Mzee Ally Hassan Mwinyi pekee alijaribu, alivunja Baraza la Mawaziri la Muungano mwaka 1990 alipoona kuna shida mahala

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,940
20,400
Tarehe 13 mwezi August mwaka 1990 magazeti yote ya Tanzania yalikuwa na vichwa vya habari vilivyohusu kujiuzulu kwa baraza la mawaziri jana yake yaani tarehe 12.

Taarifa hizo zilisema kuwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais mzee Ally Hassan Mwinyi aliwaambia mawaziri wote wakiongozwa na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, Joseph Sinde Warioba kwamba, wajiuzulu na warudi makwao na wampishe atengeneze baraza jingine la mawaziri.

Taarifa hizo zileendelea kutaarifu kuwa Rais Mwinyi alisema kuwa shughuli zote za baraza la mawaziri zingekuwa chini ya makatibu wakuu wa wizara.

Baraza hilo pamoja na mzee Warioba lilikuwa na waziri wa Fedha Cleopa Msuya, waziri wa serikali za mitaa Paul Bomani rip, waziri wa mambo ya Nje Benjamin Mkapa rip, na mzee Rashid Mfaume Kawawa rip ambae alikuwa waziri asie na wizara maalum.

Wengine ni mzee Al Noor Kassum rip ambae alikuwa waziri wa madini na nishati, Jackson Makweta rip waziri ofisi ya Rais(Ulinzi) na mzee Muhidin Kimario rip ambae alikuwa waziri wa mambo ya Ndani.

Hawa mawaziri ni baadhi ya mawaziri wa serikali hiyo ambayo iliundwa mawaziri 26 na manaibu waziri 14.

Kama kawaida mawaziri waliwasili Ikulu siku hiyo kwa mkutano wa baraza la mawaziri ambao ungechukua hadi masaa matatu.

Kwa mshangao wao kikao hicho kilichukua dakika tatu tu pale Rais Mwinyi alipotamka kwamba anataka mawaziri hao wote wajiuzulu na warudi makwao.

Waziri wa mambo ya nje, mzee Mkapa(RIP) alichanganyikiwa na kumwambia Rais kuwa alikuwa tayari ana "engagement" za mikutano Ulaya na akaambiwa "Cancel it".

Wakati hayo yote yakifanyika mwenyekiti wa CCM hayati baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa angani akielekea Rome nchini Italia.

Mwalimu pamoja na kuongea sana na siasa thabiti, moja ya udhaifu wake ulikuwa ni kutowachukulia hatua mawaziri ambao walikuwa wanamuangusha kwenye idara ya kuwajibika na ufisadi.

Kuna kipindi hayati Mwalimu aliwahi kutembezwa maeneo ya Msasani na Mikocheni na kuonyeshwa nyumba za baadhi ya mawaziri wake na alifahamu walipata kiasi gani cha mshahara kulinganisha na majumba aloyaona lakini alibakia kushangaa.

Hivyo mzee Mwinyi akiwa anaelewa hayo alimfuata hayati Mwalimu uwanja wa ndege kabla hajatimkia Rome na kuhakikisha ameondoka kabla ya kurudi Ikulu na kuchukua maamuzi hayo magumu.

Hayati Nyerere alipofika Rome na kupokelewa na vijana wa pale wakampasha habari za Dar-es-Salaam na akashangaa kweli, ila kimoyomoyo alishukuru kuona angalau Mwinyi ameweza.

Baadae, Rais Mwinyi akiongea na vyombo vya habari alitoa sababu za msingi za kuwataka mawaziri wake wote wajiuzulu na akasema kuwa ni vitendo vya rushwa na kutowajibika kwa mawaziri kulikokithiri khasa katika wizara zao.

Alitoa mifano ya wachuuzi kuombwa kitu kidogo pale walipotaka haki zao na hata wastaafu hali ilikuwa ni hiyohiyo, na hata kuambiwa "njoo kesho, njoo kesho".

Msemo wa njoo kesho ulikuja kupata maarufu baadae pale ulipotumika kukemea vitendo vya rushwa na ufisadi na hata kutungwa wimbo wa FAGIO LA CHUMA KUWAKUMBA WALE WASOWAJIBIKA.

Huku kukiwa na shauku ya kutaka kufahamu baraza jipya la mawaziri laja, wananchi walianza kuvumisha kuwa kutakuwa baraza jipya kabisa lenye sura mpya, lakini wakikatishwa tamaa pale mzee Joseph Sinde Warioba alipotangazwa ndiye waziri mkuu anaeendelea.

Si kwamba Mzee Warioba nae alikuwa ni fisadi au mla rushwa lakini wananchi walitegemea Rais Mwinyi angebadilisha kila kitu na kuanza upya "once for all" au "the beginning of new chapter".

Hivyohivyo kwa baraza la mawaziri mawaziri saba walipoteza nafasi zao Al Noor Kassum, Aaron Chiduo, Muhidin Kimario, Damian Lubuva, Chrisant Kissanji, Arcado Ntagazwa na mama Getrude Mongela.

Mzee Mwinyi akatolea mfano wa yeye mwenyewe akiwa waziri wa mambo ya ndani ilibidi ajiuzulu pale yalipotokea mauaji yasiyoeleweka kule Shinyanga ambapo polisi walihusika na mauaji yale.

Lakini uamuzi wa mzee Mwinyi kuwataka mawaziri wake wajiuzulu haukutoka bure bali kuliktokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na kamati kuu ta CCM au CC kama inavyojulikana na kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mwalimu ilibaini taasisi na wizara zipatazo 12 ndizo zilikuwa na shida.

Wizara ya sheria, mambo ya ndani, wizara ya afya na wizara ya ardhi zilisemwa kuwa hali ya rushwa na ufisadi ilikuwa imefikia kiwango cha juu.

Mwalimu akaamuru wahusika wote ambao ni mawaziri wafike kwenye kikao cha kamati kuu lakini uamuzi huo ukapigwa chenga na mawaziri khasa mzee Kimario wakaamua kujiuzulu kuliko kwenda kwa CC kujibu masuali ya Mwalimu na wajumbe.

Ila tatizo kama kawaida likajirudia na mzee Mwinyi akawarudisha mawaziri wake waandamizi kama Mkapa, Msuya, na wengine akawabadili wizara.

Ila kukaja sura mpya kama mzee Nalaila Kiula ( kukawa na kichwa cha habari kilochosema "Nalaila Kiula aula"), mazee Jakaya Mrisho Kikwete akawa waziri wa nishati, madini na maji, Charles Kabeho (elimu).

Akijitetea raisi Mwinyi akasema hakutaka kubadili baraza zima kwa sababu ilibakia miezi minne kabla ya kuvunja bunge kwa ajili ya maandalizi ya uchuguzi mkuu.

Hata hivyo raia Mwinyi aliagiza kuwepo uwajibikaji, kuondoshwa kwa vitendo vya rushwa, kupunguza safari za nje na semina zisizoeleweka.

Kuhusu balozi zetu nje, akaagiza kuwepo balozi na msaidizi wake mmoja tu na kila mwezi atakuwa akifanya mikutano na wananchi.

Wananchi wenye shida mbalimbali za ardhi, mikopo, mafao na kesi kucheleweshwa zote raisi Mwinyi alikuwa akizishughulikia mwenywe na wasaidizi wake pale CCM Lumumba.

Hata kule Zanzibar raisi Idris Abdul Wakil nae alifanya hayo na kukutana na wananchi kusikiliza shida zao na aliwaita polis, maofisa wa wizara na CCM kujibu masuali kadhaa.

Ninachotaka kusema ni kwamba matatizo ya nchi yetu hayakuanza leo na wala hayataisha leo.

Tunahitaji viongozi wetu kujituma na kufanya maamuzi khasa ya kuokomboa nchi yetu kiuchumi.

Raisi aweza kufanya mabadiliko ya hapa na pale katika baraza lake la mawaziri lakini tatizo lipo kwenye mfumo wote na khasa kule chini ambako mkurugenzi wa maendeleo au afisa mtoza ushuru ana uwezo wa kukwapua fedha za umma na kujilimbikizia mali bila kugundulika mapema.

Serikali itengeneze mifumo sahihi iliyo na ufanisi na uelevu wa kubaini wizi na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Raisi aliepo sasa asimwonee mtu aibu, kama kuna waziri hawajibiki ipasavyo apishe na kama ni baraza zima ( kwa Tanzania Bara) halielewi linafanya nini liondolewe na aanze upya hadi 2025.
 
Kwa sasa mawaziri wanapumzika baada ya mshikemshike wa miaka mitano iliyopita, tukishtuka ni 2025 tunawachagua tena wanarudi kuendelea kupumzika kwenye kiyoyozi
 
Kumbukizi nzuri na hili Rais anatakiwa kulifanya lakini awe ameshapanga vizuri safu ya ulinzi na usalama.

Kuna watu wanafanya mchezo , haiwezekani kila mtu anakuja na tamko,masuala waliyokubaliana kwenye Baraza yanakuwa ni ya Waziri husika.

Sijawahi msikia PM akizungumzia miamala zaidi ya Rais, Waziri mhusika ,VP na Waziri wa fedha yeye akiwa ndio mtekelezaji mkuu wa Serikali anajifanya halimhusu.

Pia nikiangalia IGP naona kama anafanya Kazi kwa shingo upande Sasa hapa lazima mama asafishe apate watu Royal kwake na sio wanafiki.

Hata Magu hakuwa na watu ndani ya chama Wala serikalini au kwenye vyombo vya usalama lakini aliwatafuta na akafaulu.
 
Nitajie mawaziri 10 wanaowajibika ndio tuendelee na mada yako.

Hii regime imelaaniwa. It will never come up with any tangible results. Stay eyes open.
Ummy, Waziri wa maji, Mkenda, Afya, Elimu, Uchumi, Barabara, na Madini.

Bila shaka kwenye reshuffle ya Waziri wa Ulinzi kuna watu watawekwa pembeni.

Hata Rais wa Malagasy kavunjilia mbali Baraza la mawaziri na Rais wa Tunisia kafutilia mbali Bunge na Serikali.

Mh. SSH kama Hawa hawana msaada futilia mbali anza upya ni kawaida tuu hiyo. Ukikuta wanaume wanakuletea ujinga piga pembeni weka Wamama kama kwa Kagame, Museveni na Msumbiji.
 
Nzuri nitaisoma nchi imepitia mengi sana
Tarehe 13 mwezi August mwaka 1990 magazeti yote ya Tanzania yalikuwa na vichwa vya habari vilivyohusu kujiuzulu kwa baraza la mawaziri jana yake yaani tarehe 12.

Taarifa hizo zilisema kuwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais mzee Ally Hassan Mwinyi aliwaambia mawaziri wote wakiongozwa na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, Joseph Sinde Warioba kwamba, wajiuzulu na warudi makwao na wampishe atengeneze baraza jingine la mawaziri.

Taarifa hizo zileendelea kutaarifu kuwa Rais Mwinyi alisema kuwa shughuli zote za baraza la mawaziri zingekuwa chini ya makatibu wakuu wa wizara.

Baraza hilo pamoja na mzee Warioba lilikuwa na waziri wa Fedha Cleopa Msuya, waziri wa serikali za mitaa Paul Bomani rip, waziri wa mambo ya Nje Benjamin Mkapa rip, na mzee Rashid Mfaume Kawawa rip ambae alikuwa waziri asie na wizara maalum.

Wengine ni mzee Al Noor Kassum rip ambae alikuwa waziri wa madini na nishati, Jackson Makweta rip waziri ofisi ya Rais(Ulinzi) na mzee Muhidin Kimario rip ambae alikuwa waziri wa mambo ya Ndani.

Hawa mawaziri ni baadhi ya mawaziri wa serikali hiyo ambayo iliundwa mawaziri 26 na manaibu waziri 14.

Kama kawaida mawaziri waliwasili Ikulu siku hiyo kwa mkutano wa baraza la mawaziri ambao ungechukua hadi masaa matatu.

Kwa mshangao wao kikao hicho kilichukua dakika tatu tu pale Rais Mwinyi alipotamka kwamba anataka mawaziri hao wote wajiuzulu na warudi makwao.

Waziri wa mambo ya nje, mzee Mkapa(RIP) alichanganyikiwa na kumwambia Rais kuwa alikuwa tayari ana "engagement" za mikutano Ulaya na akaambiwa "Cancel it".

Wakati hayo yote yakifanyika mwenyekiti wa CCM hayati baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa angani akielekea Rome nchini Italia.

Mwalimu pamoja na kuongea sana na siasa thabiti, moja ya udhaifu wake ulikuwa ni kutowachukulia hatua mawaziri ambao walikuwa wanamuangusha kwenye idara ya kuwajibika na ufisadi.

Kuna kipindi hayati Mwalimu aliwahi kutembezwa maeneo ya Msasani na Mikocheni na kuonyeshwa nyumba za baadhi ya mawaziri wake na alifahamu walipata kiasi gani cha mshahara kulinganisha na majumba aloyaona lakini alibakia kushangaa.

Hivyo mzee Mwinyi akiwa anaelewa hayo alimfuata hayati Mwalimu uwanja wa ndege kabla hajatimkia Rome na kuhakikisha ameondoka kabla ya kurudi Ikulu na kuchukua maamuzi hayo magumu.

Hayati Nyerere alipofika Rome na kupokelewa na vijana wa pale wakampasha habari za Dar-es-Salaam na akashangaa kweli, ila kimoyomoyo alishukuru kuona angalau Mwinyi ameweza.

Baadae, Rais Mwinyi akiongea na vyombo vya habari alitoa sababu za msingi za kuwataka mawaziri wake wote wajiuzulu na akasema kuwa ni vitendo vya rushwa na kutowajibika kwa mawaziri kulikokithiri khasa katika wizara zao.

Alitoa mifano ya wachuuzi kuombwa kitu kidogo pale walipotaka haki zao na hata wastaafu hali ilikuwa ni hiyohiyo, na hata kuambiwa "njoo kesho, njoo kesho".

Msemo wa njoo kesho ulikuja kupata maarufu baadae pale ulipotumika kukemea vitendo vya rushwa na ufisadi na hata kutungwa wimbo wa FAGIO LA CHUMA KUWAKUMBA WALE WASOWAJIBIKA.

Huku kukiwa na shauku ya kutaka kufahamu baraza jipya la mawaziri laja, wananchi walianza kuvumisha kuwa kutakuwa baraza jipya kabisa lenye sura mpya, lakini wakikatishwa tamaa pale mzee Joseph Sinde Warioba alipotangazwa ndiye waziri mkuu anaeendelea.

Si kwamba Mzee Warioba nae alikuwa ni fisadi au mla rushwa lakini wananchi walitegemea Rais Mwinyi angebadilisha kila kitu na kuanza upya "once for all" au "the beginning of new chapter".

Hivyohivyo kwa baraza la mawaziri mawaziri saba walipoteza nafasi zao Al Noor Kassum, Aaron Chiduo, Muhidin Kimario, Damian Lubuva, Chrisant Kissanji, Arcado Ntagazwa na mama Getrude Mongela.

Mzee Mwinyi akatolea mfano wa yeye mwenyewe akiwa waziri wa mambo ya ndani ilibidi ajiuzulu pale yalipotokea mauaji yasiyoeleweka kule Shinyanga ambapo polisi walihusika na mauaji yale.

Lakini uamuzi wa mzee Mwinyi kuwataka mawaziri wake wajiuzulu haukutoka bure bali kuliktokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na kamati kuu ta CCM au CC kama inavyojulikana na kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mwalimu iliabaini taasisi na wizara zipatazo 12 ndizo zilikuwa na shida.

Wizara ya sheria, mambo ya ndani, wizara ya afya na wizara ya ardhi zilisemwa kuwa hali ya rushwa na ufisadi ilikuwa imefikia kiwango cha juu.

Mwalimu akaamuru wahusika wote ambao ni mawaziri wafike kwenye kikao cha kamati kuu lakini uamuzi huo ukapigwa chenga na mawaziri khasa mzee Kimario wakaamua kujiuzulu kuliko kwenda kwa CC kujibu masuali ya Mwalimu na wajumbe.

Ila tatizo kama kawaida likajirudia na mzee Mwinyi akawarudisha mawaziri wake waandamizi kama Mkapa, Msuya, na wengine akawabadili wizara.

Ila kukaja sura mpya kama mzee Nalaila Kiula ( kukawa na kichwa cha habari kilochosema "Nalaila Kiula aula"), mazee Jakaya Mrisho Kikwete akawa waziri wa nishati, madini na maji, Charles Kabeho (elimu).

Akijitetea raisi Mwinyi akasema hakutaka kubadili baraza zima kwa sababu ilibakia miezi minne kabla ya kuvunja bunge kwa ajili ya maandalizi ya uchuguzi mkuu.

Hata hivyo raia Mwinyi aliagiza kuwepo uwajibikaji, kuondoshwa kwa vitendo vya rushwa, kupunguza safari za nje na semina zisizoeleweka.

Kuhusu balozi zetu nje, akaagiza kuwepo balozi na msaidizi wake mmoja tu na kila mwezi atakuwa akifanya mikutano na wananchi.

Wananchi wenye shida mbalimbali za ardhi, mikopo, mafao na kesi kucheleweshwa zote raisi Mwinyi alikuwa akizishughulikia mwenywe na wasaidizi wake pale CCM Lumumba.

Hata kule Zanzibar raisi Idris Abdul Wakil nae alifanya hayo na kukutana na wananchi kusikiliza shida zao na aliwaita polis, maofisa wa wizara na CCM kujibu masuali kadhaa.

Ninachotaka kusema ni kwamba matatizo ya nchi yetu hayakuanza leo na wala hayataisha leo.

Tunahitaji viongozi wetu kujituma na kufanya maamuzi khasa ya kuokomboa nchi yetu kiuchumi.

Raisi aweza kufanya mabadiliko ya hapa na pale katika baraza lake la mawaziri lakini tatizo lipo kwenye mfumo wote na khasa kule chini ambako mkurugenzi wa maendeleo au afisa mtoza ushuru ana uwezo wa kukwapua fedha za umma na kujilimbikizia mali bila kugundulika mapema.

Serikali itengeneze mifumo sahihi iliyo na ufanisi na uelevu wa kubaini wizi na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Raisi aliepo sasa asimwonee mtu aibu, kama kuna waziri hawajibiki ipasavyo apishe na kama ni baraza zima ( kwa Tanzania Bara) halielewi linafanya nini liondolewe na aanze upya hadi 2025.
 
Dogo mwaka 2007 JK alilazimika kuunda upya serikali baada ya EL kujiuzulu uwaziri mkuu

Uchumi? Una maanisha Madelu...hapo umeharibu. Edit post yako na muondoe...Tozo ni hatari. Hivi kutuma pesa unakatwa Kodi. How comes unatozwa Kodi mara 2. Unalipa Kodi kwenye biashara, na kutuma pesa unakatwa Kodi tena
 
Kwani Madelu kafanyaje? Tunazungumzia walio Royal kusimamia maamuzi ya serikali yawe mazuri au mabaya.

Kama sio Madelu unataka nani ? Utasikia Kimei,shida ya Kimei anaamini kwenye kukopa zaidi na kujaza pesa ndani na mfumuko wa bei kwake sio shida ilimradi haufiki 10% ambapo technically vitu vitakuzwa bei juu.Madelu yuko Kati ila mpango ndio kabisa alikuja na hii bajeti
 
Madelu, Mpango, hawajui kukuza uchumi. Wanachojua ni kukusanya fedha na kuzizika kwenye miradi mikubwa kusiko na tija ya haraka. Uchumi wetu unahitaji zaidi kukua, na hela kuonekana kwa watu. TUUPIGE BOOSTER SHOT HELA ZIONEKANE KWA WATU.
 
Nitajie mawaziri 10 wanaowajibika ndio tuendelee na mada yako.

Hii regime imelaaniwa. It will never come up with any tangible results. Stay eyes open.
"Business as usual" imerejea. Amini usiamini hata malipo ya Serikali kupitia "control number" yameanza kugushiwa
 
Madelu, Mpango, hawajui kukuza uchumi. Wanachojua ni kukusanya fedha na kuzizika kwenye miradi mikubwa kusiko na tija ya haraka. Uchumi wetu unahitaji zaidi kukua, na hela kuonekana kwa watu. TUUPIGE BOOSTER SHOT HELA ZIONEKANE KWA WATU.
Mbona saizi ndio mama anachofanya? Zamani tenda zilikuwa za sekta ya umma saizi sekta binafsi mambo ya force Account yamebaki kwenye vimiradi vya pesa kiduchu lakini contracts zote kutoka wizara zote zinarudi kwa sekta binafsi.

Uchumi ukiharibika kuurudisha kwenye reli huwa inachukua mda sana kwa hiyo hadi mwaka uishe ndio Hali inaweza anza kustabilize.

Serikali inataka pesa mkuu sasa unadhani ifanyaje mambo yaende? Unataka ikakope?
 
Kwanza hizi senti ndogondogo za walalahoi zisichukuliwe na kupelekwa kwenye miradi mikubwa. Ni matumizi mabaya ya pesa.

Miradi iliyofanyiwa uchambuzi wa kina na ikaonekana ina tija siku zijazo, tunaweza kukopa na kuikamilisha kwa wakati ili hiyo tija iweze kuonekana mapema. Small cash based investment zinakuwa mashakani sana. Unaweza kuona fursa ipo leo, ukaanza kufanya investment kidogo kidogo. Mpaka mradi kukamilika 30 years, majirani na washindani wakawa wameshawahi soko na kupata njia mbadala, fursa hazipo tena.

Serikali pia ingeweza kufanya tathmini ya kutoa tax incentives/breaks kwa viwanda na makampuni mapya kama njia ya kuanzisha ajira mpya. Mpaka sasa kuna kundi la vijana wanamaliza vyuo bila kuwa na mwanga wa kutosha kuwa wataajitiwa/watajiajiri wapi. Endapo kutakuwa na makampuni mapya mengi labda ajira halitakuwa tatizo kubwa kwa sasa na siku za mbeleni.

Pia ingeweza kuangalia kama kuna uwezekano wa kubadilisha tija ya kilimo chetu kwa kuondoa kodi kwenye teknolojia (Machines, Computing hardware and software) za kilimo zinazoingizwa nchini. Dunia imeshabadilika sana kwenye kilimo, na teknolojia ndiyo inaoendesha uzalishaji. Sina uhakika kama kiwango cha teknolojia kinachoendesha kilimo chetu kipo katika viwango vinavyotakiwa ili kuwe na tija.
 
Unfortunately hakuna miradi ilifanyiwa uchambuzi,sasa wewe reli ya kwenda Mwanza inafaida gani ikiwa mzigo wote unaenda Burundi,Rwanda na DRC ? Ukikopa kujenga hiyo reli inakumala
 
Kwanza hizi senti ndogondogo za walalahoi zisichukuliwe na kupelekwa kwenye miradi mikubwa. Ni matumizi mabaya ya pesa.

Miradi iliyofanyiwa uchambuzi wa kina na ikaonekana ina tija siku zijazo, tunaweza kukopa na kuikamilisha kwa wakati ili hiyo tija iweze kuonekana mapema. Small cash based investment zinakuwa mashakani sana. Unaweza kuona fursa ipo leo, ukaanza kufanya investment kidogo kidogo. Mpaka mradi kukamilika 30 years, majirani na washindani wakawa wameshawahi soko na kupata njia mbadala, fursa hazipo tena.

Serikali pia ingeweza kufanya tathmini ya kutoa tax incentives/breaks kwa viwanda na makampuni mapya kama njia ya kuanzisha ajira mpya. Mpaka sasa kuna kundi la vijana wanamaliza vyuo bila kuwa na mwanga wa kutosha kuwa wataajitiwa/watajiajiri wapi. Endapo kutakuwa na makampuni mapya mengi labda ajira halitakuwa tatizo kubwa kwa sasa na siku za mbeleni.

Pia ingeweza kuangalia kama kuna uwezekano wa kubadilisha tija ya kilimo chetu kwa kuondoa kodi kwenye teknolojia (Machines, Computing hardware and software) za kilimo zinazoingizwa nchini. Dunia imeshabadilika sana kwenye kilimo, na teknolojia ndiyo inaoendesha uzalishaji. Sina uhakika kama kiwango cha teknolojia kinachoendesha kilimo chetu kipo katika viwango vinavyotakiwa ili kuwe na tija.
Mchango wako ni mzuri but unakumbuka kipindi cha JK alikuwa anafanya hizo mambo za tax holiday watu waliishia kusema hakuna anachofanya anapendelea wafanyabiashara mara hakusanyi kodi nk

Kumbuka kuna hatua za mda mfupi,Kati na mrefu ukifanya vyote kwa pamoja utaacha pengo kubwa la fedha jinsi ya kufidia ndio mziki maana hadi uje upate tija sio leo au kesho it takes time ndio maana serikali zinasita kufuta au kupunguza VAT nk
 
Ummy, Waziri wa maji, Mkenda, Afya, Elimu, Uchumi, Barabara, na Madini.

Bila shaka kwenye reshuffle ya Waziri wa Ulinzi kuna watu watawekwa pembeni.

Hata Rais wa Malagasy kavunjilia mbali Baraza la mawaziri na Rais wa Tunisia kafutilia mbali Bunge na Serikali.

Mh. SSH kama Hawa hawana msaada futilia mbali anza upya ni kawaida tuu hiyo. Ukikuta wanaume wanakuletea ujinga piga pembeni weka Wamama kama kwa Kagame, Museveni na Msumbiji.
Sina tatizo na ushauri wako kwa mama, nina shida na paragraph yako ya mwisho kuhusu Kagame, M7 na huyo wa Msumbiji; nikwambie tu kitu, marais wengi ukiona wanaweka wanawake wengi kwenye mabaraza yao ya mawaziri, hua wana u fool ulimwengu kwamba wao wanapenda ku balance gender but the truth is, hawapendi challenge kutoka kwa wanaume wenzao. Na ndio maana karibu marais wote wanao fanya hayo hua wana elements nyingi za udikteta
 
Tarehe 13 mwezi August mwaka 1990 magazeti yote ya Tanzania yalikuwa na vichwa vya habari vilivyohusu kujiuzulu kwa baraza la mawaziri jana yake yaani tarehe 12.

Taarifa hizo zilisema kuwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais mzee Ally Hassan Mwinyi aliwaambia mawaziri wote wakiongozwa na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, Joseph Sinde Warioba kwamba, wajiuzulu na warudi makwao na wampishe atengeneze baraza jingine la mawaziri.

Taarifa hizo zileendelea kutaarifu kuwa Rais Mwinyi alisema kuwa shughuli zote za baraza la mawaziri zingekuwa chini ya makatibu wakuu wa wizara.

Baraza hilo pamoja na mzee Warioba lilikuwa na waziri wa Fedha Cleopa Msuya, waziri wa serikali za mitaa Paul Bomani rip, waziri wa mambo ya Nje Benjamin Mkapa rip, na mzee Rashid Mfaume Kawawa rip ambae alikuwa waziri asie na wizara maalum.

Wengine ni mzee Al Noor Kassum rip ambae alikuwa waziri wa madini na nishati, Jackson Makweta rip waziri ofisi ya Rais(Ulinzi) na mzee Muhidin Kimario rip ambae alikuwa waziri wa mambo ya Ndani.

Hawa mawaziri ni baadhi ya mawaziri wa serikali hiyo ambayo iliundwa mawaziri 26 na manaibu waziri 14.

Kama kawaida mawaziri waliwasili Ikulu siku hiyo kwa mkutano wa baraza la mawaziri ambao ungechukua hadi masaa matatu.

Kwa mshangao wao kikao hicho kilichukua dakika tatu tu pale Rais Mwinyi alipotamka kwamba anataka mawaziri hao wote wajiuzulu na warudi makwao.

Waziri wa mambo ya nje, mzee Mkapa(RIP) alichanganyikiwa na kumwambia Rais kuwa alikuwa tayari ana "engagement" za mikutano Ulaya na akaambiwa "Cancel it".

Wakati hayo yote yakifanyika mwenyekiti wa CCM hayati baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa angani akielekea Rome nchini Italia.

Mwalimu pamoja na kuongea sana na siasa thabiti, moja ya udhaifu wake ulikuwa ni kutowachukulia hatua mawaziri ambao walikuwa wanamuangusha kwenye idara ya kuwajibika na ufisadi.

Kuna kipindi hayati Mwalimu aliwahi kutembezwa maeneo ya Msasani na Mikocheni na kuonyeshwa nyumba za baadhi ya mawaziri wake na alifahamu walipata kiasi gani cha mshahara kulinganisha na majumba aloyaona lakini alibakia kushangaa.

Hivyo mzee Mwinyi akiwa anaelewa hayo alimfuata hayati Mwalimu uwanja wa ndege kabla hajatimkia Rome na kuhakikisha ameondoka kabla ya kurudi Ikulu na kuchukua maamuzi hayo magumu.

Hayati Nyerere alipofika Rome na kupokelewa na vijana wa pale wakampasha habari za Dar-es-Salaam na akashangaa kweli, ila kimoyomoyo alishukuru kuona angalau Mwinyi ameweza.

Baadae, Rais Mwinyi akiongea na vyombo vya habari alitoa sababu za msingi za kuwataka mawaziri wake wote wajiuzulu na akasema kuwa ni vitendo vya rushwa na kutowajibika kwa mawaziri kulikokithiri khasa katika wizara zao.

Alitoa mifano ya wachuuzi kuombwa kitu kidogo pale walipotaka haki zao na hata wastaafu hali ilikuwa ni hiyohiyo, na hata kuambiwa "njoo kesho, njoo kesho".

Msemo wa njoo kesho ulikuja kupata maarufu baadae pale ulipotumika kukemea vitendo vya rushwa na ufisadi na hata kutungwa wimbo wa FAGIO LA CHUMA KUWAKUMBA WALE WASOWAJIBIKA.

Huku kukiwa na shauku ya kutaka kufahamu baraza jipya la mawaziri laja, wananchi walianza kuvumisha kuwa kutakuwa baraza jipya kabisa lenye sura mpya, lakini wakikatishwa tamaa pale mzee Joseph Sinde Warioba alipotangazwa ndiye waziri mkuu anaeendelea.

Si kwamba Mzee Warioba nae alikuwa ni fisadi au mla rushwa lakini wananchi walitegemea Rais Mwinyi angebadilisha kila kitu na kuanza upya "once for all" au "the beginning of new chapter".

Hivyohivyo kwa baraza la mawaziri mawaziri saba walipoteza nafasi zao Al Noor Kassum, Aaron Chiduo, Muhidin Kimario, Damian Lubuva, Chrisant Kissanji, Arcado Ntagazwa na mama Getrude Mongela.

Mzee Mwinyi akatolea mfano wa yeye mwenyewe akiwa waziri wa mambo ya ndani ilibidi ajiuzulu pale yalipotokea mauaji yasiyoeleweka kule Shinyanga ambapo polisi walihusika na mauaji yale.

Lakini uamuzi wa mzee Mwinyi kuwataka mawaziri wake wajiuzulu haukutoka bure bali kuliktokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na kamati kuu ta CCM au CC kama inavyojulikana na kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mwalimu iliabaini taasisi na wizara zipatazo 12 ndizo zilikuwa na shida.

Wizara ya sheria, mambo ya ndani, wizara ya afya na wizara ya ardhi zilisemwa kuwa hali ya rushwa na ufisadi ilikuwa imefikia kiwango cha juu.

Mwalimu akaamuru wahusika wote ambao ni mawaziri wafike kwenye kikao cha kamati kuu lakini uamuzi huo ukapigwa chenga na mawaziri khasa mzee Kimario wakaamua kujiuzulu kuliko kwenda kwa CC kujibu masuali ya Mwalimu na wajumbe.

Ila tatizo kama kawaida likajirudia na mzee Mwinyi akawarudisha mawaziri wake waandamizi kama Mkapa, Msuya, na wengine akawabadili wizara.

Ila kukaja sura mpya kama mzee Nalaila Kiula ( kukawa na kichwa cha habari kilochosema "Nalaila Kiula aula"), mazee Jakaya Mrisho Kikwete akawa waziri wa nishati, madini na maji, Charles Kabeho (elimu).

Akijitetea raisi Mwinyi akasema hakutaka kubadili baraza zima kwa sababu ilibakia miezi minne kabla ya kuvunja bunge kwa ajili ya maandalizi ya uchuguzi mkuu.

Hata hivyo raia Mwinyi aliagiza kuwepo uwajibikaji, kuondoshwa kwa vitendo vya rushwa, kupunguza safari za nje na semina zisizoeleweka.

Kuhusu balozi zetu nje, akaagiza kuwepo balozi na msaidizi wake mmoja tu na kila mwezi atakuwa akifanya mikutano na wananchi.

Wananchi wenye shida mbalimbali za ardhi, mikopo, mafao na kesi kucheleweshwa zote raisi Mwinyi alikuwa akizishughulikia mwenywe na wasaidizi wake pale CCM Lumumba.

Hata kule Zanzibar raisi Idris Abdul Wakil nae alifanya hayo na kukutana na wananchi kusikiliza shida zao na aliwaita polis, maofisa wa wizara na CCM kujibu masuali kadhaa.

Ninachotaka kusema ni kwamba matatizo ya nchi yetu hayakuanza leo na wala hayataisha leo.

Tunahitaji viongozi wetu kujituma na kufanya maamuzi khasa ya kuokomboa nchi yetu kiuchumi.

Raisi aweza kufanya mabadiliko ya hapa na pale katika baraza lake la mawaziri lakini tatizo lipo kwenye mfumo wote na khasa kule chini ambako mkurugenzi wa maendeleo au afisa mtoza ushuru ana uwezo wa kukwapua fedha za umma na kujilimbikizia mali bila kugundulika mapema.

Serikali itengeneze mifumo sahihi iliyo na ufanisi na uelevu wa kubaini wizi na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Raisi aliepo sasa asimwonee mtu aibu, kama kuna waziri hawajibiki ipasavyo apishe na kama ni baraza zima ( kwa Tanzania Bara) halielewi linafanya nini liondolewe na aanze upya hadi 2025.

Kama serikali yenyewe wapo madarakani kwa wizi wa kura, unategemea uwajibikaji utoke wapi!?
 
Back
Top Bottom