Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Katika hali isiyo ya kawaida aliyekuwa mbunge wa Ukonga na kukimbilia CCM Mwita Waitara amepiga marufuku shughuli zozote za kisiasa za Chadema ikiwemo upeperushaji bendera zake katika eneo la Mwembeni Kivule Ukonga
Waitara amefanya hivyo katika kile anachodai ni eneo la mtaa ambako anaishi hivyo bendera za Chadema ni uchafu kwake.
Katika kutimiza hilo usiku wa kuamkia leo bendera zote za Chadema ziliondolewa katika mtaa huo.Ilipofika asubuhi vijana wa Chadema hawakufurahishwa na hali hiyo na kuamua kusimika bendera ya Chadema katika eneo wanapopaki bodaboda katika mtaa huo wa Mwembeni.
Mara tu baada ya kusimika bendera polisi walivamia mtaa huo na kuanza kutembeza kipigo kwa vijana wa Bodaboda na kumkamata kijana aliyeongoza zoezi la usimikaji wa bendera baada ya kumpa kipigo kikali karibu ya kuzimia.Kijana huyo anayeendesha bodaboda anafahamika kwa jina la *CHINGA* na alizolewa na bodaboda yake na kupelekwa kituo cha polisi Sitakishari Ukonga.Kijana huyo kwa jinsi alivyopigwa alibebwa kuingizwa kwenye gari kwa sababu alishindwa kupanda mwenyewe.
Wananchi kadhaa bila kujali itikadi za vyama wamekasirishwa na hali hiyo na kusema ni uonevu mkubwa huku wakilaani polisi kutumika kama vikaragosi kukandamiza upinzani