Mwl. Nyerere alifanya Kosa kubwa Kuvunjia Uhusiano na Israel

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
426
Israel ni miongoni mwa nchi ndogo sana duniani lakini imefanikiwa kuwa Taifa kubwa na lenye ushawishi mkubwa sana kakika ulimwengu huu.

Licha ya kuzaliwa upya mwaka 1948 baada ya kuwa utumwani katika kila pembe ya dunia kwa zaidi ya miaka ya 2000.

Wachambuzi wa mambo ya unabii wanasema kutawanywa kwao kulifuatia uovu mkuu waliomfanyia Mungu. Aidha kurejeswa kwao ni kutimia kwa unabii kwamba siku za mwisho MUNGU angeliwarejesha katika nchi yao ya enzi.

Watu hawa walirejea eneo lile lile kulikokuwa makao makuu ya nchi yao kipindi cha utawala wa Mfalme wao Maalufu Daudi yaani Jerusalemu, wakiwa hawajapoteza idedity yao, lugha na utamaduni licha ya kuishi mbalimbali.

Katika kipindi kifupi wameweza kubadili nchi yao kutoka kuwa jangwa lisilomea kitu kuwa nchi inayoongoza duniani kuzalisha na kuuza matunda na mboga mboga, jana Waziri Mkuu Netanyahu akiongea na marafiki wa Israel Jijini Nairobi alisema ng'ombe anayetoa maziwa mengi zaidi kuliko wote duniani anatoka Israel, pia Wayahudi wamefanikiwa kupata maji safi na salama yakiwa hayana wala chembe ya chumvi licha ya kutokuwa na mito na maziwa kama ilivyo kwa Tanzania.

Lakini pia tunafahamu namna Israel ilivyobobea katika masuala ya start-up entrepreneurship, innovation na technology management.

Hivi umewahi kujiuliza flash disc unayoitumia imetoka wapi? Jibu ni kwamba iligunduliwa na Myahudi. Hata Marekani yenyewe licha ya kuonekana kwamba inatoa msaada mkubwa sana wa kijeshi na kiuchumi kwa Israel ukweli ni kwamba wanaoendesha uchumi wa Marekani ni Wayahudi.

Kabla ya kuvunja uhusiano na Israel wayahudi walikuwa wamekwisha anza kutusaidia maeneo mengi sana ikiwemo elimu na afya ambapo walijenga ukumbi imara kabisa wa Nkurumah pale UDSM, pia naambiwa hata Bugando Hospital walijenga wao.

Wayahudi walianza pia kuwekeza kwenye kilimo. Kitendo chetu cha kuwakana wayahudi kimetuletea hasara kubwa sana. Kujifanya tunawahurumia Wapalestina umekuwa ni mzigo usiobebeka tena maana hawana msaada wowote.

Maandiko yako wazi kabisa. Nchi ile ni ya wayahudi, Mwarabu akitaka kuishi ataishi kwa amani lakini si kudai haki ya urithi wa nchi ile.

Tuwakaribishe watu hawa watusaidie katika kilimo tuachane na Waziri wa Kilimo kila siku yeye ku-deal na migogoro ya wakulima wadogo wadogo tunahitaji uwekezaji mkubwa wa kilimo. Tutumie eneo dogo lakini tuwe na output kubwa.

Katika eneo la IT wanaweza kutusaidia sana. Hata juhudi za Mhe. Rais za kutafuta msaada katika ukusanyaji wa mapato kitaalam zaidi zinaweza kupata msaada kutoka kwa hawa jamaa.

Namshauri Mhe. Rais atembelee Israel anaweza kujifunza mambo mengi sana. Nawasilisha.
 
Mkuu Matunge, kwanza mazhukuru kwa kuleta mada.

Baada ya holocust hilo taifa la wayahudi lilirudi nyuma sana kwa kila kitu na ni kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Na mambo mengi walianza kuyaweka sawa baada ya huo mwaka wa kuzaliwa kwao upya.
Lakini ni kwanini ndio taifa lenye nguvu sana hasa kijeshi kuliko hata mataifa mengine makongwe zaidi??

alafu ile ardhi kama ni ya wapalestina ni kwanini vyombo kma UN wanashindwa kusimamia haki ya wapalestina na kuwaacha wakiteketea kila leo?

..
Ni kutaka kujua tu
Asante.
 
Ni kwel kabisa Israel ni taifa imara na lenye nguvu za ki Mungu. Mungu alilibariki Milele na milele so huwez kuliondoa taifa la Israel kweny ramani ya Dunia nafikiri tuige mfano kwa hawa wenzetu wa Kenya. Mwl Nyerere alikuwa amefungamana na siasa za ujamaaa ambapo alijikuta kufungamana na USSR wakat huo wakipinga ubepari ndo madhara yake sasa Jews are more superior and successful in the world also they are under USA
 
Nimependa mno ulivyoandika, nikweli hâta USA wanaiheshimu sana Israël kwa uwezo mkubwa wa kiakili,kivitendo na historia inavyoifungamanisha na imani ya Kristu bwana.
Naamini tumekwisha tambua ni kosa kujitenga Nao Sasa tujifunze kwao vyema ktk elimu,afya,kilimo,utalii,usalama,technology ...kunamengi ya kujifunza kwao
 
Imani yangu ya ukweli inaniambia hilo ni TAIFA TEULE LA MUNGU lakini pia uzoefu wangu nilioupata kimwili unaonesha kwamba watu wa taifa hilo ndiyo wanaoongoza duniani kwa "AKILI KUBWA" katika nyanja za teknolojia, biashara, kilimo, ulinzi , etc. Almost kila kitu. Nasikia hata shirika lilosimamia masuala ya anga nchini Marekani la NASA limejaa wayahudi. FBI yenyewe imejaa wayahudi. Sasa, kwa hali hii, nitakuwa mnafiki nisipomshauri Rais wangu Mhe. JPM kuurejesha uhusiano wa Tanzania na Israel ili nasi tufaidi BARAKA ZA MUNGU. Shime Mhe. Rais tufanye hima kwani wenzetu wakenya tayari wametutangulia.
 
Israel ni miongoni mwa nchi ndogo sana duniani lakini imefanikiwa kuwa Taifa kubwa na lenye ushawishi mkubwa sana kakika ulimwengu huu. Licha ya kuzaliwa upya mwaka 1948 baada ya kuwa utumwani katika kila pembe ya dunia kwa zaidi ya miaka ya 2000. Wachambuzi wa mambo ya unabii wanasema kutawanywa kwao kulifuatia uovu mkuu waliomfanyia Mungu. Aidha kurejeswa kwao ni kutimia kwa unabii kwamba siku za mwisho MUNGU angeliwarejesha katika nchi yao ya enzi. Watu hawa walirejea eneo lile lile kulikokuwa makao makuu ya nchi yao kipindi cha utawala wa Mfalme wao Maalufu Daudi yaani Jerusalemu, wakiwa hawajapoteza idedity yao, lugha na utamaduni licha ya kuishi mbalimbali. Katika kipindi kifupi wameweza kubadili nchi yao kutoka kuwa jangwa lisilomea kitu kuwa nchi inayoongoza duniani kuzalisha na kuuza matunda na mboga mboga, jana Waziri Mkuu Netanyahu akiongea na marafiki wa Israel Jijini Nairobi alisema ng'ombe anayetoa maziwa mengi zaidi kuliko wote duniani anatoka Israel, pia Wayahudi wamefanikiwa kupata maji safi na salama yakiwa hayana wala chembe ya chumvi licha ya kutokuwa na mito na maziwa kama ilivyo kwa Tanzania. Lakini pia tunafahamu namna Israel ilivyobobea katika masuala ya start-up entrepreneurship, innovation na technology management. Hivi umewahi kujiuliza flash disc unayoitumia imetoka wapi? Jibu ni kwamba iligunduliwa na Myahudi. Hata Marekani yenyewe licha ya kuonekana kwamba inatoa msaada mkubwa sana wa kijeshi na kiuchumi kwa Israel ukweli ni kwamba wanaoendesha uchumi wa Marekani ni Wayahudi. Kabla ya kuvunja uhusiano na Israel wayahudi walikuwa wamekwisha anza kutusaidia maeneo mengi sana ikiwemo elimu na afya ambapo walijenga ukumbi imara kabisa wa Nkurumah pale UDSM, pia naambiwa hata Bugando Hospital walijenga wao. Wayahudi walianza pia kuwekeza kwenye kilimo. Kitendo chetu cha kuwakana wayahudi kimetuletea hasara kubwa sana. Kujifanya tunawahurumia Wapalestina umekuwa ni mzigo usiobebeka tena maana hawana msaada wowote. Maandiko yako wazi kabisa. Nchi ile ni ya wayahudi, Mwarabu akitaka kuishi ataishi kwa amani lakini si kudai haki ya urithi wa nchi ile.Tuwakaribishe watu hawa watusaidie katika kilimo tuachane na Waziri wa Kilimo kila siku yeye ku-deal na migogoro ya wakulima wadogo wadogo tunahitaji uwekezaji mkubwa wa kilimo. Tutumie eneo dogo lakini tuwe na output kubwa. Katika eneo la IT wanaweza kutusaidia sana. Hata juhudi za Mhe. Rais za kutafuta msaada katika ukusanyaji wa mapato kitaalam zaidi zinaweza kupata msaada kutoka kwa hawa jamaa. Namshauri Mhe. Rais atembelee Israel anaweza kujifunza mambo mengi sana. Nawasilisha.

Sijsoma makala yako lakini naunga mkono kwa kicwa cha habari kwa sababu ninajua nini kinawapata wanaokuwa adui wa Israel. Na yote hya yanaonekana katika uhalisia wa maisha lakini kiini chake kiko nje ya dunia hii tunaoyiona. Hakuna filosophia wala itikadi itaweza kubadisha ukweli huu. Hakuna mamlaka, ama utawala wowote unaweza kubadilisha ukweli huu. Sanasana hasira na matusi kwa Israel and rafiki zake nidyo petrol katika moto wa dhiki.

Maamuzi yalifanywa kwa mihemuko, kujionyesha na kupenda sifa bila maarifa wala hekima ya kidunia na ya KIMUNGU.
Ni kama wale waliosema siku moja katika mashauri yanayohusu uhai kwa kufuata mihemuko na ushabiki wakadiriki kusema "Damu Yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu", kwa sababu walitaka afe lakinia bila ushahidi wa kosa lolote laikuwa amelifanya. Yanayowakuta yanajulikana.

Hili pia ni fundisho kwa watu wanoamua mambo kwa viburi, ujinga, ushabiki, ubinafsi mihemuko, kujipendekeza, mikumbo, kujionyesha na kupenda sifa bila kujali kweli wala haki au hata kutaka kufahamu undani wa mambo.
 
Kweli usilolijua ni kama usiku wa kazi.Wote hapo juu mmeongea vitu msivyovijua ilimradi muonekane mmechangia.Nadhani umri wenu utakuwa bado ni Mdogo.
mkuu vipi mbona unatokwa povu? kwani kuna shida yoyote kwa tanzania kuwa na urafiki na Israel? kama ambavyo waislam wakienda kuhiji makka wanakirimiwa vizuri na ubalozi wa tanzania, vivo hivyo wakristo nao wana haki ya kudai ubalozi ili na wao wanapokwenda kuhiji wapate huduma kutoka ubalozi wa tanzania.

tuvumiliane wakuu halaf tuache chuki zisizo za msingi juu ya Israeli
 
Hua nacheka sana mnapozungumzia Israel mpk muhusishe na Taifa la Mungu sijui blah blah blah,

Wewe Mkristo ukamshabikie Myahudi wakati haamini unachoamini,
Halafu si ndio waliomsulubu bwana wenu Yesu hawa, bado tu mwataka uswahiba nao,

Lait mngejua wanavyowadharau ninyi wa Waafrika msingeendelea kujikomba komba kwao,

Hongera Mwl. Nyerere kwa kumtupilia mbali huyu fedhuli wa Kiyahudi,
Tanzania bila Wayahudi inawezekana na itawezekana,
Anayemuhitaji sana aende huko huko Israel, tuone kama hujarudi na jina tu.
 
mkuu vipi mbona unatokwa povu? kwani kuna shida yoyote kwa tanzania kuwa na urafiki na Israel? kama ambavyo waislam wakienda kuhiji makka wanakirimiwa vizuri na ubalozi wa tanzania, vivo hivyo wakristo nao wana haki ya kudai ubalozi ili na wao wanapokwenda kuhiji wapate huduma kutoka ubalozi wa tanzania.

tuvumiliane wakuu halaf tuache chuki zisizo za msingi juu ya Israeli
Ishu sio kuwa na urafiki na Israel, hilo hata mimi silipingi, na pia silipingi hata kwa nchi yeyote ile tukiona inafaa. Ila nje ya hapo, mengine ni porojo
 
Israel ni miongoni mwa nchi ndogo sana duniani lakini imefanikiwa kuwa Taifa kubwa na lenye ushawishi mkubwa sana kakika ulimwengu huu. Licha ya kuzaliwa upya mwaka 1948 baada ya kuwa utumwani katika kila pembe ya dunia kwa zaidi ya miaka ya 2000. Wachambuzi wa mambo ya unabii wanasema kutawanywa kwao kulifuatia uovu mkuu waliomfanyia Mungu. Aidha kurejeswa kwao ni kutimia kwa unabii kwamba siku za mwisho MUNGU angeliwarejesha katika nchi yao ya enzi. Watu hawa walirejea eneo lile lile kulikokuwa makao makuu ya nchi yao kipindi cha utawala wa Mfalme wao Maalufu Daudi yaani Jerusalemu, wakiwa hawajapoteza idedity yao, lugha na utamaduni licha ya kuishi mbalimbali. Katika kipindi kifupi wameweza kubadili nchi yao kutoka kuwa jangwa lisilomea kitu kuwa nchi inayoongoza duniani kuzalisha na kuuza matunda na mboga mboga, jana Waziri Mkuu Netanyahu akiongea na marafiki wa Israel Jijini Nairobi alisema ng'ombe anayetoa maziwa mengi zaidi kuliko wote duniani anatoka Israel, pia Wayahudi wamefanikiwa kupata maji safi na salama yakiwa hayana wala chembe ya chumvi licha ya kutokuwa na mito na maziwa kama ilivyo kwa Tanzania. Lakini pia tunafahamu namna Israel ilivyobobea katika masuala ya start-up entrepreneurship, innovation na technology management. Hivi umewahi kujiuliza flash disc unayoitumia imetoka wapi? Jibu ni kwamba iligunduliwa na Myahudi. Hata Marekani yenyewe licha ya kuonekana kwamba inatoa msaada mkubwa sana wa kijeshi na kiuchumi kwa Israel ukweli ni kwamba wanaoendesha uchumi wa Marekani ni Wayahudi. Kabla ya kuvunja uhusiano na Israel wayahudi walikuwa wamekwisha anza kutusaidia maeneo mengi sana ikiwemo elimu na afya ambapo walijenga ukumbi imara kabisa wa Nkurumah pale UDSM, pia naambiwa hata Bugando Hospital walijenga wao. Wayahudi walianza pia kuwekeza kwenye kilimo. Kitendo chetu cha kuwakana wayahudi kimetuletea hasara kubwa sana. Kujifanya tunawahurumia Wapalestina umekuwa ni mzigo usiobebeka tena maana hawana msaada wowote. Maandiko yako wazi kabisa. Nchi ile ni ya wayahudi, Mwarabu akitaka kuishi ataishi kwa amani lakini si kudai haki ya urithi wa nchi ile.Tuwakaribishe watu hawa watusaidie katika kilimo tuachane na Waziri wa Kilimo kila siku yeye ku-deal na migogoro ya wakulima wadogo wadogo tunahitaji uwekezaji mkubwa wa kilimo. Tutumie eneo dogo lakini tuwe na output kubwa. Katika eneo la IT wanaweza kutusaidia sana. Hata juhudi za Mhe. Rais za kutafuta msaada katika ukusanyaji wa mapato kitaalam zaidi zinaweza kupata msaada kutoka kwa hawa jamaa. Namshauri Mhe. Rais atembelee Israel anaweza kujifunza mambo mengi sana. Nawasilisha.
Umeandika ujinga! Unajua sababu iliyopelekea Tanzania kukatisha uhusiano na Israeli? Unaujua msimamo wa Umoja wa mataifa kuhusu Israel? Unajua ni kwanini mpaka leo Palestina sio Taifa kamili? Sababu unazijua?Usiwe mjinga mjinga kutetetea ujinga kwa usichokifahamu. Kaa kimya ukitaka kuandika focus kwenye chanzo cha tatizo ndipo uje usifie, inaoneka wewe ni mwanafunzi kwa uandishi wako huu.
 
Mwl alikuwa binadamu. asamehewe na aachwe apumzike kwa amani mwana mwema wa Tanganyika
 
Back
Top Bottom