Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
WAZIRI Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha amesema kwamba mjadala wa mafuta na gesi asilia hakuhitajiki jazba katika kufikia ufumbuzi wa suala hilo iwapo lipakie aktika orodha ya mambo ya muungano au liondolewe na kusimamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Nahodha aliyasema hayo wakati akiakhirisha kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, ambapo alisema jambo hilo linahitaji busara zaidi kuliko jabza.
Msimamo huo wa Waziri Kiongozi unaonekana kwenda kinyume na hoja nyingi za wajumbe wa baraza la wawakilishi ambao mara kwa mara wamekuwa wakisisitiza kwamba uamuzi wa kuliondoka suala hilo katika orodha ya mambo ya muungano halihitaji mjadala zaidi ya utekelezaji.
Tayari baraza la wawakilishi pamoja na baraza la mapinduzi limeamua kuliondoa suala hilo katika muungano, lakini maamuzi hayo yanaonekana kupingana na hutuba ya waziri kiongozi.
Nahodha alisema kamwe suala hilo halitaachwa kuweza kusababisha kuvuruga amani na utulivu uliopo ambao kwa muda mrefu serikali ya Tanzania iansifikana kwa kuwa na hali ya mani ya utulivu katika bara la afrika.
Waziri Kiongozi alisema suala hilo halitaweza kusababisha mgogoro kiasi ya kuigawa nchi na kwamba Serikali ipo makini kuona ufumbuzi wake unapatikana kwa njia za amani.
Waheshimiwa Wajumbe, napenda kuwajulisheni kuwa katika kulipatia ufumbuzi suala la mafuta na gesi asilia tutatumia busara katika kufikia ufumbuzi Serikali italisimamia hilo Alisisitiza Nahodha.
Katika uamuzi wake baraza la wawakilishi lilisisitiza ni lazima serikali ya mapinduzi Zanzibar iwasilishe sera katika baraza hilo ya nishati na gesi asilia ikiwa ni mchakato wa kuunda shirika la maendeleo ya petroli Zanzibar.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Baraza la Mapinduzi wameamua kuwa suala la mafuta na gesi asilia liondolewe kwenye orodha ya mambo ya Muungano.
Wawakilishi hao walisema kwamba uamuzi huo ni wa wananchi wote wa Zanzibar na kamwe si utashi wa mtu mmoja ambapo walisema ni busara kuyaondoa kwa maslahi ya kulinda na kudumisha Muungano.
Tangu kuanza kupatikana kwa gesi asilia Zanzibar imekuwa hainufaiki na mapato ya nishati hiyo licha ya suala hilo kuwa ni la Muungano na badala yake upande mmoja wa Tanzania Bara ndio umekuwa ukinufaika.
Katika uamuzi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM) limetoa maamuzi matano juu ya suala la mafuta na gesi asilia sasa liondolewe katika orodha ya masuala yanayojadiliwa na Kamati ya kujadili kero za Muungano iliyo chini ya Makamu wa Rais.
Maamuzi hayo ambayo ni pamoja na masuala yote yanayohusiana na mafuta na gesi asilia yatolewe kwenye orodha ya Muungano, usimamizi na udhibiti wa rasilimali hiyo katika maeneo yote ya ardhi na baharini pamoja na eneo la ukanda maalum wa kiuchumi ubaki kuwa chini ya SMZ peke yake.
Uamuzi wa tatu wa BLM ni Wizara husika imeagizwa kuanisha katika sera ya udhibiti wa rasilimali ya mafuta na gesi asilia kwa maeneo ya Zanzibar kama ilivyoelezwa katika mapendekezo ya Baraza la Wawakilishi.
Uamuzi mwengine wa BLM ni kuwa Wizara husika iandae mikakati ya kutayarisha sheria ya mafuta na gesi asilia Zanzibar ambayo inafuatiwa na kuanzishwa kwa Taasisi zitakazosimamia sekta hiyo Visiwani hapa.
Uamuzi wa mwisho wa SMZ kuwa ni taarifa ya maamuzi ya SMZ yawasilishwe katika kikao kinachofuata cha kujadili kero za Muungano ambapo kwa sasa kazi inayofuata ni utekelezaji wa maelekezo ya Baraza la Mapinduzi ili kuhakikisha kuwa SMZ inasimamia na kudhibiti sekta ya mafuta na gesi asilia kwa maslahi ya Wazanzibari.
SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.