Ajali za barabarani na msimu wa mavuno kwa wakulima!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,053
24,446
Wakulima hivi sasa wanachekelea tu, wanavuna kwani mvua zilikuwa za kutosha tu!

Waliopanda mahindi, alizeti, mpunga, pamba, maharage n.k hawana cha kujutia. Mavuno haya bila shaka yataendelea hadi mwezi wa tisa ndipo mashamba yataanza tena kuandaliwa na kupanda na ifikapo mwezi wa tatu hadi wa tano wengine wataanza kuvuna.

Kufuatia mavuno hayo, tukiangalia na kufuatilia kwa makini msimu huu ajali za barabarani hasa zinazohusisha magari makubwa ya biashara mfano mabasi na malori hutokea sana.

Kuanzia mwezi wa saba hadi wa tisa ni kipindi ambacho ajali nyingi zinahusisha magari makubwa kupinduka, kugongana ama kuwaka moto na hili hutokea tena kuanzia mwezi wa tatu hadi wa tano.

Miezi mingine si kwamba ajali hazitokei zinatokea lakini ni chache mno na huwa si za mara kwa mara.

Kuanzia mwezi July hadi September na March hadi May, ajali za mabasi yanayomilikiwa na makampuni makubwa hutokea sana, malori huwaka moto n.k! Mfano kwa mwezi huu July zimesharipotiwa ajali zaidi ya sita za mabasi makubwa.

Serikali kipindi hiki na nyakati nyingine hukemea sana madereva wasiofuata sheria, ila ajali yaweza tokea leo na kamanda wa traffic mkoa ajali ilipotokea anaweza kukemea sana, lakini inaweza isipitie siku ajali nyingine inatokea ndani ya eneo lake na wala sababu isiwe ya mwendokasi ama hitilafu ya gari!

By the way, nisiandike sana, wakulima wanaovuna wakumbuke kuweka akiba jamani.
 

Hizo hoja nimezipitia, ila mkuu nikuulize.., inakuwaje miezi ya January, February, October, Nov na December uzembe unakuwa si wa kiwango kikubwa maana hiyo miezi unaweza usisikie ajali ndani ya mwezi mzima ama zikatokea chache sana nyakati hizo, ila miezi tajwa kwenye uzi ajali zinatokea mfululizo.., ina maana miezi hiyo uzembe huongezeka kwa sababu zipi?
 
Ukweli usiopingika!
Kweli kuna miezi ajali zinafululizana balaa, hadi unajiuliza kunani...!
 
Back
Top Bottom