Nakerwa sana na huu ushindani wenu wa vyuo na kozi...

Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
2,089
829
Kwanza hongereni kwa mliochaguliwa kuendelea na ELIMU ya juu kwa ya maana vyuo na taasisi za elimu ya juu na poleni sana wale mliokosa MKOPO ..(kwa hili nawapa pole ya dhati sababu nafahamu maisha ya CHUO bila huu mkopo hasa wale mnaotoaka familia za chini kama mimi)...
jambo kubwa linaloniudhi sana na ambalo linaonyesha hatari kubwa sana ya WASOMI ambao ndio nguzo kubwa kwa maana ya DIRA ya nchi yeyote maana MAENDELEO bila ELIMU ni NDOTO tena ya mchana... hivyo basi ni wajibu wetu sisi kama wasomi naamini wote mliongia VYUONI mnatakiwa kufahamu MSOMI maana yake nini na kwanini uko hapo.. hili ndio jambo muhimu sana ambalo kama ujalitafakari wewe mwanachuo lizingatie sana naa anza kulizingatia na kulitafakri..

HII ISSUE YA USHINDANI WA CHUO INA MANTIKI GANI..? (kwenye hili jukwa la ELIMU...)
kama wewe ni msomi wa CHUO A unajisifu unasoma chuo bora kuliko yule wa CHUO B wakati tija yako kwenye taifa hakuna pamoja na kusoma hicho chuo nakubali kuna UBORA wa vyuo kutokana vigezo vingi tu... ila nasisitiza na kukerwa na tambo sisizo na msingi ambazo azijengi za kujitapata chuo au kozi uliochagaliwa.. MUHIMU sisi kama wasomi ni kujitambua kutambua mapungufu yaliyopo kwenye VYUO vyetu kupambana walau kujikomboa kwa KIFIKRA...

WITO WANGU KWENU tuache huu ujivuni usio na mantiki yeyote tubadilishane mawazo tuokoe nchi yetu.. .

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" ...Hosea 4:6
 
umeniwahi tu ndugu, nilikuwa nawaza kuweka uzi wa hiyo topic, hawa wanaojisifu kwa vyuo na kozi wanazochukua, hawana mantiki yoyote ya kufanya hivyo kabisa, kinachoangaliwa kwenye industry ni output ya mtu na si chuo ulichoenda
 
kwa kweli... mimi nakipenda chuo nilichosoma na najivunia kusoma huko lakini haiingii akili kila uchao humu vijana tunaotegemea ndio wawe wakombozi wa nchi kimaendeleo wanabishana issue za vyuo na tambo zisizo na maana jamani tubadilikeni tujikite kwenye maada zenye kujenga ..
 
Wazo zuri sana na ni ukweli mtupu!!! Imefikia mahali mpaka jukwaa limepoteza ladha...matusi...majivuno....kejeli...sometimes naonaga bora nkatembelee jukwaa la technolojia ..intelijensia...ujasiriamali ambapo maswala ya matusi kejeli na ligi zisizo na mantiki kule hakuna ni facts tu!!! Invisible na timu yako popote mlipo hilijukwaa liwekeeni traffic wa kutosha maana hali si nzuri!!
 
Last edited by a moderator:
Hata marekani na ulaya kwenyewe kuna ushindani wa vyuo,sembuse bongo.
 
Hata marekani na ulaya kwenyewe kuna ushindani wa vyuo,sembuse bongo.

Ushindani wa ulaya na marekan una tija, umebase katika kuonesha wababe wa research, vyuo vinavyocontribute kwenye maendeleo ya jamii kwa ujumla kwa product zake.mfano havard,yale,oxford etc.
Lakin huu wa kwetu hakuna kitu ,ni ujinga mtupu .
Nimesoma chuo bora ,nina kaz nzur lakin thread za kutambishiana vyuo naonaga siyo za hadhi yangu. Huwa nazipita tu ,sababu ni utoto na upumbavu wa hali ya juu.
Achen watu wa masoko na maPR wa hivyo vyuo watambishiane wenyewe,wajiuze kwa jamii ,wewe unachofanya ni upotevu tu wa muda wako,ni muda ambao ungeutumia kujadili mambo ya kujenga sana kuliko kujadili et GPA ,vyoo,majengo,umri etc wa vyuo.
 
alafu cha kushangaza wengine mpaka wanatukanana mi napendandaga lile jukwaa la teknolojia hakuna ujinga kama huu ukihitaji msaada unapewa yaani ful raha.
 
Nashukuru mleta mada..
Hili suala huwa linanifanya zaidi ya kunikera..kweli jukwaa la elimu ndo la kufanyia ushindani wa vyuo??!!
Inaudhi sana kwa hakika
 
mkuu umenifanya nilipende tena hili jukwaa mwanzo nilijua great thinker nimebaki peke yangu mpaka nikahama kumbe mpo!!!
facebook generation wanachangia kuharibu jukwaa!!!
 
alafu cha kushangaza wengine mpaka wanatukanana mi napendandaga lile jukwaa la teknolojia hakuna ujinga kama huu ukihitaji msaada unapewa yaani ful raha.
ni kweli kabisa kule hakuna huu utoto.. tubadilikeni ndugu zangu
 
Ushindani wa ulaya na marekan una tija, umebase katika kuonesha wababe wa research, vyuo vinavyocontribute kwenye maendeleo ya jamii kwa ujumla kwa product zake.mfano havard,yale,oxford etc.
Lakin huu wa kwetu hakuna kitu ,ni ujinga mtupu .
Nimesoma chuo bora ,nina kaz nzur lakin thread za kutambishiana vyuo naonaga siyo za hadhi yangu. Huwa nazipita tu ,sababu ni utoto na upumbavu wa hali ya juu.
Achen watu wa masoko na maPR wa hivyo vyuo watambishiane wenyewe,wajiuze kwa jamii ,wewe unachofanya ni upotevu tu wa muda wako,ni muda ambao ungeutumia kujadili mambo ya kujenga sana kuliko kujadili et GPA ,vyoo,majengo,umri etc wa vyuo.
kipindi cha mwanzo nilikuwa mdau sana kwenye hili jukwaa kutoa guidance yaninavyovifahamu mavyuoni na misaada kuhusu kozi za kusoma ila nimekuwa disappointed sana mambo yanavyoendelea ni muhimu sana kwa kila anaye jiunga angekuwa anasoma hii ....
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-forum/18051-jamiiforums-rules.html
kwa muelewa anaweza badilika .. hili ni moja ya majukwa muhimu sana hasa kwa wasomi kufahamiana kubadilishana uzoefu mavyuoni...
 
Wazo zuri sana na ni ukweli mtupu!!! Imefikia mahali mpaka jukwaa limepoteza ladha...matusi...majivuno....kejeli...sometimes naonaga bora nkatembelee jukwaa la technolojia ..intelijensia...ujasiriamali ambapo maswala ya matusi kejeli na ligi zisizo na mantiki kule hakuna ni facts tu!!! Invisible na timu yako popote mlipo hilijukwaa liwekeeni traffic wa kutosha maana hali si nzuri!!
Upuuzi wa kutambiana vyuo ndio ulinifanya niondoke jukwaa hili na kubakia na jukwaa la Tech & science. Ni vizuri umezungumzia hili jambo kwani nilishawahi kukandia sana kwenye zile thread zinazofanya comparison za vyuo but haikusaidia, it just got worse.
Ushauri wangu ni huu, ili mtu yeyote alitendee haki neno "MSOMI" ni vizuri akatumia elimu aliyopata chuo chochote alichosoma (au anachosoma sasa) kuleta maendeleo yake na ya jamii inayomzunguka.
Ahsante sana mkuu kwa hii thread.
 
Ushindani kwa nyanja gani?? Je mnashindania research mlizofanya vyuoni!!! Au kejeli na matusi!!?? Mnatia huruma nyie!!

Hii nifaida kwa wale wanaodharauliwa eti kwamba vyuo vyao siobora.Inawafanya kusoma kwa hasira ili waje wawaonyeshe hao wanaojitapa na vyuo vyao_On the other hand hawa wanaojitapa kuwa ni bora nao wanajituma ili wasijeachwa na hao wanaowaponda.SO Kujitapa ni vizur,kila mtu usifia chake.
 
Back
Top Bottom