MZEE Mustafa Jaffer Sabodo achangia tena M4C (CHADEMA) na ahadi zingine za miradi

sidhani kama kinachonitatiza ni Sabodo kuchangia; la hasha. Kuna vitu ambavyo sidhani kama vimekaa sahihi... ngoja nirudi nyuma kidogo..

Mkuu, hebu nenda mbele maana ukirudi nyuma, utapoteza muelekeo juu ya hili...FUNGUKA
 
Tumaini Makene ..mfano mzuri ni jirani zetu wa kenya, waangalieni vyama vya upinzani wanavyouana wenyewe kwa wenywe wakati mzee moi katulia kwake...shame siasa za tz hakika sitopiga kula kamwe maisha..huyu sabodo halipi kodi sasa ameona ahamie upande wa pili wa shilingi hasije sumbuliwa 2015, chadema fikirila hii kitu itawacost
 
Last edited by a moderator:
Tumaini Makene Mkuu ukisikia uzalendo wa kweli kwa Mtanzania ndio huo, bila kujali dini kabila wala chama anafanya kile kinachotakiwa kufanywa na Watanzania wote!!!VIVA MZEE SABODO VIVA MAKAMANDA WA CDM, DAIMA MBELE NYUMA NI MWIKO!!!

 
Last edited by a moderator:
Naona kama Sabodo anawadhalilisha Chadema kwa faida zake binafsi na chama chake cha mafisadi. Huwa siamini wafanya biashara ambao ukiwauliza walivyochuma huo utajiri utakuta ni mafisadi wa kunuka. Hakika penye udhia penye rupia. Chadema wanazidi kuingia kwenye tope la ufisadi.
usafi wa sabodo unajulikana tangu enzi za nyerere, huyu si mwizi ni kama wafanyibiashara waliopata pesa kihalali kama ndesamburo, aikaeli mbowe nk, siyo kila tajiri ni mwizi
 
Bila shaka watakuwa wanajiandaa kukaa kikao cha kumwita ni mdini, mkanda na mkabila. Viongozi wa kikao ni wale wanaoongoza kwa kuugua CHADEMA-phobia, Wassira, Mwigulu, Yule mpayukaji wao mkuu, Martha Mlata, Stella Manyanya, Lusinde na wengine kibao kama mnavyowajua wale ambao akili zao zimejaa ubaguzi muda wote. Mchawi huwa wa kwanza kuwaita wenzake wachawi ili kupoteza lengo la mashambulizi.

Makini, umesema sehemu ya mazungumzo ilihusu utekelezaji wa ahadi zake za nyuma, please tupe maelezo ya ziada.utekelezaji wa ahadi zake za nyuma umefikia wapi?
 
CDM inabidi warudi shule wakasome Portfolio Theory. Naona somo la diversification limewakalia kushoto kabisa. Why always wanategemea source moja ya finance? Tena mbaya zaidi kutoka kwa individual!! Hawawezi kubuni njia nyingine za kuraise fund?

CHEMBA ya iramba magharibi imewahi kusema cdm inafadhiliwa kwa siri na cdu cha ujerumani,cdm kinawaonyesha wafadhili wake hadharani CHEMBA imeumbuka, mnyama kutoka gombe alisema cdm ni wadini (wakristo) jamii ya washia (sabodo) waislam (prof. Safari) inajitokeza hadharani kuthibitisha cdm si wadini, mnyama anatamani kurudi msituni nape akawadanganya watanzania eti cdm ni chama cha kikanda m4c imewachakaza kusini (lindi na mtwara) sasa wanalaumiana, mbeya, iringa, mwanza n.k zinamfanya nape kuwa kijana wa mipasho na kutoa tafsiri mpya ya gamba kila kukicha Picha itakuwa tamu pale INJINI YA MANYANYA itakapo kuwa salo serikali itakapoumbuliwa kwa habari za utekaji nyara wa dr. ULIMBOKA
 
Cheza na hela wewe, jamaa wametoa meno kama matangazo ya whitedent. Mnawapaka mavi wadosi halafu mnafurahia vihela vyao. Zitawatokea puani hizo.
 
.....JAH akujalie baba sabodo kwa moyo wako wa kuwakumbuka wanyonge wa nchi hii ili kusaidia mapambano haya kuelekea uhuru wa kweli...
 
Hivi unataka kutuambia kwamba Sabodo ndio source pekee ya finance kwa CHADEMA tangia kianzishwe? Kaa ukijua hakuna ubaya wowote kwa chama kupata ufadhili kutoka kwa individuals, vinginevyo ungeanza kuwalaumu magamba kwa tabia yao ya kupokea misaada kutoka kwa wafanyabiashara kwa ajili ya kufinance kampeni zao.
Rejeo huwezi kukataa pesa zinazo ingia kumbuka kuwa CDM hawaombi msaada kwake bali huyu mzee anaguswa utendaji mzuri wa CDM na anamua kuwasupport

Naona mnatumia nguvu nyingi sana kukitetea CDM...tafuteni kufahamu vizuri matumizi ya hizo pesa kwanza ndio mje kufanya utetezi wenu hapa. Mimi nimejaribu tu kuwapa changamoto CDM watafute njia mbadala za kujiongezea kipato badala ya kumtegemea mtu mmoja tu.
 




    • sabodo.jpg
    • 0000001asabodo.jpg
    attachment.php



Sina ugomvi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wala mpenzi wake mpya Mustafa Jafary Sabodo. Nina ugomvi na staili ya Sabodo ya 'kukisaidia' Chadema. Kila akijisikia kupata publicity, huwaita viongozi wa Chadema na kuwapa milioni kadhaa za shilingi. Sijajua ni kwanini Chadema hawataki kujua historia ya 'utajiri' wa Sabodo anayejinasibu kama mjamaa aliyekuwa karibu na baba wa taifa Mwl Julius Nyerere. Kwa wanaojua ushupavu na uwazi wa Mwalimu wanashangaa ni kwanini uhusiano wao na Sabodo umekuwa maarufu baada ya kifo cha Mwalimu kama hakuna namna? Pia kuna utata zaidi ya nia ya Sabodo kusimama na kulala CCM lakini bado akajifanya ana mapenzi na Chadema. Je Sabodo ametumwa na CCM kuwahujumu Chadema kwa njia ya kuwadhalilisha ili wakati ukifika CCM watumia udhaifu huu kuwaumbua na kuwamaliza kisiasa?Je Sabodo anasukumwa na uzalendo na mapenzi wa demokrasia na Chadema au anatumwa na genge la wahindi linaloanza kuhofia maslahi yao kama CCM itapoteza dola? Je kwa namna hii si kuiweka Chadema kishawishini ili hatimaye iingie mfukoni mwa Sabodo na genge lake? Tunahofia hili kutokana na mazoea ya kuona karibu kila utawala kuanzia awamu ya pili unakuwa na mhindi nyuma yake akiwakilisha maslahi ya genge lake na watawala mafisi na mafisadi. Nani mara hii kasahau Gulamali aliyefikia hadi kumwita first lady Sitti Mwinyi Shemeji? Huyu alifika chini ya Ali Hassan Mwinyi sawa na Mohamed Raza alivyosifika chini ya Salmin Amour . Nani mara hii kasahau yule Mhindi, Sailesh Vithlani wa rada wa wakati wa Benjamin Mkapa? Nani haoni ujio wa Mohamed Dewji aka Mo anavyozidi kuwa maarufu chini ya serikali ya Jakaya Kikwete? Je Sabodo anacheza karata mbili yaani Chadema na CCM ili atayepita naye apete? Maana ni mwanachama wa CCM na 'mfadhili' wa Chadema. Wenye kujua siasa vizuri hawafurahishwi kuona viongozi tena wa juu wa Chadema wakipanga kama vitoto vya shule mbele ya mkuu wa shule kupokea cheki toka kwa Sabodo. Je Chadema emiridhika na kujishusha hadhi hadi kuwa chama kinachoweza kufadhiliwa na mtu binafsi tena mwenye madoa badala ya umma wa watanzania ambao wamekuwa wakikiunga mkono? Kwa wanaojua thamani ya imani ya umma wanashangaa kuona Chadema inavyozidi kujivua nguo kwa zawadi na ahadi ya vishilingi milioni kadhaa bila kujua kuwa hapo baadaye hili laweza kuigharimu madaraka. Nani atawasaidia na wakamsikiliza? Naomba nitoe hoja.

Chadema hata wewe na mimi tukiwaita wanaitikia wito.Siyo kwa Sabodo tu hebu waite wewe kama hawatakuja.Kile
ni chama cha wote haijalishi una uwezo gani.Ndio maana wana kesi nyingi walizosingiziwa kufanya mikutano isiyo halali,
wao wakipita na wananchi wakitaka kywasalimia wanasimama na sio kama magamba wanafunga vioo utafikiri wameona mbun'go.
 

Mfanyabiashara maarufu na Kada wa CCM, Mzee Mustafa Jaffer Sabodo akikabidhi hundi ya Sh10m kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa nyumbani kwa Upanga, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA, Antony Komu. Fedha hizo ilikuwa sehemu ya mchango mwingine wa Mzee Sabodo pamoja na ahadi kwa ajili ya kusaidia shughuli za chama hicho kuendelea kufanya kazi zake za kuimarisha na kueneza mtandao wake, ngazi za mitaa na vitongoji nchi nzima.




Dkt. Slaa akipeana mkono na Sabodo.
 
Naona kama Sabodo anawadhalilisha Chadema kwa faida zake binafsi na chama chake cha mafisadi. Huwa siamini wafanya biashara ambao ukiwauliza walivyochuma huo utajiri utakuta ni mafisadi wa kunuka. Hakika penye udhia penye rupia. Chadema wanazidi kuingia kwenye tope la ufisadi.

Na kweli huu ni mpayuko haswaaaa!
 
Naona mnatumia nguvu nyingi sana kukitetea CDM...tafuteni kufahamu vizuri matumizi ya hizo pesa kwanza ndio mje kufanya utetezi wenu hapa. Mimi nimejaribu tu kuwapa changamoto CDM watafute njia mbadala za kujiongezea kipato badala ya kumtegemea mtu mmoja tu.
Unatamani ungepewa wewe, Tatizo lenu si tunalijua?
 
Something is very wrong; there is something I don't LIKE about it. Can't point it out yet but it is there...


nilijua ni mimi tu mwenye mashaka na hizi charity, what if huyu mzee anajitengenezea mazingira mazuri na whoever comes to power? I mean ikitokea Chadema imeingia madarakan hawawezi kumtosa mfadhiri wao, na Ccm ikibaki hawewezi kumtosa kada wao, i think he is playing safe
 
Nimeona! CDM tunachukua nchi kiulaini kwani chama chetu kinapendwa na wengi.
 
Back
Top Bottom