Nicholas
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 25,260
- 7,195
Duh.. katik pita pita yangu iliyonipitisha miji kama mitatu hivi nimeguja gundua kuwa watu hawapo tayari kwa sensa,pia nilibahatika scan kidogo mahiojiano ya ATN na raia mitaani.Hofu yangu ni kwamba hili si kwa waislam tuu ndugu zangu.Kweli kuna idadi kubwa ya waislam wasiokuwa tayari kufanya hivyo,ila pia kuna watu kutoelewa sana, na pia watu kutokuwa na nia kabisa.
Hofu yangu ni kwamba hata kama sheria ipo je itatekelezeka kama nusu ya nchi hawatashiriki?Watawekwa magereza yapi, na watashikwa na askari au hata migambo wangapi?Na watasafirishwa na magari yapi?Kuna uwezekano wakahesabiwa watu chini ta walioandikishwa katika kupiga kura katik uchaguzi uliopita, kama watazidi basi watazidi kwa idadi ya watoto wadogo na si watu wazima. katika pitapita yangu nimegundua kwanza watu hawajui umuhimu wa sensa na hivyo kutojianda kwa lolote.
Kati ya hao wasiojua wapo waliodanganyana kwa kuambiwa kuwa mafisadi wanataka watumie majina kujipatia hela toka kwa wafadhili.Wapo wengine wanahofu kwanini ianze usiku?na wanahofu kuwa na wezi wanaweza wagongea kwa style hiyohiyo.Wapo watu mjini kabisa wenye imani zao toka vijijini wanaamini kuhesabiwa ni vibaya kwani watakufa.Na kuna wengi wanalalamika kuwa kuhesabu pamoja na mifugo ni dharau, kwamba nao ni wanyama.Wengine wanasema kuwa mifugo yao inahesabiwa ili ije chukuliwa na serikali ya mafisadi... Hayo yote kwa msomi si vigezo sana ila in reality si yakuchezea.
Katika pita pita yangu ,nimegundua kuwa katika vigenge vyote hivyo vilikuwa vikiongozwa na watu wenye ushawishi na kuaminika katika circle zao ingawa nao ama si waelewa ama wanadhamiria.Na pengine palikuwa na wazee ambao wanawaangalia hawa jamaa kama waelewa na kukubalina nao kwani sehemu nyingine nimesikia wakichangia kwa kauli kama "mbona zamani hatukuhesabiwa na tuliishi", wengine wanasema "hii ni janja ya wazungu kutuua kwa vile CCM wanahongeka" na mengine mengi sana. Hofu yangu ni kwamba serikali haikufanya vizuri sana katik kujihakikishia hadi siku moja kabla watu zaidi ta 99% wapo tayari na wanafikika,ili watakaobaki kama wanaleta za kuletwa basi waadhibiwe huku data zao zikitolewa na mtu mwingine.
Serikali haikuwa na 2-ways channel ya kuwasiliana na wananchi na wananchi kuwasiliana na serikali. Kwa muda tuliofikia ni vigumu kubadili tarehe, na vigumu serikali kukaa na kurekebisha hali,ila NI RAHISI wananchi kuelimishana,kuhimizana kuhesabiwa na hata kukumbushana na kutoana hofu kuwa watoe majibu sahihi bila kudanganya.Kwani sensa siku hizi ni zaidi ya kuhesabu idadi. Pamoja na kuwa tunahimizana kushiriki na kutoa majibu sahihi bado serikali inabidi iwe flexible katika kupokea taarifa na kuzifanyia kazi haraka na kwa uwazi ili mwisho wa zoezi pasiwe na mashaka ya makosa makubwa.Wajaribu fanya namna ya kuwafikia watu wa jamii za wafugaji ambao huhama hama katika mapori nao wakipewa habari potofu kuwaona ni kukimbizana katikati ya wanyama pori,kitu kinachoweza washawishi makarani kuishia chini ya mti n akujiandia wajuavyo.
Hakuna muda wa kulaumu tena serikali ingawa hali ni very citical zaidi ya kila mtu kuwa mwalimu.Kwa wale wana campaign wa vyama hapa ndipo kwa kufanyia mazoezi ya 2015. Mungu Ibariki TZ, Mungu ibariki Africa.