Salaam, Shalom!!!
Nilikuwa nimelala chumbani, ghafula, macho yangu ya Roho yalifunguka,
Mara nisikia sauti kuu ya tarumbeta/ baragumu juu angani, kuwapo chumbani hakukunizuia kuona yaliyokuwa yakiendelea angani,
Mara alipita farasi mweupe sanaa, kung'aa kwake farasi yule kulinishangaza, na kilichonipa kushangaa zaidi ni farasi yule alikuwa akipita Kwa Kasi akikanyaga MAWINGU,
Nilipozidi kuangalia, nilimwona aliyekuwa amekaa juu ya farasi, alikuwa mwenye mavazi meupe sana yenye kung'aa sana,
Alipokuwa akipita mbele ya macho yangu, niliona nyuma yake amefuatana na kundi kubwa la watu wenye mavazi meupe wengi sana Kila Mmoja akiwa amepanda farasi mweupe wakipita Kwa Kasi wakimfuata yule aliyepita mwanzo.
Nilipokuwa nikiendelea kuhamaki, yule mpanda farasi aliyekuwa mbele akiongoza safari, aligeuka na kunitizama, nilitamani nami niungane naye katika safari, alinitizama, akatabasamu, Kisha akaendelea mbele,
Nilistuka Kutoka katika maono Yale nikiwa na wasiwasi sana na niliamini tukio lile lilikuwa Kweli na Mimi nimeachwa,
Baada ya muda Fulani kupita, nilipata kujua kuwa, BWANA YESU alipita kunikumbusha kukaa tayari muda wote, Ili ajapo, asijenikuta sijajiandaa. Nilichoonyeshwa live, ndicho kilichoandikwa katika (Ufunuo 19:11).
Na Kwakuwa, ujumbe Ule haikuwa wangu pekeangu, nachukua fursa hii kukukumbusha mwana wa Mungu kusafisha vazi lako Kila wakati maana hatujui siku Wala saa atakayorudi Yesu kutuchukua.
Na ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala ifuatayo,
EE YESU, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI, NIWEZESHE NIISHI MAISHA MATAKATIFU.
Mungu awabariki, Amen