Mimi ni mmoja wa watoto waliotungwa mimba wakati mzazi bado ananyonyesha, bahati mbaya aliyenitangulia alifariki dunia kabla sijazaliwa. Hivyo wakati nakua niliambiwa na majirani kuwa kutungwa kwangu mimba kulisababisha afya ya dadangu kudhoofu na kupelekea kifo.
Hili suala ni kweli au vihoja na vijambo vya walimwengu.
RIP dada yangu Koku.
Hili suala ni kweli au vihoja na vijambo vya walimwengu.
RIP dada yangu Koku.
- Tunachokijua
- Kunyonyesha ni ulishaji wa watoto wadogo kwa maziwa kutoka kwenye titi la mama. Wataalamu wa afya wanapendekeza kunyonyesha kuanzia saa ya kwanza ya maisha ya mtoto na kuendelea, mara nyingi na kwa kadiri mtoto anavyotaka.
Inashauri mtoto kunyonya miezi 6 ya kwanza bila kupewa chakula au kinywaji kingine na baada ya hapo anyonye huku anapewa vyakula vingine kwa takriban miaka 2. Wataalam wa afya wanasisitiza kunyonyesha maziwa ya mama, kuwa yana faida kubwa ya virutubisho ambavyo kwenye maziwa ya fomula hakuna.
Hata hivyo huenda wakati mama ananyonyesha yawezekana akapata ujauzito mwingine kabla ya mtoto anayenyonya kufikia muda wa kuachishwa kunyonya. Kutokana na hali hiyo imekuwa ikisemwa kuwa mtoto anatakiwa kuachishwa kunyonya kwa kuwa atadhoofika kiafya.
Jamiicheck imefuatilia iwapo ni kweli mama anayenyonyesha akipata mimba mtoto hudhoofu kiafaya.
Uchunguzi wa kitaalamu unaonyesha kwamba hakuna madhara kwa mwanamke kuendelea kumnyonyesha mtoto mchanga iwapo atajikuta amepata ujauzito
Pia Jamiicheck tumezungumza na mtaalamu wa afya, Dkt. Godfrey Chale, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ambaye ameeleza kuwa:-
Mama anayenyonyesha akipata ujauzito anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto kama kawaida na Mtoto anayenyonya hatapata madhara yoyote kiafya, muhimu ni mjamzito kuzingatia lishe nzuri ili mazima yaendelee kutoka.
Miaka ya zamani Wanawake wengi walikuwa wananyonyesha Watoto muda mrefu hadi wanapofikisha miaka miwili tofauti na sasa hivi, hivyo Wazee wetu waliwaaminisha watu kuwa Mwanamke anayenyonyesha akipata ujauzito basi mtoto anayenyonya afya yake itadhoofika, hilo si kweli kitaalam.
Nadhani waliwaambia hivyo ili kutengeneza mazingira ya Wamama kupata muda wa kupumzika na mwili kujijenga vizuri kabla ya kupata ujauzito mwingine.
Kitaalamu mjamzito anaweza kuendelea kunyonyesha kama kawaida hadi miezi mitatu ya mwisho, ukifika muda huo akaacha, maziwa yatakata kisha yataanza kujitengeneza upya kwa ajili ya mtoto anayetarajiwa kuzaliwa akute yakiwa ‘fresh’.
Kutokana na wataalau wa afya kuthibitisha kutokuwepo kwa madhara kwa mtoto atakaeendelea kunyonya wakati mama yake akiwa na hali ya ujauzito ni muhimu mtoto anyonyeshwe ili anedelee kupata virutubisho muhimu kwa mtoto vinavyopatikana ndani ya maziwa ya mama huku mama akiendelea kupata lishe boora ili kulinda afya yake na ya mtoto