Naibu Waziri Kihenzile Aitaka DMI Kufungua Matawi ya Chuo Mikoani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

NAIBU WAZIRI KIHENZILE AITAKA DMI KUFUNGUA MATAWI YA CHUO MIKOANI

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameutaka uongozi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kuhakikisha wanafungua matawi mikoani ili waweze kutoa fursa kwa Watanzania wengi kupata elimu hiyo.

Kihenzile ameyasema hayo baada ya kutembelea chuo hiko na kuona kazi mbalimbali zinazofanya katika chuo hiko pia kukagua mtambo mpya wa kufundishia ulioigharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni mbili.

“Serikali imewekeza katika ujenzi wa meli na upanuzi wa bandari hivyo ni muhimu kwa chuo hiki kutoa watalaam wengi na wenye sifa hivyo ni muhimu kufungua matawi mikoani ili kutoa fursa kwa watanzania kupata elimu hii muhimu”a lisema Kihenzile.

Pia Kihenzile alisema kuwa serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewezekeza fedha kiasi cha shilingi Tirioni moja katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji kwa lengo la kukuza uchumi utokanao na sekta hiyo, hivyo ni muhimu kuwa na watalaam wakutosha hasa wanaozalishwa hapa DMI.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa chuo hicho Kaptein Erenest Bupamba amesema kwasasa wameanza mchakato wa kupata maeneo ya kujenga matawi ya chuo katika mikoa ya lindi, Simiyu na Mwanza.

Huku Mkuu wa chuo hicho Dkt. Tumaini Gurumo akitoa wito kwa wazazi kuwasomesha vijana wao elimu ya bahari kwani sekta hiyo inakuwa kwa kasi nchini na inapewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo ya nchi.
 

Attachments

  • F_sXotjXQAASJGC.jpg
    F_sXotjXQAASJGC.jpg
    170.2 KB · Views: 2
  • F_sXothXoAAo-wK.jpg
    F_sXothXoAAo-wK.jpg
    169.1 KB · Views: 2
  • F_sXothWEAAfvbu.jpg
    F_sXothWEAAfvbu.jpg
    172.6 KB · Views: 2
  • F_sXpgKXsAAJLwJ.jpg
    F_sXpgKXsAAJLwJ.jpg
    184.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom