Mzee wa Upako Apata Ajali na Kutokomea

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Hii nimeipata asubuhi hii. Mchungaji Antony Lusekelo, Mzee wa Upako' amepata ajali kwa kumgonga mwendesha pikipiki na yeye kulitelekeza gari lake eneo la tukio kwa kutoka mbio na kutokomea kusiko julikana.
Kwa mujibu wa shuhuda, ajali hiyo imetokea asubuhi hii eneo la River Side Ubungo.
Mwenye taarifa zaidi atuhabarishe.
 
haya sasa, huyo ndy mzee wa upako, tena msamalia aliyejaa roho mtakakitu
 
ajali haina mzee wa upako wala sijui nani ...kwani huyo jamaa amekata roho mpaka huyu mzee atimue mbio|?
 
Watumishi wa MUNGU waliosafi hawapaswi kufanya hivyo! Namuombea aliyegongwa apate kupona mapema na kufarijika
 
Mtu wa upako alitakiwa atoe huduma ya kwanza ikiwa ni pamoja na kumpeleka hospitali majeruhi badala ya kukimbia
 
Ohh,pole..
Yaani aksofu mkuu anajiendesha mwenyewe....nachojua cheo km hicho ni mtu mkubwab mwenye mambo mengi hapaswi kujiendesha mweneyewe.......au yeye sio sawa na pengo...
 
Kugonga ni bahati mbaya... ila hilo la kutokomea ni tatizo sana hasa kwa wenye imani!!! Nilidhani atamshika mkono na kunyanyua huyo aliyegongwa na kumpeleka kwenye matibabu

Kama ni keli amekimbia, basi kale ka imani kwamba ni mmoja wa manabii a uongo kamepata maksi 100%
 
hivikwenye biblia msamaria mwema alifanyaje vile japo si yeye aliyekuwa responsible?
 
Kama alitelekeza "HUMMER" yake lazima itakuwa scrapper sasa maana wajasiriamali na wazee wa vyuma chakavu sidhani kama walimwachia kitu.
 
Jamani, judge-not!

Hamuwezi kujua kuwa yeye mwenyewe amepata madhara gani!

Kwani madereva wote wanaokimbia baada ya ajali huwa ni makusudi?

wengine ni kuchanganyikiwa, kitu ambacho nahisi yeye pia kimemkumba...usiombe kuona damu ya binadamu inachuruzika ndugu yangu..Ni kimbembe ati.

Mi sitamhukumu hadi nilipate tukio full la kiuchunguzi...

Ahsanteni.
 
Usalama kwanza...
Mengine baadae


Kweli ndugu yangu. Nafsi haina cha mchungaji, askofu wala mtume. Kwaza unatii nguvu za adrenalini na akili inakuja baadaye. Kama amegonga kweli basi atatakiwa ajiripotishe kwa polisi na baadaye kwenda kumwona mtu aliyemjeruhi. Hakuna formula ya ku-deal na emergency. Ni kazi ya adrenalini tu. Hapo hakuna common sense wala roho mtakatifu.
 
jamni kwanini akimbie yy si mzee wa upako angemuombea fasta fasta kwa upako sasa anakimbia au alisahau upako om alitaka kwenda kuchukua afanye mambo
 
Back
Top Bottom