Naishi kama jambazi sipo huru

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,823
Niliishi mikoa iliyotanuka na kujengeka katika majiji,mikoa ambayo hata uwe na tabia zako za kipekee mfano ulevi huwezi kuwa maarufu mkoa wote utaishia kutambulika mtaani kwenu tu.Sasa ghafla maisha ya kikazi yananipeleka kituo cha kazi kilichopo kwenye kamkoa kadogo watu wachache,Sasa kama mnavyojua mahusiano ya kijamii ukitoa ya kazini hayakwepeki nikajikuta natengeneza mazoea na watu vijana na watu wazima yaani sibagui mtu akitaka urafiki simuangalii elimu yake,kipato chake,sura yake au dini yake mimi nitamchangamkia na kwa kuwa siyo mchoyo wa pombe basi ukifanikiwa kunipata katika sehemu ya kunywa kama nina hela lazima nikukunulie yaani sina uchungu sana na pesa.

Kingine tukikaa tukapiga stori huwa sipendi tuzungumzie habari za watu wengine mara sijui kumsengenya mtu me huwa naziruka kwa hiyo hiyo hali inafanya ni kama watu wanipende fulani waone sio mtu mmbea mbea .Mimi nikikaa na maraia huwa najitahidi sana kuelezea manondo ya jamiiforum yaani madini mnayoyatema wanajamiiforum mimi ndo huwa kitaa nayamwaga kwa hiyo naonekana kichwa ama nina haiba na ushawishi sana kumbe nacopy

Sasa kumbe ile hali ya kuchangamana na watu hasa wasio na kazi ili kuweza kuwatia faraja wakuone huringi inaniumiza kisaikolojia kwa sasa ni kama wanakupa umaarufu ambao huutaki wanaita uchawa siku hizi yaani unaweza kuwa sokoni au mjini ghafla mtu anakuita jina lako kwa nguvu lengo akupe hii au akutoke posho sijui wanadhani unakuwa na hela kila siku.unakuta mtu ambaye mnajuana juu kwa juu tu au labda kapewa stori yako na mtu mwingine sasa ile mimi siipendi kwa sababu ya hofu nakosa tena kujiamini nahisi kama mabaya yangu yanaweza yakaenezwa zaidi japokuwa hata mazuri yatasemwa. kingine huwa nakuwa na hofu flani labda usalama wametanda kila sehemu kuchunguzachunguza watu na wanadai watumishi ndio wanachunguzwa zaidi kwa hiyo wasiwasi unakuja labda nitaharibiwa kazini nikionekana naongea mitaani na vijana wala bangi.

Mimi huwa napenda makundi mbalimbali ya wanakitaa pengine siku una tatizo wanakuchukulia kama wewe ni mzawa kumbe wakuja ila matokeo yake yanaanza maneno ofisini mara wewe umekuja kazini lakini umekuwa maarufu kushinda wenyeji mara sijui bar zote unajulikana.kwa hiyo hiyo hali najikuta naanza kuishi maisha ya kujifungia ndani yaani hata mahitaji naenda kununua mida ya usiku lengo nisionekane na watu wanaonipa umaarufu usio na faida sana
Kwa hiyo nawapa code za kuishi mkoa wa ugenini kwanza unapokunywa pombe kama ni muoengeaji basi usipende kusemeshana na wasiokunywa utachukiwa wewe kaa na walevi wenzako piga kelele njiani au ukirudi home hata wapangaji usiwasemeshe ingia zako ndani..nadhani nimeeleweka japo uandishi sipo vizuri sana

Haters watakuja kusema ni hangover ndo linanisumbua baada ya kuchoma kibunda Weekend kwa hiyo ndo mawazo ya kukaa nyumbani na kutulia yanakuja na kama siamini nitoe lock kidogo kama sishuki bar hahahahahaha kukaa ndani kipengele huchelewi kujichukulia sheria mkononi mara kwa mara . Niko serious kisaikolojia inanitesa nawaza sana mpaka kuhama mkoa nikaanze maisha upya nisijulikane ama nisiishi kinafki kama nimeamua kuwa sele niendelee tu kuwa selemani.
 
Ulitaka kuwafurahisha watu na mwisho wa siku wamekufurahia.. Tatizo liko wapi sasa hapo boss ya mboka
Tatizo nahisi kama naonekana zinaruka kipindi kingine kumbe huwa ni vibe tu kuvimba nikishika kibunda
 
Hayo maswala ya KULEWA kwa MJUMUIKO/KIFAMILIA/KIVIKOBA/KIMAKUNDI sio kabisa.

Mimi nikitoka kulewa/starehe naenda mimi kama Mimi. Kulewa kimakundi sio kabisa maana unaweza ongea neno dogo tuu likatafsiriwa vibaya. Na mbaya zaidi kulewa na wafanyakazi wenzio maana lazima mtaongea maswala ya KAZI tu na hapo ndio zinaaanza choko choko.

Hata Kwenye ngazi ya KIJAMII usipende Mchangamano sana just limit it.
 
Ukiishi kwa kutazama watu utaumia.
Ishi maisha yako, do what's right
Asante sana Dr.santos cha kufanya nisivuke tu mipaka sana yaani nisifanye vitendo ambavyo vinamuathiri mtu familia yake,kipato chake au mahusiano yake...ila mengine niko sawa Dr?
 
Back
Top Bottom