Naibu Waziri Kigahe awataka Wakuu wa Mikoa kufanya maonesho ya Utalii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945

Naibu Waziri Kigahe Awataka Wakuu wa Mikoa Kufanya Maonesho ya Utalii

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe (Mb.) amewataka Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania kuhakikisha wanafanya Maonesho ya Utalii ili kukuza utalii na kuongeza mapato ya nchi kwa kuwa sekta hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa.

Kigahe ameyasema hayo Septemba 28, 2023 alipokuwa akifunga rasmi Maonesho ya Utalii Kusini yaliyofanyika katika Viwanja vya Kihesa Kilolo, Mkoani Iringa.

Aidha, Kigahe amewakumbusha wawekezaji wa ndani kiwekeza katika Mkoa wa Iringa kwa kujenga hoteli zenye hadhi za nyota tano na kitoa huduma nzuri kwa ajili ya kupokea wageni wengi zaidi

Aidha, katika hatua nyingine Naibu Waziri amevutiwa na kauli mbiu ya Maonesho ya Mwaka huu 2023 isemayo "Mwelekeo mpya wa uwekezaji" kwani ni kauli yenye tija na kuwakumbusha wawekezaji katika maeneo yote ikiwemo sekta ya utalii ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea

Aidha, Kigahe amepongeza maandalizi ya maonesho hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendegu kwa kishirikiana na waratibu mbalimbali kutoka Mikoa yote ya Nyanda za Juu kusini.

Vilevile, amebainisha kuwa zaidi ya bilioni 16 zimewekwa kwajili ya kukuza utalii wa karibu kusini kupitia maonesho hayo ili kuweza kutengeneza mahusiano mazuri na watalii.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amesema kuwa katika Maonesho hayo walilitarajia kupata waonyeshaji 100 lakini mwitikio umeleta waonyeshaji 110 na washiriki zaidi ya 800 kwa mwaka huu pamoja na mashindano ya magari.

Aidha, Dendego amesema Mkoa huo unaendelea kuboresha miundombinu ya uwanja wa ndege utakaoweza kubeba aina ya ndege zote na kujenga Kituo cha Utalii na Utafiti.

WhatsApp Image 2023-09-29 at 15.06.22.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 15.06.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 15.06.23.jpeg
 
Hawa Mawaziri wapewe uwaziri kulingana na area of Elimu.
  • Maonyesho yana mlenga nani?
  • kama yanalenga wa Tanzania!
  • Je wa Tanzania wanamudu?
  • Waonyeshe kitu gani?
 
Back
Top Bottom