DOKEZO Nakatuba Mkoani Mara kimekuwa Kijiji cha watu kuuawa kwa sumu na ushirikina, Serikali iamke hali inatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
423
1,050
Bora niseme na jamii ijue kinachoendelea, taarifa ni kuwa kuna taarifa za watu kuuawa kwa sumu katika Kijiji cha Nakatuba, Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara.

Pia kuna matukio yameshamiri yakihusisha imani za kishirikina na kuuana katika kijiji hicho hadi kusababisha baadhi ya vijana kukimbia na kuhama kabisa hapo kijijini.

Mbali na hapo kuna baadhi ya familia zimekimbia kwa maana ya kuhama wakihofia kuuliwa kwa sumu pamoja na imani za kishirikina.

Kwa ufupi Kijiji cha Nakatuba imekuwa ni kama eneo la kuzika ndugu zetu na kuondoka, nimetoka hapo katika hicho kijiji leo hii na ninajua ninachokizungumza.

Natoa wito kwa Serikali na Jeshi la Polisi na vyombo vinbine vya Ulinzi na Usalama kufanya jambo, la sivyo hali inaelekea kuwa mbaya.
 
Funguka vizuri mkuu yani hao wanao uwawa kwa sumu wanauwawa kwa sababu wanadhaniwa kuwa.washirikina ama?
 
Funguka vizuri mkuu yani hao wanao uwawa kwa sumu wanauwawa kwa sababu wanadhaniwa kuwa.washirikina ama?
Kuna sababu mbalimbali zinazofanya matukio hayo kutokea ikiwemo hiyo ya imani za kishirikina.
 
GENTAMYCINE ndio kijijini kwenu huko mkuu ulipozaliwa na.unapoishi tupe ufafanuzi kitu gani kinaendelea huko mkuu?
 
Back
Top Bottom