Nafasi 150 za uhakimu makama ya mwanzo

Kama ulikuwa hujastukia ndo hali ilivyo kwenye taaluma karibia zote kasoro udaktari na ualimu!
siku hizi digrii ya kwanza ni kama cheti cha darasa la saba tu!

sasa diploma ya sheria, cheti cha sheria sasa watapangiwa kazi gani................... tunakoelekea ili uwe judge inabid uwe na PHD
 
kazi zenyewe za sheria zilivyo za shida bongo! ngoja nimstue mrembo mmoja proffessional jobless, anasaka kazi for like 4 years now,labda atagundua kijijini napo kunafaa faa

Bongo za shida kwingine wanasheria wanapiga deiwaka nje ya mahakama kuvizia dili.

Sidhani kama kuna nchi yenye wanasheria wengi kama Marekani na ndiyo maana ni nadra sana kukuta wakiitana eti "wasomi".
 
Digrii ya sheria kuwa karani wa mahakama halafu nisishangae ?

Kuweni serious kidogo, sio kwa faida ya kupata kazi tu, Bali kwa kuangalia umesoma nini na unatumiaje ulichosoma kwa manufaa ya nchi. Kuandika summons? Kuandika removal order? Kuandika quorum? Kujaza fomu za dhamana?

Kama tuko makini tubadili mfumo wa mahakama ili kuaccomdate hilo.


Ni kweli inabidi mfumo wa Mahakama ubadilike! - Primary Court Criminal Procedure Code ambayo level ya Diploma anaweza kuendesha kesi!!!
 
NIMETAFUTA GAZETI NA NIMELIPATA,NA INFO NIMEZIPATA SO NAZIUPDATE NDIPO HIZI HAPA:

Hakimu Mkazi Daraja la II – TJS 2 – Nafasi 150
Msajili wa Mahakama ya Rufani anawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kada ya Hakimu mkazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo ambazo zimeorodheshwa hapo chini kutuma yao ya kazi hiyo.

Mahakama za Mwanzo zenye nafasi:
NA.
KITUO
NAFASI
NA
KITUO
NAFASI
1.
MAFIA
1
37.
MUSOMA
2
2.
KILOSA
3
38.
SERENGETI
2
3.
MAHENGE
1
39.
TARIME
2
4.
MVOMERO
1
40.
BUNDA
3
5.
DODOMA
2
41.
TABORA
3
6.
MPWAWA
1
42.
SIKONGE
1
7.
SINGIDA
2
43.
NZEGA
2
8.
KIOMBOI
2
44.
KIGOMA
5
9.
BUKOBA
2
45.
KIBONDO
4
10.
MULEBA
1
46.
KASULU
4
11.
KARAGWE
3
47.
SHINYANGA
4
12.
MBEYA
2
48.
KISHAPU
1
13.
MBARALI
1
49.
MASWA
2
14.
TUKUYU
3
50.
MEATU
1
15.
ILEJE
1
51.
BARIADI
2
16.
MBOZI
2
52.
KAHAMA
3
17.
CHUNYA
1
53.
BUKOMBE
1
18.
KYELA
2
54.
SUMBAWANGA
2
19.
MOSHI
2
55.
NKASI
2
20.
SAME
2
56.
MPANDA
3
21.
ROMBO
1
57.
SONGEA
3
22.
MWANGA
2
58.
NAMTUMBO
2
23.
HAI
1
59.
MBINGA
2
24.
MTWARA
3
60.
TUNDURU
2
25.
MASASI
2
61.
TANGA
1
26.
NEWALA
1
62.
KILINDI
1
27.
TANDAHIMBA
2
63.
LUSHOTO
3
28.
LINDI
4
64.
KOROGWE
2
29.
NACHINGWEA
3
65.
MUHEZA
3
30.
LIWALE
1
66.
PANGANI
1
31.
RUANGWA
4
67.
HANDENI
1
32.
KILWA
4
68.
IRINGA
2
33.
MWANZA
1
69.
MUFINDI
2
34.
UKEREWE
2
70.
LUDEWA
2
35.
SENGEREMA
2
71.
MAKETE
2
36.
GEITA
2
72.
NJOMBE
2
Sifa zinazotakiwa:
Waombaji wanatakiwa wawe na Shahada ya kwanza ya Sheria “Bachelors of Laws” (LL B) kutoka katika Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
Waombaji waliopitia shule ya sheria (Law School of Tanzania) na kufaulu watafikiriwa kwanza.
Kazi za kufanya:

  • Kuandaa mpango wa usikilizaji mashauri.
  • Kusikiliza mashauri ya awali ya Jinai (Criminal Cases).
  • Kusikiliza mashauri ya awali ya Madai (Civil Cases).
  • Kusikiliza mashauri ya awali ya Mirathi (Probate and Administration).
  • Kusikiliza mashauri ya awali ya Ndoa (Matrimonial Cases).
  • Kutoa hukumu katika mashauri yote anayosikiliza ya jinai, madai, mirathi, ndoa na mashauri mengine kadri sheria inavyomruhusu.
  • Kutoa amri mbalimbali za kimahakama anazoruhusiwa kisheria katika Mahakama za Mwanzo.
  • Kusuluhisha mashauri.
  • Kusikiliza rufani kutoka Mabaraza ya Kata.
Utaratibu wa kutuma maombi:
Kwa waombaji walio katika Utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao.
Maelekezo mengine:
Wale wote ambao watakidhi sifa wataitwa kwenye usaili kupitia magazeti.
Mwombaji aonyeshe kituo ambacho angependa kufanya kazi.
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 21/3/2012
Barua za maombi ziambatane na vivuli vya vyeti vya Taaluma (Academic Certificates), kuzaliwa, ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV), picha moja (Passport size) na kutumwa kwa:

MSAJILI
MAHAKAMA YA RUFANI (T)
S.L.P 9004
DAR ES SALAAM
 
Kwakweli sikutaka kusema ila hili limenifanya niseme.Kwanza ni ujuha kudhani kwamba anayeshangaa mwenye shahada ya sheria kwenda mahakama ya mwanzo, anafanya hivyo kwakuwa shahada ya sheria ni NOBLE sana au waliohitimu sheria wako wachache.Ila mtu anaweza kushangaa kwa kuwa sheria haijabadilishwa kuruhusu hilo na wala sijaona hata GN ya serikali inayoruhusu hilo.Hata hivyo mbonambona watu wanaonekana kuwa na fikra mgando sana juu ya kozi hii ya sheria kiasi kwamba kila mtu anasema chochote ili ionekane labda ni USELESS!.Kwanza wapo makarani ambao wana shahada za sheria tena mahakama za wilaya na mahakama kuu na hata ikitokea akawepo kwenye mahakama ya mwanzo, kwa hiyo si ajabu kufanya kazi hiyo na hivyo kuifanya haiwezi kuwa kigezo cha kuifanya kazi hiyo ionekane haifai kwa kiwango ambacho watu wanataka kutuaminisha.Jambo lingine si kweli kwamba kwa mwanasheria mahakama ndiyo last resort ktk suala la ajira.Mfano mimi ni HR Assistant ktk firm moja hapa mjini na nilifanya usahili na kuwatupilia mbali wale walosoma HRM, lakini pia na wapo wengi ambao nimemaliza nao wanafanya ktk mabenki, insurance firms,na tax consultancy firms.Lakini pia kuna opportunities za kuwawakilisha watu ambao wanadhani wamekuwa contracts zao zimekuwa unfairly terminated kwa CMA.Hata hivyo tunaposema wanasheria wamejaa mtaani tunamaanisha nini?.Wako wangapi? je wangekuwa wangapi ili tuseme wachache?.
 
Kama ulikuwa hujastukia ndo hali ilivyo kwenye taaluma karibia zote kasoro udaktari na ualimu!
siku hizi digrii ya kwanza ni kama cheti cha darasa la saba tu!


napingana na we una esema degree ni sawa na chet cha daras la 7,justification yako iko wapi,
ndg wana Jamii forum kwa msaada tu ni kwamba mtu ana lipwa kutokana na level ya shule alio nayo,ukiangalia hapo tangazo linasema Hakimu mkazi tena TJS2 hivvyo hata mtu angekuwa hakimu wa mahakama ya wilaya,au mkoa kama ana degree angeanza na TJS 2 labda hapa cha kuuliza ni je ni vipi huyo mtu atapnanda mpaka kufikia ngazi fulani huko juu,let say usajili na ujaji au kutoka hio TJS 2,1 na kuendelea na fikili ndo la msingi,lakini ku questiion kwamba mwenye degree iweje akawe hakim wa mahakma ya mwanzo,tufike mahalituone kwamba kuna maboresho fulani katika judicial service tuwaunge mkono

namalizia tu kwa kusema hakimu wa mahakama ya mwanzo mwenye degree hawezi akalipwa sawa na hakimu wa mahakama ya mwazo mwenye diploma tofauti ipo nawashauli vijana muombe msiache mtalipwa sawa tu kutokana na degree zenu
rergards
Baba Jose
 
lakini nimeshawai kufanya kazi mahakamani...nikajifunza kuwa mahakimu wa mahakama za mwanzo wana pesa kuliko wale wa wilaya na mkazi...isipokuwa, hao wanaoenda primary court na wana degree ya LLB, wanaweza kusahau sheria kwasababu kule primary court mambo mengi cap. 20 yaan criminal procedure Act ile ya mwenendo tuliouzoea...wanayo ya kwao na opinion of assesors is binding.....so haupo peke yako pale, kuna wazee wa balaza ambao hakika yake hawajasoma sheria kabisa...na wanatoa opinion yao pale...ila wana pesa nyingi sana, na ni miungu watu kupita maelezo....unaabudiwa unaweza hata kufuliwa nguo...watu wanakuletea pesa hata kama huzitaki..
 
lakini nimeshawai kufanya kazi mahakamani...nikajifunza kuwa mahakimu wa mahakama za mwanzo wana pesa kuliko wale wa wilaya na mkazi...isipokuwa, hao wanaoenda primary court na wana degree ya LLB, wanaweza kusahau sheria kwasababu kule primary court mambo mengi cap. 20 yaan criminal procedure Act ile ya mwenendo tuliouzoea...wanayo ya kwao na opinion of assesors is binding.....so haupo peke yako pale, kuna wazee wa balaza ambao hakika yake hawajasoma sheria kabisa...na wanatoa opinion yao pale...ila wana pesa nyingi sana, na ni miungu watu kupita maelezo....unaabudiwa unaweza hata kufuliwa nguo...watu wanakuletea pesa hata kama huzitaki..

CPA usiseme wana yakwao ni Third schedule ya MCA ambayo sio kwa ajili ya pc magistrates peke yao
 
Kuna mpango wa kuruhusu mawakili ktk mahakama za mwanzo so kuna ulazima wa maPM kuwa atleast na LLB jambo lengine ni mabadiliko jaman hv mnadhani tuaendelea kuwa na maPM wenye DL mpaka lini?
 
Nasikia wameongeza na sasa ni nafasi 300 katika magazeti ya jana, jee ni kweli????
 
hakimu.jpg
Hope itafunguka vizuri......
Au nenda hapa http://www.vijanatz.com/tz/jobs/?job_listing=hakimu-mkazi-daraja-la-ii
 
Sasa mwashangaa leo kwa mtu mwenye LLB kuwa Hakimu mahakama ya mwanzo??? Na kiukweli nafasi hizo zinatamka ya kuwa waombaji watakuwa na cheo cha HAKIMU MKAZI DARAJA II ikimaanisha ya kuwa japo kazi zako ni za hakimu wa mahakama ya mwanzo ila unaweza fanya kazi za hakimu mkazi au hata wa wilaya. Kuhusu suala la karani kwa mtu wa LLB si jambo la kushangaza kwa kuwa hata katika nafasi kama za EAC watu wa LLB wanapata nafasi hizo za Ukarani, kwa hivyo hoja ni kuwa inakubidi kuchangamkia hizo nafasi na ukipata chapa kazi kwa bidii yote!
 
Digrii ya sheria kuwa karani wa mahakama halafu nisishangae ?

Kuweni serious kidogo, sio kwa faida ya kupata kazi tu, Bali kwa kuangalia umesoma nini na unatumiaje ulichosoma kwa manufaa ya nchi. Kuandika summons? Kuandika removal order? Kuandika quorum? Kujaza fomu za dhamana?

Kama tuko makini tubadili mfumo wa mahakama ili kuaccomdate hilo.
Mbona watu hamtaki kukubaliana na wakati kumbukeni zamani watu walivaa magome ya miti na sasa wanavaa nguo katika kujisitiri. Sasa hizi Tangazo la East african community mbona hakuna anayeshangaa msimamizi wa ulizi kutakiwa kuwa na degree. Nadhani hata mwenye degree ya sheria anaweza kuomba tu muda unaruhusu
Job Title : Security Officer
Source : East African Community
Requirements : A Bachelors Degree in any field. 5 years of experience in the police service at the level of Superintendent or equivalent rank. Relevant international exposure is essential. Must possess a certificate of good conduct from current/previous employer.
Job Description :To oversee all security and safety matters of the East African Court of Justice
Apply To : The Secretary General
Full Address : The Secretary General East African Community P.O. Box 1096 Arusha - Tanzania.
Email Applications: vacancies@eachq.org
Closing Date : 27/Mar/2012
 
Hata bandari wandtangaza kazi za usimamizi wa security na speciffically law graduates
 
jamani LLB ukaitundike juu ya mti sio fair, mshahara wenyewe mgogoro...huko kijijini kwenyewe maisha shida.. sheria umeisoma kwa kusotea miaka minne...... hapana jamani ... ila kazi ni kazi kwa mwenye kuitaka aifuate kuliko kukaa mtaani kuomba hela kwa shemeji au baba.... ndio maisha ya bongo haya.....
 
Bandarini hela nzuri kaka, hebu tuambie...... nafasi za lini?

Bahati mbaya na mi niliziona deadline ikiwa imepita,ilikuwa tarehe 15/3.Lakini kama unataka kutest zali

Security Officer (Investigation)
- Tanzania Ports Authority
Dar es Salaam, Dar es Salaam
Tanzania Ports Authority
Save
Share
Apply
Date:
06-03-2012
Job Type:
Employee
Job Status:
Full Time
Categories:
Security / Protective Services
Legal
Job Details
Qualifications
First degree in law, criminology
or professional police training
Computer literate
3 yrs post qualification
experience in a reputable
security organization
Must have certificate of
electronics or CCTV operations
and mantainence
Requirements
Application Instructions:
Interested applicants should
send their CV, Cover Letter,
Copies of certificates, testimonials
and 2 references by post to
The Director of Human
Resources & Administration
TPA
P O BOX 9184
Dar es Salaam,
Tanzania


Assistant Security Officer (3
Posts) - Tanzania Ports
Authority
Dar Es Salaam, Mtwara, Tanga,,
Tanzania Ports Authority
Save
Share
Apply
Date:
06-03-2012
Job Type:
Employee
Job Status:
Full Time
Categories:
Security / Protective Services
Legal
Job Details
Qualifications
First degree in law, criminology
or professional police training
Computer literate
3 yrs post qualification
experience in a reputable
security organization
Requirements
Application Instructions:
Interested applicants should
send their CV, Cover Letter,
Copies of certificates, testimonials
and 2 references by post to
The Director of Human
Resources & Administration
TPA
P O BOX 9184
Dar es Salaam,
Tanzania
Application Deadline: Mar 20,
2012
 
Back
Top Bottom