Nahodha: Sijui DCI Manumba alikoitoa ripoti ya Mwakyembe !!

Mkuu Pasco, nikuhakikishie serikali imelikwepa hili suala si kwasababu ya uchunguzi, ni kwa unyeti wake na jinsi linavyogusa watu wasiogusika.

Waziri mkuu alikwepa, nahodha akakwepa, haji Mponda akaijitoa. Manumba amekubali kubeba mzigo asioujua au anaoujua ndani kuna nini. Leo likitokea lisilotarajiwa na mwenyezi aepushe, Manumba si mhusika tu ni mshiriki mkubwa. Hilo lipo katika kumbu kumbu za wanadamu na ataishi nalo.

Kama taarifa zilikuwa katika Cabinet, ni wazi yeye anajua hilo akiwa DCI. Kwa mtu mwenye akili asingekubali kutupiwa kamba na kuidaka. Ni wazi nahodha sasa anajua na amesoma watu wanasema nini naye anajivua mzigo wa misumari aliojitwika Manumba.

Kama Manumba angetumia fikra kidogo, angewauliza viongozi wenzake juu ya kushindwa kujibu tuhuma au kuzifanyia uchunguzi tuhuma za tishio la mauaji ya Dr Mwakyembe ambayo amekalia ofisini mwake miaka nenda rudi.

Baada ya viongozi wenzake kumkana iwe kwa ukweli uliopo au uongo, Manumba angejiuzulu mara moja. Sasa hivi heshima yake ndani ya vyombo vya dola imekwisha na amebaki kuogopwa tu kama tunavyomuogopa kiumbe yoyote anayeweza kutudhuru.

Pasco, fuatilia upandaji ngazi wa Manumba, angalia alifanya kazi na nani hutakawia kujua kuwa Manumba yupo njia panda akitafakari amtumikie nani kati ya 'mabwana wawili'. Serikali au waliomtuma awasafishe.
Unakumbuka msemo maarufu JF wa mapacha watatu?

Leo mkuu Pasco umegeuka serikali ile ile uliyosema uwezo wake wa uchunguzi umefika mwisho, na taarifa yake ni ya mwisho! Ukasema Sitta ashtakiwe kwa uzushi. Sisi tulijua wanatuchezea akili hawa akina serikali mapema kabisa.
Kwa jinsi wanavyojikanyaga na kujichanganya ndivyo shaka yetu inavyozidi.

Mshauri Manumba, kama anaona anaonewa ajiuzulu. Akiendelea kuwepo tutamuuliza kuhusu majaribio ya mauaji aliyoyaminya ofisini kwake na sasa anakurupuka na hili asilojua au analolijua Kwa kutoa taarifa za kiwango cha darasa la VI B.

Msimamo wa hoja zangu upo pale pale, tunataka ukweli na wala ukweli usifichwe kwa mwamvuli wowote.
Kama ni uharamia, maharamia watajwe na kama ni uzushi, basi wazushi watajwe.
Mkuu Nguruvi3, mimi bado nasimama na DCI Manumba, ripoti ndio ile wala msitatajie kipya!. Maadam Nahodha ametoa maagizo mapya ya kufanyika forensic investigations, sasa ni busara tukasubiri hayo matokeo yatakayoweka hadharani mbivu na mbichi!.

Mtakumbuka mwanajf Hutaki Unaacha alisema nini kuhusu Dr. Omar Ali Juma!. Hivyo vyovyote itakavyo kuwa huo uchunguzi wa forensic utakuja with nothing new!.

Tumuombee tuu Mwakiyembe apate uponyaji wa haraka na arejee nyumbani bukheri wa afya ili yaliyomsibu yabaki kuwa ni "live to tell".
 
Mkuu Nguruvi3, mimi bado nasimama na DCI Manumba, ripoti ndio ile wala msitatajie kipya!. Maadam Nahodha ametoa maagizo mapya ya kufanyika forensic investigations, sasa ni busara tukasubiri hayo matokeo yatakayoweka hadharani mbivu na mbichi!.

Mtakumbuka mwanajf Hutaki Unaacha alisema nini kuhusu Dr. Omar Ali Juma!. Hivyo vyovyote itakavyo kuwa huo uchunguzi wa forensic utakuja with nothing new!.

Tumuombee tuu Mwakiyembe apate uponyaji wa haraka na arejee nyumbani bukheri wa afya ili yaliyomsibu yabaki kuwa ni "live to tell".

i don't trust lowassa. he's greedy.

i dont trust mwakyembe. he's a hypocrite.

swali.....which of the two would you be "happier" to stay away from??

i know where my choice lies.
 
ukweli utabaki kuwa ukweli wala hauwezi kubadilishwa na mitizamo yetu,jeshi letu la polisi na idara zake zote imejaa 'WAHUNI' watupu sampuli ya kina Manumba!,ripoti ya uchunguzi ya tuhuma za kutaka kuuawa kwa Mwakyembe amekaa nayo tangia mwanzoni mwa mwaka jana mpaka leo sasa nashangaa anaporopoka tena hovyo,watashiriki sana dhambi za Lowasa mpaka warudi kwenye moyo wa nchi.
 
Hakika hii movie mbona tamu,ngoja nikoroge hahawa kwani dci r.manumba yuko wapi?mbona haonekani series inaingia episode ya tatu
 
Tatizo hapa ni mawaziri wa Kikwete ambao wanafanya siasa na kukwepa majukumu ya kazi zao. Haiwezekani mtumishi wa umma,ngazi ya unaibu waziri atibiwe nje ya nchi miezi kadhaa eti waziri wa afya hajui anatibiwa nini siku zote hizo.
 
Out of topic: Hivi wenzangu mmenote ukifungua pages zinazofuatia ile starting thread haipo!. Au ni kwangu tuu maana niko mobile?!.
 
i don't trust lowassa. he's greedy.

i dont trust mwakyembe. he's a hypocrite.

swali.....which of the two would you be "happier" to stay away from??

i know where my choice lies.
Between the two devils, choose the lesser!.
 
Mkuu Ngumijiwe, sio kidogo ana make sense, he is making all the senses kwa sababu hii ndio mara ya kwanza serikali imekiri inafanya uchunguzi wa kipolisi na uchunguzi huu sio tuu utahusu uwezekano wa kupewa sumu bali madai yote ya Mwakyembe ambayo huko nyuma waliyapuuza!.

Huu uchunguzi umeanza kufanyika lini? Au ni reactionary uchunguzi unaondeshwa na matukio, na kwa nini hawezi kusema utakamilika lini! I bet this is all gimmick!
 
Ni kitu kimoja tu kilichosimama katika swala zima, kuhusu ripoti aliyoitoa DCI Manumba, kuhusu ugonjwa
wa Dr. Mwakyembe, ni pesa za mafisadi wahusika, ambazo wamezisambaza kuvuruga haki na ukweli wa
jambo husika na kuongezea kutoa vitisho kwa wanaotetea haki ya ugonjwa wa Dr.Mwakyembe.
Na sio rushwa hiyo kapewa DCI Manumba peke yake, bali hata kwa watu ambao uwezi kuwategemea.
Hapa inahitajika tusubiri ripoti kamili ya kiutaalamu, kutoka kwa Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya
Apollo India. Kitendo cha DCI Manumba, kusema umelipeleka faili kwa DPP. linalohusu ugonjwa wa
Dr. Mwakyembe, na mtu aliyesema kama kalishwa sumu, huo ni muendelezo wa vitisho ulio na lengo lilelile
la kuwatetea mafisadi kwa rushwa uliochukuwa. Hapo hamna kilichofichika kila kitu kiko wazi, Be intelligence.
 
SERIKALI INACHUNGUZA KITU GANI ZAIDI KWA AFYA YA DK MWAKYEMBE NJE YA RIPOTI YA MATOKEO YA KITAALAM ILIOTOLEWA NA JOPO LA MADAKTARI BINGWA WANASANSI WA HOSPITALI MAARUFU DUNIANI LA APOLLO NCHINI INDIA???????

I.
SERIKALI ICHUNGUZE SWALA LA 'NANI AU AKINA NANI WANAAHUSIKA NA SUMU KWA MWAKYEMBE' NA WALA SI KUCHUNGUZA 'KAMA ALILISHWA SUMU AU LA'

Serikali iache mara moja kupoteza kodi za wananchi eti kuchunguza KAMA DR MWAKYEMBE ALIPEWA SUMU AU LA, kwa kuwa yeyote anayeendelea kujikita katika mstari huu ajue kwamba kwanza anatupotezea muda, napoteza rasilmali za taifa kwa malengo butu yasiokua na tija si kwa Umma wa Tanzania wala kwa Dk Mwakyembe mwenyewe kwa kuwa majibu ya hilo swali tayari tunayo kitaalam zaidi toka Apollo Hospital wa kule nchini India.

Kwa mantiki hiyo, hoja yangu hapa ni kwamba uchunguzi wa serikali ni sharti sasa ulenge kutafuta majibu ya maswali zaidi juu ya sakata hili la 'Gogoro la Afya la KUCHONGA' ambayo mpaka sasa hayapata kujibiwa. Kwa msingi huu, hivo ijulikane wazi kwa serikaali hii ya Kikwete kwambaa sisi wananchi ambao ndio wenye dhamana wanayotumikia wote hapo serikalini tunapenda kusikia kwamba kodi zetu zinatumika kwa njia ya kuleta majibu mapya yenye tija kwetu na familia ya Dk Mwakyembe na wala si kufanya kazi za kurudufu shughuli ambazo taayari yako wazi mitaani.

Kwa matarajio yetu, swala jipya na zito zaidi kuhitaji majibu mapya ni 'JENI NANI AU AKINA NANI HAO WANAOHUSIKA NA ULISHWAJI SUMU KWA DK MWAKWEMBE NA WANAFANYA HIVO KWA NJIA ZIPI NA MALENGO GANI NA KITU GANI KIFUATE', full stop!!! Hatutaki mizunguko zaidi, miduara zaidi na kule kutupiana kwingi mpira kati ya maafisa waandamizi na vyombo vyao vilivyokwishaonyesha ubutu wa kustaajabisha toka huko nyuma.

Hivyo, mpaka hapa, ni kwa kuendeleza matarajio hayo hayo ya wananchi juu ya sakata hili ambapo tungependa kuaagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulika na maswala ya Afya na Usalama wa Raia, ifanye hima kuunda kamati murua itakayo kuna chombo huru, chenye weledi zaidi na hadidu za rejea za wazi kwenda kuchunguza swala zito zaidi kwamba 'NI NANI AU AKINA NANI HAO WANAOHUSIKA NA ULISHWAJI SUMU KWA DK MWAKWEMBE NA WANAFANYA HIVO KWA NJIA ZIPI NA MALENGO GANI NA KITU GANI KIFUATE', full stop!!!

Haya yote yanatokana na ukweli kwamba taarifa zozote juu ya afya wa kiongozi yeyote wa umma ni mali na na haki ya walipakodi wa nchi hii kuujua tena ki-undani zaidi.

Msingi wa hoja yangu hii ni kwamba mtu anapokua kiongozi anapewa dhamana na umma na pindi inapotokea kwamba ameugua tena ni umma hiyo hiyo ndiyo hugharamia tiba yake mwanzo mpaka mwisho. Hadi hapo si haki kwa mtu yeyote kuficha taarifa zozote mbali na umma kwa kuwa ndiye mwenye dhamana yake pamoja na ufadhiliya kiongozi yeyote

Kama haitoshi, nasema swala la serikali kupanga kuendelea kuchunguza sakata juu ya afya ya Dk Mwakyembe KAMA NI SUMU AU SI SUMU hadi hivi sasa ni AN IRRELEVANT ENDEAVOUR isiomsadia mtu yeyote yule ndani y nchi hii. Hivyo endapo kuna mtu au chombo kuna chombo (pengine CCM) kinataka kujiridhisha zaidi juu ya hilo bali kiendeshe uchunguzi binafsi kwa gharama binafsi na matokeo hayo yaje yatumike kwa kukidhi matakwa yao binasi huko mbali na macho yetu.

Katika eneo hili la pili nako hoja yangu nzito sana ni kwamba hadi sasa ni wazi kwamba jopo la Madaktari Bingwa na Wana-Sayansi wa hospitali Maarufu sana duniani, Apollo Hospital kule nchini India, wao walitumia MUDA MFUPI UNAOJULIKANA kuchunguza vipimo toka kwa Dokta Mwakyembe na KUTUWEKEA JIBU HADHARANI.

Katika msururu mzima wamambo ya uchunguzi wa kitibabu na kisayansi huko Apollo Hospital, katika ulimwengu wa sheria, tunatambua wazi kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa niaba ya Umma wa Tanzania ambao ndio wenye dhamana yote KIKATIBA na wenye kugharamia kila kitu kifedha kupitia kodi zetu) inajitokeza kuwa ni mteja na kwamba Jopo lile la Wataalam waliobobea katika Sayansi ya Tiba pale Apollo Hospital wao pamoja na vyombo vyao vya kisasa ambavyo vilipata kukiridhisha serikali yetu, wao ni waajiriwa katika mtiririko mzima huu.

Hivyo mwisho wa siku wakatoa RIPOTI YA KIUFUNDI WA SAYANSI YA TIBA ILIOTUKUKA ZAIDI DUNIANI PALLE APOLLO HOSPITAL na kuikabidhi kwa serikali hii ya JMT kwa niaba yetu ili sisi kama wateja tujiridhishe nini kinachomsibu mgonjwa wetu (Dk Mwakyembe) ambaye
Umma wa Tanzania tunacho cha kupoteza kwa kiasi kikubwa endapo atadhurika zaidi na hata pindi inapotokea kibahati mbaya akapoteza maisha.

Sasa kunapotokea mtu au watu wanajipenyeza katikati ili watu tusipate kujiridhisha na ripoti hiyo ambayo serikali iliipewa tayaari nadhani hili huenda tukaidai vizuri zaidi kupitia mahakama ili mwajiriwa wetu huyo wa kumtibu Dk Mwakyembe aje akaitoe yote yote bila hata ya nukta kufutwa kwenye ripoti hiyo; and that is a fact to come sooner than later anyway!!

Naam, kitendo hiki kilitokea mara baada ya Madaktari Bingwa na Wataala wote wa Maswala ya Ngozi nchi KUKIRI KWA LUGHA YA MATENDO yao, pale hospitali yetu ya rufaa Muhimbili, kwamba kuhusu sakata la ki-afya ya Dokta Mwakyembe wao ama imewazidi utaalam au kule kukosekana kwa zana za kisasa zaidi ya sayansi ya tiba hapa nchini hivyo serikali ikalazimika kumpeka huyu kiongozi wetu huyo kwa tiba zaidi huko nje ya nchi.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba kuna taasisi bora za tiba zaidi ya milioni moja kote duniani, kitendo cha serikali ya JMT kuamua kumpeleka mtumishi wetu Apollo Hospital na wala si kwingineko maana yaake ni kwamba kuna umakini wa hali ya juu ulitumika kufikia chaguo hilo.

Ndio, tungependa kuendelea kuamini hadi sasa kwamba serikali nayo iliamini sana chombo hicho cha hapo nchini India kwa utaalamu wake wa sayansi ya tiba, mazingira na vyombo vyake vya kisasa zaidi ya hali hlisi tulionayo kokote kule hapa nchini hivyo hata kunapotokea wao kutukabidhi RIPOTI YAO YA KIUCHUNGUZI JUU YA AFYA YA MGONJWA WETU DK MWAKYEMBE, ni imani ile ile inatarajiwa kuewndelea hadi kutafuna yale yaliomo mle ndani ya faili ile ya mgonjwa wetu.

Sasa kama hali hali ni kwa serikali ya JMT kulazimika kukidhi matarajio tajwa hpo juu kuhusiana na ripoti ya Dk Mwakyembe toka kwa wataalam wa saynsi ya tiba waliosifika kote duniani sasa hili la kuibuka mtu kama vile katoka usingizini au kwenye sayari nyingine, na ghafla tu eti anaanza kutunatangaia kundi lingine kufanya kazi ile ile ambayo tayari wao kama serikali walishawaajiri wataalam wa Apollo Hospital kufanya na kutoa hitimisho ya yote, ni nani anajaribu kuchezea akili ya nani hapa na kwa kuteketeza rasimali adimu ya taifa kwa sababu gani hadi hapo????????

Wananchi kote nchini sasa ni wakati mwafaka kusema NO kwa hilo kundi la pili la WANA-SAYANSI UCHWARA WA WAZIRI VUAI NAHODHA eti kwenda kuendesha uchunguzi juu ya uchunguzi wakati maswali zaidi yanayolilia majibu mapya yanaendelea kubaki bila kushughulikiwa.

Kero kubwa zaidi tena juu ya WANASANSI WA VUAI NAHODHA ni kwamba wao tunaambiwa kwamba WATATUMIA MUDA USIOJULIKANA kurudia kazi hiyo hiyo. Hivi tunafanyia ngonjera uhai wa mtu mzito kama Waziri wa nchi na Mpiganaji kwa fida ya wanyonge wa nchi hii kiasi hiki?


II. UCHURO WA NGONJERA ZA MAAFISA WAANDAMIZI SERIKALINI KUHUSU RIPOTI YA GOGORO LA AFYA YA DK MWAKYEMBE


KUHUSU sakata la mgogoro wa afya na 'Ngonjera na Midura Mirefu' inayoendelezwa na Maafisa Waandamizi ndani ya serikali ya Kikwete juu swala nyeti linalogusia uhaai wa Naibu Waziri wa Miundombinu, Mbunge wa Kyela na Mwanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, Dk Harrison Mwakyembe, wananchi sasa tunasema HATUTAKI MBICHI HIZI tena!!

Katu haingii akilini hata kidogo DCI ambaye ndiye Mchunguzi Mtaalam Mkuu nchini Tanzania, awe tu amekurupuka na ki-jiripoti mbele yake tena kwa kuzingtia maelekezo ya weledi wa kazi yake inavyosema, halafu leo hii mtu aibuke na kusema bila aibu eti 'mimi kama Waziri Mwenye dhamani sikujua'.

Mchezo huu maafisa waandamizi wa serikali hii ya Kikwete wa kutupiana mpira kushoto kulia juu ya ripoti ya kitaalam toka Hospitli ya Apollo nchini India hivi sasa unakera kuliko kawaida. Mambo yalianza na Blandina Nyoni wa Wizara ya Afya kushonea faili yenye majibu ya afya ya Dr Mwakyembe kwenye gauni lake ikawa ni vigumu kupakitaka.

Waziri Mwenye dhamana ya Afya, Dk Mponda naye akageuka bubu ghaafla juu ya ripoti hiyo, na wananchi tuliposhinikiza uchunguzi wa NANI ALIYEFADHILI Dk Mwakyembe kutiliwa sumu ili tujue ukweli wa mmbo, hapo ndipo akaibuka Mtetezi wa kujitolea kwa MAFISADI kwa jina la DCI Manumba aliyeendesha uchunguzi ndani ya wiki moja na kuweka mambo hadharani kwa jinsi upeo wake unavyomwelekeza - jibu likawa HAKUNA SUMU HAPA.

Sasa leo hii kaibuka afisa mwingine serikalini kwa jina la Vuaai Nahodha ambaye mpaka hivi majuzi wengi tumekua tukimuona tu kama Waziri sawa tu na picha ukatani (kwa kipindi chake ndio kumetokea mauaji mengi zaidi ya raia mikononi mwao dola wa nchi hii kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii), nae sasa ana-bullshit kila jitihada zilizofanywa na kijana wake Manumba na kuanza kutuaminisha juu ya uchunguzi mwingine juu ya uchunguzi ambao hata wajumbe wake hatuwajui, hadidu za rejea kwao hatuzijui, taaluma zao na uzoefu hakuna anayejua, muda gani na upana wa uchunguzi wao ni swala la kufikirika tu hewani.

Kwa kadiri tujuavyo sisi huku mitaani, DCI Manumba au Saed Mwema anapofanya kazi yoyote ile ni kwamba anayefanya kazi hiyo kimsingi ni Waziri wa mambo ya Ndani ambaye ni Vuai Nahodha. Vile vile, nae huyu waziri naye u waziri mwingine yeyote yule naye anapofanya kazi yoyote kwa jina la serikali yetu hii by extension ni kwamba mwenye kupokea pongezi na au lawama ni Rais wa nchi ambaye ndiye hasa wanayemsaidia kazi zake hizi.

Sasa kwa mtaji wa mizunguko hii yote, kupoteza kote muda zaidi juu ya swala hili sasa tunasema kweli mbichi hizi htuzitaki teeena!!

Kimsingi songombingo hizi zoote zilianzia pale mara baada ya kurejea nchini Dr Mwakyembe kutoka matibabuni nchini India, wananchi tulimbana mbavu kisawasawa AKATUAMBIE KULIKONI juu ya afya yake na kwamba wataalam huko wameona nini?

Kutokana na utaalam wake wa mambo ya sheria na pia maelekezo tu ya Malaika wanaomlinda kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, Dk MwakyembeHapo nyuma kidogo

Hivi kweli enyi maafisa waandamizi wa serikali hii inayofanya kazi kwa niaba ya maelekezo, udhibiti na faida ya MAFISADI waliokubuhu nchini, leo hii mnadiriki kuchezea kamari kweli swala linalogusia uhai wa KIPENZI CHA WANYONGE wan nchi hii kiasi hiki!! Hivi kweli mnajua matokeo ya Ngonjera kama haya ya kutupiana mpira kwetu sisi wananchi huku mtaani kitu gani huenda kikafuatia kweli???????????


III. HITIMISHO JUU YA NGONJERA ZA SERIKALI KWA UHAI WA DR MWAKYEMBE

Wananchi kote nchini sasa ni wakati mwafaka kusema NO kwa hilo kundi la pili la WANA-SAYANSI UCHWARA WA WAZIRI VUAI NAHODHA eti kwenda kuendesha uchunguzi juu ya uchunguzi wakati maswali zaidi yanayolilia majibu mapya yanaendelea kubaki bila kushughulikiwa.
 
Wananchi tunasononeshwa na hizi ngonjera za serikali juu ya uhai wa Dr Mwakyembe. Ukweli ni kwamba michezo yote hii haukubaliki hivyo mwenye kudhamiria kununua muda hapa ajue kwamba ki-uhakika anajiuzia muda kwa bei rejareja kupindukia.
 
Kwenye nchi zinazoelewa maana ya utawala bora na uwajibikaji, huyu Manumba/Manumbu/Kanumba/kanumbu angekua ameshajiuzulu kwa kitendo cha Waziri wake kuikana repory yake. Kwa kifupi Nahodha anamaanisha kwamba DCI ni MUONGO... Sasa sijui anaendelea kufanya nini ofisini.
 
They are playing a minding game wanataka watz wasahau utendaji mbovu juu ya serikali legelege mfano suala la posho, ufisadi n.k Kwa waerevu hatudanganyiki ng'oo
 
Utawala wa kufuata sheria(rule of law), hapa kusiwe na ubabaishaji hao Mawaziri wote hao wanagongana tu. Kisheria kwa mfano mtu 1 apigwe risasi na mwingine alishwe sumu,watu hawa wanatakiwa kukimbizwa hospitali kwa matibabu, jambo la kwanza Hospitali itahitaji PF3 toka police before treating them, after treatment then report huandikwa kwenye PF3. report zitakuwa kwa aliyepigwa risasi doctor atacomment kuwa amepigwa risasi ambayo ilitolewa mwilini na aliyelishwa sumu kama ikibainika itaandikwa alilishwa sumu na ni ya aina gani. Kwa Mtazamo wangu Mimi naona Nchi yetu inafuata rule of law. Kama ni hivyo basi waziri wote wanayo hiyo report ya doctor Mhindi, kwa kuwa Mwakyembe alipoondoka kama alishatoa taarifa hizi kwenye vyombo husika basi obvious hiyo PF3 imedhihirisha kuwa alipewa sumu. Sasa hapa tunaelezwa utafiti wa Kisayansi wa nani tena? kama siyo report ya doctor Mhindi on the PF3?. Kama Mh. Mwakyembe hakupewa huduma kama hiyo basi mawaziri hawa yaani wa Mambo ya nje, Afya , Usalaama wa raia na police hawana report hiyo kwa sababu doctor hawezi kutoa report ya mgonjwa kwa mtu mwingine bila ruhusa ya Mgonjwa au ndugu wa karibu wa Mgonjwa. Ngonjera za nini , the point here ni kufuata rule of law ya Tz waarifu jamii yetu.
 
Mkuu Nguruvi3, mimi bado nasimama na DCI Manumba, ripoti ndio ile wala msitatajie kipya!. Maadam Nahodha ametoa maagizo mapya ya kufanyika forensic investigations, sasa ni busara tukasubiri hayo matokeo yatakayoweka hadharani mbivu na mbichi!.

Mtakumbuka mwanajf Hutaki Unaacha alisema nini kuhusu Dr. Omar Ali Juma!. Hivyo vyovyote itakavyo kuwa huo uchunguzi wa forensic utakuja with nothing new!.

Tumuombee tuu Mwakiyembe apate uponyaji wa haraka na arejee nyumbani bukheri wa afya ili yaliyomsibu yabaki kuwa ni "live to tell".
Mkuu Pasco, hoja inayosumbua siyo matokeo ya uchunguzi ni mchanganyiko wa mambo mengi na hivyo hatutegemei serikali iliyombakiza Manumba, Mponda na Nahodha madarakani kuja na kitu kipya.

Tunachosema hapa ni kuwa kwa kadri serikali inavyojichangaya ni ngumu kuamini kuwa hii ni serikali inayofanya kazi kama timu au ni mkusanyiko wa watu waliopeana nyadhifa tu. Total chaos! na hicho ndicho kinazidi kutia shaka kuhusu Mwakyembe na ugonjwa unaomsumbua.

Waziri mkuu alisema ni suala binafsi. Nahodha akasema ni siri ya mgonjwa na hapaswi kutoa taarifa.
Ni Nahodha huyo huyo anatuambia uchunguzi unaendelea. Ukisoma kwa makini amesema' uchunguzi unaendelea.... na hatutarajii ukamilike katika wiki mbili au mwezi' Ukisoma zaidi anasema hatujui matokeo yatapikana lini.

Hii maana yake ni kucheza na maneno ili kuzuia mjadala huu ulioligubika taifa na uanonekana kuwaweka 'watuhumiwa' matatani zaidi na hata kuharibu mipango yao ya urais 2015. Anachotaka kufanya waziri Nahodha ni kuzuia mjadala.

Pili, amesema uchunguzi wa kisayansi. Hii haitoshi kuwa forensic investigation. Uchunguzi wake unaweza kulenga katika 'Toxicology' ambayo si lazima iwe na matokeo ya forensic ingawa forensic inaweza kuwa nayo. Ninachosema ni kuwa uchunguzi wa kisayansi siyo lazima uwe forensic kama unavyojaribu kutushawishi.
Kwa vile hakusema aina ya uchunguzi wa kisayansi bado anajikanganya and the debate is still open

Wakati uchunguzi aliouendesha ukiendelea bila kujulikana mwisho wake, msaidizi wake muhimu katika uchunguzi DCI Manumba ametoa taarifa. Hii maana yake ni kuwa tayari kuna matokeo na ni suala la muda.
Kama Nahodha anadhani Manumba kakosea basi aombe mamlaka imwajibishe, na Manumba naye ajiuzulu kama anaona ameingizwa mkenge. Hakuna! Hawa wote ni sehemu ya 'sirikali'

Lakini pia kumbuka kuwa uchunguzi huo ni lazima umhusishe Mwakyembe kwasababu zote za kimaadili na kisayansi.
Kama ingekuwa hivyo Mwakyembe asingetoka na taarifa ya kumlaani Manumba
Jiulize, uchunguzi wa kisayansi ni ku-review medical report in order to establish forensci investigation? au ni forensic investigation without 'pre-requisite'?Je uchunguzi wa kisayansi ni 'criminal investigation'?

DCI Manumba haieleweki alipeleka faili kwa DPP kufanya nini. Ina maana alishajiridhisha kuwa kuna jambo lenye ushahidi. Je ni dhidi ya Sitta au Mwakyembe? Ni watu walio hai kutoka ofisi ya Mwakyembe? Ni watuhumiwa tusiowajua?

Kinachofanyiaka hapa ni Nahodha kutaka kuua huu mjadala kwasababu unaonekana si tu kuwaweka pabaya 'watuhumiwa' wanaojulikana bali pia kuichafua serikali ambayo imechafuka ab initio.

Pasco, ukifuatilia kwa makini utaona kuwa lipo jambo zito linafichwa. Hilo ndilo linalojenga hoja kuwa ipo hujuma vinginevyo serikali makini haiwezi kufanya kazi kama genge la wanywa kahawa.
Hata hivyo kama ni uzushi basi wazushi wawajibishwe kwa kutumia ushahidi usio na mashaka

Kwa jinsi serikali ilivyovurugika na kuparaganyika hili suala halitatulia na sasa wale wenye hofu wapo karibu kusema
'The nominees are...'
 
Back
Top Bottom