Nafasi za Kazi, Ofisi binafsi ya Mbunge wa Nzega Mjini

Fandre

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
320
225
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mh. Hussein M. Bashe inapenda kuwatangazia watanzania wote kuwa imeanza kupokea maombi ya kazi kwa nafasi mbili ambazo ni LEGAL OFFICER na ADMINISTRATIVE OFFICER watakaokuwa wanafanya kazi katika Ofisi Binafsi ya Mbunge iliyopo Nzega Mjini.

Waombaji ni lazima watambue ya kuwa vituo vya kazi ni Nzega hivyo watalazimika kuwa tayari kuishi Nzega na kujitoa kwa moyo wao wote katika kuwatumikia wana Nzega kulingana na nafasi ambazo wataomba kama ambavyo zimeelezwa katika Viambatanisho(Attachments).

Ikumbukwe Ofisi ya Mbunge haitakuwa na upendeleo wa aina yeyote katika upatikanaji wa wafanyakazi hawa na mchakato utakuwa huru, wazi na haki kwa waombaji wote.
Nia na madhumuni ya kutoa nafasi hizi kwa watanzania wenye sifa tajwa ni kutokana na maono ya Mh. Bashe kuongeza uwezo wa kuwasaidia wananchi wa Nzega katika kutatua kero zao na kutimiza ahadi zake kwa wananchi.

Unaombwa usome maelekezo vizuri kabla ya kutuma maombi yako, hakikisha unatuma nyaraka ulizoombwa tu kulingana na wakati, kwenda kinyume na masharti ni kujiondoa katika hatua ya mwanzo kabisa mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11 Januari saa sita usiku.

Pakua(download) viambatanisho ili uweze kujua kwa undani zaidi kuhusiana na nafasi hizi za kazi.


Imetolewa na;
OFISI YA MBUNGE
JIMBO LA NZEGA MJINI
 

Attachments

  • Job Description - Administrative Assistant.pdf
    227.4 KB · Views: 81
  • Job Description - Legal Officer.pdf
    226.6 KB · Views: 47
Back
Top Bottom