Naishauri Serikali ya Rais Samia kuwawezesha Wafanyabiashara wa Kitanzania kuwa mabilionea, Ili Uchumi wetu uwe Mikononi Mwetu Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,351
9,779
Ndugu zangu watanzania,

Huo Ni ushauri wangu kwa serikali ya Rais Samia kuhakikisha kuwa inawapa kipaombele wafanyabiashara wakubwa wa kitanzania katika kila aina ya fursa ya kibiashara,Tenda katika miradi ya serikali na maeneo mengine makubwa makubwa yanayogharimu kiasi kikubwa Cha fedha katika kupata huduma fulani au bidhàa fulani au vitendea kazi fulani au malighafi fulani.

Iwe Ni katika ujenzi wa miradi ya serikali Ni lazima serikali yetu ihakikishe kuwa watanzania wanapewa kipaombele kikubwa,Na kwa mahali ambapo itaonekana mradi umekuwa mkubwa Unaohitaji mtu au kampuni kutoka nje ya nchi Ni lazima na muhimu ikahakikisha mtanzania mmoja wapo anapata fursa ya kuwepo katika mradi Husika ili fedha zilipwapo zisiendi zote nje ya nchi mabillioni kwa mabillioni..

Tukiwa na wafanyabiashara wakubwa wa kitanzania Ndio kuiweka nchi kiuchumi mikononi mwa watanzania,Hawa watanzania Mabilionea ndio watakaotengeneza fursa za ajira kwa wingi na kuwaajiri vijana wa kitanzania kwa wingi tofauti na Hawa wageni ambao uongozi wote wa Juu unakuta umetawaliwa na wageni ambao hawana uchungu Wala hawawajali watanzania kimaslahi zaidi ya kuwalipa hela ambazo zinawafanya Kama watumwa wa kampuni licha ya kuvuja jasho jingi.

Lakini pia kutengeneza wafanyabiashara wakubwa wa kitanzania itasaidia kuhakikisha kuwa fedha zote zinakuwepo na kubakia nchini na hivyo kusaidia katika mzunguko wa fedha na kusisimua uchumi wetu,Hawa pia watasaidia mabenki yetu kuwa na fedha za kutosha zitakazosaidia kutoa Mikopo kwa wahitaji,Hawa watasaidia kuchangia katika huduma za kijamii katika maeneo yao,

Hawa watasaidia serikali kujiamini na kutowanyenyekea Wala kuwahofia Wale ambao huwa wanaleta mikwala ya kusema nitafunga biashara yangu au nitahamisha biashara yangu na wakati mwingine Hawa wageni ndio huwa wanakuwa wakwanza kutuchafua kimataifa kwa kueneza taarifa za uongo na upotoshaji na hivyo kutujengea picha mbaya kwa wawekezaji na hata watalii,wakati wazawa huwa wanatafuta suluhu ya kimazungumzo na serikali yao kwa njia ya amani maana wanajuwa serikali Ni Kama mzazi wao.

Hapa ni lazima serikali ihakikishe kuwa wafanyabiashara Hawa wanasaidiwa katika kila namna,wasionewe na kubambikiwa makodi ya kukomolewa na watumishi wasio waadilifu,wasikilizwe Mara kwa Mara kwa njia za chini ya kapeti, waitwe Mara kwa Mara kwa Siri ili waeleze mawazo yao na jinsi ya kusonga mbele kwa pamoja na kuifanya serikali yao inapata Kodi stahiki,

lakini pia serikali yetu kufanya ujasusi wa kiuchumi katika mataifa yanayotuzunguka kuona fursa za kiuchumi ambazo wafanyabiashara wetu wanaweza kujipenyeza kuvuna fursa, serikali yetu pia kijasusi Ni lazima iwe inakusanya taarifa kwa majirani zetu ili wafanyabiashara wetu wasije wakawekeza maeneo hatarishi ya kupoteza mitaji yao,lakini pia kunusa harufu za kuwahujumu wafanyabiashara wetu na kuwashitua mapema wafanyabiashara wetu wanaowekeza nchi za jirani,Ni lazima walindwe kwa wivu mkubwa Sana na kupiganiwa Sana,wasiachwe wapweke wapatapo shida ugenini,Balozi zetu ziwe za kwanza kutoa taarifa na usaidizi.

Tuliona namna bilionea Marehemu Reginad Mengi alivyokuwa anaisaidia watanzania mbalimbali,Vipi tukiwa na akina mengi hata hamsini au Mia hapa nchini walio katika mikoa mbalimbali na maeneo mbalimbali? Hamuoni itakuwa faida kubwa Sana? Hamuoni Ni faida? Ndugu zangu Naiomba serikali katika hili ilifanyie kazi kimkakati,kijasusi na kiinterejensia.

Kazi Iendeleee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Lucas hebu dadavua zaidi kuhusu asili ya Utanzania ya wafanyabiashara hao. Ni wale asili ya ngozi nyeusi ama wale wenye asili ya Asia, au una maana wote pasipo kujali asili zao.

Nasema hivyo kwa kuwa, wale wenye asili ya Asia wapo wengi sana, na mfumo uliopo unawapendelea na kuwafanya waingie wengi zaidi kwenye "billionaire club" zaidi ya hili kundi la watu weusi.
 
Lucas hebu dadavua zaidi kuhusu asili ya Utanzania ya wafanyabiashara hao. Ni wale asili ya ngozi nyeusi ama wale wenye asili ya Asia, au una maana wote pasipo kujali asili zao.

Nasema hivyo kwa kuwa, wale wenye asili ya Asia wapo wengi sana, na mfumo uliopo unawapendelea na kuwafanya waingie wengi zaidi kwenye "billionaire club" zaidi ya hili kundi la watu weusi.
Lazima ujiulize mtanzania Ni Nani? Sifa ya kuitwa Raia wa Tanzania unatakiwa uwe na sifa zipi
 
Lazima ujiulize mtanzania Ni Nani? Sifa ya kuitwa Raia wa Tanzania unatakiwa uwe na sifa zipi
Kuna uraia wa kuzaliwa, na pia upo wa kupewa kwa kutimiza masharti muhimu yaliyowekwa. Kwa sasa sheria haitambui uraia pacha, ingawaje tunao watu wengi nchini ambao wanaishi isivyo kihalali kwa uraia pacha. Lakini wote hao ni wana sifa ya kuwa raia wa Tanzania
 
Kuna uraia wa kuzaliwa, na pia upo wa kupewa kwa kutimiza masharti muhimu yaliyowekwa. Kwa sasa sheria haitambui uraia pacha, ingawaje tunao watu wengi nchini ambao wanaishi isivyo kihalali kwa uraia pacha. Lakini wote hao ni wana sifa ya kuwa raia wa Tanzania
Mimi nazungumzia Raia wa Tanzania bila kujari rangi yake,hao ndio naotaka wawezeshwe na serikali yetu na kukuzwa Hadi kuwa na mitaji mikubwa Sana kwa kuwapatia fursa mbalimbali huku wakilipa Kodi stahiki serikalini
 
Back
Top Bottom