Na hii ni siasa au ni Kushindwa kuwajibika?

Dereck Tito

Senior Member
Feb 8, 2011
102
15
Kwa nini watu tuishio kusini, mikoa ya Lindi na Mtwara serikali haitujali?

Ni kuhusiana na kipande cha barabara kuanzia mbele kidogo ya daraja refu Tanzania maarufu kama daraja la Mkapa kupitia Malendego na Muhoro hadi Somanga. Ni kipande cha km 54 tu. Kipande hiki kimekuwa kero mno kwa sisi wa kusini; Serikali/Magufuli/wakuu wa mikoa, Wilaya wanalijua, wabunge wa maeneo haya, waandishi wa habari; mashirika yasiyo ya kiserikali na hata yale ya serikali wanajua. Kuna, nini hapa au wote wamehongwa?

Inashangaza sana kwa sababu yupo mkandarasi anayefanya shughuli ya ujenzi wa barabara hii lakini amekuwa kwenye utendaji wa taratibu sana na hakuna yeyote kati ya hawa watajwa ambaye anahoji, pamoja na kelele zote za wananchi; sasa tunauliza kuna nini? Au serikali imechakachua fedha za ujenzi wa barabara hii? Manake tumezoea kusikia "mtu mmoja tu anakula fedha za kuweza kujenga barabara kutoka DAR hadi ZAMBIA!!"

Tetesi ni kuwa mkandarasi aliyepo alianza ujenzi wa barabara hii kwa fedha zake mwenyewe kwa makubaliano kuwa serikali ingemrudishia na kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo. Cha ajabu ni kuwa pamoja na jitihada ambazo zimeonyeshwa na mkandarasi huyu za kutengeneza madaraja na culverts zote na hivyo kubakiza usawazishaji, side drains, kokoto na hatimaye lami, hajalipwa fedha. Kwa nini serikali hamtaki kumlipa mtu huyu atutengenezee barabara nzuri nasi watu wa kusini tusafiri kwa raha kwa kutumia magari mazuri ya viwango kama sehemu zingine za nchi hii? Halafu hata sehemu zingine za barabara hii iendayo mtwara, pamoja na kuwa ilishajengwa siku chache zilizopita, mbona bado ipo chini ya kiwango? Maeneo mengi tu yameharibika!! Mbona mnatula sana sisi watu wa kusini?

Hivi sisi tumemkosea nini Mungu? Mbona ninyi viongozi hamtaki kuleta maendeleo kusini au hii si Tanzania? Tuanze mikakati ya kuanza kujitenga, yaani kuanzisha nchi yetu? Mh. Magufuli umekuwa mstari wa mbele sana katika kushughulikia masuala kama haya na pia ukizingatia kuwa wewe ndiwe waziri mhusika; kwanini husemi chochote kuhusu barabara hii?

Hivi kweli barabara ya urefu mdogo kama huu unaifanya serikali kushindwa kujenga uaminifu japo mdogo kwa wananchi wake ambao ndio wanaowaweka madarakani? Hivi kama CCM itashindwa kutekeleza hili kwa sasa wanategemea sisi wananchi wa kusini tuendelee kuwapa tena ridhaa na nafasi ya kutuongoza kweli? Kwa nini tusiwape wa vyama vingine nao tukawajaribu kama CDM tuwaone??

Mh. Nnauye, hivi ulikuwa ukipita kwenye barabara hii au ulikuwa ukipita tu juu kwa juu ulipokuwa unaenda kwenye ukubwa wako huko masasi? Unasema mmejivua gamba, mbona sisi tunaona kama gamba ni lilelile tu?

Sasa kamammetuchoka watu wa kusini, basi endeleeni na ubaya mnaotufanyia, ila kweli nasi tupo mbioni kuwachoka na mtajutia nafasi zenu hizi.

MAWAZO YANGU!!!!
MLIPENI KANDARASI FEDHA ZAKE AMALIZIE BARABARA NASI TUIFURAHIE NCHI YETU TANZANIA!! HATUITAJI KUSAFIRIA MAGARI YALIYOOOOOZA TENA AMBAYO YANAHATARISHA MAISHA YETU.

Siku moja tutamtaka mke wa kigogo mmojawapo ambaye atakuwa mjamzito, apande moja ya mabasi yetu mfano 'WIFI NAYE' kwenye seat za mabalozi/nyuma uone kama hajajifungulia njiani au hata kufa!! Sisi ndivyo tunavyosafiri na wake zetu na watoto na wakwenu na Mashangingi, mnajisahau kuwa hayo tumewapa sisi! ANGALIENI MWISHO UNAKUJA!!!! ILA MKIJIREKEBISHA KWA KUVUA GAMBA LA UFISI NA KUTUJALI, MTATAWALA HADI MESIYA ATAKAPORUDI, MTAKULA MEMA YA NCHI!!!!

Watu wanalala njiani kwa ajili ya kipande hiki! Mara nyingine watu wanaugua na siku wakifikishwa hospitalini wanafariki, Serikali mnashindwa nini? Mnataka kuwaongoza watu wa namna gani?
 
Back
Top Bottom