Naidai Serikali milioni 65 tangu 2018

Serikali ikikopa huduma zako. Uwe mpole, utafilisika na makabrasha, kulikuwa na mambo ya pembejeo na mashamba darasa, watu walikopwa huko Magu akaingia madarakani, akajidai kuhakiki madeni. Hawajalipwa, wamefilisika, wamepata stroke, visukari!

Sikopeshi serikali NEVER labda niwe mwenyewe waziri kwenye hiyo Wizara yenye tenda!
 
mzee serikali mali yake haikamatwi sikuiz kisa deni...

huto kamata gari wa chaki au panadol, sheria ipo wazi...

mkurugenzi ata kubali kulipa kwa utaratibu basi...

una shinda ata msaada wa mwanasheria hukupata?
 
Habarini,
Kila leo serikali inakopa fedha nje za riba ili kutumia kwenye mambo yenye faida kwa viongozi hasa 10% kwanini haikopi pesa ilipe madeni inayodaiwa na wananchi?

Mimi naidai serikali zaidi ya 65mln tangu 2018 nimeenda mahakamani nimeshinda kesi niekazia hukumu nimeenda hadi TAMISEMI na Hazina mkurugenzi wa halmashauri husika kaelekezwa anilipe lakini kwa kiburi tu amegoma mahakama nayo inaogopa kutoa amri ya kumkamata, sasa hilo la serikali ya Tanzania kuwajali na kuwa sikivu kwa wananchi wake linatoka wapi?

RAIS SAMIA SERIKALI YAKO NA VIONGOZI WAKO WANAKAIDI AMRI ZA MAHAKAMA NA AWALIPI MADENI YETU TUNAOMBA UINGILIE KATI
pole ndg,jamaa na rafiki.usikate tamaa mana utampa adui nafasi zaidi.endelea kupambana utapata.
 
Serikali ikikopa huduma zako. Uwe mpole, utafilisika na makabrasha, kulikuwa na mambo ya pembejeo na mashamba darasa, watu walikopwa huko Magu akaingia madarakani, akajidai kuhakiki madeni. Hawajalipwa, wamefilisika, wamepata stroke, visukari!

Sikopeshi serikali NEVER labda niwe mwenyewe waziri kwenye hiyo Wizara yenye tenda!
Umeandika kweli tupu.
 
Serikali inadaiwa Malimbikizo ya mishahara ya Watumishi tangu 2017 na 2018 haijawalipa wahusika halafu kuna wa 2020 na 2021 wamelipwa.

Hii serikali ipo makini kweli? Au kuna rushwa hapo.


Serikali ilisimamie hili haki itendeke.
 
Tenda za serikali sio za kukimbilia hasa kwa hii serikali dhalim ya CCM. Mzee wangu alikua anaidai serikali 460million toka 2017 holla, mzee akingia kwenye madeni sana sababu yeye ndo alikua MD kwenye hii kampuni.

April mzee ndo amelipwa nusu 230m baada ya kiongozi fulani kula teuzi ambaye ni rafiki sana na mzee ndo aliyemsaidia mpaka malipo yameanza fanyika hio ilobaki wameahidi december wata deposit. Mzee hana ham tena na serikali baada ya kumlipa hio nusu wakaja tena waingie mkataba mwingine mzee akaiuza hio tenda kwa kampuni nyingine kwa 3%.

Watu wengi wanaidai serikali ila malipo ndo shida sasa sijui hizo peswa zinaliwa au laaah. Haiwezekan unampa mtu tenda anatumia pesa zake anakamilisha kazi yenu afu malipo tunanza sumbuana. Serikali badilikeni.
 

Commission for Mediation and Arbitration, hii ni tume ya upatanishi na usuluishi juu ya migogoro ya mwajiri na mwajiriwa.Nafikiri ndio hatua ya kwanza pindi usiporizishwa na maamuzi ya mwajiri wako basi unaenda fungua shauri huku na baadae usuporizishwa na tume hii basi ndipo utakiwa kwenda mahakamani.​

Lakini kumbuka taasisi na mamlaka za serikali huwa hazipelekwi CMA!
 
Back
Top Bottom