Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #21
Wakuu mpaka sasa kuna vigezo vya kimaandishi vya nani anayetakiwa kuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za Chama na kuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali za seriklai kwa tiketi ya chama. Na kuna vision na manifesto ya chama ambayo wanaogombea nafasi yoyote ile wanatakiwa kuwa na jukumu la kuitekeleza. Lakini kuna vigezo vingine ambavyo havipo kiimaandishi ndio vinaangaliwa na kuzingatiwa kabla ya kuruhusu mtu kupewa nafasi ya kuwa mgombea wa nafasi uongozi, inawezekana hivyo ndio vina nguvu zaidi kuliko vile vilivyoandikwa. It is a matter of having those unwritten qualities and mimick the written ones. So we have official criteria and real criteria, the official one ni ya kuwadanganya watu, na real one is the one which actually work .
Inasikitisha sana kuona kuwa kiongozi anasema wazi kuwa ana msimamo huu kuhusu jambo hili na ana mtazamo ule kuhusu jambo lile, lakini ukiangalia utendaji wake na vitendo vyake huwezi kuamini kinachofanyika. So the idea that we should judge them on their statements and views on policies, budget and how they will work around them is questionable. There is plenty of evidence that what they say and what they actually do, are two different things. Umetoa mfano mzuri sana wa "maisha bora kwa kila mtanzania", angalia nani alileta maisha bora kwa mtanzania, at least aliyejaribu. JK au BM?
Ni vizuri ku-strengthen institutions na kuwapima watu kwa walichofanya kutekeleza kile kilichoandikwa kwenye katiba ya chama, manifesto ya chama na katiba ya serikali na malengo ya kuiboresha Tanzania. Nadhani kuna haja ya kuwa na uniformity kwenye katioba za vyama vyote inapokuja kwenye mambo ya kugombea nafasi za urais. Sasa hivi techinically kuna uwezekano wa any party to win presidency, kwa hiyo ni vizuri kuwe na utaratibu wa kitaifa wa kuscreen wanaotaka kwenda kugombea urais.
NEC yenyewe (hata ya Chadema na vyama vingine) ukiangaza ndani yake unaweza kuona ni chombo chenye jina kubwa lakini kuna members ndani yake ambao are worse than you and me who are not in there. Pamoja na kuwa kweli katiba haisemi mgombea Urais awe mjumbe wa NEC, lakini huo ndio ukweli. Na kama ukiweza kurally support ndani ya NEC kwanza (kwa ulaghai au ukweli) unakuwa na nafasi nzuri kuteuliwa kuwa mgombea urais. Hiyo ni weakness kubwa sana ya real unwritten Constitution of CCM.
Naona kizuri ni kuimarisha miondo na taasisi iliziwe na nguvu zaidi ya kuwabana wanaogombea nafasi waweze kudeliver baada ya kuchaguliwa. sasa hakuna.
Nakubaliana na wewe. Hoja zako kuhusu utendaji wa kazi wa viongozi, sera, kauli mbiu n.k, zimeniacha na maswali kadhaa, kwa mfano, kwa mujibu wa katiba ya CCM, moja ya majukumu ya NEC ni: "Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi na kutoa msukumo wa utekelezaji wa Ilani hiyo". Je, nini ni Key Performance Indicators ya Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri? Ni utekelezaji wa ilani ya CCM? Au hizi indicators zipo ndani ya vikao vya baraza la mawaziri? Je, zina compliment au pingana na Ilani ya CCM? Na matakwa ya donors yanaingiaje katika mchakato wote huu? Do we have a standardised way of measuring performance ya executive branch - cabinet kwa mfano, au what we have ni kwamba, Aggrey Mwanri kwa mfano anapimwa kivyake, Magufuli kivyake, Pinda nae kivyake n.k, n.k? Nakumbuka miaka ya mwanzio ya 2000, Mkapa alitamka nadhani akiwa mkoani Pwani kwamba JK na Lowassa na sijui nani mwingine ndio mawaziri wake wachapa kazi, sijui alikuwa ana base on what indicators, wadau mnalionaje hili, any ideas juu ya uwepo wa hizi indicators ambazo umma hauna taarifa nazo?