Mwl. Nyerere alifanya Kosa kubwa Kuvunjia Uhusiano na Israel

Kweli usilolijua ni kama usiku wa kazi.Wote hapo juu mmeongea vitu msivyovijua ilimradi muonekane mmechangia.Nadhani umri wenu utakuwa bado ni Mdogo.

Tuambie unachofahamu....umeongea kiujumla bila kutoa mawazo yako.
 
Mkuu wewe umenielewa

Mediocre....itakuwa ombaomba kama Tanzania? have you been to Israel? Tuacheni kujifurahisha. Let fact be said. Kila nchi inahitaji misaada kwa njia moja au nyingine. Lakini kusema Israel isipopewa misaada itakuwa "ombaomba" ni high level of ignorance.
 
Hivi mnavyosema ni taifa la mungu mnamzungumzia mungu gani? au yule aliyekong'otwa na kudhalilishwa na viumbe wake? Maana kama ni huyo namfananisha na simba wa kuchora asiye na meno wala hawezi kuunguruma sasa sijui anawezaje kumbariki mtu mwingine wakati ameshindwa kujibariki mwenyewe hadi akapata kichapo cha mbwa mwizi!

Wanaongea kuhusu Mungu wa christians. Ambaye hakuna dhambi nzito isiyosameheka, na tena anawatafuta zaidi wenye dhambi....Siyo Mungu yule unayemzungumzia wewe hapo juu.
 
Hua nacheka sana mnapozungumzia Israel mpk muhusishe na Taifa la Mungu sijui blah blah blah,

Wewe Mkristo ukamshabikie Myahudi wakati haamini unachoamini,
Halafu si ndio waliomsulubu bwana wenu Yesu hawa, bado tu mwataka uswahiba nao,

Lait mngejua wanavyowadharau ninyi wa Waafrika msingeendelea kujikomba komba kwao,

Hongera Mwl. Nyerere kwa kumtupilia mbali huyu fedhuli wa Kiyahudi,
Tanzania bila Wayahudi inawezekana na itawezekana,
Anayemuhitaji sana aende huko huko Israel, tuone kama hujarudi na jina tu.

Kwani likiwa taifa la Mungu kuna makosa gani????? kama una preference ya taifa unalotaka kuliita hivyo just tell us. Watu wote ni sawa mbele ya Mungu.
 
Mbona hata Tanzania ni taifa la Mungu? naona watu wanatoa mapovu wanasikia Israel ni Taifa la Mungu.....
 
Tuwakaribishe watu hawa watusaidie katika kilimo tuachane na Waziri wa Kilimo kila siku yeye ku-deal na migogoro ya wakulima wadogo wadogo tunahitaji uwekezaji mkubwa wa kilimo. Tutumie eneo dogo lakini tuwe na output kubwa.

Katika eneo la IT wanaweza kutusaidia sana. Hata juhudi za Mhe. Rais za kutafuta msaada katika ukusanyaji wa mapato kitaalam zaidi zinaweza kupata msaada kutoka kwa hawa jamaa.

Namshauri Mhe. Rais atembelee Israel anaweza kujifunza mambo mengi sana. Nawasilisha.

Mkuu umenisiktisha sana katika thread yako, na inaonekana hujawahi kumuelewa Nyerere hata kwa chembe ndogo. Kama una mtazamo huu juu ya Nyerere kuvunja uhusiano na Israeli, basi muda si mrefu utatoa thread yenye kichwa "Mwalimu Nyerere alifanya kosa kubwa kutokuwa na uhusiano na serikali ya Makaburu".

Kwanza kabla ya kutoa matamko mazito kama haya, unapaswa uzielewe sababu za Nyerere kuvunja uhusiano na Israeli, ambazo ndizo zilikuwa sababu za Nyerere kutokuwa na aina yeyote ya Uhusiano na serikali ya Makaburu, na pia wakati fulani kuwaunga mkono Biafra katika vita ya Nigeria, na vile vile wakati fulani kuvunja uhusiano wa Kibalozi na Uingereza na serikali ya Ujerumani Magharibi.

Kwa mfano, Nyerere alipowaamuru Ujerumani Magharibi waondoke nchini, walikuwa katikati ya kujenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa msaada. Nyerere alijua hilo, na kweli waliondoka na ramani zote za chuo pamoja na hata mfumo wa mabomba ya maji! Unajua kwamba Nkuruma Hall halikuisha kwa kufuata plan iliyochorwa na ilibidi limaliziwe kinamna namna? Unajua kwa nini Ma-Hall ya UD unaona kama kila Hall limejengwa na nchi tofauti? (Hall 3 Tower Wachina, Hall 2 Waisreli, Hall 3- Dag - Wa Denmark nk). Ilikuwa ni msaada wa nchi rafiki baada ya West Germany kufungashwa virago! Na zaidi ya hayo, West Germany walikuwa wakitoa vifaa vingi vya JWTZ. Kama wewe ni wa zamani, kuna wakati JWTZ ilikuwa na magari mengi sana ya kijeshi kutoka West Germany kutia na Benz. Nyerere alijua misaada yote hii ingekoma, na bado aliwaambia West Germany ondokeni na mkitaka bebeni na matofali yenu mliyofyatua pale UD!

Sasa kwa nini Nyerere alifanya maamuzi hayo japo alijua yangeumiza maendeleo ya nchi yetu changa sana wakati huo?

Kumbuka msimamo wa Nyerere; "Watanzania tuko tayari kujenga urafiki na nchi yeyote hapa duniani, yenye kupenda amani na kuthamini utu, haki na usawa wa wanadamu".

Unapaswa kutafakari sana juu ya mambo hayo kabla ya kutoa thread kama hizi dhidi ya Nyerere. Ushabiki wa kidini kwa Israel isiwe sababu ya kutoa thread kama hizi dhidi ya Nyerere. After all, Nyerere naye alikuwa devoted christian.
 
Mkuu synthesizer umejitahidi kueleza, mi nashindwa maana ntachoka kuandika kwa kuelezea hawa wadogo zetu. Ila ahsante
 
Mkuu synthesizer umejitahidi kueleza, mi nashindwa maana ntachoka kuandika kwa kuelezea hawa wadogo zetu. Ila ahsante

Mkuu, we acha tu, tuna kazi kubwa kuielimisha hii Y generation! Ndio maana wakati mwingne Raisi Magufuli akisema anataka kuteua vijana mwili unanisisimka kwamba hivi kweli tumewaandaa ipasavyo!
 
Israel ni miongoni mwa nchi ndogo sana duniani lakini imefanikiwa kuwa Taifa kubwa na lenye ushawishi mkubwa sana kakika ulimwengu huu.

Licha ya kuzaliwa upya mwaka 1948 baada ya kuwa utumwani katika kila pembe ya dunia kwa zaidi ya miaka ya 2000.

Wachambuzi wa mambo ya unabii wanasema kutawanywa kwao kulifuatia uovu mkuu waliomfanyia Mungu. Aidha kurejeswa kwao ni kutimia kwa unabii kwamba siku za mwisho MUNGU angeliwarejesha katika nchi yao ya enzi.

Watu hawa walirejea eneo lile lile kulikokuwa makao makuu ya nchi yao kipindi cha utawala wa Mfalme wao Maalufu Daudi yaani Jerusalemu, wakiwa hawajapoteza idedity yao, lugha na utamaduni licha ya kuishi mbalimbali.

Katika kipindi kifupi wameweza kubadili nchi yao kutoka kuwa jangwa lisilomea kitu kuwa nchi inayoongoza duniani kuzalisha na kuuza matunda na mboga mboga, jana Waziri Mkuu Netanyahu akiongea na marafiki wa Israel Jijini Nairobi alisema ng'ombe anayetoa maziwa mengi zaidi kuliko wote duniani anatoka Israel, pia Wayahudi wamefanikiwa kupata maji safi na salama yakiwa hayana wala chembe ya chumvi licha ya kutokuwa na mito na maziwa kama ilivyo kwa Tanzania.

Lakini pia tunafahamu namna Israel ilivyobobea katika masuala ya start-up entrepreneurship, innovation na technology management.

Hivi umewahi kujiuliza flash disc unayoitumia imetoka wapi? Jibu ni kwamba iligunduliwa na Myahudi. Hata Marekani yenyewe licha ya kuonekana kwamba inatoa msaada mkubwa sana wa kijeshi na kiuchumi kwa Israel ukweli ni kwamba wanaoendesha uchumi wa Marekani ni Wayahudi.

Kabla ya kuvunja uhusiano na Israel wayahudi walikuwa wamekwisha anza kutusaidia maeneo mengi sana ikiwemo elimu na afya ambapo walijenga ukumbi imara kabisa wa Nkurumah pale UDSM, pia naambiwa hata Bugando Hospital walijenga wao.

Wayahudi walianza pia kuwekeza kwenye kilimo. Kitendo chetu cha kuwakana wayahudi kimetuletea hasara kubwa sana. Kujifanya tunawahurumia Wapalestina umekuwa ni mzigo usiobebeka tena maana hawana msaada wowote.

Maandiko yako wazi kabisa. Nchi ile ni ya wayahudi, Mwarabu akitaka kuishi ataishi kwa amani lakini si kudai haki ya urithi wa nchi ile.

Tuwakaribishe watu hawa watusaidie katika kilimo tuachane na Waziri wa Kilimo kila siku yeye ku-deal na migogoro ya wakulima wadogo wadogo tunahitaji uwekezaji mkubwa wa kilimo. Tutumie eneo dogo lakini tuwe na output kubwa.

Katika eneo la IT wanaweza kutusaidia sana. Hata juhudi za Mhe. Rais za kutafuta msaada katika ukusanyaji wa mapato kitaalam zaidi zinaweza kupata msaada kutoka kwa hawa jamaa.

Namshauri Mhe. Rais atembelee Israel anaweza kujifunza mambo mengi sana. Nawasilisha.
Hatuhitaji mahubiri yasiokuwa na mashiko, Tanzania haina dini, jenga hoja yako kuhusu kosa aliolofanya Nyerere kukata uhusianao na wauaji na wakandamizaji wa haki za wapelestina, yaani Israel.

Nyerere alichukua hatua hiyo kulinda utengemano wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na uhusiano wa kibalozi na Plestine na Tanganyika na Israel. Tanzania isingeweza kuwa na balozi mbili zinzopingana kwenye nchi moja.

Haki, heshima ya utu wa binadamu juu ya Palestine na msimamo wa Zanzibar ndio uliopelekea Tanzania kuchukua upande wa kufuata. Unyama unaofanywa na waisrael bado unaendelea kwa hivyo vigezo vya kuvunja uhusiano na madhalimu hawa wa kizioni bado viko hai. Kuheshimu utu na kuthamini uhai wa binadamu ni zaidi ya msaada wa IT na umwagiliaji maji mashamba na kupata n'gombe wanaotoa maziwa mengi.

Pengine umesahau siasa za vijiji vya ujamaa na bughudha na idhlali kwa wananchi wa Tanzania walioipata. Vijiji vya ujamaa ni sera ilioazimwa kutoka mashetani wa kiyahudi.Wao wanaviita KIBUT. Unataka turejee zama za ushenzi, unyanyasaji na kudharauliana?

Kama wameweza kufanya uovu mkuu kwa mungu watashindwa kuwafanyia ouvu maradufu wapelestine au watanzania? Waisraeli tuwaogope kama ukoma!
 
Hua nacheka sana mnapozungumzia Israel mpk muhusishe na Taifa la Mungu sijui blah blah blah,

Wewe Mkristo ukamshabikie Myahudi wakati haamini unachoamini,
Halafu si ndio waliomsulubu bwana wenu Yesu hawa, bado tu mwataka uswahiba nao,

Lait mngejua wanavyowadharau ninyi wa Waafrika msingeendelea kujikomba komba kwao,

Hongera Mwl. Nyerere kwa kumtupilia mbali huyu fedhuli wa Kiyahudi,
Tanzania bila Wayahudi inawezekana na itawezekana,
Anayemuhitaji sana aende huko huko Israel, tuone kama hujarudi na jina tu.

wayahudi hawajaanza ubaguzi leo...... hata wakat wa YESU waliwabagua *WASAMARIA*
 
Wakristo kama mtoa post ni wa kupuuzwa. Hata hiyo biblia inaonekana huwa hamsomi. Wapalestina ile ni nchi yao ya halali na sababu zinazotolewa na Israel hazikubaliki. Pia kusema kwamba Israel ni taifa la Mungu ni kuzidi kudhihirisha upuuzi wa baadhi ya wakristo. Kabla ya kupost mada kama hii someni kwanza.
 
Mkuu umenisiktisha sana katika thread yako, na inaonekana hujawahi kumuelewa Nyerere hata kwa chembe ndogo. Kama una mtazamo huu juu ya Nyerere kuvunja uhusiano na Israeli, basi muda si mrefu utatoa thread yenye kichwa "Mwalimu Nyerere alifanya kosa kubwa kutokuwa na uhusiano na serikali ya Makaburu".

Kwanza kabla ya kutoa matamko mazito kama haya, unapaswa uzielewe sababu za Nyerere kuvunja uhusiano na Israeli, ambazo ndizo zilikuwa sababu za Nyerere kutokuwa na aina yeyote ya Uhusiano na serikali ya Makaburu, na pia wakati fulani kuwaunga mkono Biafra katika vita ya Nigeria, na vile vile wakati fulani kuvunja uhusiano wa Kibalozi na Uingereza na serikali ya Ujerumani Magharibi.

Kwa mfano, Nyerere alipowaamuru Ujerumani Magharibi waondoke nchini, walikuwa katikati ya kujenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa msaada. Nyerere alijua hilo, na kweli waliondoka na ramani zote za chuo pamoja na hata mfumo wa mabomba ya maji! Unajua kwamba Nkuruma Hall halikuisha kwa kufuata plan iliyochorwa na ilibidi limaliziwe kinamna namna? Unajua kwa nini Ma-Hall ya UD unaona kama kila Hall limejengwa na nchi tofauti? (Hall 3 Tower Wachina, Hall 2 Waisreli, Hall 3- Dag - Wa Denmark nk). Ilikuwa ni msaada wa nchi rafiki baada ya West Germany kufungashwa virago! Na zaidi ya hayo, West Germany walikuwa wakitoa vifaa vingi vya JWTZ. Kama wewe ni wa zamani, kuna wakati JWTZ ilikuwa na magari mengi sana ya kijeshi kutoka West Germany kutia na Benz. Nyerere alijua misaada yote hii ingekoma, na bado aliwaambia West Germany ondokeni na mkitaka bebeni na matofali yenu mliyofyatua pale UD!

Sasa kwa nini Nyerere alifanya maamuzi hayo japo alijua yangeumiza maendeleo ya nchi yetu changa sana wakati huo?

Kumbuka msimamo wa Nyerere; "Watanzania tuko tayari kujenga urafiki na nchi yeyote hapa duniani, yenye kupenda amani na kuthamini utu, haki na usawa wa wanadamu".

Unapaswa kutafakari sana juu ya mambo hayo kabla ya kutoa thread kama hizi dhidi ya Nyerere. Ushabiki wa kidini kwa Israel isiwe sababu ya kutoa thread kama hizi dhidi ya Nyerere. After all, Nyerere naye alikuwa devoted christian.

kosa la Nyerere lilikua hilo,,, alikua tayar sie tufe na njaa ili maslah yake yalindwe....... ehe tumepata faida gan sasa kwa S.A kua huru??........

yan km taifa nini kimeongezeka kwetu baada ya kupigania yote hayo???? no wonder tunazidowa na kila nchi tuliyoisaidia.........

S.A si ndio hao hao leo wanalipa 4% kwenye migodi yetu? alifanya yote hayo for his legacy sio kwa faida yetu......
 
Ahsante sana Mkuu.

Umeandika ujinga! Unajua sababu iliyopelekea Tanzania kukatisha uhusiano na Israeli? Unaujua msimamo wa Umoja wa mataifa kuhusu Israel? Unajua ni kwanini mpaka leo Palestina sio Taifa kamili? Sababu unazijua?Usiwe mjinga mjinga kutetetea ujinga kwa usichokifahamu. Kaa kimya ukitaka kuandika focus kwenye chanzo cha tatizo ndipo uje usifie, inaoneka wewe ni mwanafunzi kwa uandishi wako huu.
 
kosa la Nyerere lilikua hilo,,, alikua tayar sie tufe na njaa ili maslah yake yalindwe....... ehe tumepata faida gan sasa kwa S.A kua huru??........

yan km taifa nini kimeongezeka kwetu baada ya kupigania yote hayo???? no wonder tunazidowa na kila nchi tuliyoisaidia.........

S.A si ndio hao hao leo wanalipa 4% kwenye migodi yetu? alifanya yote hayo for his legacy sio kwa faida yetu......

Kwa hiyo Mkuu uko tayari kufanywa chochote wewe binafsi, au kuachia ndugu yako, au rafiki yako au jirani yako, afanywe chochote, ili mradi hicho kitu hakina maslahi kwako ya sasa au ya baadaye, sivyo?

Kwa maneno mengine, huna "values" sivyo?
 
Nimependa mno ulivyoandika, nikweli hâta USA wanaiheshimu sana Israël kwa uwezo mkubwa wa kiakili,kivitendo na historia inavyoifungamanisha na imani ya Kristu bwana.
Naamini tumekwisha tambua ni kosa kujitenga Nao Sasa tujifunze kwao vyema ktk elimu,afya,kilimo,utalii,usalama,technology ...kunamengi ya kujifunza kwao

Wayahudi hawakumtambua Bw Yesu, hawamtambui na hawatamtambua mpaka mwisho wa dunia, ni wao ndio waliodai "ni bora aachiwe huru jambazi Baraba kuliko kuachiwa huru Bwana Yesu" na ndio waliodai 'asulubiwe' Moja ya sababu aliyoitoa Adolf Hitler (Mkatoliki) ya kuwaua Wayahudi kwa wingi ni hiyo. Nyerere pia alikuwa Mkatoliki, kwahiyo kama unaishabikia Israel wewe ishabikie tu kwa mapenzi yako, usinasibishe na masuala ya Bwana Yesu, wenzio hawataki hata kumsikia. Isitoshe uliza Waafrika wenzio wakueleze ubaguzi na udhalilishaji wanaoupata huko, hata wale Waethiopia wenye asili ya kiyahudi.
 
Wakristo kama mtoa post ni wa kupuuzwa. Hata hiyo biblia inaonekana huwa hamsomi. Wapalestina ile ni nchi yao ya halali na sababu zinazotolewa na Israel hazikubaliki. Pia kusema kwamba Israel ni taifa la Mungu ni kuzidi kudhihirisha upuuzi wa baadhi ya wakristo. Kabla ya kupost mada kama hii someni kwanza.

Na wewe umeleta "madai" kama ya unaowaita wa kupuuzwa. Do your research and come back with evidences of what you are saying... mnatuchosha na blabla. Tunataka ushahidi ili tuone nani wa kupuuzwa.
 
Wayahudi hawakumtambua Bw Yesu, hawamtambui na hawatamtambua mpaka mwisho wa dunia, ni wao ndio waliodai "ni bora aachiwe huru jambazi Baraba kuliko kuachiwa huru Bwana Yesu" na ndio waliodai 'asulubiwe' Moja ya sababu aliyoitoa Adolf Hitler (Mkatoliki) ya kuwaua Wayahudi kwa wingi ni hiyo. Nyerere pia alikuwa Mkatoliki, kwahiyo kama unaishabikia Israel wewe ishabikie tu kwa mapenzi yako, usinasibishe na masuala ya Bwana Yesu, wenzio hawataki hata kumsikia. Isitoshe uliza Waafrika wenzio wakueleze ubaguzi na udhalilishaji wanaoupata huko, hata wale Waethiopia wenye asili ya kiyahudi.

What are you preaching here? you preaching LOVE by spreading HATE, and you still want us to believe you?
 
Back
Top Bottom