SMZ yaipongeza TANESCO kuimarisha upatikanaji wa umeme Zanzibar

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,744
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Joseph Kilangi ameipongeza Wizara ya Nishati kupitia shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kupeleka umeme wa uhakika katika Kisiwa cha Zanzibar.

Pongezi hizo zimetolewa 06 Desemba, 2023 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Tanzania Bara pamoja na Wizara ya Maji, Nishati na Madini kutoka Zanzibar.

Amesema kuwa Zanzibar kuna umeme wa uhakika kutoka TANESCO ambalo ni Shirika lililopo chini ya Wizara ya Nishati, hali ambayo imeendelea kuimarisha Sekta ya Utalii Zanzibar pamoja na shughuli nyingine za maendeleo.

“Kwa matumizi bora ya umeme nawashauri watanzania wote kutoka Zanzibar na Tanzania bara kuwa na matumizi bora ya umeme kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyotumia umeme mdogo, kuliko kutumia vifaa ambavyo vinatumia umeme mwingi bila sababu,” amesema Kilangi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, CPA. Michael Marandu amesema uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme katika mfumo wa Gridi ya Taifa ni MW 1,872.05 na kiasi hicho kinatokana na vyanzo mbalimbali.

Ametaja vyanzo hivyo ni Umeme wa maji unaozalisha MW 574.60, Gesi asilia inayozalisha MW 1,198.82, Mafuta yanayozalisha MW 88.13 na Tungamotaka inayozalisha MW 10.5

‘’Tunapongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzabar kupitia Wizara ya Maji, Nishati na Madini kwa kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Nishati nchini hasa Sekta ya Umeme, Gesi na Mafuta, jambo linalochangia Sekta hii kukua kwa kasi hapa nchini,” amesema CPA. Marandu.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO, Mamlaka ya Huduma ya Udhibiti Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Maji, Nishati na Madini kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Taasisi zake.

=======

My Take: Bara subirieni kwanza mvua zijaze mabwawa 😁😁
 
Wamesamehewa deni la umeme, huku tumeongezewa kodi ya pango kupitia umeme ili tuwalipie, wana umeme wa uhakika wakati sisi tunateseka ! Huu muungano wa hovyo sana.
 
Back
Top Bottom