Mzimu Nyangeta uliopo katika mji mdogo wenye mambo ya kishirikina na utajiri wa kishirikina uitwao Lamadi

Robidinyo

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
3,797
7,947
Nimefika pembeni kidogo ya haka kamji ka kibiashara nimekutana stori za kuogofya kuhusu ushirikina. Ni Mwezi uliopita kamanda Kova alidhuru kwenye haka kamji

Kulikua na wimbi la watoto wa kike na akina mama kuuwa na viungo vyao kukatwa, kisha kuvipeleka kwa Waganga ili kujipatia utajiri

Basi Bwana Kova alikuja akatandika mkwara wa kutosha baada ya siku mbili akatinga Mkuu wa Mkoa. Kesho yake zikaingia defender mbili zikaanza kuzoa Waganga wa kienyeji waliopo ndani na nje ya haka kamji

Kuna kijana ni tajiri sana hapo Lamadi nae akazolewa, ndo stori zikaanza kuzagaa kwamba yule kijana ana msukule wa kuitwa Nyangeta Zoa Mapesa

Wanasema uyo Nyangeta ni kama chuma ulete akija dukani kwako akinunua kitu ukimrudishia chenchi ndo pesa zako au mauzo yako yanatoweka, ukimstukia ukitoka nje humkuti

Wanaendelea kusema huyo Nyangeta anakodishwa unakuja umkodi akakufanyie kazi, kwa Mfano unakuja kumkodi unaenda nae Mbeya unakodi chumba yeye kazi yake ni kuzunguka kwenye biashara za watu anakukusanyia pesa

Wanasema babake Nyangeta ni tajiri hatari na huyo kijana alimnunua toka kwa huyo babake Nyangeta. Wadau wanasema Nyangeta aliwaikufa Baadae akaja kuonekana

Wanasema huko Polisi, dogo alipewa kichapo akakiri kuwa na huo msukule na anapesa nyingi sana ndani ila hazionekani. Anasema yeye hamtumi Nyangeta hapo Lamadi kwa sababu hakuna pesa, anamtuma mikoani yenye Pesa

Muwe wavumilivu kwa uandishi na mtiririko wa story, najua JF ina Member kila sehemu wale wa Lamadi hebu shukeni hapa na hiyo stori ya Nyangeta na huo Ushirikina wa Lamadi
 
Hakuna cha Nyangeta wala nini,Imani za hovyo hovyo tu.

Kata Panga wapumbavu hao kama utaona huu ujinga ujinga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom