Nahisi kuna watu wanachuki binafsi na Lowasa

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Nafikiri kuna watu wenye chuki tu na Lowasa, nimelazimika kusema hivi kwani nimeona kuna watu wanamwangalia Lowasa kama malaika ambaye hakupaswa kukosea. Nafikiri huu ni wivu tu maana tumeshuhudia watu waliothibitika na makosa ya wazi wakifikishwa mahakamani na hatua kuchukuliwa lakini mpaka sasa hivi Lowasa haijaelezwa ni kosa gani hasa alilofanya ambalo ni kubwa kupita viongozi wengine. Watu wengi nafiki hawampendi tu Lowasa, siamini kama Lowasa ndiyo chanzo cha matatizo katika nchi hii wala siamini kama Lowasa amefanya kosa ambalo halisameheki. Lowasa alijiuzuru ili kutoa nafasi kwa yeyote mwenye ushahidi juu ya tuhuma zilizomkabili kwenda mahakamani, mpaka leo kimya hatuoni hatua zozote za kisheria zikichukuliwa dhidi yake.

Ninaghadhibishwa sana ninapoona mtu mmoja akiwa ndiyo chanzo cha habari kwenye vyombo vingi vya habari, Lowasa hata akipenga kamasi kesho yake tutapewa taarifa. Inamaana Lowasa ni muhimu kihivyo? Wakati Lowasa anagombana na Mzee mwinyi wakati ule Lowasa akiwa waziri wa ardhi viwanja vya mnazi mmoja vilipouzwa kwa waarabu Lowasa alisimama kidete kukataa maamuzi ya Mwinyi, aligeuka shujaa hayo hayakumbukwi, Lowasa huyu huyu ndiye aliyesimama kidete bila mzaha kuhakikisha shule za kata zinaenea kila kata mngeweza kupeleka watoto wenu st. Paul nyie?. Lowasa ndiye aliyekuwa anakataa ripoti za uongo zilizoandaliwa na viongozi mbalimbali wa wilaya lakini hayo yote hatuyakumbuki tunakumbuka kitu kinachoitwa Dowans ambapo mapaka sasa inavyoelekea serikali haina pa kukimbilia inarudi tena kupigia magoti Dowans ambayo ilileta mvurugano mkubwa kiasi cha huyo Lowasa kujiuzuru.
watanzania kinachutusumbua ni roho mbaya na chuki zisizo na sababu kwa Lowasa kila jengo zuri utasikia la Lowasa hilo, hayo mambo yanakuhusu nini kama sheria na taratibu za nchi zimekaa kimya? Watu walimwandama hapa mzee wa vijisenti kila kukichwa ni chenge mwisho wa siku hakuna ushahidi wa maana tunaona akitukebehi mitaani kiasi cha kusema inabidi tumuombe radhi!!

Sioni sababu za maana za kumbeba Lowasa kiasi hicho, sijaona sababu za kumhofia Lowasa kama atapenda kugombea urais au vyovyote maana kitakachoamua ni sanduku la kura sio kujaribu kupandikiza unafiki na chuki kwa kila mtu. Tusiwachukiwe watu kwa hatua za maendeleo walizofikia ila tujichukie kwa kuwa wazembe na kutowajibika. Amini unachoamini usilazimishe kila mtu aamini unachoamini.
 
Back
Top Bottom