Mwingira aporomosha matusi ya nguoni ibadani baada ya kuumbuliwa na JF

Acha uongo wa kusingizia watumish wa Mungu. unatafuta faraja kwa kuwa unataka kwenda? au ushaenda na hujapona? au umesikia wamepona ila hujathibitisha! pole
Hommie angalia usije ukapasua keyboard hizo si unajua kupata nyingine ilivyo shida....!!!! lol
 
Hommie angalia usije ukapasua keyboard hizo si unajua kupata nyingine ilivyo shida....!!!! lol
Mkuu, haya mambo ya imani yanataka uelewa na busara.
Mi hapa naona kuna wenye uelewa, na kuna wenye busara na kuna ambao hawana hata kimoja, hawa ndo wafuasi wa kibwetere....yeyote atakayesema mungu yupo hapa tu, wanakimbilia hapohapo,wanajazwa ujinga coz hawana maarifa na wanakuwa mazuzu.
 
Ivi Unabii na Utume unajipa unapewa?
hehehe na bado watatoka povu sana! mi nashindwa kuelewa ivi mtu unatekwaje kiimani na watu kama kina Mwingira &Co.

That is a very good question! Huwa mimi nashangaa sana na nadhani tatizo ni serikali yetu haijatupa elimu ya kutosha kupambanua mambo.
 
Mwakasege kasema watu waende wakapate kikombe......


Acha kumuwekea Mwalimu Mwakasege maneno asiyoyatamka kwani we all know hajasema na hawezi kutoa statement kama hiyo hata akiulizwa na waandishi wa habari.

Ndio maana kwa wale waliohudhuria semina yake iliyoisha juzi hapo biafra alipokuwa anafundisha namna ya kukazania maombi yako kwa Mungu hadi ujibiwe walimsikia akisema, "hapa sizungumzii dini ya mtu, na wala hautonisikia nazungumzia dini ya mtu" bali ninakufundisha namna ya kujifunza neno la Mungu..........
 
Kiukweli mimi simuamini huyu mtumishi kabisaaaa. Kuna wakati alithubutu hata kuwafukuza waumini wake ambao hawakuwa na sadaka. Sasa mtu utajiuliza, katika mchakato wa kumtafuta Mungu na uzima, masikini hawatashiriki? Tujiulize na kutafakari kabla ya kuamua kuhamahama kiimani kwani kwa upeo wangu mdogo najua kuwa Mungu yupo popote. Watu wanadhani kuwa uwepo wa Mungu unaambatana na miujiza tuuu. Kwa maana hiyo, watu wengi wanaotangatanga kiimani huwa wanatafuta miujiza na nguvu za ziada.
 
Katika ibada ya jumapili iliyokuwa inafanyika kwenye kanisa la EFATA Nabii na mtume mwingira aliporomosha matusi ya nguvu kwenye ibada hiyo kwa watu wote wanaokwenda Loliondo na waandishi wa habari wanaojifanya kumuandika kwenye vyombo vya habari baaadhi ya maneno yenye lugha iliyopitiliza sitaweka ila mojawapo ni haya " Nasema wale wanaokwenda Loliondo ni wajinga!! nasema niwajinga!! waandishi wa habari ambao wanatabia ya kuniandikaandika kwenye vyombo ya habari ni wajinga'' nasema niwajinga, mawaziri wanaokwenda Loliondo ni wajinga!!! wanaonisema kuwa ninalaaana ya Kanisa la Moja ni wajingaaaa!!! baada ya kuporomosha maneno ambayo sio rahisi kwa mtu yeyote wa mungu kuyatamka alimalizia kwa kuwataka wamumini waitikie kwa kusema ameeen. Hata hivyo alibainisha wazi kuwa anajua kuna waandishi wa habari wapo ibadani hapo hivyo waandike wanavyoweza maana ni wajinga.

Kwenye Ibada ya jumapili ya tarehe 13/03/2011 mwingira alitoa amri mafundi waliokuwa wanarusha ibada ya jumapili kwa njia ya TV wazime ili wanachi wanofuatilia ibada hiyo wasione kashfa aliyoitoa kumkashifu babu wa loliondo hata hivyo bila kujua kuwa JF member alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wametinga ndani ya ibada hiyo. Hata hivyo inaonesha kuwa mwingira anashida kubwa kiroho hivyo kwani taharuki na ghadhabu aliyoionyesha ibadani juu ya kuanikwa na vyombo vya habari mimi binafsi sijui nitafanyiwa maombi gani ili niamini kuwa mwingira ni nabii. Baada ya ibada baadhi ya waumini wake walisikika wakimlaumu kwa lugha alizotumia kuwasilisha hisia zake!! nimeona niwajuze wenzangu ili mjue msimamo wa nabii huyu!!!!

.
Ujuo wa babu ni anguko kwa wengi na pia ni kuinuka kwa wengi.
Ni anguko kuu hasa kwa wale wachumia tumbo kupitia maradhi ya watu kwa kisingizio cha kuwarisisha ufalme wa Mungu, ambao kiukweli hata wao wenyewe hawatauingia.
.
 
Mwingira ukimsikiliza tu unajua background yake sio ya kujivunia, na hizo elements bado hazijamtoka. Huwa anaongeaaa anafika mahali unaona kabisa anataka kupitiliza kwenye yasiyofaa halafu anashituka na kujizuia. Now he is full of fear kuwa anawapoteza wafuasi, sasa hata ile kujizuia haiwezekani tena, anatoa full blast.
 
Jama mwenye profile ya mwingira atuwekee hapa ili tumjue huyu mtu kiundani
 
Mkuu, haya mambo ya imani yanataka uelewa na busara.
Mi hapa naona kuna wenye uelewa, na kuna wenye busara na kuna ambao hawana hata kimoja, hawa ndo wafuasi wa kibwetere....yeyote atakayesema mungu yupo hapa tu, wanakimbilia hapohapo,wanajazwa ujinga coz hawana maarifa na wanakuwa mazuzu.

Birigita, wengine ni waelewa na busara zao, bali shida haina adabu, haswa shida ya maradhi yoyote sugu, wengi hujikabidhi kwenye imani baada ya kukata tamaa na lolote watakaloambiwa, watalitekeleza kwa sababu wanakuwa wamesha ji submit!.

Ukisha ji submit, unakuwa under control, lazima pia tukubali, hawa wahubiri wote, ili kuwashika waumini, lazima uwa controll vizuri by playing with their mind to make belive hayo wasemayo, ni sauti ya Mungu.

Ujio wa Babu, umepelekea wale wole walijipeleka makanisa ya wokovu kwa shida za maradhi bila kupona, wametimkia kwa Babu na wakipona, unadhani watarudi?. No, watajirudia dini zao za awali. Ili kuzuia kupoteza waumini wengine zaidi, wahubiri hawa inawabidi wampige vita sana Babu.
 
Imekula kwake huyo nabii uchwara. Ana tofauti gani na mafisadi? Afunge na kuomba nae aonyeshwe kawa hiyo dawa ni kweli. Yeye anakuwa na gadhabu kama vile kaibiwa! hawa jamaa hawanatofauti na wanasiasa wananpondana. Mi simo, mwache aendelee kumkashifu Babu yetu, hajui kuwa hata yeye anaweza pata dawa na akapona.
 
Acha kumuwekea Mwalimu Mwakasege maneno asiyoyatamka kwani we all know hajasema na hawezi kutoa statement kama hiyo hata akiulizwa na waandishi wa habari.

Ndio maana kwa wale waliohudhuria semina yake iliyoisha juzi hapo biafra alipokuwa anafundisha namna ya kukazania maombi yako kwa Mungu hadi ujibiwe walimsikia akisema, "hapa sizungumzii dini ya mtu, na wala hautonisikia nazungumzia dini ya mtu" bali ninakufundisha namna ya kujifunza neno la Mungu..........


Ni kweli. Mwakasege anahubiri sana neno bila kuleta mipasho. Alivutia sana aliposema, 'kama mtu kazama muokoe kwanza, muweke mahali salama, ndo umuulize kwa nini uliingia majini na nguo?' Nguo zitakufanya usiogelee na ushindwe kuogelea. Huyu Mwingira mara nyingine unaweza hata kuogopa kusikiliza mahubiri yake maana hakawii kwenda off-side.

Ushauri kwako Nabii, "Instead of cursing darkness, light a candle'. Kama unaona watu kwenda kwa babu ni laana, basi washa mshumaa wa matumaini ndani yao, wapate kuuona ukweli na siyo kulaani hilo unaloliita 'giza'.
 
katika ibada ya jumapili iliyokuwa inafanyika kwenye kanisa la efata nabii na mtume mwingira aliporomosha matusi ya nguvu kwenye ibada hiyo kwa watu wote wanaokwenda loliondo na waandishi wa habari wanaojifanya kumuandika kwenye vyombo vya habari baaadhi ya maneno yenye lugha iliyopitiliza sitaweka ila mojawapo ni haya " nasema wale wanaokwenda loliondo ni wajinga!! Nasema niwajinga!! Waandishi wa habari ambao wanatabia ya kuniandikaandika kwenye vyombo ya habari ni wajinga'' nasema niwajinga, mawaziri wanaokwenda loliondo ni wajinga!!! Wanaonisema kuwa ninalaaana ya kanisa la moja ni wajingaaaa!!! Baada ya kuporomosha maneno ambayo sio rahisi kwa mtu yeyote wa mungu kuyatamka alimalizia kwa kuwataka wamumini waitikie kwa kusema ameeen. Hata hivyo alibainisha wazi kuwa anajua kuna waandishi wa habari wapo ibadani hapo hivyo waandike wanavyoweza maana ni wajinga.

Kwenye ibada ya jumapili ya tarehe 13/03/2011 mwingira alitoa amri mafundi waliokuwa wanarusha ibada ya jumapili kwa njia ya tv wazime ili wanachi wanofuatilia ibada hiyo wasione kashfa aliyoitoa kumkashifu babu wa loliondo hata hivyo bila kujua kuwa jf member alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wametinga ndani ya ibada hiyo. Hata hivyo inaonesha kuwa mwingira anashida kubwa kiroho hivyo kwani taharuki na ghadhabu aliyoionyesha ibadani juu ya kuanikwa na vyombo vya habari mimi binafsi sijui nitafanyiwa maombi gani ili niamini kuwa mwingira ni nabii. Baada ya ibada baadhi ya waumini wake walisikika wakimlaumu kwa lugha alizotumia kuwasilisha hisia zake!! Nimeona niwajuze wenzangu ili mjue msimamo wa nabii huyu!!!!

mungu amsaidie
 
Walikuwepo ila inavyoelekea wameshaanza kushtuka maana hapo tu aligawa bahasha ili watu wachangie pesa, Kibaya zaidi waumini wemeshtukia maana binti wake mwingira amepigwa mimba na mhuni mmoja wa kimara. Pia mtoto wake wa kiume ndiyo utajua watumishi wa mungu nao wanamisalaba!!!
He! Umesahau ule usemi ya kuwa Kahaba atazaa bikra na Sheikh atazaa jambazi?
 
Mkuu Anold,

Kumbuka ya kuwa.......dini ni mpango wa MUNGU kumkomboa Mwanadamu, na dhehebu ni mpango wa Mwanadamu kumtafuta MUNGU!

Sasa kwenye kumtafuta MUNGU si wote wanakuwa/tunakuwa kwenye RIGHT TRACK.

Hii definition yako umekosea, Dini ni mpango wa Mwanadamu kumtafuta mungu lakini Wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu. Kwa maana nyingine huwezi kumuona Mungu kwa kupitia Dini ila unamuona Mungu kwa kupitia Wokovu soma Yohana 3: 16. Wokovu haupatikani kupitia dini, ndo maana utakuta kuna dini nyingi sana na kila dini inadharau mwenzie.
 
Weka vizuri hili, kwamba dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, WOKOVU ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu si vinginevyo_OGOPA mungu.
 
That is a very good question! Huwa mimi nashangaa sana na nadhani tatizo ni serikali yetu haijatupa elimu ya kutosha kupambanua mambo.
Mkuu hivi mambo ya dini yanahitaji serikali na yenyewe kuingilia kutupa elimu. Think and Think again.
 
ANGALIZO:
Wana "jf" tafadhari epukeni kuzusha usicho kuwa na uhakika nacho kumbuka tuta poteza maana halisi ya safu hii
Tutalingana na wale tunaowakosoa.

Asante!

Mc!
 
Walikuwa na macho hawakuona,walikuwa na masikio hawakusikia,walikuwa na mdomo hawakusema........mh!yote yalishatabiriwa si wote wamwitao Bwana Bwana wataurithi ufalme wa mbinguni,tujitahidi tu kusoma kwa makini maandiko kwa kadri ya imani zetu na kuelewa, kwani Bwana wa majeshi alishatamka acheni ngano na magugu yakue pamoja ,siku ya siku ni yeye ndo anajua atakavyochambua kama huyu ni nabii wa ukweli au wa uongo
 
Back
Top Bottom