Mzee Sitta tunaomba ushauri wako kuhusu malipo ya dowans

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,030
2,553
Kutokana na hukumu iliyotolewa hivi karibuni kuhusu malipo ya Dowans, ingekuwa ni muda muafaka kwa Mzee Samwel Sitta na Dr Mwakiembe kutueleza msimamo wao kwani tangia mwanzo walikwishawaeleza watanzania kuwa malipo ya Dowans sio halali kabisa.
 
Since both Sitta and Mwakyembe are both lawyers,let us hear their interpretation of this latest Dowan's judgement.
 
Huyo Sitta na Maembe ni nani kama hukumu imeshatolewa? ni kupoteza muda na kutaka longo longo tu. Cha msingi wahusika waliotufikisha hapo ndio wanatakiwa kutiwa kitanzi. Hata kama siyo leo lakini huko tuendako lazima ipo siku atakuja mkuru 'mwendawazimu'. It is just the matter of time. Kama watu walilazimika kujiuzuru nyadhifa zao kwa kashfa ya Richmond iliyozaa Dowans, iweje watu hao waendelee kula bata mitaani huku sisi tukikibebeshwa mzigo wa kulipa tozo hili la mabilioni? Je, pesa hizo hizo si watakazotumia kununua uongozi ili wafikie malengo yao ya kuimaliza kabisa raslimali za nchi hii?. Eti leo baadhi yao wanajifanya wema na kutoa misaada makanisani. Pesa hizo hazitokani na kodi zetu? Tutakuja kushtuka kuvuta blanketi wakati kumeshakucha.
 
Hawataongea kitu wote wanafiki tu kama kweli wanapingana na hilo wasingeendelea kuwepo CCM hadi leo, wamepewa uwaziri ili wanyamaze na hata wakiongea,jaribu kuangalia kauli zao na msisitizo wao utakuwa tofauti na awali sasa hivi wameshanyamazishwa!sitoshangaa wakikaa kimya kabisa
 
Shame on them. Sio wao waliokataa sheria kurekebishwa ili kuinununa mitambo hiyo - ambayo sasa ni SIMBION miezi mitatu kabla ya mkataba kuisha? Siku 90 ni nini kwa umri wa serikali????. Laiti tungeskiza ushauri wa ZITTO ZUBERI KABWE tusingefika hapa tulipo. Wanasheria wa nchi hii akina sitta ni wachumia tumbo na watu wa majungu tu.

Pia ni aibu kwa wana jamii forum waliokuwa mstari wa mbele kumpinga ZITTO aliposema nchi inaweza kufilisiwa wasipolipwa jamaa. Tukambeza sana eti ana %ge kapewa. UFINYU wa kufikiri. YAMETUTOKEA PUANI SASA. kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi!!!!!!!!!
 
A strongman stands alone. Hizi nyazifa walizopatiwa six and little mango ni rushwa ili weak gvt izidi kujitanua ktkt kuiba resources. I hate them coz they have showed their weakness before the society.
 
siku zote huwa nashangaa sna kwa hawa jamaa wanaotuambia wapambanaji wa ufisadi hivi najiuliza ni ufisadi gani waliowahi kupambana na wakawaonesha wananchi kwamba wamepambana? hata japo kwamba wameshidwa zaidi ya kutuletea porojo za kisiasi na chuki za kimakundi hakika kwa hili sitakaa nimsahau mhe.kabwe zuberi kwa ushauri wake wa kizalendo kwa taifa letu ingawa alipigwa majungu ya kila aina nilitakiwa niseme bravo mhe.kabwe lakini kwa kuwa taifa limeshindwa na wafedhuli wachache wamefanikiwa nasema mhe.kabwe pole sna lakini usikate tamaa siku moja haki itasimama na wazalendo wakweli haswa watasikilizwa na sio waleta majungo na porojo za kisiasa kwa maslahi yao wenyewe.
 
Hawana lolote hao wanasiasa uchwara,wachumia tumbo na wanafiki kupita maelezo!
 
Ukiona manyoya ujue keshaliwa huyo ohooo hakuna cha Sita wala Mwakyembe wote kimya kama hujui hii ndo Tanzania utapiga makelele mpaka mapovu yakutoke lakini mpango upo pale pale
 
sasa mimi nashangaa, why did Lowas resign? maana inaonekana hakuna kinachoeleweka hapo, ubabaishaji tu

Huyo Sitta na Maembe ni nani kama hukumu imeshatolewa? ni kupoteza muda na kutaka longo longo tu. Cha msingi wahusika waliotufikisha hapo ndio wanatakiwa kutiwa kitanzi. Hata kama siyo leo lakini huko tuendako lazima ipo siku atakuja mkuru 'mwendawazimu'. It is just the matter of time. Kama watu walilazimika kujiuzuru nyadhifa zao kwa kashfa ya Richmond iliyozaa Dowans, iweje watu hao waendelee kula bata mitaani huku sisi tukikibebeshwa mzigo wa kulipa tozo hili la mabilioni? Je, pesa hizo hizo si watakazotumia kununua uongozi ili wafikie malengo yao ya kuimaliza kabisa raslimali za nchi hii?. Eti leo baadhi yao wanajifanya wema na kutoa misaada makanisani. Pesa hizo hazitokani na kodi zetu? Tutakuja kushtuka kuvuta blanketi wakati kumeshakucha.
 
Hawana lolote...wanafiki wakubwa hawa walio changia matatizo makubwa ya nchi yetu kwa unafiki na uendawazimu wao.
 
Watanzania wengi tunaongozwa na matumbo zaidi kuliko akili. Au tunafikiri kwa kutumia alichokisema Dk. Masaburi. Utakuta hoja ya mtu inaweza kuwa na mantiki ya kuokoa Taifa lakini kwa sababu anaitikadi fulani ya chama anapuuzwa na kukejeliwa. Sasa gharama za kuilipa Dowans zinatoka wapi kama si katika kodi zetu bila kujali huyu ni wa chama fulani cha siasa? Kingine ni kwamba; hata kwa wasomi wetu tulionao hawaisaidii nchi kwa kutumia taaluma zao. Wote wamejiingiza kwenye siasa uchwara za wazi au za chini chini na kujikuta wakishangilia kila ujinga unaotolewa na aina fulani ya watu. Wanatenda na kufikiri sawa na watu hao bila kujali kama wana najisi taaluma zao, kusariti vizazi vijavyo. Tujikumbushe Dowans imetoka wapi. Richmond ile kampuni iliyopewa mkataba kishikaji ndiyo chanzo kikuu. Hivyo Lowahasaaa+ Rosti tamu= bilioni 96
 
TAIFA LETU TULIPENDALO SAAANA LA TANZANIA HIVI SASA LIKO NJIANI KUANGAMIA SHAURI YA KUKOSA UONGOZI SIKIVU, ADILIFU NA WENYE HEKIMA

"Taifaa la Tanzania linaumwa tena linaugua ugonjwa wa hatari sana tangu uchaguzi wa Oktoba 2010, kufanyike juhudi za haraka kulitibu taifaa," alisikika miezi michahe akitoa hii kauli yenye hekima tele yule Mhe Mbuye wa Arusha alie likizoni Godless Lema.

Hata hivyo, ni wangapi ndani ya nchi hii walau waliweza kumuazima sikio na kutafakari ki-undani zaidi hii kauli???????????

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na maswahiba wake wanaoendelea kufilisi nchi hii kupitia Dowans, EPA na rundo la fedha za ki-shetani kwenye Benki Uswisi, wataendeleaa kuishi kwa matumaini ya ulinzi wa FFU mpaka lini?????????

Ama kweli Tanzania taifa langu linaangamia kwa kukosa uongozi wenye hekima na uadilifu.

Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine.

Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.
 
Back
Top Bottom