.
 
Semaji la Simba kaongea maneno ya mpira, Yanga wako vizuri sana sasa hivi na sio ajabu uwezo wao dimbani wakiongezea na mambo yao ya nje ukifanya masihara lazima ukae.

Tuombe mungu tu Derby iishe salama lakini jamaa hawa wameshazifunga timu zote, wamejipanga mno kuhakikisha wanatufunga ili tukose cha kusema.Kila la heri nguvu moja.
Kama wamezifunga timu zote wanaongoza LEAGUE bila shaka
Eti ni kweli?
 
Semaji la Simba kaongea maneno ya mpira, Yanga wako vizuri sana sasa hivi na sio ajabu uwezo wao dimbani wakiongezea na mambo yao ya nje ukifanya masihara lazima ukae.

Tuombe mungu tu Derby iishe salama lakini jamaa hawa wameshazifunga timu zote, wamejipanga mno kuhakikisha wanatufunga ili tukose cha kusema.Kila la heri nguvu moja.
Ni kweli hata Ihefu wamemfunga.

Tukutane tarehe 5
 
Back
Top Bottom