ogakison
Member
- Nov 26, 2013
- 68
- 12
Hayo mavitabu yaliyoletwa kwenye majahazi yanawachanganya sana akili watu hadi wengine wanajilipua! Mavitabu yenyewe yana contradiction kibao! Yanajichanganya tu. Hakuna kitu humo.
Hayo mavitabu yaliyoletwa kwenye majahazi yanawachanganya sana akili watu hadi wengine wanajilipua! Mavitabu yenyewe yana contradiction kibao! Yanajichanganya tu. Hakuna kitu humo.
Acha uongoUnaposema Bible haipingani unamaanisha nini ??? Hebu soma hapa ndipo ujue
YESU NI MUNGU, SAWA NA MUNGU, AU NI MDOGO KULIKO MUNGU?
YOH 10:30 " Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
MKINZANO WAKE:
YOH 14:28 "Kumbukeni nilivyowaambia, ‘Ninakwenda, na nitarudi.’ Kama kweli mngalinipenda mngefurahi, kwa kuwa nakwenda kwa Baba; na Baba yangu ni mkuu kuliko mimi."
NANI BABA HALISI WA YOSEFU? YAKOBO AU ELI?
MAT 1:16 " Yakobo alikuwa baba yake Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, aliyemzaa Yesu anayeitwa Kristo."
MKINZANO WAKE
LUKA 3:23 "Yesu alikuwa na umri wa miaka kama thelathini hivi alipoanza kazi ya kuhubiri. Yesu alijulikana kama mtoto wa Yusufu. Yusufu alikuwa mwana wa Eli."
MFALME SULEMANI ALIKUA NA VIBANDA VINGAPI NA WAPANDA-FARASI WANGAPI?
1WAFALME 4:26 "Na Sulemani akawa na vibanda 40,000 vya farasi kwa ajili ya magari yake na wapanda-farasi 12,000."
MKINZANO WAKE
2NYAKATI 9:25 Na Sulemani akawa na vibanda 4,000 vya farasi na magari na farasi wa vita 12000, naye akaviweka vitu hivyo katika majiji ya magari na karibu na mfalme katika Yerusalemu.
JE, NI UPUMBAVU AU SI UPUMBAVU KUWA NA HEKIMA?
METHALI 4:7 "Hekima ndilo jambo kuu. Jipatie hekima; na pamoja na vyote unavyojipatia, jipatie uelewaji."
MKINZANO WAKE
MHUBIRI 1:18 "Kwa maana katika wingi wa hekima mna mambo mengi yenye kuudhi, hivi kwamba anayeongeza ujuzi anaongeza maumivu."
hii ni baadhi tu ya mistari inayokinzana.
uko siriasi kweli wewe?
Usahihi wa biblia ni uhakika wa safari ya mtu kwenda kuonana na Mola wake, na makosa kwenye biblia ni mashaka kwenye safari hiyo. Hao watu ni mitume ni manabiii au ni akina nani mpaka wawe na pawa ya kuedit maneno ya Mungu na kuamua makosa mengine yaendelee kubaki, ambapo maana yake watu wengine wendelee kupotea. Mwezi Julai mwaka huu Papa amesema Mungu kamuamuru abadilishe mari 10 za Mungu ili ziendane na wakati uliopo, Kweli? Amri ya nne itabadilishwa ili iendane na sheria ya mashoga kuruhusiwa kuasili watoto waso wao! Kweli? Kwenye biblia ushoga ulipingwa, je Mungu aliyepinga Ushoga ndiye huyu aliyemuambia papa sasa anaridhia ushoga mpaka waruhusiwe kuasili watoto? Uko siriasi kweli. Je mashoga walio uliwa kwa dhambi hiyo watasameheka sababu amri ya nne inabadilishwa?
Hii ishi ni very siriasi kama unatumia akili zake mwenyewe na siyo za kushikiwa.
Badala ya "kuskia" tu kwa watu, ambao hauna uhakika wakweli au la, kuhusu Qur'an, kwanini usiisome wewe mwenyewe halafu uje na jibu.Naamini Mungu yupo, na ndo ametujaalia akili na utashi wa kupambanua mambo. Mara zote linapokuja suala la kuhoji origin ya hivi vitabu vitakatifu, viongozi wetu wa dini wanakimbilia neno moja tu, "AMINI", Kwamba tuamini kwamba hivi ni vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu.
Kwenye biblia tunaambiwa iliandikwa na watu KWA MWONGIZO WA ROHO MTAKATIFU, swali langu ni je? Mimi nikikaa mezani kwangu nikaanza kuandika kitabu, wewe uliyeko jirani yangu utajuaje kwamba ninachoandika ni kwa uwezo wa roho mtakatifu au kwa uwezo wangu mwenyewe. Nikisema kwamba kuna group la watu kwa interest zao, waliamua kuanzisha hiyo project na wakaihalalisha kwa kusema ni neno la Mungu na tuliamini nakosea?
Mimi sio Muislam, hivyo sijui sana kuhusu origin ya Qur'an but, naskia kwamba Qur'an ilishushwa kutoka mbinguni, sijui ni ushahidi gani uliopo wa kuthibitisha hilo au pengine ni dhana ambayo imelalia kwenye imani zaidi. Lakini nikisema kuna watu walitengeneza hayo yote na ili kuyahalalisha wakayaweka chini ya miliki ya Mungu, nitakuwa nakosea.
Tafadhali, usiniambie niamini, nipe sababu za msingi za kwanini nisiamini kuwa biblia na qur'an hazikutengenezwa na kundi flani la watu kwa manufaa yao.
Mbona unajaribu kumsilimisha mtu kiintelijensia?Badala ya "kuskia" tu kwa watu, ambao hauna uhakika wakweli au la, kuhusu Qur'an, kwanini usiisome wewe mwenyewe halafu uje na jibu.
Kwanini uandikie mate na wino upo?
Mkuu kwanini unasema nakosea kusema kuwa Qur'an imetungwa, usiniambie niamini nipe ushahid. Unaamije kwamba Muhammad alipokuwa anaandika qur'an kule pangoni alikuwa haongozwi na shetani, au alikuwa hajitungii mwenyewe. Kwann useme alikuwa anaambiwa na Mungu, why?
Quran is not correct and here is the evidenceBadala ya "kuskia" tu kwa watu, ambao hauna uhakika wakweli au la, kuhusu Qur'an, kwanini usiisome wewe mwenyewe halafu uje na jibu.
Kwanini uandikie mate na wino upo?
Tht's why he did not have his facts correct and here are some few examples from his book quranNani alikudanganya kuwa Muhammad Salma Allahu Alayhi Wasalam alikuwa anajuwa kuandika?
Juu huko umeambiwa kama huamini kuwa imetoka kwa Allah na ni binadam tu aliyeandika, na wewe si binadam? basi andika japo aya moja tu inayofanana nayo kama u mkweli, tena kusanyana na wenzako wote na ukiweza na mashetani waite wakusaidie mtupe aya moja tu inayofanana nayo, tena aya ndogo kabisa ya mistari midogo mitatu tu.Tatizo unanipa unanipa maandiko yaliyoko ndani ya qur'an ambayo yanaihalalisha kuwa imetoka kwa Mungu, hayo maneno hata binadamu anaweza kuyaandika mkuu kwann unahs binadamu hawez kuyaandika hayo maneno?
Utajua kwamba Biblia imeandikwa na Roho Mtakatifu kwa sababu zifuatazo:
1. Biblia haipingani
2. Mtiririko wa wazo ni mmoja ijapokuwa waandishi ni wengi walioishi vizazi tofauti, nchi tofauti, mahali tofauti karne tofauti.
3. Neno liiloandikwa lina unabii uliotimilika ingawa ulitolewa miaka mingi nyuma.
4. Neno la Mungu katika Biblia limekuwa na uwezo wa kubadili maisha ya watu wengi walipoiamini.
Zpo dini za kutengeneza na vitabu vya wanadamu kujitungia wenyewe na kuviita "Maandiko matakatifu", lakini si Biblia.
Nimesemea Biblia wenye vitabu vyao vingine wavisemee vya kwao.
Kuna kaukweli flani hivi..!Je baadhi ya concepts ambazo biblia imekuwa ikisema kuhusiana na ulimwengu na mwanadamu, mfano creation (uumbaji) hauna ushahidi nje ya biblia. Unasemaje hapo?
Pia kuna watu wengi maisha yao yamebadilika kupitia njia nyingine bila neno la Mungu.
Duuuh mkuu wewe umemaliza kila kitu, THATS EXACTLY what this topic is all about. Nashukuru umeisummarize kwenye few lines. "...tunaaminije kwamba binadamu hawakuwa na uwezo wa kuandika vitabu hivi kwa uwezo wao binafsi" Asante sana brother.Yaani Mungu amestop now kufikisha ujumbe kwa watu???na hata alipokuwa akifikisha huo ujumbe alikuwa akiwapendelea watu wa far east tu na sio kwengine???mm sijui umeishi miaka mingapi hadi sasa hapa duniani...lkn sidhani km unawajua vizuri binadamu kiasi unaweza kuwaamini kila waachokiandika km ni sahihi na sio kwa maslahi yao wao...namaanisha hao waliochapisha au kuufikisha huo ujumbe wa Mungu...tunayo mifano hai hapa duniani marais wanavyoibia wapiga kura wao,majaji wanavyo hukumu watu kwa upendeleo nk
Hahahahaaaa we jamaa, u made my day aisee, hiyo ndio argument ya msingi sasa. Ngoja nilale na kulala. Asante sana brother.Sioni sababu ya Mungu kutafuta njia ya kuwafikishia ujumbe wanadamu,kama ni kweli ameweza kuwaumba na kuiumba hii dunia na kila kilichomo ndani yake,basi ujue kumfikishia mwanadamu ujumbe ni jambo dogo mno kwake,halafu ujumbe wa nini wakati ww binadamu ni sawa tu na wanyama mbona wao hawana quran yao?
Sasa hiyo ndo argument inayofuata baada ya wote kukubaliana kwamba hivi vitabu vilitengenezwa na binadamu kwa interests zao. Swali je? Ni nini lilikuwa dhumuni la kufanya ivo? Kwann waandike vitabu biblia na qur'an na vingine ambavyo sivijui na kuwaaminisha watu kwamba ni maneno ya Mungu? Kwann? What was a reason?Inawezekana kweli viliandaliwa na kuandikwa na watu
Swali linakuja hivi "ni wapi waliyatoa haya mawazo na yalilenga kitu gani hasa na kwa sababu zipi?"
Nani alikwambia Kwamba Mohamad alikuwa hawezi kusoma wala kuandika? Au kwa sababu Qur'an imeandika ivo?Nani alikudanganya kuwa Muhammad Salma Allahu Alayhi Wasalam alikuwa anajuwa kuandika?
Naamini Mungu yupo, na ndo ametujaalia akili na utashi wa kupambanua mambo. Mara zote linapokuja suala la kuhoji origin ya hivi vitabu vitakatifu, viongozi wetu wa dini wanakimbilia neno moja tu, "AMINI", Kwamba tuamini kwamba hivi ni vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu.
Kwenye biblia tunaambiwa iliandikwa na watu KWA MWONGIZO WA ROHO MTAKATIFU, swali langu ni je? Mimi nikikaa mezani kwangu nikaanza kuandika kitabu, wewe uliyeko jirani yangu utajuaje kwamba ninachoandika ni kwa uwezo wa roho mtakatifu au kwa uwezo wangu mwenyewe. Nikisema kwamba kuna group la watu kwa interest zao, waliamua kuanzisha hiyo project na wakaihalalisha kwa kusema ni neno la Mungu na tuliamini nakosea?
Mimi sio Muislam, hivyo sijui sana kuhusu origin ya Qur'an but, naskia kwamba Qur'an ilishushwa kutoka mbinguni, sijui ni ushahidi gani uliopo wa kuthibitisha hilo au pengine ni dhana ambayo imelalia kwenye imani zaidi. Lakini nikisema kuna watu walitengeneza hayo yote na ili kuyahalalisha wakayaweka chini ya miliki ya Mungu, nitakuwa nakosea.
Tafadhali, usiniambie niamini, nipe sababu za msingi za kwanini nisiamini kuwa biblia na qur'an hazikutengenezwa na kundi flani la watu kwa manufaa yao.
Wewe uliyezua kuwa "kaandika pangoni" ndiyo utueleze nani alikudanganya hayo ?Nani alikwambia Kwamba Mohamad alikuwa hawezi kusoma wala kuandika? Au kwa sababu Qur'an imeandika ivo?
Yaani Mungu amestop now kufikisha ujumbe kwa watu???na hata alipokuwa akifikisha huo ujumbe alikuwa akiwapendelea watu wa far east tu na sio kwengine???mm sijui umeishi miaka mingapi hadi sasa hapa duniani...lkn sidhani km unawajua vizuri binadamu kiasi unaweza kuwaamini kila waachokiandika km ni sahihi na sio kwa maslahi yao wao...namaanisha hao waliochapisha au kuufikisha huo ujumbe wa Mungu...tunayo mifano hai hapa duniani marais wanavyoibia wapiga kura wao,majaji wanavyo hukumu watu kwa upendeleo nk
Kwani aya ni nn hadi iwe a big deal kuiandika??watu wanaandika novel Hardley Chase sembuse aya moja tu...tena basi aya zenyewe km ndio km zile za muhammad alipanda farasi wake mweupe mwenye mabawa akampeleka hadi mbingu ya saba njiani akakutana na musa,ibrahim adam na yesu hahahaha hizo nakuandikia hata elfu moja ukitaka pembeni nina ganja zng kadhaa utanikubali tu aiseeJuu huko umeambiwa kama huamini kuwa imetoka kwa Allah na ni binadam tu aliyeandika, na wewe si binadam? basi andika japo aya moja tu inayofanana nayo kama u mkweli, tena kusanyana na wenzako wote na ukiweza na mashetani waite wakusaidie mtupe aya moja tu inayofanana nayo, tena aya ndogo kabisa ya mistari midogo mitatu tu.
Mkishindwa utupe jibu kwanini mmeshindwa?