Naibu Spika awatoa nje ya Ukumbi wa Bunge, Wabunge wote wanawake wa Upinzani (UKAWA)

Kwa hiyo unataka kutuambia na NS naye amepatikana kwa Kulala na kiongozi huko CCM?Use your brains tafadhali
mbn umepaniki mkuu.....naibu spika alipigiwa kura au ulikua umehama kwenye ule msimu wenu.....???
 
Mbona jambo hilo dogo tu ilibidi wao ndio wathibitishwe kama hivyo viti walivipata kihalali na waonyeshe ilikuweje wakawa wao ni si wengine.
Usiende huko mkuu. Watu wana data wasije wakafunguka.
 
Wewe ni third party Zitto mwenywe alimpa promo Mbowe kwa kusema kwa sauti ndiye aliyemtrain kuingia kwenye ulingo wa siasa,na akaenda mbali kumshukuru kumfikisha hapo.SO nimetoa kutoka kwenye Mdomo wa Zitto.
kwanza kabla kujibu UMTAKAFARI huyo unayemjibu.. ushaona anaitwa DOMOKAYA unateMEGEA nini humo kwenye domo ??
 
Mwenyekiti wa Chadema , Freeman Aikaeli Mbowe , Amezaa watoto 2 na mbunge wa viti maalumu chadema , Joyce Mukya .

Sasa mnapinga nini au mnakataa ukweli mnaambiwa ukweli mnalia lia.

Wewe mwenyewe tukikuchunguza unaweza kukuta umezaa na Sugu
Chonde chonde jamani, msimwage mtama kwenye kuku wengi
 
Dawa siyo kutoka nje nikupanga mikakati tu kuwa kama naibu spika ananyamazia matusi basi kila mmbunge wa Ukawa akisimama aanze na kumshukuru naibu spika kisha tusi kwanzia kwake mpaka wabunge wenzie wa chama cha majizi
 
Kabla ya hapo alikuwa nani??Hakuwa Mbunge wakati wa Mkapa??

Naona unabahatisha mambo,Siasa zinawafanya hata uwezo wa kufikiri unapungua.Kombani ameanza kuwa mbunge 2005 na ameanzia Ulanga Mashariki .
1995-2005 Alikuwa anafanya kazi SUA
 
Wabunge wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na mbunge mmoja wa CCM kuwa wanapewa viti hivyo kwa kuwa na mahusiano na viongozi wao wa juu.

Wabunge hao waliomba muongozo kwa naibu spika lakini hawakusikilizwa ndipo waliposimama wote na naibu spika kuwataka kukaa chini na ndipo kulipoibuka sekeseke la wabunge hao na kuamua kususia kikao hicho cha bunge asubuhi hii na kutoka nnje huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa huku naibu spika tulia akifurahia tukio hilo

Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge wanawake wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kufuatia Mbunge wa viti maalumu Sophia Mwakagenda kuomba mwongozo wa Spika wa Bunge kwa kauli aliyotoa jana Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga kuzungumza bungeni kuwa wabunge wa CHADEMA ili wapate ubunge wa viti maalumu lazima wawe na mahusiano na viongozi wao.



=================

Update;


Taarifa za hivi punde kutoka bungeni, wabunge hao wamezungukwa na watu wa Usalama kwenye ofisi za KUB ambako walikuwa wanaendelea na kikao baada ya kutoka bungeni. Wanausalama hao ni wa kiume lakini ndo wameanza kuwaita WPs kupanda ghorofa ya pili ziliko ofisi hizo. Ni mwendelezo wa sakata lililoanza jana hadi NS akaagiza askari wamtoe Mbunge wa Ukonga, Waitara.

Maelezo mafupi juu ya hasa kilichotokea jana bungeni kuhusu Mbunge wetu Waitara Mwita Mwikabwe akatolewa nje kwa amri ya Naibu Spika. Kisha yatafuatiwa na maelezo (katika sauti) ya kina kutoka kwa Mbunge mwenyewe Ndugu Waitara alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea kwa ufasaha kilichotokea jana bungeni ambao ni mwendelezo wa 'maelekezo' ya namna ya kuliendesha bunge kwa kudhibiti sauti na nguvu za hoja kutoka UKAWA kwa manufaa ya CCM na Serikali yake.

Jana mara baada ya Bunge kurejea session ya jioni Naibu Spika alionekana kuyumba katika kulisimamia bunge kwa kuruhusu matusi, lugha za kejeli na upotoshaji kutoka kwa wabunge wa CCM walionekana kupangwa kimkakati huku yeye akizuia juhudi zote za Wabunge wa UKAWA waliokuwa wakitumia haki yao ya kikanuni kuomba miongozo, kutaka kutoa taarifa na kuhusu utaratibu ili baadhi ya mambo yatolewe ufafanuzi. Jambo ambalo ni mojawapo ya misingi ya uendeshaji na usimamiaji wa mabunge.

Alianza Mbunge wa CCM kutoka Zanzibar akisema kuwa Wabunge wa Upinzani (UKAWA) wanaharishia mdomoni badala ya nyuma.

Naibu Spika hakuchukua hatua yoyote kama ambavyo hata akili ya kawaida ingetarajia ifanyike hivyo. Akapiga kimya huku akizuia wabunge wetu kuhoji.

Mbunge wa Ulanga ambaye ni mtoto wa marehemu Celina Kombani naye akaendeleza lugha za kejeli na kupotosha. Akasema eti Wabunge wa UKAWA wamerudi Bungeni kuchangia baada ya yeye kumshauri shemeji yake Mbowe (Freeman, KUB) ili aturuhusu. Kwa hiyo wako pale bungeni kwa sababu yake.

Akaendelea kudai kuwa sifa ya Wabunge wanawake wa Chadema kupata Ubunge ni kila mtu lazima aitwe Baby kabla ya kupata Ubunge viti maalum.

Akaendelea kudai tena kwamba Wabunge wetu wanafanya vitendo vya kishoga.

Wabunge wetu kadhaa wakasimama kuomba miongozo, kutoa taarifa na kuomba utaratibu. Lakini kiti hakikujali. Hakikutoa nafasi hiyo.

Baada ya kuwepo kwa kelele nyingi na baadae kukawa na utetezi kutoka kwa Jenista Mhagama kwamba hata wabunge wa upinzani walikuwa wamesema matusi, kelele zikawa nyingi zaidi, ndipo NS akamtaka mwandishi wa Hansard afute maneno machafu yote.

Akafuata Mbunge mwingine wa CCM kutoka Kigoma, Kasulu akasema yeye ana ushahidi kwamba Ndugu Lissu ana jalada la ugonjwa Hospitali ya Milembe!

Wabunge wetu ambao hadi hatua hiyo walikuwa wamenyimwa nafasi ya kuzungumza, wakaendelea kupiga kelele na kusimama.

NS akamtaka afute au adhibitishe kauli yake baada ya Lissu kuomba muongozo. Yule Mbunge wa CCM badala ya kufuta maneno akawa anazunguka zunguka mtu ooh mara ni maneno yako mtaani, mara hivi mara vile.

Baada ya kuona kiti kinazidi kuyumba, ama kwa makusudi au kwa kujua kinachofanya, Mbunge wetu Waitara akalazimika kusimama akimtaka yule Mbunge wa CCM afute kauli zake hizo za upotoshaji. Ndipo akafuta.

Akafuta lakini tena akasema Mnyika anaumwa na anajua yuko Mhimbili anatibiwa.

Kitendo hicho cha yule mbunge kuendelea kutoa lugha za kejeli, kupotosha na kuzungumza mambo ambayo hawezi kuthibitisha huku kiti kikiwa kimya, kikamfanya Waitara asogee kwake ili kuwa karibu naye.

Baada ya kuona hivyo Naibu Spika akaagiza askari wamtoe nje, kama ambavyo inaonekana kwenye picha inayosambaa.

Hicho kilichotokea jana jioni, ndiyo mwendelezo wake wa asubuhi hii ambapo wabunge wanawake wa Ukawa wametolewa bungeni baada ya kutaka ufafanuzi na hatua dhidi ya hizo kauli za udhalilishaji zilizotolewa jana, mbele ya Naibu Spika ambaye naye ni Mbunge wa Viti Maalum.

Wabunge hao wameshazungumza na wanahabari kuelezea suala hilo na sasa wanaendelea na kikao. Tusubiri maamuzi ya kikao hicho.

Lakini jambo la kushangaza sana ni kwamba wakati lugha za kudhalilisha zikitolewa jana, si tu NS alikuwa anaonekana kunyamazia lkn pia viongozi wa Umoja wa Wabunge Wanawake (wote) walikuwa wanapiga makofi.

Hayo ni mbali na majibu ya mmoja wa Manaibu Waziri aliyesema jana bungeni kuwa anaweza 'kuwatia/kuwapiga za uso' wabunge wa upinzani, kisa walihoji alivyokuwa akijibu hoja zao bungeni

Makene

Ukiwa unaishi katika nyumba ya vioo usiwe wa kwanza kutupa mawe. Tundu Lisu katika hotuba yake yote ilikuwa mipasho tu ambayo inaibua hisia. Pia wachangiaji wa upinzani nao hasa wa UKAWA hakuna anayezungumzia matatizo ya jimbo lake bali ni kuongelea mipasho na vijembe tu. Mbaya zaidi wapinzani si wavumilivu kusikia maneno ya kuudhi yanayopelekwa upande wenu.
Msipobadirika bunge huenda mkaathirika katika chaguzi zijazo. Umekuwa kila mara unaleta taarifa humu jamvini hasa zile zinazotolewa na wabunge wenye mipasho na maneno ya shombo kama kina Tundu Lisu. Hotuba zenye mchango wa kujenga nchi huzileti.
Unashadidia kitendo cha huyo Mwikabi kwenda kukaa karibu na mbunge wa ccm ili amfanyie fujo badala ya kukilaani kitendo hicho na vyote vya kufanya fujo.
 
Mbona jambo hilo dogo tu ilibidi wao ndio wathibitishwe kama hivyo viti walivipata kihalali na waonyeshe ilikuweje wakawa wao ni si wengine.
HAHAHAMMENIKUMBUSHA ENZI ZA EKOTIKE ALIKUWA ANAWEKA VITU MAALUM HAHAAAAAA KWAVILE CCM WALISHAZOEA UBAZAZI WANADHANI KILA KIUMBE WA TZ NI BAZAZI SHAME UPON U
 
Tulia Ackson atavuruga bunge , imethibitika kwamba hana uwezo .
Ni ajabu sana kuona wanatoka nje kwa swala hilo kwani ni wabunge hawahawa ambao Kubenea alisema amechungulia shanga na nguo zao za sirini lakini hawakutoka nje,sasa kuambiwa baby nini kimewauma hasa? Au kwa kuwa katamka mtu tofauti na ukawa?
 
NS nilitegemea uwe kama mahakimu wanawake, ukitaka kujua kuwa wako makini basi kesi imuhusu mwanamke.......!! sasa wewe maneno ya fedheha kama hayo bado unaangalia huoni kwamba maneno hayo hayachagui yanajumlisha wanawake woote mlioko humo.........?
 
hili swala la ushoga nakumbuka ni chadema waliwatuhumu wenzao wa cuf juu ya hili miaka iliyopita,hivi chadema walifuta hii kauli yao??
 
kumbe baby tusi,sasa ole wake mtu aniite baby kuanzia leo,ataambulia kipigo cha panya paka mwizi.
 
HAYA MAMBO KAMA YAKIENDELEA KUFUMBIWA MACHO IPO SIKU MBUNGE ATAKUJA KUINGIA NA SILAHA BUNGENI NA KUFANYA YASIYOTARAJIWA NA CCM WATABEBA LAWAMA ZOTE.
 
Back
Top Bottom