My Political Analysis on Jambo Leo: Unaweza Kuudanganya Umma kwa Muda Mfupi tu, Sio Wakati Wote!

CHADEMA ni chama cha wachaga hata iukiseamaje hauwezi kuheshimika , kinachoheshimika ni Fedha tu ndio maana mzee wa kichaga mwanaeakiwa na fedha anamuamkia SIKAMOO MWANANGU , SIKAMOO SA KASI , kwa hiyo hapa hapendwi mtu bali fedha , fedha ikionekana popote pale inatafutwa hata kama kuna hatari.

Na kama kuna mtu atataka kuvuruga dili lazima atokomezwe. Wazee mpo hapo!!!
 
Chadema ni chama Kikuu cha Upinzani nchini kinachoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mbunge na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, kilianzishwa Mwaka 1992 na Muasisi wake Mkuu aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu na Waziri wa Fedha Mzee Mtei kwenye miaka ya 70. Kwenye Uchaguzi wake wa kwanza chama hicho kilifanya vibaya sana kwenye chaguzi zote kuanzia Urais ambako kilipata Asilimia 3 tu ya kura zote zilizopigwa, Wabunge 4 tu kati ya Wabunge 269 wa Jamhuri na kikashika Manispaa 75 tu kati ya Manispaa 1500 za taifa hili.

Hapo ndo umemaanisha nini ndugu mwandishi? Naona kama kuna makosa au macho yangu yanaukungu?
UNAWEZA KUUDANGANYA UMMA KWA MUDA MFUPI LAKINI SIO WAKATI WOTE.

Chadema ni chama Kikuu cha Upinzani nchini kinachoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mbunge na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, kilianzishwa Mwaka 1992 na Muasisi wake Mkuu aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu na Waziri wa Fedha Mzee Mtei kwenye miaka ya 70. Kwenye Uchaguzi wake wa kwanza chama hicho kilifanya vibaya sana kwenye chaguzi zote kuanzia Urais ambako kilipata Asilimia 3 tu ya kura zote zilizopigwa, Wabunge 4 tu kati ya Wabunge 269 wa Jamhuri na kikashika Manispaa 75 tu kati ya Manispaa 1500 za taifa hili.

Toka kuanza kwake historia ya chama hiki ni kwamba kimekuwa na tabia ya kukwepa sana Demokrasia na Ukweli wa kisiasa kwa maana ya haki kwa wote wanaoshiriki katika chama hicho kuanzia Wananchama wake mpaka Viongozi wake wa juu na wa chini. Kwa mfano Muasisi huyo wa Chadema aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho alipoamua kupumzika Uongozi huo alipokewa na Mwenyekiti mpya Marehemu Bob Makani, aliyewahi kufanya naye kazi Benki Kuu ya Taifa na ambaye pia alikuwa ni Shemeji yake yaani mtu aliyemuoa Dada wa damu wa Muasisi huyo. Muda wake ulipoisha Mwenyekiti huyu mpya alipokewa na Mwenyekiti mpya Kijana lakini pia aliyewahi kufanya kazi Benki hiyo kuu ya Taifa na ni mkwe wa Muasisi huyo wa Chadema kwa maana ya kuwa ameoa mtoto wa kike wa Muasisi huyo Mzee Mtei.

Ni historia inayotakiwa kuleta maswali mengi sana miongoni mwa wanachama na wafuasi wa Chadema kuliko majibu, lakini kwa maajabu makubwa sana chama hicho kimefanikiwa sana kuwaaminisha wanachama wna wafuasi wake kwamba ni chama cha Demokrasia Makini sana kuliko vyama vingine vyote nchini na hasa chama tawala CCM. Haingii akilini hata kidogo kwa mtu mwenye akili timamu kama mimi kwamba kila Kiongozi Mkuu wa chama hicho toka kianzishwa ni lazima awe na uhusiano wa undugu na Muasisi wa chama hicho na hata pia kuwa lazima awe amefanya kazi Benki Kuu ya Taifa aliokokuwa akifanya kazi Muasisi huyo.

Wananchama na wafuasi wa Chadema hivi ni kweli wanaamini kwamba hayo yote yalitokea tu kwa bahati mbaya au nzuri kwamba Viongozi wao wote wakuu kuwa na ukaribu wa kiundugu na kikazi na Muasisi wao au kuna namna nyingine iliyokuwa ikifanyika kwa kutayarishwa mapema na wao kuja kuhalalisha tu kwenye vikao kitu wasichokujiua? Mwalimu Baba wa Taifa hili aliwahi kusema kwamba "Ukweli una tabia mbaya sana, ukiminywa huwa una tabia ya kurudi na adhabu kwa wahusika" na ndicho hasa kinachotokea sasa hivi katika chama hicho hatimaye ukweli umeanza kurudi kwa kasi na adhabu ya ajabu sana.

Ukweli kwamba ndani ya Chadema kuna tatizo sugu la ukiukwaji wa Demokrasia toka kilipoanza, ulianza kujitokeza Mwaka 2008 wakati Makamu wa Mwenyekiti wa Chama hicho wa wakati huo ambaye sasa ni Marehemu, alipoanza kuuuliza Uongozi wa juu wa Chama hicho kuhusu ukweli wa Demokrasia katika chama hicho. Kukatokea matatizo makubwa sana mpaka kupelekea maswali mengi kuhusiana na kifo chake kilichomtokea katika kipindi hicho hicho huku akiwa amesimamishwa uongozi Julai Mwaka 2008. Maswali ya msingi kuhusiana na mwenendo wa Demokrasia ndani ya Chama hicho aliyokuwa ameyauliza yakaishia kwenda naye kaburini.

Kwenye uchaguzi wa Taifa Mwaka 2005 chama hicho kikaongeza Wabunge na kufikia 11, Manispaaa 103 tu, ingawa kwenye uchaguzi wa Mwaka 2010 kikionekana kukubalika sana na wananchi hasa Vijana na wasomi nchini kikajiongezea Wabunge hadi 48, Asilimia 27 ya Kura za Urais na Manispaa 467. Chadema kikawa sasa ni chama kikuu cha upinzani nchini huku Viongozi wake wakuu wa Taifa wakijipambanua mbele ya umma kuwa ni wasafi wasio na madoa kama vile Viongozi wengi kama sio wote wa chama Tawala CCM.

Tarehe 15/9/2007 wakaenda mbali na kulisimamisha taifa zima na tuhuma zao mpya nzito kwenye Mkutano wao wa kihistoria pale Mwembe-Yanga wakataja majina ya Viongozi wa Taifa wa CCM 12 waliodai kwamba ni hatari sana na ndio maadui wakubwa wa Taifa kutokana na kujihusisha sana na Rushwa katika nyadhifa zao na miongoni mwa waliowataja ni Viongozi wawili Waheshimiwa Rostam na Mkono ambao wote walikuwa Wabunge wakati huo na Mkono bado ni Mbunge mpaka leo. Akizungumza baada ya Mkutano huko Mbunge wa Chama hicho Mnyika alifafanua zaidi na kusema kwamba Ilani ya Chama hicho ipo wazi sana na ishu ya Ufisadi na Rushwa kwa waliotajwa na kwamba iwapo Chadema itashika Dola basi ndani ya siku 180 viongozi hao 12 waliotajwa watafikishwa mahakamani pamoja na hukumu watakayopewa na mahakama, Serikali yake itatifisha mali zao mara moja ambazo chama hicho kina uhakika mkubwa sana kwamba zimeptikana kwa njia za kifisadi kwa maana ya wizi na Rushwa. Na majuzi Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Mheshimiwa Zitto, alipoanza mbio kama zile za Marehemu Chacha Wange Makamu wa zamani wa Mwenyekiti wa Chama kutaka kujua ukweli kuhusu Demokrasia ndani ya chama hicho Uongozi wa juu wa chama hicho ukarudia tabia yake ile ile waliyomfanyia Marehemu Wangwe ya kumshambulia kila kona na Kumsimamisha uongozi wa chama hicho na safari hii wakenda mbali sana na kuanza kumuita pandikizi, mamluki, mhaini na msaliti.

Nyimbo hizi za Usaliti wa Zitto zikafikia kilele hivi karibuni wakati Mwanasheria Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge kupitia chama hicho alipopasuka mbele ya umma kwa hasira sana kwamba Mbunge huyo wa Kigoma mjini sio kwamba ni msaliti tu bali amepokea rushwa kutoka kwa Viongozi wawili wa CCM Rostam na Mkono huko siku za nyuma, ili kukihujumu chama hicho hasa kwenye jimbo la Musoma Mjini jimbo ambalo ni la Mheshimiwa Mkono. Zitto akajibu tuhuma hizo haraka sana kwa kumwita Mwanasheria huyo kifaranga wa siasa yeye yupo tayari kusimama na Mwenye kifaranga lakini sio kifaranga akimaanisha mtoto mdogo kisiasa ndani ya chama hicho kwa sababu alitakiwa kujua madhambi mengi ya Mwenyekiti wake wa sasa yanayohusiana na kupokea rushwa kutoka kwa Viongozi hao wawili. Hakuna mahali Zitto alipokataa kuhusika na kupokea rushwa kama alivyotuhumiwa lakini na yeye akavunja ukimya na kutoboa siri nzito ya rushwa dhidi ya Mwenyekiti wake ambaye kwa kuyaelewa maelezo yake ndiye anayemtuma Mwanasheria huyo kumshambulia Mbunge huyo maarufu sana na kijana anayekubalika sana na wananchi wa Mkoa wake wa Kigoma.

Kwa mshituko mkubwa sana Mwenyekiti wa chama ambaye naye ni Mbunge pia na Kiongozi wa Upinzani Bungeni akamjibu Naibu Katibu Mkuu wake kwa njia ya vyombo vya habari akijisalimisha mbele ya umma kwamba usimuhukumu kwa kupokea pesa hizo toka kwa Viongozi hao wa CCM ambao chama chake kiliwatuhumu Mwembe Yanga kuwa ni maadui wa Taifa kwa ufisdadi wao, bali wamuhukumu kwa kuangalia nia yake katika kuzipokea. Lakini Zitto hakuishia hapo tu bali akasema na sababu za Mwenyekiti huyo kupokea rushwa hizo toka kwa Viongozi hao wawili wa CCM, kwamba ilikuwa ni pamoja na kuwazuia Chadema kutogusa jimbo la Musoma Vijijini ambalo ni Mh. Mkono. Watafiti wa siasa kama mimi tukaanza kufuatilia rekodi ya tuhuma hizo kwa makini sana katika kutafuta ukweli wa tuhuma za Zitto.

Nilichogundua ni kwamba Chadema iliwahi kupeleka "Operation Sangara" ilipoanza tu Mwaka 2008 Mkoani Musoma katika Wilaya zote za Mkoa huo lakini katika mazingira ya ajabu sana Operation hiyo haikugusa Wilaya ya Mbunge Mkono yaani Musoma Vijijini, na hata Chadema tena walipokwenda na "Operation M4C" wakarudia tena kwenda kila Wilaya ya Mkoa huo lakini ilipofikia zamu ya kwenda Musoma Vijijini Viongozi hao wa Taifa wakaishia kwenda kutembelea kaburi la Baba wa Taifa kijiji cha Butiama.

Sasa, kwa akili ya kwaida ya kuambiwa na kufikiria ni dhahiri kwamba Zitto anaonekana kuwa na hoja ya kimsingi hapa kuliko wanaomtuhumu ndani ya Chadema, kwa mfano Mheshimiwa Mkono amekuwa Mbunge kwa vipindi vitatu sasa na mara zote amegombea bila upinzani wa Chadema kabisa na kuzidi kuhalalisha tuhuma za Zitto kwa Mwenyekiti wake kwamba amekuwa akipokea rushwa kutoka kwa Mkono ili asiiguse kabisa Wilaya ya Musoma ya Vijijini ya Mbunge huyo. Na hapa ndipo utimilifu wa ule usemi "Unaweza kuwadanganya watu kwa muda mrefu sana, lakini sio kwa wakati wote" kwamba vyama hivi vya Upinzani kuwa ni Nyoka wa hatari sana kwa Taifa kuliko hata waliowaita mafisadi.

Kiongozi wa kwanza Upinzani kunaswa na mtego kama huu alikuwa ni Mchungaji Mtikila huko siku za nyuma, akiwa juu sana katika siasa za Taifa hili na akiwashambulia sana waliotajwa kwenye listi ya Ufisadi na Chadema ndipo ikatokea habari kwamba yeye binafsi amewahi kupewa Shllingi Millioni Tatu kama mkopo kutoka kwa mmoja wa Viongozi hao mafisadi yaani Mh. Rostam ambazo mapaka habari inatoka kwa umma alikuwa hajalipa na wala hakuonyesha dalili za kuzilipa. Ukawa ndio mwanzo na mwisho wa kisiasa wa Kiongozi huyo kwamba haiwezekani ukamshambulia Kiongozi wa CCM mbele ya umma mchana kwenye majukwaa kwamba ni shetani halafu usiku wewe huyo huyo ukamfuata kiongozi yule yule na kupokea pesa zake ili kukupunguza spidi na bado ukadai uhalali wa uongozi wa kisiasa katika jamii hii hii ni dhambi kubwa sana kama sio kisiasa basi hata kwa Mungu haikubaliki na vitabu vya dinia vipo wazi sana.

Chadema hatimaye inavuna ilichopanda yenyewe siasa za chuki, unafiki na magomvi kurushia mawe na kuwazomea viongozi wa Taifa wa CCM pamoja na kuwarushia matusi kwenye simu zao na mitandao kama walivyowafanyia Masikini Spika wa kwanza Mwanamke wa Bunge letu la sasa na Kijana mdogo sana Naibu waziri wa Mawasiliano walipojifanya mbele ya umma kutoridhika na matendo yao na huku wakijua wazi katika nafsi zao kwamba walikuwa ni waongo na wanafiki wakubwa kwa sababu hata matendo yao ndio haya ya kuvaa ngozi ya kondoo mchana na usiku kuwa kama walivyo yaani Nyoka wa hatari sana.

Tunashuhudia matunda ya mbegu zao mahakamani wanapokwenda kusikiliza kesi zao na Zitto, wanapigana wanarushiana mawe michanga mpaka matofali ni mara ya kwanza taifa hili la amani Duniani kujionea mambo ya kihuni kama haya yakitendeka mbele ya macho yetu. Ni mahakama hiyo hiyo wameshitakiwa wahaini wakati wa Awamu ya kwanza, Mahakama hiyo hiyo wameshitakiana Wabunge wa CCM kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wao lakini Miaka 52 ya Uhuru wetu hii ni mara ya kwanza tunajionea vitendo vya kihuni vikifanywa na wafuasi masikini wa akili wa wa Viongozi hawa ambao wote ni wapokea rushwa usiku kutoka kwa Viongozi wale wale wanaowatukana mchana. Kumbe Viongozi wa Chadema sio waadilifu na wana bei ya vichwa vyao, sasa inaanza kuingia akilini ni kwa nini Chadema huwa haiwagusi baadhi ya Viongozi wa Taifa hili wanaotuhumiwa sana kuhusika na rushwa au ukosefu wa maadili ya uongozi wa juu.

Kwa mfano, baada ya kutangaza majina 12 ya mafisadi pale Mwembe-Yanga walfanya Mkutano mwingine mkubwa kama ule Mkoani Tabora na kwa maajabu makubwa kabisa kuna majina machache kati ya yale 12 ambayo hawakuyarudia kuyataja tena kwenye umma sasa ndio inajisema wazi kwamba kumbe walikuwa wakitumia njia maarufu sana kwenye siasa za Magharibi inyoitwa "Carrot and Stick" ikiwa na maana ya Karoti na Fimbo, yaani upande mmoja unamchapa Kiongozi mbovu na fimbo na mwingine unamgusa gusa na karoti kwa kupokea pesa zake chafu kwenye giza.

Ni hawa hawa Chadema wameanzisha maandamano ya ajabu nchini na kuwashawishi wananchi kuwaunga mkono na wakati mwingine kuwahamasisha kuvunja sheria za maandamano na kuishia kupoteza maisha yao na wao wakiwa wa kwanza kukimbilia kwenye mazishi ya wananchi wanyonge wasiojua kitu waliopoteza maisha yao na ndugu zao kwa kuwasikiliza viongozi hawa wanafiki wakubwa na wala sio siri hatari sana kwa Taifa letu sio kwa Upinzani tu.

Kwa muda mrefu sana sasa Chadema wamekuwa wakilia lia sana kwa umma kwamba CCM inatumia Usalama wa Taifa kuwasambaratisha na wananchi wafuasi wa chama hicho mambumbu wamekuwa mstari wa mbele sana kuamini uongo huo ndio maana kwenye hotuba yake moja hivi karibuni Rais Kikwete aliwafananisha viongozi hao kuwa sawa na wamiliki wa viwanda vya kutengeneza uongo. Halafu bila hata ya aibu mpaka leo bado hata Muasisi wao anasimama mbele ya umma na kudai Zitto ni msaliti hatakiwi tena ndani ya chama hicho kwa sababu alipokea magari mawili toka kwa Mbunge wa CCM Mkono, lakini Muasisi huyo hasemi lolote kuhusu mkwe wake, yaani mtu aliyeoa mtoto wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema na aliyekubali mbele ya umma kwamba tatizo sio kwamba kwa nini alipokea pesa toka kwa Mafisadi, bali ni alizipokea kwa sababu gani na hasa kwa nia gani! Aibu ya mwaka kwa chama ambacho wakati mmoja Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM alipowatuhumu kupokea pesa toka nje ya nchi ili kuvuruga amani nchini walimtishia mpaka kumfikisha mahakamani, lakini hatujawasikia wakimstishia kumepeleka mahakamani Zitto kwa kumtuhumua Mwenyekiti wao kupokea pesa za rushwa kutoka kwa Rostam na Mkono.

Taifa la Tanzania tunawalipa Chadema ruzuku ya Shillingi Billioni Tatu kwa Mwaka yaani Shillingi Millioni 254 kwa kila mwezi ili kufanya siasa za kukosoa CCM chama tawala, lakini leo wananchi wa Taifa hili kwa kupitia Kamati ya bunge na mujibu wa Sheria ya Jamhuri tumewadai kuona uhalali wa matumizi ya pesa hizo kitu ambacho ni cha kawaida sana Duniani majibu yao ni aibu sana, kwamba Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wao Zitto ni msaliti kwa nini hakuwaambia mapema kwa siri kwamba kamati hiyo ina huo mpango ili wajitayarishe mapema.

Sisemi CCM ni chama kikamilifu, hapana na ndio maana kwa kujua mapungufu yake mengi ikakubali kuruhusu Upinzani nchini pamoja na kwamba wananchi kwa Asilimia 80 wa hili taifa walikataa kata kata kuingia kwenye siasa za upinzani. Chadema wamekuwa wakijitangaza kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hasa uadilifu wake kwa Taifa, kumbe ni unafiki na uongo wa hali ya juu sana kwa wananchi wasiowajua kwa undani na ajabu kuwa ni kwamba hata sasa ambapo ukweli umeshajitokeza wazi kwamba ni genge la wahuni tu wachumia tumbo bado kuna mamluki wanaowashangilia na kuwatetea hasa kwenye mitando ya kijamii kama vile wamepungukiwa na akili. Chadema mlipaswa kujua kwamba uongo una siku zake za mwisho zikifika hauna msalie mtume wala huruma, yanayowakuta sasa hivi ni mbegu za kinafiki mlizozipanda wenyewe yanayowakuta sasa hivi hayana uhusiano wowote na Usalama Wa Taifa kama ambvyo mmekuwa mkilia lia sana kwamba ndio wanaowasmbaratisha mnajisambaratisha wenyewe na tamaa mbele mauti nyuma.

Tanzania tumechoshwa sana na siasa uchumia tumbo zinatuvuruga Taifa zinaturudisha nyuma sana kimaendeleo, zinaturudisha sana nyuma kisiasa na cha ajabu kuliko yote ni jinsi Viongozi hao wakuu wa huko Chadema wanavyozidi kunga'ng'ania madaraka na kusingizia wengine kuwa ndio mamluki, wasaliti, mapandikizi na wahaini ingawa wote wao na wanaowatuhumu makosa yao ni yale yale kupokea rushwa.

Rais wa maarufu wa Marekani Bw. Ronald Reagan akiwa na hasira kali baada ya Ndege ya abiria yaNchi hiyo kupigwa bomu na kuua abiria wote 350 waliokuwemo kwenye ndege hiyo iliyoangukia nchini Uingereza, alisema "Unaweza kuudanganya umma kwa muda tu, lakini sio kwa wakati wote" akimaanisha waliohusika na bomu hilo ambalo baadaye ilifhamika kwamba ni Libya ndio iliyohusika na ikalipa fidia kwa familia za abiria na kukamatwa kwa afisa usalama wa Taifa hilo aliyehusika na kuwekwa kwa bomu hilo ndani ya ndege.

Ni wakati muafaka sasa Viongozi wa juu wa Chadema na hasa Mwenyekiti wa chama hicho wakajipima wenyewe kwamba baada ya haya yote kutulia hivi ni kweli bado watakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya wanachama na wafuasi wao na kuwaongoza? Watakaporudi Bungeni watasimama na kusema nini tena mbele ya hili Taifa ambalo majuzi tumeona Mawaziri 4 wakijiuzulu kwa makosa ambayo hayafikii ya kwao kwa ubaya kwa sababu wao sio waliohusika ila ni watendaji walio chini yao tu, tofauti kabisa na huko Chadema ambako ni Viongozi hao ndio waliopokea pesa za rushwa wao wenyewe sio watendaji wao kama hawa mawaziri 4 waliojizulu kulinda heshima zao na za chama chao ni wakati muafaka sasa Chadema nao wakijipima na kusimama wahesabiwe ili kulinda heshima ya chama chao ingawa sio siri kwamba wametuangusha sana wananchi wa Taifa hili na hasa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye wanadai sana kumuenzi uadilifu wake kumbe ni Kondoo wa mchana wanaivaa ngozi za o za chui usiku.

Chadema pia wajipime na kwenda kuwaomba radhi familia zote za wananchi waliopoteza maisha yao kwa kufuata maneno ya kichochezi ya Viongozi wao wa taifa ambao sasa siri wananuka sana na rushwa. Na mimi ninasema hivi Taifa tukiamua kufanya utafiiti wa kina kwa Viongozi wote wa Chadema, tutakuta madudu mengi sana na ya kutisha na hasa sasa hivi na hizi mbio za kuelekea kwenye uchaguzi wa Rais mwakani.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA

William J. Malecela
 
Article yk le mutuz ipo very bias, haipo std balanced, ipo kimajungu na kimapasho zaidi bro!
popote pale waasisi ni watu muhm hasa ktk ushaur ju ya nn chama kfanye ama kisifanye.
umemtaja mtei ju ya kupendekeza majina ya bob makan na mbowe na pia umeendelea kumcfia hayat baba wa taifa j.K nyerere kama icon ya tz ambay cdm knajfanya kufuata misingi yake.
bt hutak kukumbuka kuwa ni huyo icon ya tz hayat baba wa taifa mwl. nyerere ndiye alipendekeza jina ally hassan mwinyi kuwa mwnykt wa ccm na kuwa rais wa tz.
ni huyo icon ya tz hayat baba wa taifa mwl.Nyerere ndiye alimpendekeza w.B.Mkapa awe mwnykt wa ccm na rais wa tz na j.M.Kikwete afuate,na ndivo ilivokuwa.
ni huyo icon ya tz muasisi wa ccm alichomoa jina la baba yako J.S.Malecela ktk wawania urais na umwenykt ndan ya ccm na ilikuw hvo!
popote pale waasisi wanaheshmika kwa mawazo,michango km ina maslah kwa chama!
 
CCM siku hizi wamejaa online,wakisambaza propaganda.,ccm itauliwa na wataalam na wasomi wasioipenda,subiri upepelez unaendelea dhidi ya vigogo wa CCM utakapowaumbua wauza madawa ya kulevya,
 
Le Mutuz[/QUOTE]

Tunajua siku hizi hawa wote wanajifanya wakereketwa wa ccm wanapigania kusafirisha unga china, mabosi wao wawatumie kubeba sembe pole sana william thats y unatumia neno mamen lugha ya wala nawavuta bangi, siwezi hata kukuajiri kuwa konda kwenye daladala langu.
 
Ilitakiwa uwashauri ccm watuchie Lowasa wetu agombee uraisi maana 2015 tutakuwa na raisi kutoka kaskazini.Dr Slaa au Lowasa.
 
William unajua lowassa akiwa raisi atafanya na kushirikiana na chadema? Kalagha bao utarudi chamwino ukachunge ng'ombe wa samuel malecela maana huna makazi mahala popote mjini
 
Yaani kuna watu waliamini kabisa kwamba Mbowe ana lengo la kuingia na CHADEMA madarakani?

seriously?

Kwa Mbowe CHADEMA kuwa top opposition party ndio lengo...

ruzuku za kumwaga,influence na connections za business tele.....

deep down ndani ya moyo wake haamini wanaingia Ikulu..sio 2015
wala sio mwaka wowote ule.....

ndo maana wana mipango ya uchaguzi wa mwaka 2015 na mwaka 2020
tayari as if 2015 washajua CCM watashinda.....

Mbowe na Mtei hatimae ile family business now ina pay off....
this is it......

hayo ya kuingia Ikulu ni ya 'mashabiki'
na 'mashabiki' wa siasa hawana tofauti na 'mashabiki' wa Liverpool na Yanga...

Nimesema mara nyingi huyu dj Mbowe ni mtu mjanja mjanja tu na siyo mwanasiasa makini na kiongozi mzalendo anayetaka kuleta mabadiliko ya kweli nchini..calculation zote za mbowe kugombea Urais mwaka 2005, kumlazimisha Slaa 2010 na yeye kua mkuu wa upinzani bungeni yote ni kupata keki yake upande wa pili wa watawala.
 
Article yk le mutuz ipo very bias, haipo std balanced, ipo kimajungu na kimapasho zaidi bro!
popote pale waasisi ni watu muhm hasa ktk ushaur ju ya nn chama kfanye ama kisifanye.
umemtaja mtei ju ya kupendekeza majina ya bob makan na mbowe na pia umeendelea kumcfia hayat baba wa taifa j.K nyerere kama icon ya tz ambay cdm knajfanya kufuata misingi yake.
bt hutak kukumbuka kuwa ni huyo icon ya tz hayat baba wa taifa mwl. nyerere ndiye alipendekeza jina ally hassan mwinyi kuwa mwnykt wa ccm na kuwa rais wa tz.
ni huyo icon ya tz hayat baba wa taifa mwl.Nyerere ndiye alimpendekeza w.B.Mkapa awe mwnykt wa ccm na rais wa tz na j.M.Kikwete afuate,na ndivo ilivokuwa.
ni huyo icon ya tz muasisi wa ccm alichomoa jina la baba yako J.S.Malecela ktk wawania urais na umwenykt ndan ya ccm na ilikuw hvo!
popote pale waasisi wanaheshmika kwa mawazo,michango km ina maslah kwa chama!


makosa makubwa sana kumfananisha JK nyerere na Mtei..hamna mwanasiasa tz anakaribia kufikia political goodwill ya Nyerere, moja, mbili anachosema Le mutuz ni kua tofauti na Mwinyi, Mkapa ambao hawakua na uhusiano wowote binafsi na Nyerere kifamilia, kidini au kikanda, Mtei na Makani na Mbowe wako connected kifamilia zaidi yaani chama hakiamini mtu nje ya familia ya muasisi so far​
 
With all due respect regardless of the contents of your article, naapa! 'HII SI AKILI YAKO. UMEANDIKIWA'

- Kaka hii article nimeiandika jana Jumamosi Asubuhi sana baada ya kutoka Elements Club kwenye kujirusha, siku nikiandikiwa na mtu utakuwa mwisho wangu wa kuandika anything, ninazo article nyingi sana nilizowahi kuandika nikiwa nasoma ninaweza kuzitundika hapa labda ndio utaelewa kwa nini nilipokuwa Shule Wamarekani walikuwa wananililia nibadili Urais waniajiri kwenye mashirika yao ya ujajusi nikagoma kata kata,

- Wewe nakupa heshima kidogo kwamba unakubali ukweli wa maneno yangu ingawa ni kianina sana, saafi sana one page!!

Le Mutuz
 
melecela naona pesa ya lumumba iakupagawisha elfu tano inakutesa namna hii kuandika pumba

- Sherehe yangu majuzi ya kufungua rasmi blog imefgharimu mamilioni kaka, wachana na maneno ya kitoto, kata ishu nimeandika jibu ishu wachana na hizi haiwezi kulisaidia Taifa, by the way simu ya kwanza iliyoniamsha leo imepigwa kutoka Japan na mtu aliyesoma hii article akikubali kwamba kuanzia alipoisoma imembadili mawazo sasa hawaamini tena Chadema, so sim 150, nimepokea 120 wakisema nimewabadili mawazo na hii article, 20 wakinitukana na 10 hawana uhakika, so kwenye political science tunasema article imefanikiwa sana nia yake ya kuelimisha na kumsha watu usingizini!!

- Ndivyo inavyotakiwa kufanya mambo kisayansi sio kukurupuka tu!!

Le Mutuz
 

Tunajua siku hizi hawa wote wanajifanya wakereketwa wa ccm wanapigania kusafirisha unga china, mabosi wao wawatumie kubeba sembe pole sana william thats y unatumia neno mamen lugha ya wala nawavuta bangi, siwezi hata kukuajiri kuwa konda kwenye daladala langu.[/QUOTE]

- No thank u mamen ndio kwanza juzi nimeajiri wananchi wawili kunifanyia kazi ya blog kwa hiyo sihitaji ajira yako, thanks kwa ushauri wako na maneno yako kwamba huna ulivhoelewa kwenye article kabisaaa pole sana!!

Le Mutuz
 
W. J. Malecela,
Unapotosha watu, lakini unapotosha wajinga tu. so long mtu amechaguliwa, hata kama wanatoka familia moja hakuna shida. Ngoja nikupe mfano tu, anayeongoza sasa hivi Thyland ni Yingluck Shinawatra ambaye ni dada wa kiongozi alyeondolewa madarakani anayeitwa Yingluck Shinawatra. Sasa hivi kuna watu wanaleta shida mtaani wakimpinga huyu mama, lakini hawataki uchaguzi kwa sababu wanajua kuwa uchaguzi ukifanyika, huyu mama atashinda hata kama alikuwa ndugu wa jamaa wa zamani aliyeondolewa madarakani. In fact, mama ameshaitisha uchaguzi lakini wapinzani wake hawataki uchaguzi kwa sababu wanajua watapigwa chini tu. ina maana hawakubaliki. What we want is leadership not your relationship with former leader. Nikukumbushe tu kuwa mwaka 2000 chaguo la CCM Zanzibar lilikuwa Mh. Ghalib Bilal na wala sio Aman Karume, lakini nyie CCM mlivyo na mentality ya usulutani na kukosa demokrasia mkampa Aman Karume. Na hii dhambi italitafuna taifa hata kwenye bunge la katiba.
Wewe William, unapenda kuochonga sana kuhusu CHADEMA, wakati CCM hakuna demokrasia. Nikuulize, je katibu mkuu, makamu mwenyekiti wa chama na mtunza hazina, anachaguliwa na nani? Ili ujue kuwa nyani haoni kundule, CCM hakuna uchaguzi wa mgombea uraisi. Kila awamu ikipita ya kwanza, awamu ya pili hakuna anayeruhusiwa kuleta pua yake. in fact, katibu wako Yusuf Makamba kuna siku alisema kuwa CCM baada ya awamu ya kwanza wanakuwa na form moja tu ya kugombea kupitishwa kugombea uraisi. Sasa niambie umejifunzia wapi demokrasia ya kweli leo uwe na uwezo wa kuchambua demokrasia ndani ya vyamba vingine wakati chama ulichopo hakina demokrasia?
By the way, wewe ndiye mchumia tumbo, na kazi unayofanya inajidhihirisha hivyo. Kwa sababu ni mjinga ndiye atakayeamini kuwa Mh. Mbowe ni mchumia tumbo wakati unajua kabisa kuwa anatoka kwenye familia inayojiweza sana na yeye mwenyewe anajiweza sana kifedha hata kabla hajawa kiongozi wa siasa. Ni mwendawazimu tu ndiye tu atakubaliana na maneno yako kuwa viongozi wa vyama kama CHADEMA ni wachumia tumbo wakati inafahamika wazi kuwa ukitaka upate fedha gombea ubunge kupitia CCM. Kwa sababu ukikosa tu ubunge, angalau ukuu wa mkoa au ukuu wa wilaya utapewa, hata kama uwezo wa uongozi huna.
Unasema CCM ni imara. Yes, CCM ni imara kwa mambo makubwa matatu ambayo yanaligharimu taifa.
Moja, NDIO MZEE MENTALITY. Hata kiongozi akosee, itabakia zidumu fikra ya mwenyekiti. Ndio maana pamboja na viongozi makini wa Taasisi ya Mwlaimu Nyerere (akina Dr. Salim Ahmed Salim, Joseph Butiku, Joseph Sinde Warioba) kutoa mapungufu makubwa ya raisi mwaka 2009 na 2010, bado hakuna aliyeleta pua yake kugombea kupitia CCM kumpinga raisi mwaka 2010.
Mbili, KULINDANA. CCM ni kulindana, ufanye ufisadi, uibe, ubake udhalilishe, so long you are in CCM family, nothing will happen to you. Ndio maana vidagaa tu vya EPA ndio unasikia vinahukumiwa, wenye Kagoda hawataguswa. Ndio maana afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani amedhalilisha mtoto lakini hakuna adhabu aliyopewa, ndio maana David Jairo alifanya uovu mkubwa wizara ya nishati na madini lakini sana sana baada ya kuwa wazi sana alisimamishwa tu na nothing more step taken against him, ndio maana maazimio ya bunge kuhusu Richmond yaliwaumiza tu watu wa chini, wakubwa ambao ndio hasa decision making hawakuguswa.
Tatu, KUSHINDWA KUCHUKUA MAAMUZI MAKUBWA. With CCM ni usitegemee maamuzi makubwa. Nakuambia walisema watajivua gamba na wakawataja watu watatu ambao wamekidhalilisha chama kwa ufisadi mkubwa, nikiwa na maana ya RA, Vijisenti na EL, niambie mpaka leo what has been done? CHADEMA wanaokidhalilisha wataondoka na wataondolewa wakibisha. Mamluki wataondoka mmoja mmoja.
 
naona the boss umeamua kuua kabisa. du! ama kweli waTz tumekua mazombie

Yaani kuna watu waliamini kabisa kwamba Mbowe ana lengo la kuingia na CHADEMA madarakani?

seriously?

Kwa Mbowe CHADEMA kuwa top opposition party ndio lengo...

ruzuku za kumwaga,influence na connections za business tele.....

deep down ndani ya moyo wake haamini wanaingia Ikulu..sio 2015
wala sio mwaka wowote ule.....

ndo maana wana mipango ya uchaguzi wa mwaka 2015 na mwaka 2020
tayari as if 2015 washajua CCM watashinda.....

Mbowe na Mtei hatimae ile family business now ina pay off....
this is it......

hayo ya kuingia Ikulu ni ya 'mashabiki'
na 'mashabiki' wa siasa hawana tofauti na 'mashabiki' wa Liverpool na Yanga...
 
- Kaka Demokrasia imara ya Marekani sasa ina miaka 300 ndio maana ipo imaraa sana imepitia mengi sana ukisoma hisotira yao, lakini never before kwenye historia yao unaweza kukuta madudu kama ya Chadema, aibu tupu halafu kumbuka nimewaonea huruma sana kutokugusa maisha yao ya binafsi na uongozi wao ingeakuwa aibu kubwa sana, biased waulize Tanzania Daima maana ya biased ndio uje unililie mimi, tuliza boli nashangaa majibu yote so far hakuna anayegusa hoja za msingi kwa mfano ni sahihi kwa Mwenyekiti wa Chadema kupokea pesa toka kwa Rostam na Mkono kwa nia njema?

Le Mutuz

ni sahihi kabisa kupokea ela kwa nia njema ata kama zinatoka kwa shetani ili mradi zinzkwaenda kufanya kazi ya mungu sadaka za kanisani ulishawi kusikia unaulizwa zimetoka wapi,?maandiko yanasema nitawarudishia vile vilivyoliwa na nzuge (mwizi),mandumandu(fisadi),nk.kama unachangisha pesa kwa aijli ya maendeleo ya jimbo na ukaletewa na fisadi kama el,rostam,jk,ridhiwan,mkono kwa nini uzikatae wakati ni za wananchi?.mimi nacho ona kwako umekuja kivingine baada ya dili la zitto kubm.watashindana lakini HAWATASHINDA.your are failure like ur papaaa
 
W.Malecela unakosea unaposema CDM haikwenda Musoma Vijijini wakati ina madiwani kule zaidi ya watatu,akiwemo yule wa Kiabakari.uwe na takwimu kabla ya kuandika kaka
 
Back
Top Bottom