Nakubaliana na Spika wa Bunge Job Yustino Ndugai lakini si katika yote aliyoyasema jana

Tuache utani hivi kati ya Ndugai na Prof Assad hatuoni Ndugai ni Liability tu?
Eti nayeye kakomaa kusema Prof ajiuzulu wakati yeye kama Spika sioni kazi anayofanya zaidi ya kula hela zetu.

Yaani Ndugai ameji-rate kama mtu muhimu sana kuendelea kuwepo pale wakati mi naona hana kazi yoyote anayofanya, kwa sasa nafasi ya spika na Humphrey Polepole hawatofautiani

Sent using Jamii Forums mobile app
hahahaaaa ******* ana chekesha saana, halafu jaama uwa anajiona kichwa kumbe majanga
 
Nilikua namsikiliza kwa umakini na kumsoma body language yake.. alipotamka hilo juu ya Rais ni kama kaelemewa sasa anahitaji msaada wa haya aliyofikiri wananchi hawatayafatilia.

Kumtaja Rais ni ameonyesha kwamba Rais ambaye tunaamini hana lolote katika hili kwamba yumo..

Inasikitisha kuona viongozi kama yeye anatumia mapaparazi kumfikishia CAG ujumbe wa kumtaka aende kwa Rais.. kwani hawaandikiani barua kiofisho hadi iwe anamrushia kama nenda huko akajieleze.. ya kitaka ajiudhuru.. yaani anasimamia sheria pia mbona hakutaja lolote!!!

Wakili nambie sasa hapa ni akajieleze nini eti? Ajiuzuru kwa lipi haswa? Kasema hataki kufanya nae kazi.. sasa si angekaa kimya.. haya mengine ya nini?

Ndio maana huwa nacheka pale ninapoona wengi hawajui kupanga.. hawafikirii dk 5 itakuwaje na waweje..
Siamini leo umeongea point
 
Halafu, lugha ya staha iwe inatumika wakati wa kuipinga lugha inayodaiwa kuwa ni ya kuudhi. Vijembe na kejeli hazijengi
Hili la kulalamikia lugha iliyotumika na wakati huo huo unatumia lugha isiyo na uungwana linasikitisha. Cheo cha Uspika hakienda na lugha ya " ukimwaga mboga na mimi na mwaga ugali". Makosa mawili hayafanyi moja kuwa sahihi!
 
Nilikua namsikiliza kwa umakini na kumsoma body language yake.. alipotamka hilo juu ya Rais ni kama kaelemewa sasa anahitaji msaada wa haya aliyofikiri wananchi hawatayafatilia.

Kumtaja Rais ni ameonyesha kwamba Rais ambaye tunaamini hana lolote katika hili kwamba yumo..

Inasikitisha kuona viongozi kama yeye anatumia mapaparazi kumfikishia CAG ujumbe wa kumtaka aende kwa Rais.. kwani hawaandikiani barua kiofisho hadi iwe anamrushia kama nenda huko akajieleze.. ya kitaka ajiudhuru.. yaani anasimamia sheria pia mbona hakutaja lolote!!!

Wakili nambie sasa hapa ni akajieleze nini eti? Ajiuzuru kwa lipi haswa? Kasema hataki kufanya nae kazi.. sasa si angekaa kimya.. haya mengine ya nini?

Ndio maana huwa nacheka pale ninapoona wengi hawajui kupanga.. hawafikirii dk 5 itakuwaje na waweje..
Huwa sikubalianagi na hoja zako, KI-HOJA, lakini katika post hii KULA TANO TENA ZILE ZENYEWE...

UMENENA YA MAANA SANA HAPA
 
Mh. Job Ndugai kuna mahali alijichanganya, au alichanganyikiwa akaanza kuikosoa ripoti yenyewe (alitoa mfano kwamba aliyeenda kukagua alikaa siku moja badala ya tatu!)....akamchanganya na Mh. Rais kwenye hoja zake.

Alisema usiutukane mkono unaokulisha pia.
Hataki kuangalia ukweli kwamba katiba kwa makusudi imemlinda CAG ili asiogope kufanya kazi yake kwa kigezo cha anayemlisha (anayemlipa mshahara), kawekewa mazingira ya kutoogopa kuondolewa kwenye nafasi yake anapoona serikali ina matumizi mabaya.
Kwa mtazamo wa JOBU ni kwamba CAG analishwa na raisi hivyo hata raisi akichemsha CAG anatakiwa asifie maana ANALISHWA....
 
Mh. Job Ndugai kuna mahali alijichanganya, au alichanganyikiwa akaanza kuikosoa ripoti yenyewe (alitoa mfano kwamba aliyeenda kukagua alikaa siku moja badala ya tatu!)....akamchanganya na Mh. Rais kwenye hoja zake.

Alisema usiutukane mkono unaokulisha pia.
Hataki kuangalia ukweli kwamba katiba kwa makusudi imemlinda CAG ili asiogope kufanya kazi yake kwa kigezo cha anayemlisha (anayemlipa mshahara), kawekewa mazingira ya kutoogopa kuondolewa kwenye nafasi yake anapoona serikali ina matumizi mabaya.
kwan hao wote si tunawalipa sisi wananchi asimtishe CAG waeleze wamefkia asilimia ngap ktk r
kufanyia kazi report iliyopta

MiM
 
halafu kejeli eti Asaad anependa kujiita profesa na kuona wengine ni wajinga wajinga. akasema Ulaya maprofesa hawapendi kuitwa maprofesa. hii ina maana gani! kwamba huo uprofesa si chochote au. naona kama ilikuwa personal attack. na waliosikiliza hawajatoa credit yoyote. conference ilikuwa ni faida kwa wasikilizaji kuliko kwa aliyeiitisha. watu wamejifunza mengi sana
Kweli kabisa. Personal attack. Character assassination! Ndugai alikuwa Sweden. Mambo mengi yaliendelea nyuma na dhidi yake. Asingeitisha kikao na waandishi wa habari. Angechukua ushauri kwanza. Ameitisha na kuongea tayari. Tumeelewa his true colours. Very dull and black. Hata Shetani mwenyewe hawezi kutilia shaka uprofesa wa Assad. Kosa kuliko yote analofanya Ndugai. Ukitaka kupambana na adui mwelewe vizuri. Elewa strong joints zake. Tafuta cha kuzilegeza ukijua ni strong joints. Usijepeleka kilegeza weak joints huko. Sure, you're doomed. Naona huruma. Binadamu ni mnyama. Mtu ni binadamu. Mtu si mnyama. Hapo hesabu haiingii. Animal psychology has never been human psychology! Veterinary doctor will never attend sick people. It's no wonder hon. Ndugai behaves exactly as he does. He has a vet background. Mind you, I'm not talking of his godfather. Huyo yupo nyuma ya pazia. Anajitahidi kumleta jukwaani. Kosa lake jingine hilo. Aliyezoea kudukua hugwaya yaliyo wazi!
 
Nilikua namsikiliza kwa umakini na kumsoma body language yake.. alipotamka hilo juu ya Rais ni kama kaelemewa sasa anahitaji msaada wa haya aliyofikiri wananchi hawatayafatilia.

Kumtaja Rais ni ameonyesha kwamba Rais ambaye tunaamini hana lolote katika hili kwamba yumo..

Inasikitisha kuona viongozi kama yeye anatumia mapaparazi kumfikishia CAG ujumbe wa kumtaka aende kwa Rais.. kwani hawaandikiani barua kiofisho hadi iwe anamrushia kama nenda huko akajieleze.. ya kitaka ajiudhuru.. yaani anasimamia sheria pia mbona hakutaja lolote!!!

Wakili nambie sasa hapa ni akajieleze nini eti? Ajiuzuru kwa lipi haswa? Kasema hataki kufanya nae kazi.. sasa si angekaa kimya.. haya mengine ya nini?

Ndio maana huwa nacheka pale ninapoona wengi hawajui kupanga.. hawafikirii dk 5 itakuwaje na waweje..
Leo nimekupa like coco,
 
Bunge ni muhimili unaopashwa kujitegemea wananchi wanategemea ndio chombo cha kuthibiti serikali hili utawala wa sheria uende kama inavyotakiwa..
 
Nilibahatika kufuatilia mkutano wa Spika Ndugai na Waandishi wa Habari alioufanya jana jijini Dar es Salaam. Nilifuatilia kuanzia maelezo yake;maswali aliyoulizwa;majibu yake na maswali aliyowauliza wauliza maswali.

Lipo jambo la kikatiba ambalo Spika Ndugai amelizungumza ili kujenga hoja yake kuwa kauli ya Prof. Assad juu ya udhaifu wa Bunge imemgusa hadi Rais Magufuli. Spika alisema kuwa Rais ni sehemu ya Bunge. Hilo nakubaliana na Spika Ndugai.

Lakini, katika utendaji wa Bunge, Rais huwa sehemu ya Bunge katika masuala mawili tu: katika utungaji wa Sheria na katika masuala ya kibajeti. Katika masuala mengine kama kuisimamia Serikali, Rais 'si' sehemu ya Bunge. Rais hawezi 'kujisimamia' mwenyewe akiwa sehemu ya Bunge na mkuu wa Serikali kwa upande mwingine.

Kauli ya Prof. Assad, kwa uelewa wangu, ililenga kwenye wajibu wa Bunge katika kuisimamia Serikali hasa katika kuhakikisha matumizi yanakuwa sawa na ufisadi unadhibitiwa. Katika hilo, Rais hawi sehemu ya Bunge. Hivyobasi, kauli ya Prof. Assad haikumhusu Rais Magufuli kama Spika Ndugai anavyotaka kutuaminisha.

Nasema tena kuwa kauli ya Prof. Assad haikumhusu Rais, Waziri Mkuu au Baraza la Mawaziri. Ililihusu Bunge katika muktadha na sura ya kuisimamia Serikali kwa kuisimamia na kutekeleza mapendekezo ya CAG kwenye Ripoti zake.

Si vyema kumleta Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri kwenye sakata hili ili ionekane kuwa Prof. Assad amewakosea hata wakuu wake. Halafu, lugha ya staha iwe inatumika wakati wa kuipinga lugha inayodaiwa kuwa ni ya kuudhi. Vijembe na kejeli hazijengi.

Hakukuwa na haja ya kumshauri Prof. Assad kujiuzulu au kwenda kwa Rais kuzungumza naye kwa sababu mbili. Kwanza, azimio la Bunge limeshamwadhibu kwa kutofanya naye kazi na si kumshauri ajiuzulu. Pili, Prof. Assad hana mgogoro wowote na Rais ili akazungumze naye kwa kuomba radhi. Katika kuisimamia Serikali,Rais 'si' sehemu ya Bunge.
Haya mambo yataisha lini? Nani ananufaika nayo?
 
Back
Top Bottom