Mzee Butiku: Watanzania hawajaridhika na uwekezaji wa bandari, serikali isione aibu kuachana nao

Dirham za urojo labda
Watu wanaweka sawa TEHAMA za kisasa bandarini saa hizi, umelala?

Unafikri wafanya biashara wana kungoja kuongoja. Ukishawapa MoU tayari wanaingia kazini.

Unaelewa kuwa MoU baina ya DP World na TPA ya Dollar Million 500 ilishasainiwa na kazi zieshaanza? Jisomee:

The funds from the agreement will be spent on developing Tanzania's ports, targeting key areas of Information and Communication, Technologies (ICTs) systems, training for capacity building among TPA staff and improvements in port infrastructures.

The funds are also expected to enable the country's ports to increase their competitiveness at the regional and global level and improve services.

Vimbwanga kidogo tu vya TEHAMA hata havijaanza kazi kisawasawa, tayari tumeshaipita bandari ya Mombasa kwa mizigo. Cheza na Waarabu wewe?
 
Kuiondoa Serikali ya CCM ni ngumu hata kama kukiwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, maana wanashikilia majeshi.

Njia pekee ni coup d'etat itakayofanywa na wanajeshi wenyewe.
Wananchi wenyewe wanatosha kuimaliza kazi hiyo. Usiwasumbue wanajeshi wetu kuhangaika na jambo ambalo sasa ni rahisi kabisa kwa wananchi kulifanya.

Kilichobaki tu sasa hivi ni uongozi wa kuleta haya mabadiliko yatakayofanywa na wananchi wenyewe.

CHADEMA ni kama Samia kawaroga; hawako sawa tena tokea Mwenyekiti wao alipoingia kwenye mazungumzo ya maridhiano.
 
Watu wanaweka sawa TEHAMA za kisasa bandarini saa hizi, umelala?

Unafikri wafanya biashara wana kungoja kuongoja. Ukishawapa MoU tayari wanaingia kazini.

Unaelewa kuwa MoU baina ya DP World na TPA ya Dollar Million 500 ilishasainiwa na kazi zieshaanza? Jisomee:

The funds from the agreement will be spent on developing Tanzania's ports, targeting key areas of Information and Communication, Technologies (ICTs) systems, training for capacity building among TPA staff and improvements in port infrastructures.

The funds are also expected to enable the country's ports to increase their competitiveness at the regional and global level and improve services.

Kwa hiyo ulitaka majizi yakurupushwe hata kabla haijajulikana kuwa tayari yamo ndani?

Subiri uone kitakachofuata.

Unajitia moyo tu hapa JF huku ukijua moyoni mwako kwamba majambazi sasa hivi yanakabiliwa sawasawa.
 
Amesema watanzania wasichokozwe kwenye mali zao wasikilizwe na wasibezwe mambo wanayoyahoji kabla jua halijazama

Usiku mwema wakuu naona swala la Dp world likileta anguko kubwa kwa serikali ! maana ccm imeona wao ndio wenye akili kuliko wananchi wenyewe wanaoshauri mkataba wa bandari urekebishwe, wengi wamejiuliza ni elimu gani wananchi wanatakiwa kuipata kuhusu mkataba huo?
Wamejaa na dharau Viongozi wetu
 
Spinning doctors wapo kazini, mzee anasema mengine mleta mada hayasemi anayosema huyo mzee.

Hata muuliza maswali anajaribu kumtowa njani mzee lakini kapangua vizuri sana. Kidiplomadia na hekima.

Watu wangoje HGA. Simple.
Duh pole,unapitia uchungu mkali sana
 
Spinning doctors wapo kazini, mzee anasema mengine mleta mada hayasemi anayosema huyo mzee.

Hata muuliza maswali anajaribu kumtowa njani mzee lakini kapangua vizuri sana. Kidiplomadia na hekima.

Watu wangoje HGA. Simple.
Umekumbwa na nini wewe!!?
 
Huyu si ndo alikuwa mshauri wa Nyerere ambapo ilifika kipindi hadi watu walikuwa wanapanga foleni kununua bidhaa madukani kutokana na uchumi wa nchi kudhoofu kwa Sera za hovyo?

Mnawapa umaarufu wa bure tu hawa watu ambao historia inatuonesha wazi hawajawahi kufanya lolote la maana kiuchumi!

Kuhusu Bandari Rais na Serikali yake wako sawa. Hakuna kurudi nyuma!
 
Sijui ugumu Uko wapi kuachana na hili dude DP ila nahisi kuna maslahi ya wachache na ndio wanaolazimisha hili dude lipewe bandari.

Na inatumika nguvu kubwa kulazimisha hii ajenda.

Mimi naamini figisu za mikataba ya huko nyuma kutokufaidika direct kwa wananchi ndo maana mjadala umegoma kufika mwisho.

Basi tu Serikali na Chama wamezoea kuziba masikio.

Lakini iko siku watanzania uoga wa kuwawajibisha viongozi utawaisha tujipe muda tu!
Maslahi gani ya wachache?
 
Wananchi wenyewe wanatosha kuimaliza kazi hiyo. Usiwasumbue wanajeshi wetu kuhangaika na jambo ambalo sasa ni rahisi kabisa kwa wananchi kulifanya.

Kilichobaki tu sasa hivi ni uongozi wa kuleta haya mabadiliko yatakayofanywa na wananchi wenyewe.

CHADEMA ni kama Samia kawaroga; hawako sawa tena tokea Mwenyekiti wao alipoingia kwenye mazungumzo ya maridhiano.
Jaribu uone chizi wewe
 
Kwa jinsi CCM ilivyo geuka chama cha wapigaji, sidhani kama watasikia kilio hiki kutoka kwa waasisi wa TANU na hatimaye CCM mwaka 1977.
 
Mzee Butiku anasema kwa namna kelele zilivyo nyingi kuhusu suala la bandari serikali Ina namna mbili tu..
1. Kiheshimu hofu na maoni ya wananchi kwamba hawajaridhika na suala hili, au
2. Kuwapuuza wananchi na kuendeleza na suala hili.

Lakini wapime madhara ya kila uamuzi watakaoifanya.

Alipoulizwa kuhusu ushirikishwaji wa wananchi kama haukuwa wa kutosha. Mzee Butiku amesema hadhani kama ushirikishwaji ulikuwepo, na kama uliikuwepo basi ulifanywa ktk namna ambayo haikuwa bora, kwani hata yye ni mwananchi lkn hajauona huo ushirikishwaji.

Ameulizwa endapo hoja za serikali kutetea suala la DP je, zinajibu hoja za wananchi? Mzee Butiku amejibu kuwa hazijubu ndiyo maana mjadala haukomi.

Ameonya wale wanaowatisha wanaotoa maoni kinzani na kusema tabia hii inajenga hofu na kujenga taifa la woga.

Anaongeza kwa kusema kuendelea na suala hili ni kuhatarisha umoja na muungano wetu.
---

Mzee Butiku: Rais ameruhusu tuzungumze, Watanzania bado waoga
"Nianze kwa kutoa shukrani kumshukuru na kumpongeza Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mabo mawili kwanza kuruhusu Watanzania kuzungumza...tulikuwa na woga...lakini tangua Rais aingie ametuambia tuzungumze, waziwazi...ukweli

"Kwa maoni yangu Watanzania bado wanao uwoga...wana wasiwasi...hawana hakika kama maamuzi haya yaliyofanywa na serikali ni kwa faida ya nchi yao, hiyo sauti unaisikia wakati wote kwa ngazi zote"

Source: ITV Kipindi cha dk 45.
Kabisa.
 
Naunga mkono hoja,in fact sio aibu Kwa sababu wenye maamuzi ni wao waachane nao..

Niliwahi andika siku nyingi kwamba Serikali iachane na hili suala Kwa sababu sio lazima
 
Hivi kushirikishwa maana yake halisi ni nini? tukubaliane sote au percentage fulani wakipitisha basi au bunge ambali ndio wawikilishi kisheria wa wananchi. Katika hili tuwekane sawa maana haitatokea tukubaliane hata 90% hakuna na nchi nyingi duniani kuna serikali zinaundwa kwa 51% tu lakini wanakuwa na Mandate ya kufanya maamuzi.

Sasa tujengeni hoja ni ushirikishaji wa wananchi upi tunaongelea hapa na wa kiasi gani au baadhi ya watu waombwe maoni yao basi maana huwezi kuongelea jambo na watu mil 61 tukafikia muafaka. Hata haya ma team yetu ya mpira yana watu wengi lakini maamuzi yanafanywa na watu hawazidi alfu 2 na utakuta wengine wanapiga kelele hawataki ni mambo ya kawaida. CCM wamesema wanatekeleza ilani 2020 to 2025 au huwa tunachagua chama hatujui ilani? Demokrasi ni majority wins 51% wewe unashida dola huna haja kuuliza kila kitu kwa watu, na watu wanachagua wabunge wa chama wanachotaka kuwakilisha hao ndio unatuwakilisha sisi. Shida tunaongelea kijumla ushirikishi wa watu ni ushirikishi upi tunaotaka? tusiongee kijumla kijumla tu hata family zetu vikao sio ukoo mzima unakaa kuamua ni baadhi tu.
 
Back
Top Bottom