Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe !!

Napata shaka na DCI Manumba anatoa wapi utashi wa kuendelea kulitumikia taifa wakati uadilifu wake mbele ya jamii haupo tena. Mawaziri watatu wameshamkana na wamekana vyanzo vyake vya taarifa zake, waziri ambae ni boss wake anasema uchunguzi unaendelea wakati yeye anasema amekamilisha na jalada lipo kwa DPP
 
nashindwa kuielewa hii movie,huyu nahodha kama waziri mwenye zamana inamaana hakuwa na taarifa ya anachokifanya mtumishi wake (manumba)?ikizingatiwa kuwa ni ishu iliyoanza mda mrefu,kwa nini nahodha hakutoa taarifa kama anayotupa leo,mpaka manumba alipokuruka na taarifa yake,na ni muda wa manumba kuja kuuleza umma kilichopo nyuma ya pazia ..tunahitaji kujua nani yuko sahihi na nani anatuongopea..
 
Mkuu Ngumijiwe, sio kidogo ana make sense, he is making all the senses kwa sababu hii ndio mara ya kwanza serikali imekiri inafanya uchunguzi wa kipolisi na uchunguzi huu sio tuu utahusu uwezekano wa kupewa sumu bali madai yote ya Mwakyembe ambayo huko nyuma waliyapuuza!.
Nahodha ni muaminifu sijui wa kumchafua!!
 
Movi inaendelea,stelingi sijui atafia kwenye majani kama picha la kihindi?ngoja tusupiri
 
Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli hawa jamaa wanatuzeveza tuu na kujibaraguza!.

1.Nikianzia na taarifa ya DCI Manumba, japo sasa wote wanamruka, yeye alitoa taarifa ya kilichopo, " a bird in the hand worth two in the bush". Amini nawaambieni, Dr. aliporejea kutoka Apollo amekuja na complete medical report ya kilichopo!. Report hiyo iko serikalini, Dr. Mponda anajua, Nahodha anajua na JK aliisoma kwenye kikao cha Cabinet!. Hivyo DCI hakuzusha kitu and infact kazi yake ya awali alishamaliza, report yake iko kwa DPP kusubiri uamuzi zaidi.
2. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda ni muongo mkubwa na mnafiki kujifanya serikali haina report hiyo bali aliyenayo ni mgonjwa mwenyewe tuu!. Huu ni uongo mtakatifu unaofaa kuwadanganya watoto na humu jf tuna watoto kibao wa kifikra wakindanganywa tuu hata kwa issie ndogo, wanadanyanyika!.
3. Alichotakiwa kusema ni ukweli kuwa ripoti hiyo ipo ila ni personal report mgonjwa ndio mwenye full rights za disclosure na sio DCI Manumba!. DCI Manumba alitakiwa aseme uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini hakutiliwa sumu bila kui site report ile!.
4. Waziri Nahodha sasa ndio amekwenda deep, hapa sasa ndio tumepewa kitu kipya, kumbe ameagiza uchunguzi mpya wa forensic ya kubaini jinai ya sumu!. Tangu ameanza kuumwa hadi kupelekwa Apollo hakukufanyika forensic investigation yoyote sasa ndio Nahodha kaagiza ifanyike na ripoti hiyo ataitoa yeye Nahodha. This is something new and something else!. DCI Manumba alishatimiza wajibu wake na jalada liko kwa DPP, lakini kwa sababu waziri sasa ndio kaagiza uchunguzi mpya, jalada litarudi kwa DCI lipelekwa kwa watu wa forensic na hata Apollo sasa ndio wataarifiwa kuwa uchunguzi kwa mgonjwa huyo sio just the ordinary medical report bali ni forensic investigation ambayo ni kazi ya kipolisi na sio ya kidakitari, hata hao Apollo hivyo vipimo sasa watavipeleka kwa watu wao wa forensic for certification just in case kesi itatinga mahakamani!.
5. Kunapotokea ubishani kama huu unaohusisha hard facts, kama unaamini kwenye ukweli, unasimama na ukweli huo unaouamini hata kama utabaki peke yako kwenye ukweli huo kama Yesu alivyosulubiwa kwa kusimama kwenye kweli. DCI Manumba pia ataishia kusulubiwa ili serikali ijikoshe kuwa atleast sasa it is doing something kwenye tuhuma za Mwakyembe ambaye alizifikisha kwa IGP Mwema na wakuu wote wakiwemo Tiss, Waziri hadi Ikulu na alipeleka copy kwa baadhi ya wanabalozi just incase something inge imtokea kabla uchunguzi haujafanyika!. Tiss walimpuuza, IGP alimpuuza na kila mhusika walimpuuza only wanabalozi walikuwa concerned ila hawakuweza kuingilia kati kwa sababu haya ni mambo ya ndani!.

Wajameni Mnyonge tumnyongeni ila haki yake, mpeni!.

Pasco.
Pasco.......Kweli wewe ni kigeugeu.......Nimeamini
 
Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe Send to a friend
Monday, 27 February 2012 19:55
0digg

nahodha-vuai-top.jpg
Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha

ASEMA UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA NA MATOKEO ATATANGAZA YEYE, ATAKA MANUMBA AULIZWE MWENYEWE CHANZO CHA TAARIFA YAKE
Ramadhan Semtawa
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amesema uchunguzi kuhusiana afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe bado unaendelea na ni yeye atakayetangaza matokeo ya kama alipewa sumu au la baada ya kukamilika huku akiikana ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna, Robert Manumba.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nahodha kutoa tamko hilo tangu kuibuka kwa mjadala kuhusu afya ya Dk Mwakyembe hasa baada ya DCI Manumba kuutangazia umma kwamba ripoti kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaonyesha kuwa Naibu Waziri huyo hakulishwa sumu, kauli ambayo ilipingwa na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Dk Haji Mponda na Dk Mwakyembe mwenyewe.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Nahodha alisema uchunguzi kuhusu afya ya Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na hauwezi kufanyika ndani ya wiki mbili au mwezi.

“Ninachosema ni kwamba uchunguzi nilioutangaza bado unaendelea,” alisema na kuongeza: Sasa mimi nimetangaza matokeo ya uchunguzi? Mimi ndiyo Waziri nasema uchunguzi bado unaendelea na mimi ndiyo nitatangaza hitimisho la jambo hilo.”

Alisema suala la Dk Mwakyembe ni zito na siyo la mtu kukurupuka kwani linagusa hisia za watu na kutahadharisha baadhi ya watu wanaojaribu kulifanya jepesi wanachezea kitu hatari.

“Ndiyo maana nasema ni jambo linalohitaji weledi wa hali ya juu katika kulichunguza. Ni jambo zito la kisayansi, naomba nipewe muda ili uchunguzi nilioagiza ufanyike kwa kina. Nasisitiza ni jambo linalohitaji weledi wa kisayansi.”

Waziri Nahodha alisema uchunguzi huo unafanyika kwa kuhusisha jopo la wataalamu wa sayansi hivyo kuwataka Watanzania kutambua kwamba uchunguzi huo unaendelea na ni vigumu kutamka utakamilika lini.

Kuhusu ripoti ya DCI

Alipoulizwa ni kwa nini asimchukulie DCI Manumba hatua kwa kutoa tamko wakati uchunguzi alioagiza haujakamilika alisema: “Ndiyo maana nasema, uchunguzi wa suala hili unaendelea. Sasa hatima yote hayo unayozungumza nasema nipeni muda.”

Alipoulizwa ni wapi DCI Manumba alipata ripoti ya Dk Mwakyembe wakati mgonjwa mwenyewe na Waziri wa Afya wameikana, alijibu: “Sasa, hilo ni vyema ukamtafuta yeye mwenyewe DCI aseme. Mtafute aseme yeye na Waziri wa Afya, hao watu wawili wanaweza kuzungumzia ripoti hiyo, lakini mimi nasema uchunguzi wa jambo hili la Dk Mwakyembe ni wa kisayansi na bado unaendelea.”

Alisema alichokisema DCI Manumba kinaweza kuwa na msingi ambao anaujua mwenyewe hivyo, ni vyema akaulizwa yeye kuhusu undani wa ripoti yake huku akisisitiza: "Mimi ninavyoliangalia jambo hili la Dk Mwakyembe linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulishughulikia. Hilo la DCI mtafute mwenyewe akueleze.”

Nahodha pia hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani hata pale alipoulizwa ikiwa haoni kwamba kukanwa kwa kiwango hicho kikubwa kwa ripoti ya DCI Manumba kunawafanya wananchi waanze kutilia shaka utendaji kazi wa jeshi la polisi.

Hata hivyo, alipoulizwa jana kuhusu kukanwa kwa ripoti yake na mawaziri, akiwemo wa Mambo ya Ndani ambayo ndiyo wizara mama inayosimamia Jeshi la Polisi, DCI Manumba alisema kimsingi hawezi kujibizana na waziri yeyote kwani kufanya hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu katika utumishi wa umma.

Alisema alichokifanya ni kuandaa jalada ambalo tayari liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye kwa mamlaka na utaalamu wake wa kisheria, ataamua cha kufanya baada ya kulipitia.

“Siwezi kujibizana na waziri wangu au waziri yeyote. Kama amesema uniulize mimi, ninachoweza kusema ni kwamba tayari nimeandaa jalada liko kwa DPP. Sasa nikianza kuzungumza hili au lile itakua haina maana watu watasema nimeanza kujitetea,” alisema.

DCI, Dk Mwakyembe na Dk Mponda

Akizungumza na waandishi wiki mbili zilizopita, DCI Manumba alisema: “Ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu.”

“Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria,” alisema Manumba.

Hata hivyo, siku moja baada ya kauli hiyo ya DCI Manumba, Dk Mwakyembe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema: "Napata tabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa ‘nyingine’ na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au ‘walisomewa!’

“Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (uboho) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti au kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “Hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu.”

Dk Mwakyembe pia alitoa sababu kuu tatu za kupinga ripoti ya DCI Manumba: “Kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake, unaoendelea katika Hospitali ya Apollo, India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu, pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa ‘sikunyweshwa sumu’ wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.

Tatu ni kitendo cha Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima sasa, halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

Januari 19, mwaka huu gazeti hili pia lilifanya mahojiano maalumu na Waziri Mponda ambaye naye alisema kwa utaratibu, ripoti ya daktari ni ya mgonjwa... “Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi.”

Alisema wanaoweza kuzungumzia maradhi ya Dk Mwakyembe ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo.

KWANI SHAMSI SI NDIYO BOSS WAKE? AU WANAOGOPANA KAMA KAWAIDA YA MAGAMBA?
Kuitumikia serikali ya JK ni sawa kufanya kazi kile chumba cha Safari ya mwisho paleee Muhimbili..Du
 
Pasco bana!!!
​
Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli hawa jamaa wanatuzeveza tuu na kujibaraguza!.

1.Nikianzia na taarifa ya DCI Manumba, japo sasa wote wanamruka, yeye alitoa taarifa ya kilichopo, " a bird in the hand worth two in the bush". Amini nawaambieni, Dr. aliporejea kutoka Apollo amekuja na complete medical report ya kilichopo!. Report hiyo iko serikalini, Dr. Mponda anajua, Nahodha anajua na JK aliisoma kwenye kikao cha Cabinet!. Hivyo DCI hakuzusha kitu and infact kazi yake ya awali alishamaliza, report yake iko kwa DPP kusubiri uamuzi zaidi.

Pasco, kwa hiyo DCI alisoma report ya hospitali ya Dr. Mwakembe? if yes, Report ya Hospitali ndio report ya uchunguzi wa kuwekewa sumu? Kazi aliyoifanya DCI ni ipi? uchunguzi alioufanya ni upi? na ani alimpa ruhusa ya ku-disclose report ya ugonjwa wa mtu bila consent yake? Dont be ridiculous!

2. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda ni muongo mkubwa na mnafiki kujifanya serikali haina report hiyo bali aliyenayo ni mgonjwa mwenyewe tuu!. Huu ni uongo mtakatifu unaofaa kuwadanganya watoto na humu jf tuna watoto kibao wa kifikra wakindanganywa tuu hata kwa issie ndogo, wanadanyanyika!.

ARROGANT SIDE OF YOU!!

3. Alichotakiwa kusema ni ukweli kuwa ripoti hiyo ipo ila ni personal report mgonjwa ndio mwenye full rights za disclosure na sio DCI Manumba!. DCI Manumba alitakiwa aseme uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini hakutiliwa sumu bila kui site report ile!.
4. Waziri Nahodha sasa ndio amekwenda deep, hapa sasa ndio tumepewa kitu kipya, kumbe ameagiza uchunguzi mpya wa forensic ya kubaini jinai ya sumu!. Tangu ameanza kuumwa hadi kupelekwa Apollo hakukufanyika forensic investigation yoyote sasa ndio Nahodha kaagiza ifanyike na ripoti hiyo ataitoa yeye Nahodha. This is something new and something else!.

Something New? mwanzoni walukuwa wanafanya uchunguzi wa nini? alicholalamikia Mwakembe kilikuwa nini? na wao walikuwa wanafanya uchunguzi wa nini?? Ridiculous!!

DCI Manumba alishatimiza wajibu wake na jalada liko kwa DPP, lakini kwa sababu waziri sasa ndio kaagiza uchunguzi mpya, jalada litarudi kwa DCI lipelekwa kwa watu wa forensic na hata Apollo sasa ndio wataarifiwa kuwa uchunguzi kwa mgonjwa huyo sio just the ordinary medical report bali ni forensic investigation ambayo ni kazi ya kipolisi na sio ya kidakitari, hata hao Apollo hivyo vipimo sasa watavipeleka kwa watu wao wa forensic for certification just in case kesi itatinga mahakamani!.

Pasco, usijichanganye, unasoma/sijui umeshamaliza kusoma sheria, nani anafanya forensic investigation? na inakuwa chini ya nani?
Kwanza, DCI alifanya uchunguzi wa kitu gani in the first place? na sasa hivi akirudishiwa file kutoka kwa DPP, anakwenda kufanya uchunguzi gani? this proves kwamba DCI and the rest of the team are a bunch of mediocre, good for nothing.

Halafu na wewe kwa taarfa yako, madaktari hawawezi kuifanyia taarifa ya mgonjwa forensic investigation unless asked so by a specified authority!! wao kazi yao ni kutambua ugonjwa, kisababishi na kutibu. The investigation related to crime (forensics) hawahusiki nayo - from the traditional meaning of the word and its liberal meaning!

5. Kunapotokea ubishani kama huu unaohusisha hard facts, kama unaamini kwenye ukweli, unasimama na ukweli huo unaouamini hata kama utabaki peke yako kwenye ukweli huo kama Yesu alivyosulubiwa kwa kusimama kwenye kweli. DCI Manumba pia ataishia kusulubiwa ili serikali ijikoshe kuwa atleast sasa it is doing something kwenye tuhuma za Mwakyembe ambaye alizifikisha kwa IGP Mwema na wakuu wote wakiwemo Tiss, Waziri hadi Ikulu na alipeleka copy kwa baadhi ya wanabalozi just incase something inge imtokea kabla uchunguzi haujafanyika!. Tiss walimpuuza, IGP alimpuuza na kila mhusika walimpuuza only wanabalozi walikuwa concerned ila hawakuweza kuingilia kati kwa sababu haya ni mambo ya ndani!.

Wajameni Mnyonge tumnyongeni ila haki yake, mpeni!.

Pasco.
 
kwa hiyo waziri ana ka unit kake kakuchunguza nje ya mfumo unaomhusisha DCI?
 
Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli hawa jamaa wanatuzeveza tuu na kujibaraguza!.

1.Nikianzia na taarifa ya DCI Manumba, japo sasa wote wanamruka, yeye alitoa taarifa ya kilichopo, " a bird in the hand worth two in the bush". Amini nawaambieni, Dr. aliporejea kutoka Apollo amekuja na complete medical report ya kilichopo!. Report hiyo iko serikalini, Dr. Mponda anajua, Nahodha anajua na JK aliisoma kwenye kikao cha Cabinet!. Hivyo DCI hakuzusha kitu and infact kazi yake ya awali alishamaliza, report yake iko kwa DPP kusubiri uamuzi zaidi.
2. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda ni muongo mkubwa na mnafiki kujifanya serikali haina report hiyo bali aliyenayo ni mgonjwa mwenyewe tuu!. Huu ni uongo mtakatifu unaofaa kuwadanganya watoto na humu jf tuna watoto kibao wa kifikra wakindanganywa tuu hata kwa issie ndogo, wanadanyanyika!.
3. Alichotakiwa kusema ni ukweli kuwa ripoti hiyo ipo ila ni personal report mgonjwa ndio mwenye full rights za disclosure na sio DCI Manumba!. DCI Manumba alitakiwa aseme uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini hakutiliwa sumu bila kui site report ile!.
4. Waziri Nahodha sasa ndio amekwenda deep, hapa sasa ndio tumepewa kitu kipya, kumbe ameagiza uchunguzi mpya wa forensic ya kubaini jinai ya sumu!. Tangu ameanza kuumwa hadi kupelekwa Apollo hakukufanyika forensic investigation yoyote sasa ndio Nahodha kaagiza ifanyike na ripoti hiyo ataitoa yeye Nahodha. This is something new and something else!. DCI Manumba alishatimiza wajibu wake na jalada liko kwa DPP, lakini kwa sababu waziri sasa ndio kaagiza uchunguzi mpya, jalada litarudi kwa DCI lipelekwa kwa watu wa forensic na hata Apollo sasa ndio wataarifiwa kuwa uchunguzi kwa mgonjwa huyo sio just the ordinary medical report bali ni forensic investigation ambayo ni kazi ya kipolisi na sio ya kidakitari, hata hao Apollo hivyo vipimo sasa watavipeleka kwa watu wao wa forensic for certification just in case kesi itatinga mahakamani!.
5. Kunapotokea ubishani kama huu unaohusisha hard facts, kama unaamini kwenye ukweli, unasimama na ukweli huo unaouamini hata kama utabaki peke yako kwenye ukweli huo kama Yesu alivyosulubiwa kwa kusimama kwenye kweli. DCI Manumba pia ataishia kusulubiwa ili serikali ijikoshe kuwa atleast sasa it is doing something kwenye tuhuma za Mwakyembe ambaye alizifikisha kwa IGP Mwema na wakuu wote wakiwemo Tiss, Waziri hadi Ikulu na alipeleka copy kwa baadhi ya wanabalozi just incase something inge imtokea kabla uchunguzi haujafanyika!. Tiss walimpuuza, IGP alimpuuza na kila mhusika walimpuuza only wanabalozi walikuwa concerned ila hawakuweza kuingilia kati kwa sababu haya ni mambo ya ndani!.

Wajameni Mnyonge tumnyongeni ila haki yake, mpeni!.

Pasco.

Mkuu Pasco, sikusomi vizuri - si kwenye tundiko hili tu ila ni katika kila ninapojaribu kuunganisha na mengi uliyo comment kuhusu sakata la kulishwa sumu Mwakyembe. Sitta alitoa tuhuma pale Kawe kesho yake wewe uliandika - sitoi nukuu ila najua unakumbukumbu vizuri.
Kila kigogo aliye connected with Mwakyembe's saga anamruka DCI kwamba hiyo ripoti siyo or rather a fake one. But you're an exception since you seem to be siding with him. This makes me believe that either you've got an hand in this or rather you know too much to disclose.
Kwa uliyoandika hapo juu naona unataka ku imply that Mwakyembe is all wrong ku comment kuhusu riport ya DCI, hivi jiweke wazi basi unambie kama wewe umebobea katika sheria zaidi yake.
DCI alipeleka jarada la kesi ya Mwakyembe akiwa na mapendekezo ya Sitta kuwa prosecuted for incitement by using provoking words that Mwakyembe kalishwa sumu na mafisadi.
Ngoja tuone kama kweli faili litarudishwa kwa DCI, alkini sisi huku mtaani tunawaona DCI na IGP kama watu amabao matendo yao yanaratibiwa na remote. Hapa hapana shaka kwani na wewe unajua jinsi 'syste' hii inavyfanya kazi kwani na wewe ni beneficiary. Kumbuka ya Nyamongo na Arusha, aibu kwa jeshi letu la usalama wa raia.
Tungekuwa na utawala wa sheria, hawa jamaa wana mengi ya kujibu.

Du! Yaani kulumbana na waziri Sitta ni sawa, ila kulumbana na Mponda na Nahodha ni
utovu wa nidhamu.
Mponda ameongelea kikazi na Nahodha ni kikazi hili suala lime husisha wizara ya afya na mambo ya ndani
 
Wana JF Wengine ni vigumu sana kuwaelewa, Wanajichanganya kila siku kwa kila wanachoandika, Kama Mwakyembe alikuja na taarifa toka Appollo Manake matibabu yamekamilika!?, Na kama matibabu yamekamilika hakupaswa kurudi tena Appolo? Right ??, Sasa kama Dr. Mwakyembe amerudi tena kwa madakitari manake ni wao walimtaka arudi tena na kwa sababu hajapona!!, Na taarifa aliyopewa na madakitari ni kwamba kuna vitu kwenye Uboho wake ndivyo vinavyochochea Hali aliyonayo!!!! Kama ndivyo ilivyo manake Taarifa aliyonayo toka Appollo ndivyo inavyosema, Na ndiyo Taarifa iliyosomwa kwenye Baraza la Mawaziri. Kama ndivyo sivyo manake kuna taarifa mbili tofauti toka kwa madakitari hao hao wa Appollo. Kuna taarifa aliyopewa mwakyembe na nyingine wamepewa serikali. Ipi ni sahihi na ipi si sahihi!!!???
 
Mkuu Nguruvi3, kusema ukweli hawa jamaa wanatuzeveza tuu na kujibaraguza!.

1.Nikianzia na taarifa ya DCI Manumba, japo sasa wote wanamruka, yeye alitoa taarifa ya kilichopo, " a bird in the hand worth two in the bush". Amini nawaambieni, Dr. aliporejea kutoka Apollo amekuja na complete medical report ya kilichopo!. Report hiyo iko serikalini, Dr. Mponda anajua, Nahodha anajua na JK aliisoma kwenye kikao cha Cabinet!. Hivyo DCI hakuzusha kitu and infact kazi yake ya awali alishamaliza, report yake iko kwa DPP kusubiri uamuzi zaidi.

2. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda ni muongo mkubwa na mnafiki kujifanya serikali haina report hiyo bali aliyenayo ni mgonjwa mwenyewe tuu!. Huu ni uongo mtakatifu unaofaa kuwadanganya watoto na humu jf tuna watoto kibao wa kifikra wakindanganywa tuu hata kwa issie ndogo, wanadanyanyika!.

3. Alichotakiwa kusema ni ukweli kuwa ripoti hiyo ipo ila ni personal report mgonjwa ndio mwenye full rights za disclosure na sio DCI Manumba!. DCI Manumba alitakiwa aseme uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini hakutiliwa sumu bila kui site report ile!.

4. Waziri Nahodha sasa ndio amekwenda deep, hapa sasa ndio tumepewa kitu kipya, kumbe ameagiza uchunguzi mpya wa forensic ya kubaini jinai ya sumu!. Tangu ameanza kuumwa hadi kupelekwa Apollo hakukufanyika forensic investigation yoyote sasa ndio Nahodha kaagiza ifanyike na ripoti hiyo ataitoa yeye Nahodha.

This is something new and something else!. DCI Manumba alishatimiza wajibu wake na jalada liko kwa DPP, lakini kwa sababu waziri sasa ndio kaagiza uchunguzi mpya, jalada litarudi kwa DCI lipelekwa kwa watu wa forensic na hata Apollo sasa ndio wataarifiwa kuwa uchunguzi kwa mgonjwa huyo sio just the ordinary medical report bali ni forensic investigation ambayo ni kazi ya kipolisi na sio ya kidakitari, hata hao Apollo hivyo vipimo sasa watavipeleka kwa watu wao wa forensic for certification just in case kesi itatinga mahakamani!.

5. Kunapotokea ubishani kama huu unaohusisha hard facts, kama unaamini kwenye ukweli, unasimama na ukweli huo unaouamini hata kama utabaki peke yako kwenye ukweli huo kama Yesu alivyosulubiwa kwa kusimama kwenye kweli. DCI Manumba pia ataishia kusulubiwa ili serikali ijikoshe kuwa atleast sasa it is doing something kwenye tuhuma za Mwakyembe ambaye alizifikisha kwa IGP Mwema na wakuu wote wakiwemo Tiss, Waziri hadi Ikulu na alipeleka copy kwa baadhi ya wanabalozi just incase something inge imtokea kabla uchunguzi haujafanyika!. Tiss walimpuuza, IGP alimpuuza na kila mhusika walimpuuza only wanabalozi walikuwa concerned ila hawakuweza kuingilia kati kwa sababu haya ni mambo ya ndani!.

Wajameni Mnyonge tumnyongeni ila haki yake, mpeni!.

Pasco.

hivi jalada la kesi iwepo au isiwepo linapelekwa kwa dpp wakati uchunguzi haujakamilika, si ni kupoteza muda wa ofisi ya dpp, je uchunguzi ukikamilika ukawa tofauti na hali ilivyo onekana mwanzo nani wa kulaumiwa? unajua kuna vitu vingine hata kama wewe si mtaalamu lakini bado unatakiwa kuwa na akili ya kujiuliza?
 
Mkuu Ngumijiwe, sio kidogo ana make sense, he is making all the senses kwa sababu hii ndio mara ya kwanza serikali imekiri inafanya uchunguzi wa kipolisi na uchunguzi huu sio tuu utahusu uwezekano wa kupewa sumu bali madai yote ya Mwakyembe ambayo huko nyuma waliyapuuza!.

Hii nchi bwana yaani haieleweki kama bwawa la kambare tu,mama ana ndevu,baba ana ndevu,na watoto wanandevu,huo uchunguzi kabla haujakamilika kuna mikono ya wahusika itakuwa mingi sana hapo,hata report ikija kutoka hakuna kipya,ngoja tusubiri Part 2 tuone!!!!
 
Back
Top Bottom