MZEE Mustafa Jaffer Sabodo achangia tena M4C (CHADEMA) na ahadi zingine za miradi

Iam smelling something fishy.In corporate theory,nothing should go for nothing.
 
sidhani kama kinachonitatiza ni Sabodo kuchangia; la hasha. Kuna vitu ambavyo sidhani kama vimekaa sahihi... ngoja nirudi nyuma kidogo..
 
CDM inabidi warudi shule wakasome Portfolio Theory. Naona somo la diversification limewakalia kushoto kabisa. Why always wanategemea source moja ya finance? Tena mbaya zaidi kutoka kwa individual!! Hawawezi kubuni njia nyingine za kuraise fund?
 
Iam smelling something fishy.In corporate theory,nothing should go for nothing.

Kuna sinema ya Ki Nigeria niliiona inaitwa Nothing for Nothing imeigizwa na kamanda Kanayo O Kanayo! ina maana kubwa kwamba hakuna free lunch katika dunia hii!
 
CDM inabidi warudi shule wakasome Portfolio Theory. Naona somo la diversification limewakalia kushoto kabisa. Why always wanategemea source moja ya finance? Tena mbaya zaidi kutoka kwa individual!! Hawawezi kubuni njia nyingine za kuraise fund?

Duh Rejao kumbe wewe mzee wa finance na mambo ya investment? Umenikumbusha mbali
 
CDM inabidi warudi shule wakasome Portfolio Theory. Naona somo la diversification limewakalia kushoto kabisa. Why always wanategemea source moja ya finance? Tena mbaya zaidi kutoka kwa individual!! Hawawezi kubuni njia nyingine za kuraise fund?


Hivi unataka kutuambia kwamba Sabodo ndio source pekee ya finance kwa CHADEMA tangia kianzishwe? Kaa ukijua hakuna ubaya wowote kwa chama kupata ufadhili kutoka kwa individuals, vinginevyo ungeanza kuwalaumu magamba kwa tabia yao ya kupokea misaada kutoka kwa wafanyabiashara kwa ajili ya kufinance kampeni zao.
 
Mwisho wa siku hata wanachama wenyewe wa CDM walivyo maz*** hawawezi hata kuulizia kuhusu michango yao inavyofanya kazi.Endeleeni tu kuchangia huo mradi wa watu fulani wa kaskazini kuwapiga pesa, mnadanganywa M4C
 
Watakayosema kuhusu Sabodo na CDM kwasasa hayatakuwa na Nafasi M4C inasonga kwa mwendo wa light!
 
user-offline.png
mpayukaji
CCDM kupokea pesa toka kwa huyu ndg si kosa kumbuka kuwa CDM kwenye mikutano yake ya hadhara imekuwa ikipokea michango toka kwa wananchi wanahudhuria mikutano hiyo na wenye mapenzi mema na chama pia nchi hii tofauti yake ni kiwango cha pesa tu

issue ya namna pesa zinavyo patikana hilo ni suala la serikali yetu. Labda sema kinacho weza kuwaua CHADEMA ni transpancy dhidi ya matumizi ya hizi pesa na umakini mkubwa kufanya kile kilicho kusudiwa tena kwa WAKATI kama
Kimbunga anavyo lalamika.
 
CDM inabidi warudi shule wakasome Portfolio Theory. Naona somo la diversification limewakalia kushoto kabisa. Why always wanategemea source moja ya finance? Tena mbaya zaidi kutoka kwa individual!! Hawawezi kubuni njia nyingine za kuraise fund?
Rejeo huwezi kukataa pesa zinazo ingia kumbuka kuwa CDM hawaombi msaada kwake bali huyu mzee anaguswa utendaji mzuri wa CDM na anamua kuwasupport
 
CDM inabidi warudi shule wakasome Portfolio Theory. Naona somo la diversification limewakalia kushoto kabisa. Why always wanategemea source moja ya finance? Tena mbaya zaidi kutoka kwa individual!! Hawawezi kubuni njia nyingine za kuraise fund?
Unataka watumie ile njia ya CCM ya kuiba kodi za wananchi nafikiri ndio diversification unayoizungumzia
 
Kabla hamjaanza kusingizia watu wengine kuwa ni mafisadi, wakamateni na kuwashtaki kwanza wale ambao walishatajwa tena kwa ushahidi ulio wazi. Badala ya kuwashughulikia mnazidi kuwapatia nafasi kwenye viti vya mbele, hasa bungeni. Leo watuhumiwa wakubwa Richmond, Kagoda, Rada n.k, ni nani kwenye chama chenu cha magamba/mafisadi na kwenye serikali yenu na kwenye bunge 'lenu'.

Kabla hamjaanza kusingizia bila ushahidi hata chembe, twambieni mmefikia wapi kujivua gamba na watuhumiwa wa ufisadi mliwataja kwa majina wenyewe...

Kabla hamjaanza kushusha shutuma zisizo na msingi zikiwa ni dalili ya kuendelea kukubali kushindwa kwenye kila angle ya battle hii, kwanza waambieni Watanzania wale mawaziri waliokabiliwa na shutuma kubwa za ubadhirifu karibuni wako wapi vile, lupango eeh, kule Segerea, si ndiyo.

Kabla hamjaanza kuhukumu kila mfanyabiashara kwa kumwita ni fisadi bila ushahidi hata wa kuokoteza achilia mbali genuine, waambieni kwanza Watanzania wale wafanyabiashara mnaonedelea kushirikiana nao katika kujitajirisha kupitia rasilimali na ofisi za Watanzania, wako wapi.

Usitake kulinganisha misaada yenu iliyokuwa ikitolewa kwenye giza totoro, nyuma ya pazia bila Watanzania kujua. Mchangiaji mwenye nia njema na mwenye nia mbaya unamjua kuanzia hapa katika namna anayochangia. Hivi wale wenu walishawahi kukiri na ninyi mkakiri hadharani kuwa waliwachangia mamilioni na mabilioni kwa sababu gani...mpaka mkaamua kuwalipa EPA, Kagoda, TANGOLD, Meremeta, Migodi ya madini, mashirika yetu ya umma, nafasi za uongozi, n.k.

Mnafikiri mlivyofadhiliwa na ********** kama uliowataja mwenyewe kwenye maandiko yako (umemuacha RA), kila mmoja atafanana na ninyi eeh! Msaada wa Sabodo utaendelea kuchukuliwa kwa thamani ile ile anayopewa Mwananchi wa kawaida kule Mtwara, Lindi, Mwanza, Dar es Salaam

Kwa CHADEMA anachotoa M4C haitabagua watu hata mmoja kwa sababu ya rangi yake, kabila lake, dini yake au mahali anapotoka au uwezo wake wa kipato. Never. Kila mtu atakuwa na mchango sawa katika hili vuguvugu. Anachotoa Sabodo kitapata thamani ile ile wanayotoa wananchi wanaokuja kwenye mikutano ya hadhara ambao nao wanatoa hadharani bila kificho.

Hebu leo hii acheni kuwatisha wafanyabiashara wengi tu wasafi na wafanyakazi wengine, wakiwemo watumishi wa umma na sekta binafsi, lakini bado wamejaa uoga kwa kutishwa na vyombo vya serikali kama TRA na vyombo vya dola...mkiwaacha na wakaona wazi mazingira yako safi wao kuchangia harakati hizi kwa chochote kidogo/kikubwa walichonacho, mtakwisha saa 2 asubuhi.

Na kitu muhimu zaidi kwa Sabodo inaweza isiwe michango yake pekee, bali staili yake ya utoaji ambayo inasukuma kwa kasi sana dhana ya kuondoa uoga miongoni mwa Watanzania wa kada mbalimbali ambao mpaka leo wanapenda kweli mabadiliko lakini bado hawajaweza kuogopa na kuukimbia UOGA...nothing to fear but fear itself.

Mwacheni Sabodo awatie ujasiri wengi zaidi walio wasafi wachangie M4C, maana Watanzania kuondolewa uoga na kutiwa ujasiri ndicho kitu kinachowaogopesha kabisa ninyi.
 
Naona kama Sabodo anawadhalilisha Chadema kwa faida zake binafsi na chama chake cha mafisadi. Huwa siamini wafanya biashara ambao ukiwauliza walivyochuma huo utajiri utakuta ni mafisadi wa kunuka. Hakika penye udhia penye rupia. Chadema wanazidi kuingia kwenye tope la ufisadi.

Mkuu kwa hilo la biashara zake nadhani hakuna shaka,kama ingekuwa ni fisadi yule mlopokaji original aka vuvuzela angepiga kelele mpaka angelazwa,si unamjua alivyo na kihelehele?
 
Mimi nimekuwa nikisikia Sabodo anachangia n kusema atachimba visima lakini sioni am kusikia siku moja CDM wakisema leo tunazindua visima vilivyochimbwa kwa pesa za Sabodo. Hivi mchakato wa kuchimba visima unachukua miaka mingapi?

Mkuu Kimbunga uchimbaji wa visima huamki tu asubuhi na kuanza kuchimba ni lazima kuwe na survey ya kutosha na uhakika wa maji yatakayokuwepo kwa muda mrefu. Otherwise utajikuta mmetumia raslimali pesa vibaya na tutaanza kuwanyooshea vidole chadema kwa matumizi mabaya ya pesa. Ndo maana hata yeye kawaambia hiyo jana kuwa watafute wakandarasi wenyewe wa wafanye detailed survey wenyewe ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi.
 
Back
Top Bottom