Mzee Aboud Jumbe Mbona uko Kimya Sana ?

Wakuu.
Hivi tunaposema yuko kizuizini tuna maana kuwa yuko Gerezan ama ?
Mimi sielewi kabisa aisee

Kuwekwa kiuzini kwa Mzee Jumbe ni kitendo cha Nyinyiemu kutomshirikisha kwa lolote kwenye historia ya nji hii.
Bila kujalinafasi zake alizoshika.
 
Mzee jumbe hayuko kizuizini, Yuko Mjimwema Kigamboni, unaweza kwenda ila ni Mzee sana anaongea kama cassette inakula mkanda pia anawatambua watu wa familia yake kwa sauti! Anakiti cha matairi huwa wanatumia kumtoa nje na kumrudisha ndani.

Bado yuko kizuizini, manake hawajakausha tangu Lissu afunguke, mengine yote wamemjibu pale bungeni.
 
Hii inamaana gani FF?
Kuwa yuko Gerezani ama ?
Watu wanaposema kizuizini wana maanaisha nini ?

Kuwekwa kizuizni na Serikali kunaweza kuwa na maana nyingi, amma usiongee in public, amma usitoke nje ya sehemu ulizopangiwa, amma usisafiri zaidi ya sehemu ulizopangiwa, amma usinane na fulani fulani na fulani. Kizuizini inaweza kuwa na namna nyingi ya vizuizi.

Bedridden inamaanisha, ni mtu anaesumbuliwa na matatizo a kiafya aina moja ama nyingine yanayomfanya muda mrefu awepo kitandani.

Unaweza kuwa bedridden na upo kizuizini.
 
Mzee jumbe alishamaliza kila kitu..sasa hivi anaona kama marudiao tu
 
Wakuu JF Amani iwe Nanyi.


Tunapozungumzia katiba Mpya katika kipindi hiki ambacho Serikali 3 haziepukiki.
Binafsi nimekuwa nukijiuliza sana ni kwanini Mzee Aboud Jumbe Yuko Kimya sana.


Hii ni Seheme ya Wasifu wa Mzee Aboud Jumbe Kutoka Wikipedia



Inasemekana kuwa hata wazo la kuunga TANU na ASP Lilikuwa ni la huyu Mzee.
Huyu Mzee inasemekana kuwa alisalitiwa na Maalim Seif pale alipokuja na wazo la Serikali 3.
Si Mpango wangu kujadili issue ya Maalim Seif, Lakini kwa wanaojua Siasa za Tanzania wanajua kuwa hata Maalim Seif Baada ya kupewa Mikoba ya Uwaziri Kiongozi, haikumchukua muda kuyaona na kuyashuhudia yale Mzee Jumbe alikuwa ameyaona, hii ilipelekea hata Maalim kuwekwa kizuizini na kuachiwa wakati almost nchi iko kwenye Mfumo wa vyama vingi na kujiunga na CUF kuendeleza Mapambano.
Sasa kwa kuwa Maalim anasimamia yale Mzee Jumbe aliyoyaona, hivi hatuoni kuwa ni wakati Muafaka sasa wa Mzee Jumbe kutoa Maoni yake.
Naandika post hii nikiwa na imani kuwa Mzee Jumbe yupo buheri wa Afya.

cc Barubaru , zanzibar huru, Mzee Mohamed Said , Bobwe
\

Msimamo wake upo katika kitabu chake alichotunga kuhusu muungano wenu.

Wewe fanya jitihada ukisome utamfahamu vizuri sana.

Pole sana

 
Back
Top Bottom