Nafundisha civics form 2 muungano vipi?

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,258
274
Mimi mwl wa Tempo (mwl wa muda) civics kidato cha 2. Wengi mnafahamu hapo suala kubwa ni serikali pamoja na maswala ya muungano. Swali: mbona yaliyopo kiuhalisia ni tofauti na darasani? mbona tunadanganya watoto? au silabas itabadilisha miaka 20 ijayo. walim wanaimba darasani kuhusu umuhimu wa muungano wakati watoto wanatazama TV na kusikiliza radio na kuona vijiweni watu wakikataa 'laiv' muungano na sasa wanaosema uvunjwe ndio wengi lakini; hili hawaelezwi watoto wetu mashuleni? My take: wizara ya elimu iangalie hili swala. Kwa macho ma3.
 
Muungano bomoa tu,waambie watoto wachoma makanisa wanakuja bala kuangamiza wakristo,waupinge muungano
 
fata kitabu kinasemaji Nepi anasema hao ni majambaz tu, wahuni
 
walimu wanakazi sana. Ndio maana mwigulu aliwaita mashetani, wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana.
 
Mimi mwl wa Tempo (mwl wa muda) civics kidato cha 2. Wengi mnafahamu hapo suala kubwa ni serikali pamoja na maswala ya muungano. Swali: mbona yaliyopo kiuhalisia ni tofauti na darasani? mbona tunadanganya watoto? au silabas itabadilisha miaka 20 ijayo. walim wanaimba darasani kuhusu umuhimu wa muungano wakati watoto wanatazama TV na kusikiliza radio na kuona vijiweni watu wakikataa 'laiv' muungano na sasa wanaosema uvunjwe ndio wengi lakini; hili hawaelezwi watoto wetu mashuleni? My take: wizara ya elimu iangalie hili swala. Kwa macho ma3.
Hii ndio shida ya walimu ma vodafasta! nenda chuo ukasomee ualimu usidandie kazi za watu we kicheche!
 
hata waliosomea hawawez kuuelezea muungano hvyo swal aliloulza ni la msing, c lazima awe mwalimu kamil ndo aweze kudil na changamto ya muungano ambayo hata viongoz wa nch hawana maelezo ya kutosha cha zaid anaendelea kuwadanganya watoto naye anaona c vyema thats why ameulza jaman,
 
Muungano kama yalivyo Mapinduzi ya Zanzibar ni michakato iliyoshirikisha MIKONO pengine na MIDOMO mingi lakini ROHO na VICHWA vya haya ni vichache,yaani nikimaanisha malengo ya watu kama NYERERE, KARUME,BABU,KAWAWA,na THABIT KOMBO,nikitaja wachache.Kwa miaka mingi utafiti, na majadiliano ya kisomi kuhusu muungano mara nyingi ikiepukwa kwa woga ama ukifanyika kwa upotoshaji.
Yafaa mwalimu uutafiti muungano upate vyanzo vya kutosha kuuelewa.Watoto wa kidato cha pili yawatosha kuujua kama mfano wa jitihada za bara hili kutafuta nguvu kubwa kiuchumi,kiulinzi,kisiasa na hata kiutamaduni,
Vyovyote utawasilisha kuwa umegundua muungano huu siyo wa kawaida,utagundua pia haujakamilika wala kuzeeka, pia utagundua kuwa hata wewe ulidanganywa shuleni pia lakini utawapa wanafunzi wajue ulikotoka ,ulipo sasa na mwelekeo!hiyo yatosha,maana mwalimu unatoa 25% wanafunzi wanatafuta 75%
 
...swali alilouliza ni la msingi!km unavyoona hali halisi

Sana. Natumaini litakuwa miongoni mwa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu hususan kutoka kwa KUB na pia ni miongoni mwa maswali anayopaswa kuulizwa Waziri wa Elimu.

In fact issue ya Zanzibar almost kila Wizara ina issue yake ya kujibu kuanzia Wizara ya Muungano (kero za Muungano), Katiba na Sheria (Uhalali wa Muungano), Ulinzi (ulinzi wa Mipaka yetu dhidi ya akina Al-Shabaab ambao ni dhahiri wa nchini).

Nyingine ni Mambo ya Ndani (Usalama wa Raia na mali zao), Fedha, Elimu (swali alilouliza mleta thread), Afrika Mashariki, Mambo ya Nje, Mahusiano ya Jamii (Udini Zanzibar), Utumishi wa Umma (Watumishi wa Umma kutoka Zanzibar kufanya kazi bara hadi jikoni ilhali hawautaki Muungano - Usalama wa Tanganyika).

Pia zimo Wizara za Ajira (wabara kutakiwa kutofanya kazi Zanzibar ilhali wapemba wamejazana Kariakoo na kwingineko), Nishati na Madini (kanuni ya chao chao, changu chetu waliyo nayo Wazenji), Maliasili, Ardhi na Makazi , n.k. Yaani ni suala mtambuka.
 
We fundisha unalopaswa kufundisha kwa kufuata muhtasari kadili ya Wizara ya elimu achana na watu wasemavyo au maoni ya wazanzibari baadhi!!!!!
 
...swali alilouliza ni la msingi!km unavyoona hali halisi
Swali halina msingi wowote zaidi ya uzandiki. Kama angelikuwa mwalimu aliyesomea ualimu na sio mbabaishaji angefundisha kufuata matakwa ya muhtasari (syllabus) na wala asingepata shida ya wanaopinga muungano au waandamanaji wa mitaani. Na ingekuwa fursa kwakekuwapa wanafunzi wake nafasi ya majadiliano ya kisomi juu ya mada husika. Sasa kwa kuwa sio mwalimu ameishia kulia lia hapa na kuwaamusha watu wasiotumia akili kufikiri angalia matokeo yake;

MANGUNGO;4042804]wewe ku***m****@ acha kuneng'eneka mwl katoa ya msingi naona ki...............washa cameroon mkubwa we![/QUOTE]

MARCKO;4043339]sasa ndugu yangu mbona unanitukana? Kweli inaudhi.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom