Mzungu avua nguo airport Dar

Akashtaki kokote!
Kwani alilazimishwa kuvua nguo zote au alitaka mwenyewe kuvua? Mbona inapotokea kuwa mashine imetoka mlio unapopita wanakukagua bila kukutoa nguo zako! Mimi nashangaa hawa wazungu. Wakiwa kwetu wanataka wasipitie taratibu.Kitendo cha yeye " kuvua nguo zote" nakitafsiri kama dharau.Huko kwao tukienda mbona tunasumbuliwa hivyo hivyo tena kibaya zaidi wanaweza kuacha kila mtu wakakuchukua wewe mtu mweusi na kusema computer imeku pick randomly for thorough search..huwa hatupendi lakini kwa vile ni sheria za usalama basi huwa tunakubali.Tena wakati mwingine wanakulazimisha utoe viatu wavifanyie swabbing..vyote tunapambana navyo na hatujawahi kutishia kwenda kushtaki kokote.Hizi taratibu za ukaguzi ni za kimataifa..akashtaki popote!

hapo kwenye bold dada pamenigusa sana, niliwahi kulazimika kuacha mfuko mzima uliokuwa na vipodozi vyangu airport ya beijing kwa sababu ya usumbufu kama huu. zimebaki dk kumi mlango wa ndege ufungwe eti wanasema bado wanaususpect ule mfuko, tena walinichagua mie peke yangu (sijui kwa kuwa nilikuwa mweusi?) mfuko wenyewe ulikuwa simple sana wala haukuwa mkoba. mie niliwaachia wasachi hadi wachoke na mie nikapanda ndege na kuondoka. kweli wanaboa sana, basi tu tunalazimika kuvumilia
 
Hii mitambo imeanza kwao na imeletwa na wao kwa kuhofia akina OSAMA na Mulla. Kwa hiyo asijifanye hapa pambafu kabisa.

Ukienda US unapigwa X-ray na kana kwamba haitoshi waweza kukufanyia ukaguzi wa ziada maadam ngozi yako ni black
 
Dah,tatizo ni mashine zetu hapo airport.ni kweli zina shida.
mi kuna siku nilikuta hazifanyi kabisaaaa hivyo ikabidi wanikague kwa kunipapasa mwili.
kimashine cha mkononi kilikua kimoja na foleni ipo kubwa domestic na int.mwenye haraka ya kupita ulikua unapapaswa kama hutaki subiri hicho kimashine cha mkono kikufikie.
 
Back
Top Bottom