Naibu Waziri Khamis Hamza akumbusha Wananchi kuchukua Tahadhari juu ya Maambukizi Mapya ya VVU na Ukimwi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Khamis Hamza ameiasa jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI nchini kwa kuendelea kuzingatia elimu inayotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini ili kuunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya mapambano hayo na kuyafikia malengo yaliyopo.​

Ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu alipotembelea na kujionea shughuli zinazoratibiwa na ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Wiki ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya zamani ya mabasi Babati mkoani Manyara.

Maonesho yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambapo yameambatana na uwepo wa maonesho mbalimbnali ya shughuli za uzalishaji, burudani, ujasiriamali na michezo iliyobeba jumbe za elimu kwa vijana katika kuipamba wiki hiyo.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa, jamii haina budi kuendelea kujilinda na kuwalinda wengine kwa kuzingatia ushauri na elimu inayotolewa ili kuhakikisha hali ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI nchini ipungua na kuyafikia malengo ya kuzifikia sifuri tatu ifikapo 2030.

“TACAIDS imeendelea kufanya kazi nzuri ya kuifikia jamii kwa njia ya elimu, ila endeleeni kuongeza nguvu kwa vijana kwani ndilo kundi linaloongoza kwa maambukizi bila kusahau ni kundi muhimu katika uzalishaji na kujiletea maendeleo yetu, hivyo elimisheni kwa nguvu watu wabadili mitazamo yao,” alisema Mhe. Hamza

Aliongezea kuwa, Tume iendelee kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Kondomu ili kupunguza maambukizi ya VVU na UKIMWI hasa kwa kundi la vijana nchini.

“Endeleeni kufunga makasha ya kondomu katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo; kumbi za burudani, baa na nyumba za wageni lengo ni kuendelea kupunguza maambuki ya VVU na UKIMWI,” alisisitiza

Kwa upande wake Mratibu wa UKIMWI kutoka TACAIDS Bw. Gilbert Mbwambo akieleza majukumu ya Tume hiyo alisema kuwa Serikali imeboresha huduma za VVU na UKIMWI
 

Attachments

  • F8QRd5uW0AALmvv.jpg
    F8QRd5uW0AALmvv.jpg
    159.7 KB · Views: 5
  • F8P_WMmXEAAiZji.jpg
    F8P_WMmXEAAiZji.jpg
    78.2 KB · Views: 6
  • F8P_Bp_WYAAmz7Z.jpg
    F8P_Bp_WYAAmz7Z.jpg
    89.5 KB · Views: 5
  • F8QQ2gCWgAATq0p.jpg
    F8QQ2gCWgAATq0p.jpg
    340.7 KB · Views: 5
  • F8P-MeQWsAAK-IB.jpg
    F8P-MeQWsAAK-IB.jpg
    244.5 KB · Views: 5
Back
Top Bottom