Mzee Wassira: Ujenzi wa Hospitali ya kumbukumbu ya Mwl. Nyerere sifa wapewe wananchi wa Mara na siyo Serikali

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,827
21,425
Mzee Wassira ni mmoja kati ya wazee ambao huwa haonyeshi kucheka cheka pale anapoongelea jambo, mfano aliongelea jambo urais ambao wengi wanaonyesha nia wkt huu na kusema muda wao bado na hata yeye aliwahi kuutaka ila kwa sababu ya muda basi muda wake umepita na hawezi tena.

Mimi ni mmoja kati ya wananchi tuliokuwa tunafaham kwa kinaga ubaga kuwa majengo ya hospitali ya kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ilikuwa ikijengwa kwa nguvu ya serikali ya awamu ya kwanza.

Kwa taarifa za mzee wetu asiyepepesa macho wala kucheka kaweka wazi kuwa wananchi wa mkoa wa Mara wakishirikiana na wanachama wa iliyokuwa Tanu kipindi cha Mwl. Nyerere ndiyo wakichangishana kujenga hiyo hospital.

So amesema sifa isipewe serikali bali wananchi wa mkoa wa Mara na kama ilishindwa kuendelea basi lawama ziende kwa wananchi na kama bi sifa basi wapewe wananchi wa mkoa wa Mara.
 
Back
Top Bottom