Naibu Waziri Kihenzile: KADCO Ongezeni Ubunifu Kuvutia Mashirika ya Uwekezaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945

NAIBU WAZIRI KIHENZILE: KADCO ONGEZENI UBUNIFU ILI KUVUTIA MASHIRIKA YA UWEKEZAJI

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ameutaka Uongozi wa Kampuni ya Uendeshwaji na Uendelezwaji wa Kiwanja Cha Ndege Cha Kilimanjaro (KADCO) ambao ndiyo waendeshaji wa Kiwanja Cha Ndege Cha Kilimanjaro (KIA) kuongeza ubunifu ili kuvutia zaidi Mashirika ya Kimataifa

Akizungumza Jijini Arusha wakati wa mwendelezo wa ziara zake za kuongea na Viongozi na Kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo amesema mpaka Sasa KIA inahudumia Mashirika 13 ya Kimataifa Kiwango ambayo ni machache ukilinganisha na uwekezaji na jitihada mbalimbali za Kiserikali zilizofanyika

"Kiongozi wetu mkuu Rais wa Awamu ya Sita Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaanza yeye mwenyewe kuigiza kwenye filamu ya Royal Tour ambapo alitua hapa ili kuvutia wageni zaidi Sasa ni wakati wa Kampuni kuwa na Mikakati ya Masoko inayoonekana, inayokunalika na inayotekelezeka ya kutafuta masoko nje ya Nchi ili kuvutia Mashirika ya Kimataifa zaidi" amesisitiza Kihenzile

Mhe. Kihenzile amesema uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Arusha upo eneo la kimkakati kwani Mkoa huo ni kitovu Cha utalii Kwa ukanda wa Kaskazini Kwa kuwa na vivutio bingo vya utalii pia Kuna ushindani mkubwa wa kibiashara na Nchi jirani hivyo kutoa Rai jitihada za dhati zifanyike kujitangaza Kimataifa ili kuunga mkono maono makubwa ya Rais ya kuifungua Nchi Kimataifa

Amesema amefurahi kuona Maboresho ya Maeneo ya maegesho ya magari ambapo Sasa yanahidumia magari zaidi ya 120 ikiwa ni ongezeko la mara mbili zaidi ya ilivyokuwa awali, ukamilifu wa Maeneo ya kuhifadhia bidhaa ya ubaridi(Cold Rooms) sambamba na ukamilifu wa mindombinu ya kuingia uwanjani hapo ambavyo vitavutia watumishi zaidi hasa wakulima

Pamoja na hayo ameutaka Uongozi wa KADCO na Taasisi zote za Uchukuzi kuwa na utaratibu mzuri wa kutekeleza maelekezo ya viongozi wa Serikali Kwa kuwa na mfumo wa ufuatiliaji na utekelezaji wa maelekezo hayo

Kihenzile amesema yapo maagizo mengi hutolewa na viongozi mbalimbali ila utaratibu uliopo hivi Sasa hakuna ufuatiliaji makini wa maagizo hayo hivyo ameielekeza Kampuni ya Uendeshwaji na Uendelezwaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Arusha kuhakikisha inawasilisha Wizarani taarifa kamili ya maelekezo yote yaliyotolewa na Viongozi Mbalimbali wa Serikali Kwa nyakati tofauti na utekelezaji wake

Akitoa salamu za utangulizi Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO ambao ndiyo waendeshaji wa KIA Bi Christine Mwakatobe amesema kiwanja hicho kilojengwa na Serikali na kuanza kutumika rasmi mwaka 1971 kikiwa na lengo la kutoa Huduma Bora za Usafiri wa anga na kuimarisha shughuli za utalii Nchini

Kuhusu mafanikio Bi Christine amesema Hali ya utendaji na shughuli mbalimbali za KIA kuanzia mwaka 2019 Hadi 2023 ni wa ufanisi mkubwa ambapo idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 794,337 mpaka 929,553, Mizigo kutoka kilo mil 3 mpaka Mil 4.3, idadi ya miruko kutoka 20,756 mpaka 22,715 huku mapato yakipanda kutoka Bil 26 mwaka 2019/2020 mpaka Bil 31.7 sawa na ongezeko la asilimia 59.
Kwa upande Mwingine Mhe Kihenzile alipata fursa ya kutembelea na Kukagua maendelea ya Maboresho mbalimbali na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Moshi uliopo poa Mkoani Kilimanjaro unaosimamiwa na TANROAD ambapo kinafanyika ujenzi wa njia mbili za miruko ya Ndege Kwa lami mita 1,200 na changalawe mita 1,400 utakaogharibu shilingi Bil 12 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika July, 2024
 

Attachments

  • F8xgbCKWoAAl2ki.jpg
    F8xgbCKWoAAl2ki.jpg
    73 KB · Views: 2
Back
Top Bottom