Nahitaji kuonana na Rais, nina jambo la kuzungumza naye

Status
Not open for further replies.

Executivesister

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
514
593
Jamani naomba mtu anayeweza kunipeleke mguu kwa mguu kwa Mama bila maswali mengi, nimewatafuta watu wengi ambao naamini wangenipeleka wananizungusha.

Ina maana sisi raia tukitaka kumuona Rais ni ngumu hivi? Nina agenda ya msingi sana kwa taifa na mimi Sio mwanasiasa kabisa ni mwananchi wa kawaida, na sijawahi kupost kwenye siasa. Kila mtu ninaemuomba aniunganishe ananilazimisha nimpe ujumbe hadi watu wanaonifahamu vizuri wanataka huo ujumbe. Kwa wakatu huu nchi ilipofikia Mama ukuona Ujumbe huu tafadhali nitafute.

Nitawajibika kwa chochote kitakachotokea, siwezi kumwambia mtu kwa sababu mwenye ujumbe wake akiupata atajua tuu kwa sababu ni mama kama mimi.

Nina uhakika chakula kikipelekwa mezani kama wewe hujapika itajulikana tuu kuwa hichi ni cha hapa hapana kimezidi chumvi, noo hapa ni fake hii sukari haifai kuwekwa kwenye pilau. Ka sababu MAMA ndo ana mamlaka na kila kilicho hai na kisicho hai katika nchi hii. Baada ya kumpa huo ujumbe atajua. Na ana mamlaka ya kuchuka hatua yoyote.

Naamini Jf itanikutanisha nae ndani ya masaa 24.Kaka Chogolo nimepewa namba yako nimekupiga najua umetingwa namba yangu inaishia 98.Siajataja jina kwa sababu za kimsingi kabisa akiupata ujumbe wake atajua, nina nia njema na Taifa na sina maslahi yoyote binafsi akipata ujumbe huu atasoma na kwa sababu ana moyo mweupee ataniona hata kwa rohoni.

Nitampa huo ujumbe kwa namna yoyote ile atakayochagua baada ya kuniona. Ujumbe nieandika kwa mkono, upo sehemu nyingine mimi nipo sehemu nyingine atakaponiita nikimuona ataagiza mtu yoyote yeye mwenyewe anaemuamini either tuakauchukue au uletwe yeye ndo ataamua.

HUU UJUMBE HAUHITAJI MTU YOYOTE ISIPOKUWA HUYO.
TUKIRUDI KATIKA SANAA KAZI IKICHELEWA KUIFIKIA JAMII ULE UJUMBE UTAANZA KUCHAKAA NA HAUTAFANYA KAZI HATA UKILAZIMISHA UFANYE KAZI KILA MTU ATAKUWA AMECHOKA KUANZIA MLETA UJUMBE. Na usipomfikia maana yake ni kwamba ukifika kwa mtu asiyehusika.

Ile ndoto ya Yusuph kupelekwa utumwani na ndugu zake itatimia.Nyie akina Rubeni kwa nini mnataka kumpeleka Yusuph utumwani?
Asanteni sana.

Huo ujumbe hauihusu dini au kabila lolote kwa sababu
Babu yangu dini ingine kwa baba
Mama yangu dini ingine
Baba yangu mchaga mama yangu mnyamwezi.

Nimezaliwa uchagani nimeolewa kanda ya ziwa,Nimezaliwa Lutheran nimeolewa sabato. Ni muhimu kuweka wazi ili nyie manabii mnaojituma wenyewe mnikome.
 
Kaz Kweli Kweli!!

Kwamba Ile ndoto ya Yusuph kupelekea utumwani itatimia!!

Kwann ninyi kina Reuben mnataka kumpeleka Yusuph utumwani!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom