Mzungu ataka uraia wa Tanzania, agoma kurudi kwao

Hakuna binadamu anaependa Vita wala kubebeshwa silaha, huyu kijana toka Uingereza ameamua kuukana Uraia wake na kumuomba Rais Samia ampatie Uraia wa Tanzania.

ANGALIA VIDEO HAPA
View attachment 2890507

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
Yule mwenyekiti wa CCM huko Mwanza alipokuwa anapigia chapuo DP WORLD alisema wanatak kuchanganya rangi, ni muda muafaka kwa huyu sasa kuchukuliwa na wasukuma akawape mbegu nyeupe.
 
H

uko uingereza alihamia tu, si mwingereza wa asili.
Huyu aliwahi kuhojiwa na mtandao fulani huko YouTube akadai kuwa mama yake ni mzungu wa Uingereza na baba yake ni mwarab wa Misri aliehamia Uingereza miaka mingi iliyopita.

Aliwahi kuishi Malawi na baadae kuhamia Tanzania.

Alisema anatamani kupata mtoto mzuri wa kiswahili alietulia ili akamtolee posa amuowe.
 
Huyu aliwahi kuhojiwa na mtandao fulani huko YouTube akadai kuwa mama yake ni mzungu wa Uingereza na baba yake ni mwarab wa Misri aliehamia Uingereza miaka mingi iliyopita.

Aliwahi kuishi Malawi na baadae kuhamia Tanzania.

Alisema anatamani kupata mtoto mzuri wa kiswahili alietulia ili akamtolee posa amuowe.
Mkuu, Anaishi nchini kama mwekezaji au mtalii?
 
Mkuu, Anaishi nchini kama mwekezaji au mtalii?
Alidai alikuja Afrika kupambania haki za watoto kama vile ukeketaji, watoto wa kike kufungishwa ndoa wakiwa wadogo, uteswaji wa watoto nk.

Kwanza harakati zake alianzia Malawi, ila alikoswa koswa kuuwawa, baada ya kuingilia mission ya zee moja la miaka zaidi ya 70 huko Malawi kutaka kuowa kabinti kabichi ka miaka 15. Nasikia zee lilikuwa na mpunga, hivyo lilikuwa linailisha na kuihudumia familia ya hako kabinti.

Lakini sasa kabinti pamoja na kaka yake hawakupendezewa na swala hilo, ndo walipopata taarifa ya huyo mzungu kupitia watu fulan ikabidi wamfuate ili awasaidie. Kweli jamaa alijitahidi kumsaidia huyo binti hadi kupelekea mmoja wa wapambe wake apigwe panga la mkono, ila yeye mzungu, binti na kaka wa binti wakafanikiwa kuingia katika gari alilokuwa anatembeza mzungu na kutokomea bila kujeruhiwa.

Lakini kwa vile zee ni lizawa na lina pesa za kuwahonga vijana pamoja na askari wa eneo anapofanyia mishe zake ili wampoteze kiaina, basi jamaa akapata tumbo joto na kuamua kuvuka boda kukimbilia nchi jirani ambayo ndio Tanzania.

Story ni ndefu alikuwa anahojiwa ipo youtube.
 
hao wengi wanafanya hivyo kutafuta umaarufu, wala sio uraia. usifanye mchezo na uraia wa Uingereza, unaupotezaje uraia wa uingereza kwa mfano? passport ambayo unapita kirahisi tu nchi kibao, unaheshimiwa kwenye airports huko, na ukinyanyaswa tu ubalozi wao huo hapo unakutetea popote duniani? ati uamue kuje Tanzania ambako kijana kwa mfano anauawa kule gaza tena sisi wenyewe ndio tulimpeleka, lakini hadi raias kanyamaza kimya? nchi yenye mabalozi wasiosaidia raia wao.
 
Back
Top Bottom