Nadharia: Jinsi law of magnetics itakavyozuia ajali barabarani

Mkuu hii karne hakuna kilichoshindkana labda space explorations ndo kuna unsolved myseries.

Mfumo wa Collission Avoidance System unafanya kazi tatu.

1. kugundua uwezekano wa ajali kwa kutumia sensors; all weather radars, cameras na gps kwa kupima umbali, speed na uelekeo wa chombo na vitu vingine barabaran kama wapita njia, zuio la barabara, na vyombo vingine vya usafiri.

2. kutoa taarifa kwa dereva kuhusiana na hatari inayoweza kujitokeza.

3. Ni kuengage driver-overide ili kuzuia ajali ambapo hapa itahusika Automatic Emergency Braking.

Mimi ni critics mkubwa wa Ai lakini hii system ni moja ya sababu kwanin artificial intelligence ni life saver.

kwenye huo mfumo ni primary prevention kama chanjo swali vipi kama gari mojawapo lita feli break ghafla inauwezo wa kuzuia yasigongane? Mi nadhani huo mfumo ni mzuri ila unamapungufu labda walilenga njia zenye obstacle
 
Kwanza kwa Nini magari yanagongana,
Haya magari yanagongana upande wa mbele ,pembeni na kuanguakiana, kwa hiyo mda mwingine magari hayo yatàvutana hasa pale zinapokutana N S pole
 
Mkuu hii karne hakuna kilichoshindkana labda space explorations ndo kuna unsolved myseries.

Mfumo wa Collission Avoidance System unafanya kazi tatu.

1. kugundua uwezekano wa ajali kwa kutumia sensors; all weather radars, cameras na gps kwa kupima umbali, speed na uelekeo wa chombo na vitu vingine barabaran kama wapita njia, zuio la barabara, na vyombo vingine vya usafiri.

2. kutoa taarifa kwa dereva kuhusiana na hatari inayoweza kujitokeza.

3. Ni kuengage driver-overide ili kuzuia ajali ambapo hapa itahusika Automatic Emergency Braking.

Mimi ni critics mkubwa wa Ai lakini hii system ni moja ya sababu kwanin artificial intelligence ni life saver.
bado hujapata point yangu mkuu ni kwamba huo mfumo upo kama chanjo swali ni je ikitokea kati ya magari mawili moja wapo limefeli break ghafla ktk umbali mfupi huo mfumo unaweza kuzuia automatic gari moja lisi collide na lingine? Pia huoni hapo kuna hatari ya kudukuliwa?
 
Kwanza kwa Nini magari yanagongana,
Haya magari yanagongana upande wa mbele ,pembeni na kuanguakiana, kwa hiyo mda mwingine magari hayo yatàvutana hasa pale zinapokutana N S pole
vipi kama mbele na nyuma pakawekwa ncha zinazofanana? Vipi kama ubavuni mwa gari patakuwa coved na material ambazo hazivutwi na sumaku mfano kucover chuma na plastic, cotton boksi au mbao? Vipi sijajibu swali lako mkuu?
 
Mkuu hizo ni hitilafu za mifumo, and what man has made man can break..!

bado hujapata point yangu mkuu ni kwamba huo mfumo upo kama chanjo swali ni je ikitokea kati ya magari mawili moja wapo limefeli break ghafla ktk umbali mfupi huo mfumo unaweza kuzuia automatic gari moja lisi collide na lingine? Pia huoni hapo kuna hatari ya kudukuliwa?
 
1. Niungane na mdau wa posti namba 6 hii itaondoa gharama zisizohitajika .

2. Sitaki kuzama deep kwenye hesabu za umeme maana zitanipotezea muda anyways ila nikupe mfano mmoja ambao nadharia yako haitofanya kazi zaidi ya kuzidisha maafa .

Kwanza chukua mapulizo mawili halafu yajaze kwa hewa kisha yakutanishe kwa nguvu huku ukiayaachia yaani (free collision) kisha utakachokiona kinatokea ndicho jibu la nadharia yako .

Ukihitaji maelezo zaidi ninaweza kukuelezea kisayansi zaidi.
 
teh! Mkuu umemaanisha yataacha njia?
 
vipi kama mbele na nyuma pakawekwa ncha zinazofanana? Vipi kama ubavuni mwa gari patakuwa coved na material ambazo hazivutwi na sumaku mfano kucover chuma na plastic, cotton boksi au mbao? Vipi sijajibu swali lako mkuu?
Mbinu za kuzuia ajari ni kudhibiti mwendo Kasi, pili kuweka mfumo ambao gari lipatapo hitilafu yoyote lta piga break automatically hata kama linatelemka mlima, magari kuachiana nafasi Kati ya gari na gari, kutanua barabara, na kuepuka overtake zisizo na msingi. Kufuata Sheria za barabarani
 
Picha hapa chini inaonyesha semi trailer na V8 zikikutana uso kwa usoView attachment 2958136
Semi trailer kikawaida ina maximum speed ya 80 km/h na ina uzito wa 42345kg.
VX V8 ina maxmum speed ya 300Km/hr na ina uzito wa 3350kg

kitu chochote chenye uzito na speed kina FORCE kwa muujibu wa newton fitst law of motion

F = M × {(V2 - V1)/t}
F -FORCE
M-MASS
V2 -FINAL VELOCITY
V1-INITIAL VELOCITY

Gari namba moja lina force 1
Pia lina magnetic fotce 1
Gari la pili lina force 2
Pia lina magnetic force 2
Umerudia mara kdhaa ila nitakujibu post moja tu.

Wazo hilo ni interesting lakini siyo feasible kwa sababu lina unintended consequences nyingi zitokanazo na interactions za magnetic filds baina ya magari yote yatakayokuwa na sumaku zenye nguvu kiasi hicho. Yanaweza kuvutana na kugongana bila kupenda, na yanaweza kuskumana na kuangushana mitaloni pia bila kupenda. Halafu magari hayo hayatatakiwa kuwa karibu na binadamu yeyote aliyewahi kuwekewa vyuma mwilini au anayetumia pace maker. Too many unintendede consequences.

Hata hivyo colision avoidance technologies zipo ambazo zinatumia radar na ama lidar (ultrasonic ilijaribiwa ikashindwa) ingawa hazijasambaa sana kwenye magari ya kawaida. Technogies hizo zinafunga brake zenyewe kusimamisha gari lisigonge; kwa sasa zinapatikana kwenye magari ya pesa nyingi tu.
 
Ni wazo zuri.

Ila mimi napinga kwa sababu zifuatazo.

1. Ajali zitaongezeka kwa sababu, sumaku itakuwa inavutia gari la mbele na kulivuta nyuma kuja kugonga gari hilo lenye sumaku.

2. Ukisema hizo ncha mbili zipishane bc tambua kuwa lazima hayo magari yagonge vitu vya pembeni kama vile magari, biashara za watu au makazi ya watu kutokana na kasi ya kupishana kwa hizo sumaku.

3. Kwa ukubwa au kasi ya hizo sumaku itasababisha vitu vingine vya chuma kuvutwa kuja kwenye hilo gari lenye sumaku.

Ushauri wangu japokuwa najua kwa hapa bongo ni vigumu kufanyika.

1. Upana wa barabara uongezwe na kuwe na line maalum kwa kila gari, mfano line no. 1 iwe ni magari makubwa ya kwenye mikoani tuu, line no. 2 ni magari makubwa yenye mizigo/mafuta, line no. 3 magari binafsi, line no. 4 ya tahadhari.

2. Sheria kali za barabarani, mfano kuna hawa wapuuzi wa kuitwa Sauli na New Force ingekuwa ni uwezo wangu nngefunga biashara zao.

3. N.k
 
hufikirii gharama za ujenzi wa barabara za namna hiyo ni ghali sana nchi nyingi hazina huo uwezo
Binadamu kufikiria solution ya mambo ni jambo zuri. Lakini jinsi Internet ilivyokuwa advanced, ukiwa na wazo kama hili basi lifanyie kazi kwanza hata kwa kufanya research ndogo ili uone wazo lako kama lina make sense kwa mazingira au hali halisi. Vinginevyo unaonekana kituko kama yule aliyesema abiria wawe wanavaa helmet ili kuzuia kuumia kwenye ajali au yule jamaa wa Zenji na li-helkopta lake la mabati eti anaombea kibali cha kuruka. Hivi wewe unadhani pamoja na utaalam wooote dunia iliyofikia, wazo dogo kama hili limewashindwa watu kufikiria?
 
Ni wazo, lakini in practice itakuwa ngumu kwa sababu zifuatazo.

1. Nguvu ya sumaku ni mdogo, haitaweza kusimamisha gari ambalo liko kwenye mwendo mkali. Hakuna mbinu ya kutengeneza nguvu kubwa ya sumaku kiasi hicho huku bado gari likawa jepesi.
2. Sumaku ita interfere nutendaji kazi kazi wa components nyingine za gari ambazo pia zinatumia sumaku kama alternator na vifaa vingine vya umeme.
3. Ita interfere operations zingine za barabara.

Kimsingi it is not practical. Ndo maana sasa hivi watu wamekuja na njia ya sensor ambazo zina uwezo.wa.ku detect object mita kadhaa na kuifanya gari ipunguze mwendo. Hii iko kwenye magari ya umeme. Na magari yanayojiendesha yenyewe
 
Binadamu kufikiria solution ya mambo ni jambo zuri. Lakini jinsi Internet ilivyokuwa advanced, ukiwa na wazo kama hili basi lifanyie kazi kwanza hata kwa kufanya research ndogo ili uone wazo lako kama lina make sense kwa mazingira au hali halisi. Vinginevyo unaonekana kituko kama yule aliyesema abiria wawe wanavaa helmet ili kuzuia kuumia kwenye ajali au yule jamaa wa Zenji na li-helkopta lake la mabati eti anaombea kibali cha kuruka. Hivi wewe unadhani pamoja na utaalam wooote dunia iliyofikia, wazo dogo kama hili limewashindwa watu kufikiria?
hata JF ni mtandao unaotumia intarnet mkuu, wewe umekariri research mpaka utembee na makaratasi? hata hapa tunafanya research na wewe umechangia bila kujua AHSANTE
 
Daaah hii nzuri sana mkuu hapo nimekuelewa...
HIi litapunguza hizi anazo zungumzia jamaa hapo juu kweli kabisa
Ndiomana nikasema huko juu sio kwamba wataalamu hawakuwahi kufikiria ulichokisema mleta mada ila application yake no ngumu sana na obstacles ni nyingi kwahiyo solution ni kuwa na barabara zinazoruhusu magari kuelekea upande mmoja tu na si kupishana. Wenzetu Ulaya na America hili wameshalifanyia kazi kitambo tu.
 
Sio wameshindwa nadhani ni sisi ndio tumeshindwa kufikiria ipasavyo kwasababu ni swala la kitaalamu zaidi.

Hivi kwa kufikiri tu unadhani utahitaji sumaku ngapi katika gari ili uweze kuwa secured na ajali?

Vipi kwenye swala la parking na kuendesha chombo kwenye barabara yenye foleni?

Maana yake itahitajika kuwepo na gape kubwa kutoka kwenye gari moja hadi lingine.

So ili kuepuka collisions itabidi kutoka Vingunguti stendi mpaka Mfugale iwe ni distance ya kutosha magari matano tu.

Tungetoboa mpaka hapo?

Lakini fikiria tu power ya hiyo sumaku jinsi ambavyo ingekuwa.

Kwasababu kama Sumaku imefumwa kwa nguvu ya kuweza kufanya gari lenye uzito wa tani kuweza kusukumwa maana yake hiyo ni nguvu kubwa mno.

Hivyo maana yake kama ni gari inatoka Mbeya kuja Dar basi kila kipande cha chuma kilichokuwa njiani lazima kivutwe na sumaku.

Hapo unaweza kujikuta umetengeneza ajali nyingine kwasababu hiyo force ya hivyo vyuma jinsi vitavyovutwa itakuwa ni kubwa mno kiasi iweze ku damage gari lenyewe.
wazo linatekelezeka tgeoretically lakini ukija practically inakua ngumu kwa sababu kadhaa

moja,kwenye list ya forces magnetusm inaangukia kwenye fundamental forces ambazo ukitooa nuckear forces za ndani ya atommbili zinazobaki(weight na electromagnetism) ni weak sana ukilinganisha na force nyingine kama hii inayozungumziwa hapa(inayotokana na momentuma change rate)

mbili,ingewezekana kutumia electromagnet(sumaku za kuzalishwa na umeme) lakini changakoto yake ni kwamba kiasi cua usumaku kitakachozalishwa kitategemea na nguvu ya umeme unaotimika kuzalisha usumaku(hapa sasa unatakiwa kuwa na mtambo mkubwa sana wa kuzalisha umeme kwenye hayo magari mawili ili uwezo kupata force kubwa kiasi cha kuzidi force ya Newton kwenye magari

tati,ukisema sumaku zile mbili ncha zitazamane ndio gari zisigongane ukumbuke pia kuna magari mengine ambayo nayo yatakua yamefungwa hizo sumaku,lklakini pia kuna vifaa vya chuma na vitu vingine kibao ambavyo vinaaathiriwa na usumaku…pindi ambapo sumaku huzi kaoi zimewasha hivyo vutu vyote vitaathirika

kwahiyo inawezekana kabisa kuwaza lakini ngumu kutekeleza…unaweza tengeneza tu models za kujaribu elezea lakini ili ulete jwenye reality utahitaji mambo mengi sana kufanya wazo likamilike

lakini kwenye sayansi hakuna kunachofeli kama hakuhusishi roho na uhaki,tujipe muda
 
Wakuu habari!

Leo nikiwa barabarani niliona magari mawili yaliyotaka kugongana uso kwa uso ghafla likanijia wazo ambalo limenisukuma kuandika uzi huu namna ya kuzuia ajali kama hizi.

View attachment 2958107
Picha nmetoa mtandaoni

Kikawaida ncha mbili za sumaku zikikutana hukwepana, mfano angalia hapa chini kwenye pichaView attachment 2958106
Sasa ikiwa magari yote yatatengenezwa kwa sumaku kwa mbele ktk mtindo wa ncha mbili zinazofanana yakikutana uso kwa uso yatakwepana (yatasukumana bila kugongana) yaani kama ule mchezo wa kusukumana lakini hapa itakua bila kugusana,

Chukulia mfano semi trailer inakutana uso kwa uso na V8, ili zisigongane zikwepane itahitajika sumaku kubwa sana iwekwe mbele ya gari mfano sumaku yenye ukubwa wa shina la mbuyu kwa kila gari yaani semi na V8, kitu ambacho kitaathiri uzito wa kila gari na balance haitakuwdpo,

Kwa vile chuma laini kikizungushiwa nyaya kwa mtindo wa coil kisha kuunganishwa na umeme huwa kinakua sumaku hii njia itafaa zaidi kutengeneza sumaku yenye nguvu kubwaView attachment 2958127
Zingatia pia ujio wa magari ya umeme.

Chini ntatoa ufafanuzi wa kimahesabu , Nakaribisha maoni kinzani.
Wazo zuri sana, ila itafutwe namba ya kutovuta metalic materials zote zilizopo barabarani. AU unaweza kuta zile kingo za chuma barabarani zinasababisha gari isimame hapo kwa hiyo magnetic force.

AU utani tu, utakuta vijiko vyote vya nyumba zilizopo barabarani vinakusanywa na gari
 
kwa sababu hoja ni kuzuia ajali basi wataalamu wanaangalia solution rahisi kwa vigezo vingi…kwa hili la ajali solution ni miundombinu rafiki ya barabara,kufuata sheria (hakutumii hata mia), kutumia vyombo vya usafiri salama ,kuwa na watu wasio na msongo wa mawazo(uchumi)

zipo nchi ambazo ajali ni almost hakuna
 
Imeshaonekana;

1. Kufuata sheria zabarabarani ni mtihani kwa wengi na hata kwa wasimamizi wa sheria hizo.

2. Kufanya matengenezo ya magari pamoja na wakaguzi wake ni shida.

3. Kuzuia msongo wa mawazo si rahisi kama unavyoisema.

4. Miundo mbinu rafiki nao ni mtihani.

Hayo yote hapo juu yanasababisha wataalamu wafikirie njia nyingine ya kuzuia ajali, ikiwemo hii ya sumaku.

BTW, HAKUNA SOLUTION YENYE GHARAMA KUBWA INAYOZIDI GHARAMA YA KUPOTEZA UHAI
 
Wakuu habari!

Leo nikiwa barabarani niliona magari mawili yaliyotaka kugongana uso kwa uso ghafla likanijia wazo ambalo limenisukuma kuandika uzi huu namna ya kuzuia ajali kama hizi.

View attachment 2958107
Picha nmetoa mtandaoni

Kikawaida ncha mbili za sumaku zikikutana hukwepana, mfano angalia hapa chini kwenye pichaView attachment 2958106
Sasa ikiwa magari yote yatatengenezwa kwa sumaku kwa mbele ktk mtindo wa ncha mbili zinazofanana yakikutana uso kwa uso yatakwepana (yatasukumana bila kugongana) yaani kama ule mchezo wa kusukumana lakini hapa itakua bila kugusana,

Chukulia mfano semi trailer inakutana uso kwa uso na V8, ili zisigongane zikwepane itahitajika sumaku kubwa sana iwekwe mbele ya gari mfano sumaku yenye ukubwa wa shina la mbuyu kwa kila gari yaani semi na V8, kitu ambacho kitaathiri uzito wa kila gari na balance haitakuwdpo,

Kwa vile chuma laini kikizungushiwa nyaya kwa mtindo wa coil kisha kuunganishwa na umeme huwa kinakua sumaku hii njia itafaa zaidi kutengeneza sumaku yenye nguvu kubwaView attachment 2958127
Zingatia pia ujio wa magari ya umeme.

Chini ntatoa ufafanuzi wa kimahesabu , Nakaribisha maoni kinzani.
Wazo lako sio la kipuuzi mkuu Tena zifungwe ubavuni mbele na nyuma kiukweli ita saidia Sana iki boreshwa
 
Scars sumaku itakayotumika ni ya umeme (solenoid) badala ya bar magnet, kuhusu umbali wa gali moja hadi jingine ktk foleni ni simple kusolve unacheza na magnitude za magnetic force zifanye kazi kwa umbali uliowekwa sasa hivi gari moja linalolifuata lingine kwa nyuma linatakiwa kuacha space ya metre ngapi? Hapo kwenye kuvuta vyuma vilivyo barabarani ndo penye changamoto lakini kuhusu parking ukizima mfumo wa umeme kwa muda ile hali ya u sumaku inatoweka sijui unafahamu hiki kitu?
Nguvu ya Solenoid magnetic hutegemea na kiwango cha umeme kinachozalishwa na gari husika.

Na hiyo sumaku inabidi ifungwe katika pande zote nne za gari.

Kwa maana hiyo italazimika gari zote ziwe na umeme sawa ya ku power hiyo sumaku na kwasababu hiyo ni sumaku yenye nguvu sana basi tutegemee uharibifu wa vitu vingi kama card za ATM.

Sio tu hivyo bali hata pikipiki na baiskeli nazo zitahitaji kuwa na sumaku hiyo vinginevyo zikikaribiana na hayo magari zitavutwa na kusababisha ajali nyingine.

Sasa pikipiki ina uwezo wa kufua umeme wa kutosha ku power hiyo sumaku au pikipiki zipigwe marufuku barabarani?

Umesema kwenye parking gari ikiwa off sumaku inakuwa inactive, sasa assume gari ya kwanza imepaki tayari ipo off halafu ya pili nayo inakuja kupaki, nini kitatokea?

Kwasababu gari ya kwanza sumaku yake haipo active maana yake itavutwa na hili gari la pili ambalo sumaku yake ipo active kwasababu gari lipo on linatafuta upenyo wa kupaki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom