Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Mtume na nabii kushindwa kuona maono kuhusu uhalali wa babu wa Loliondo, inatilisha shaka utume wao! Mimi naamini hii ni vita ya kihuduma kuliko kiroho. Haiwezekani mtu umtukane mwenzie kuwa ni roho itokayo kwa shetani wakati hata wewe unashutumiwa na wengine ni roho itokayo kusikojulikana! Hizi kweli ni nyakati za mwisho.
 
Maajabu ya mwingira.
yeye na mkewe liakunda ndiyo wamiliki wa efadha foundation. ambayo inamiliki makanisa, mashamba , televisioni. na benk wao ndio wamiliki.
na pia mwingira huwa anatakasa mabinti ushahidi upo.
babu anachaji 500 na katika hizo yeye huambulia sh 100 zingine huenda kwa wachimbaji na wachemsha dawa. mwingira anaweza kutuambia alikopata pesa za kujenga jumba la kifahari maeneo ya mbezi beach. gari ya mwingira ilinunuliwa marekani na ikaretwa na ndege ina dhamani ya karibu 400m.
Kibabu cha watu baada ya kustaafu uchungaji kimejenga kanisa wa pesa za kuunga unga bila kumchangisha mtu na kuna watu wanasali hapo mpaka kesho. leo kinachimba dawa na kuambulia sh 100 mwingira maneno yanamtoka jamani. kiache kibabu cha watu
 
Nakuambia funga domo lako!!Nyang'au mkubwa we!!Kinachokufanya umseme babu ni nini??Hii michungaji gani haina busara wala hekima??Umekalia biashara tu,hivi ni nani anakaa chini ya wehu hawa.shame kwa waumini wako pia!!!Babu hajamuita hata mtu mmoja,tunaenda wenyewe tena kwa usafiri mgumu,babu hachagui wa kumponya-wote uwe mpagani,budha,mkristo,muislamu nk,babu hajamwambia mtu aingie katika imani yake(kanisa),unakunywa dawa unaondoka-wewe unaumia nini-unahukumu kama nani-usinifanye nitoe mengine yasiyofaa humu ila think twice....................
 
Hizo laana zingeanza kuwapata kwanza wakina Manyaunyau, Prof Maji Marefu na Mti Mkavu na Sheikh Yahya.
 
Watanzania tunatakiwa kuwa makini kuhusu ili, si kwamba namuunga mko Mwigira ila kwa kuwa ni swala la kiimani tunatakiwa kuwa makini na kila mtu kwa dini yake ajaribu kuliangalia hili kwa jicho la tatu, na tusikurupuke kuibeza au kuikubari moja kwa moja tiba hii, kwani hata shetani naye ana miujiza!
 
give me a break.... hivi Mwingira ni askofu? hivi vyeo vya uaskofu unaweza kujipa tu? au imekuwa kama kina Prof Maji marefu?

kama alijiita Mtume baada ya kuwa na waumini wengi akakataa uchungaji kwa madai kuwa ni cheo cha chini, atashindwaje kujiita askofu? au mkewe ndiye askofu wa mtandao wa efatha yake?
 
Wivu wa watu umefikia kiwango cha juu!!
Mwingira si ameanzisha benki, awe anagawa pesa bure kwa mtu yeyote asiekuwa na kazi nchi hii!
Mbona anaona kibanzi ndani ya jicho la mwenzie huku yeye anaboriti imejaa jichoni!?

Mwingira ndivyo alivyo mfano anamchukia sana Mwalimu Nyerere na humwita shetani,..............kisa, aliwahi kumfunga ndugu yake waziri Mwingira aliekuwa waziri wa uchukuzi enzi za mwalimu waziri huyo alipatika na hatia ya kula rushwa.
 
Watanzania tunatakiwa kuwa makini kuhusu ili, si kwamba namuunga mko Mwigira ila kwa kuwa ni swala la kiimani tunatakiwa kuwa makini na kila mtu kwa dini yake ajaribu kuliangalia hili kwa jicho la tatu, na tusikurupuke kuibeza au kuikubari moja kwa moja tiba hii, kwani hata shetani naye ana miujiza!

heri yako mpendwa umeliona hilo, manke watu wamemu-endorse babu moja kwa moja bila hata kutafakari. inashangaza na inasikitisha sana jinsi wakristu wetu wa leo tulivyo na tunavyoenenda!

ubarikiwe na Bwana

Glory to God
 
heri yako mpendwa umeliona hilo, manke watu wamemu-endorse babu moja kwa moja bila hata kutafakari. inashangaza na inasikitisha sana jinsi wakristu wetu wa leo tulivyo na tunavyoenenda!

ubarikiwe na Bwana

Glory to God

Mimi binafsi kilichonitisha, si tu kuwa sina proof kuwa alionyeshwa na Mungu maana ni ngumu kuithibitisha hiyo maana hata sauti ya Mungu siijui. Bali natishika kwamba ikiwa ni kweli mti unaotumika ni sumu ya ku-patch kwenye mikuki na mishale, ikiwa haina side effects in long run!!
 
Mimi binafsi kilichonitisha, si tu kuwa sina proof kuwa alionyeshwa na Mungu maana ni ngumu kuithibitisha hiyo maana hata sauti ya Mungu siijui. Bali natishika kwamba ikiwa ni kweli mti unaotumika ni sumu ya ku-patch kwenye mikuki na mishale, ikiwa haina side effects in long run!!
Hivi ile mishale ya sumu ikiua mnyama haliwi??? alikiwa ina kuwaje mtu aliekula atakufa baada ya muda gani? kama hafi kwanini ilhali ile sumu ilimuingia yule mnyama?
 
Katika aibada iliyofanyika jumapili ya tarehe 13/03/2011, Mwingira ambaye pia anajiita nabii, alifanya maombi ya nguvu kumuomba Mungu ili Mchungaji Mwasapile wa Loliondo afe. Mwingira ambaye alikuwa akionyesha dhahiri kuwa amekasirishwa na uwepo wa Babu huyo aliwataka waumini wake waombe kwa nguvu zao zote ili babu huyo atoweke katika dunia hii. Muumini mmoja ambaye hakuridhika na maombi hayo nilimsikia akikiri wazi kuwa ameshangaa mtu anayejiita nabii kufanya maombi ya kutaka mtu afe huku akijua wazi kuwa kisasi sio cha Binadamu bali ni cha Mungu. Kitu ambacho kimemuudhi mwingira ni kutokana na ukweli kuwa mchungaji mwasapile anapata umaarufu siku hadi siku kitu ambacho ni tishio kwa makanisa mengi ya aina ya mwingira yanayotegemea shida na matatizo ya waumini wao kujinufaisha. Aidha kwa wale wanaofuatilia mahubiri ya mwingira watakubaliana nami kuwa mwingira anahasira na KKKT kutokana na namna alivyoondoka huko akiwa kama mwinjilisti.

Kwa watu wasiomfahamu Mwingira, kwa kifupi ni kuwa Mwingira alikuwa Mwinjilisti wa kanisa la KKKT jimbo la kibaha kwa miaka kadhaa. Mwingira pamoja kwamba alikuwa mwinjilisti Dayosisi ya mashariki na Pwani, pia kwa nyakati tofauti alikuwa akifanya mikutano ya kiunjilisti ya nje (hadhara) iliyokuwa ikiandaliwa na sharika pia huduma mbalimbali za kanisa hilo. Kwamfano kwenyE miaka ya 1996 alipokuwa anafanya mikutano ya injili katika mikoa ya Ruvuma na Kilimanjaro, Mwingira ambaye sasa anadai ni nabii, aliwahi kutamka na kuapa kuwa kamwe hataanzisha Kanisa kwani huduma aliyoitiwa ni kuhubiri injili. Baada ya kuona itikio la waumuni kwenye mikutano aliyokuwa akifanya, mwingira akaanza tabia ya kuondoka kituo chake cha kazi bila ruhusa ya mchungaji kiongozi wa usharika, hata baada ya kuonywa mara kadhaa akitakiwa afuate utaratibu mwingira alikuwa akikaidi. Baada ya mchungaji kiongozi wake kuchoka na tabia yake ya kufanya mambo bila utaratibu, ilibidi azuie kumpa mshara wa mwezi mwingira kitu kilichomuudhi mwingira na kumfanyia fujo aliyekuwa mchungaji wake jimbo la Kibaha. Baada ya tukio hilo kufika Makao makuu ya Dayosisi ya Mashariki na pwani wakati huo Askofu akiwa Mzee Sendoro, kwa hekima za kimungu mwingira alipewa uhamisho kwenda kutumika Zanzibar kwenye usharikia wa Mwanakwerekwe, jambo hilo lilimuudhi sana mwingira kwani alichokifanya ni kukusanya nguo alizokuwa anazivaa akiendesha ibada (majoho) na kwenda kumtupia mchungaji wake na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mwingira KKKT. Alipoibuka ndiyo amesema kuwa yeye ni mtume tena nabii. Hivyo dunia ielewe sababu za mwingira katika mahubiri yake mengi kukandia KKKT pamoja na watumishi wake. Huyo ndiye nabii aliyeondoka katika huduma moja kwa ugomvi, dharau na jeuri
 
Hayo anayomuombea BABU yampate yeye!!!! Nabii gani anawaombea watu watoweke duniani!
Masikini Mwingira wasiwasi wake waumini wanamkimbia na ndio chanzo cha mapato yake!!!
 
Mungu hawezi kuyapokea maombi ya Mwingira, na badala yake babu ataishi maisha marefu ili watu waendelee kupata uponyaji.
 
Sijapata soma ktk bibilia Yesu kuombea mtu afe! Nasema sijasoma huo mstari. Nachofahamu ni kuwa chuki na hasira vyatoka kwa shetani na si kwa Mungu. Nakubaliana na Anold kuwa ni chuki na KKT ndio inamsukuma Mwngira na kwa maana hiyo amempa shetani nafasi.
 
kama ni kazi ya Mungu yy hana nguvu ya kuizuia subirini mda sii mrefu mtaona Mungu atakavyompiga kiboko na ataaibika sana.Mungu si wa kuchezea hata kidogo,wote tunamjua ni fisadi wa sadaka za waumini wake,anaishi kifahari sana,,,,,siku yaja ukwlei utadhihirika wazi.
 
Back
Top Bottom