Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Nafikiri wao pia wezi, Kakobe na Mwingira wanadanganya watu ndiyo maana wanamshambulia Babu wanamjua pia anadanganya watu. Someni biblia
 
Hawa akina Kakobe, Mwingira and the like wanasumbuliwa na wivu tu kwani wao wanatumia nguvu za giza huko kwenye mahekalu yao na hata miujiza inayotokea huko siyo endelevu kwa vile shetani wanayemtumika ni msanii tu,hivi sasa nguvu zao zimechujuka hakuna uponyaji tena wameng'ang'ania kuwakamua waumini wao kwa mafungu ya kumi. Kakobe kanisa lake limekimbiwa na waumini wengi kwa maelfu kwa jinsi alivyokuwa anakamua bila huruma mpaka wengine wamefilisika. Wachungaji aina ya Kakobe , Mwingira, Lwakatare ndiyo wanastahili kulaaniwa hadi wafe kwani ni matapeli tu.
 
jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

tusaidiane please

Glory to God

Babu ni mchungaji mstaafu, au mnataka afungue kanisa lake aanze upya kuhubiri? Kama dawa imetoka kwa Mungu itaendelea kuwepo licha ya hivi vipingamizi vya binadamu
 
Mimi sijategemea kabisa kama Ambilikile angepata upinzani kutoka kwa viongozi wa dini ya Kikristo.
Mimi nilitegemea hayo since day one. Kwa wale wachungaji/mitume/manabii/wazee wa upako/maaskofu wanaoombea miili nikimaanisha Maradhi, mali, magari,fedha, na uchumi kwa ujumla ni ngumu sana kukubaliana na Babu wa Loliondo kwani wao wako kimaslahi zaidi. Hofu yao kubwa ni kupoteza wateja. Kama unaenda kwa Mchungaji anakwambia usiseme nahitaji gari, sema nahitaji prado! Au mwingine anakwambia njoo umtolee Bwana mali zako zote aweze kukuponya ukimwi, sasa amepatikana mkombozi kwa sh. 500 tu, ni hatari sana kwa kipato cha hao wachungaji.

Tena Babu anapata upinzani mkubwa kutoka kwa wakristu kulikoni hata waislamu. Cha kushangaza kuna waislamu wengi sana wameipokea dawa hii kwa imani kubwa. Lakini wakristo wengi mioyo imekuwa migumu.
Sasa kama huyo anayesema Mchungaji gani hatumii biblia kuponya , au hahubiri, anategemea umlete mtu kwenye machela hajitambui utamhubiria ki2 gani? Ni kiasi 2 cha kutumia akili kidogo bila hata kuumiza kichwa. Je akianza kuhubiri, watu wanakuja kwa maelfu atatibu sa ngapi? Na ndiyo sababu akasema hatafunga kwaresma ili aweze kuhudumia wa2 wengi zaidi. Tukumbuke hata Yesu alitengua sheria ya kutoponya siku ya sabato na akaponya watu na wakapona. Its obvious huu ni wivu na insecurity ya hawa "wapakwa mafuta wa bwana"
 
Mungu wa rehema aingilie kati hili jambo, vinginevyo Tz tutaangamia..!

Si vizuri kuwasema watumishi wa Mungu kwani wao ni kama mboni ya jicho la Mungu, na ukiwasema vibaya ni kuitafuta hasira ya Mungu!

Mi naomba Mungu ainue watu watakaoweza kuelimisha umma juu ya hii dawa ya babu!
Mpaka sa hivi mi sijui tena nasema sijui kama hii dawa ni kutoka kwa Mungu au ni uvumbuzi wa kawaida wa kibinadam au ni shetani kajivika upole ili watu wasiende kwenye maombezi ya kweli.

Kwa jinsi ninavyo elewa, kila MUUJIZA ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili watu wamsifu na kumtukuza Muumba na zaidi ya yote ili kumwamini, Mungu haitaji kufanya miujiza kama shoo ,,,

nawasilsha
 
Ukitupa jiwe kwenye kundi la watu na ukasikia mtu analia basi ujue huyo ndiye limempata
 
alafu siku hizi kama umemsikia ameanza kutishia watu wanaohama kanisan kwake ati nakwambia wewe ulieenda uko upati kitu kama mungu wa MWINGIRA amekuandalia mwingira utaruka koteeeeeeeee
jamani kuna Mungu wa ambilikile wa mwingira..huyu MUNGU wako wangapi..majuzi nilienda na mdogo wetu mmoja anasali DPC kinondoni alisema mwanzo na mwisho kumpeleka pale..alipofika akaanza kukandia na nyie mnaokimbia makanisa yenu kukimbilia ibada za EFWATA nawaambia mmepoteza muda wenu hapa baraka natoa kwa wana efwata tu hata ukae mpaka saa moja..nikaona watu wanaanza kuondoka kichekecho ati kuna walinzi wamefunga mlango akuna kutoka mpaka amalize ibada..sasa kama akuna baraka mnangangania watu wabaki kanisan wa nini???waachen watu wawe huru usibague makanisa MCH MWINGIRRA HUU SIO MUDA WAKE....muwen na upendo na amani na si Kujiona huyu zaidi mimi zaidi amtafika kumbukeni lengo lenu ni kusudi la MUNGU litimizwe lakini naona WACHUNGAJI WENGI SASA WAMEKUWA ZAIDI YA MAGUFULI WANATAFUTA UMAARUFU WAO BIINAFSI BADALA YA KUTAFUTA SIFA ZA BWANA YESU

WENU
MTUMISHI/KANISA LA MWINGIRA


Huyo Mwingira msameheni bure, busara na hekima kwake ni ZIRO! Ukienda kanisani kwake kama una hekima na busara zako unaweza usimalize ibada. Hajui aongee nini, wapi, wakati mwingine anaongea matusi! Mimi alishanishinda! Mimi naelewa watumishi wote wa Mungu, ambao wanasimama katika kweli ya Mungu wanakuwa na busara, na ndiyo maana kwa kweli siamini kama ni mtumishi wa Mungu au ni mjasiriamali wa Biblia! Binafsi kuhusiana na swala la babu ni kama Askofu Pengo alivyosema, naendelea kushangaa mpaka Mungu aseme nami. Lakini kitendo cha yeye kumlaani afe kama DECI ilivyokufa sijakipenda. Hata kama mtu ni adui yako, Biblia inatuambia wapendeni adui zenu na kuwaombea. Yesu mwenyewe hakuwahi kumlaani mtu, nakumbuka aliulaani mti unaoitwa mtini, baada ya muda ukakauka! Sasa analaani mtu anajua kuitengeneza Roho! Nasi kama waumini hatukomi, kila kukicha tunaenda kanisani kwake wakati tunazidi kuadhirika na magonjwa na umaskini! Mungu atuhurumie
 
Unajua haya makanisa mimi huwa nayaita "Mushroom churches" manake yanachipuka kila siku yanategemea sana waumini kujiendesha. Wengi wa hawa waumini ni wale waliokata tamaa ya maisha kutokana na kusumbuliwa na magonjwa sugu hivyo kukimbilia kwa wachungaji matapeli ili waombewe wapone.

Sasa ghafla kaibuka babu wa loliondo anatoa tiba ya uhakika kwa sh 500, lazima waanzilishi wa haya makanisa feki wamchukie manake wateja wao ambao ni waumini wamekimbilia Loliondo. Unadhani mtu akipona kupitia babu wa loliondo atarudi tena kwa Mwingira au Kakobe aliemuombea apone kisukari na hakupona??

Conflict of interest kati ya Babu na kina Mwingira, Kakobe nk.
 
Nilitarajia nabii na mtume amuombee babu mibaraka zaidi ili awatibu watu wengi zaidi. Sasa hii lugha ya kumuombea laana mwenzako siielewi. "It sounds very unchristian". Labda na yeye atuambie amewasiliana na mungu wake amemtuma kumlaani mchungaji wa loliondo. Babu amesema ni mungu ndiye aliyemfunulia hii dawa na kwa wakristo wanaamini kuwa yesu ni mungu sasa suala la kuwa hajamtaja yesu linatoka wapi?

Kuhusu kukusanya pesa sidhani kama kuna kanisa ama mchungaji/askofu/mtume/kasisi anayeendesha huduma zake za uponyaji bila tozo za fedha. Sana sana wanachofanya ni kubadili majina tu mara waite ZAKA, mara SADAKA, mara MICHANGO mara FUND RAISING na huwa ni pesa nyingi sana zinatolewa. Ukiangalia TV shows nyingi wakimaliza tu wanatoa za account zao za benki ili watumiwe kile wanachokiita michango ili huduma iendelee.

Kwa hiyo sioni kama kuna ubaya wowote babu wa loliondo kuomba michango ya shs 500 kila mtu ili huduma yake iendelee. Babu anahitaji kuwalipa wachimba dawa na wanaomsadia kuchemsha na kugawa dawa. Mimi naona mchango wa babu ni mdogo sana ukilinganisha na hii michango ambayo kina mwingira na wenzake wanawatoza waumini wao. Na kama mchango ndio kigezo pekee cha kupima uhalali wa huduma basi kimsingi babu ana uhalali zaidi kuliko hawa wengine.
 
Sadaka sadaka sadaka!!!! Mwingira mbona unatoa kibanzi katika jicho la babu na huoni boliti katika jicho lako...usanii wako unakaribia mwisho wewe na wachungaji wenzio feki wote....
 
mbona topic haindani na maelezo uliyoyatoa? tujuze huyo nabii mwingira kasemaje kuhusu mchungaji babu ktk vyombo vya habari sio ishu ya yeye kua na benk au kumiliki shule.
Hata mimi nimejaribu kutafuta wapi na nini mwingira amesema ili ikibidi tumwanike huyo mwingira maana wengi hawamjui, hata hivyo nimejaribu kuweka hapo juu kwenye topiki iliyomgusa mwigira baadhi ya mambo ya mwingira ila kama kuna mtu ana kauli yeyote aliyotoa mwingira ya kumkandia huyo mchungaji wa Liliondo atuwekee barazani ili tuweke mambo ya hawa manabii wa siku za mwisho.
 
Hayo ni maneno makali sana kutoka kwa mtumishi wa Mungu. Hata kama hakubaliani na Mchungaji Ambikile Mwasapile kuna jinsi ya kusema. Biblia inatufundisha tuwaombee na kuwabariki adui zetu. Sasa hata kama adui ni wakuombewa, yeye iweje amlaani? Jamani tutawajua watumishi hawa kwa matendo yao. Ee Mungu wa neema kikombe chako cha rehema kamwe kisikauke

Ubarikiwe!
 
Mwingira, Mwingira, mbona kama hujui maandako aau Biblia unayotumia ni tofauti na ninayoisoma,kumbuka katika Kitabu cha Mithali 17:13 Neno la Mungu linasema "Yeye arudishaye mabaya badala ya mema ,Mabaya hayataondoka nyumbani mwake"
Wewe kama Mtumishi wa Mungu hupaswi hayo uanyoyasema kwa mtumishi mwenzako achilia mbali muumini wa kawaida.
Kumbuka katika Neno la Mungu tunaonywa sana ukijidhania kuwa unajua neno hujui bado bali wanaompenda Mungu wamejulikana naye(1Wakorintho 8:2-3) hivyo usidhanie kutumia Neno la Mungu kuwa unalifahamu sana kuliko wengine umepotoka.
Mwingira kwanini unakuwa kwazo 2Wakorintho 6
"Tusiwe kwazo la namna yeyote katika jambo lolote ili utumishi wetu usilaumiwe"
Kwanini unaruhusu kuwa kwazo kwa wengine na kupata lawama juu ya utumishi wako.
Katika Neno la Mungu mambo mengi yamekatazwa kwa hawa watumishi wa Mungu lakini ndiyo kama vile wanayafumbia macho
Tito 1:7-9 "Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno kwa kuwa ni wakili wa Mungu asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mgovi asiwe mpenda mapato ya aibu bali awe...........................
Lakini haya ndiyo tunayashuhudia kwenu nyie watumishi mnasimama wapi?
Katika kitabu cha Yakobo napo kuna mambo mengi tu ya kujifunza.
tumeonywa juu kuwalaani watu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu
Yakobo 3:9 "kwa huo twamhimidi Mungu baba yetu,na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu"
Unatumia ulimi huo kumlaani mtu badala ya kumbariki tena Mtumishi mwenzako,na huo huo unatumia kumwomba na kumtukuza Mungu.
Mwingira na Kakobe kumbukeni tumekuwa tukiona upendeleo unaofanyika toka kwa watumishi kwa kuwajali wenye navyo.
ila kwa babu sijasikia upendeleo na ni hiyo shilingi 500 ni kwa wote
Yakobo 2:1 "Ndugu zangu,imani ya Bwana wetu Yesu Kristo ,Bwana wa utukufu,msiwe nayo kwa kupendelea"
ndiyo hayo kama si mwana efatha,au huko kwingineko unaonekana hufai kupata baraka zilizopo kwneye neno,ndiyo maana kwa babu wala hajapendelea uwe nayo ,mpagani utapata huduma ya uponyaji.
ONYO
Kumbuka Mungu hawezi kuwaacha watu wake wateseke hata siku moja katika mikono ya watumishi walo kondoo na kuwatelekeza.
Kwa wale wasomaji wa Bibli wakasome Ezekiel 34:1-31
Ila nitanukuu michache kwa faida ya wengine mstari wa 4 unasema
"wagonjwa hamkuwatia nguvu,wala hamkuwaponya wenye maradhi,wala hamkuwafunga waliovunjika............
Kweney mstari wa 10 Neno linasema Bwana MUNGU asema hivi;Tazama,mimi ni juu ya wachungaji;nami nitawataka kondoo zangu mikononimwao;nami nitawaachisha hiyo kaziya kwalisha kondoo;nao wachungaji hawatajilisha wenyewetena;nami nitawaokoa kondoo zanguvinywani mwao,wasiwe tena chakula chao.
watumishi wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ya watu mtaji hasa magonjwa,bila kujua kuwa hilo Mungu halimfurahishi.
Hivyo mkumbuke kama mlitegemea kuwanyonya tu kondoo wa Bwana badala ya kuwatumikia hawezi kuruhus hali hiyo tena.
Loliondo ilikuwa eneo ambalo hakuna mtanzania ambaye angependa kuishi huko ndiyo maana hata kaya zipo chache sana 500,ila leo tuanona jinsi gani wingi wa watu huko toka mataifa mabalimbali wanaelekea huko
Isaya 60:15-22
"Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa hata hapana mtu aliyepita nadani yako (Loliondo/Babu)
nitakufanya kuwa fahari ya milele
Furaha ya vizazi vingi
Utanyonya maziwa ya mataifa(mataifa mbalimbali yanaenda huko)
Utanyonya matiti ya Wafalme(viongozi wengi wanaelekea huko)
MWISHO NATAMKA BARAKA KWA LOLIONDO NA BABU
Isaya 54:17
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu juu yako utahukumiwa kuwa mkosa.Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA,na haki yao inayotoka kwangu mimi asema BWANA"
SIFA NA UTUKUFU NI KWA MUNGU KWA HUDUMA YA UPONYAJI INAYOPATIKA LOLIONDO
NA KILA MWENYE PUMZI ASEME AMEEN
 
Mwingira fara tu, yeye anachofanya ni nini pale alipokaa. Mbona anadai watu saaana kanisani? huyu ni mpuuuzi ambaye yuko kipesa zaidi.
 
point of collection kwenye red:ccm,cuf,nccr,tlp,udp Vs CDM

I think you mean point of Correction.

Suala la matibabu anayotoa babu mimi sina cha kuongea. nabaki kumwomba Mungu tu kama mkristo aweze kuangaza neema zake kwa taifa hili katika kipindi hiki cha mchanganyiko wa mawazo. Nina imani na mipango ya Mungu kwani huwa hana kitu kinaitwa dharura au bahati mbaya bali yote yanayotendeka yanajulikana kwake.

Jamii ya kichungaji nadhani inabidi wajifunze namna gani wanatoa mawazo na maoni yao kwa hadhira hasa hawa wanaojiita mitume, manabii Mwingira, Mzee wa Upako, Kakobe, et al. wanatakiwa watafakari vizuri maandiko na waepuke kuhukumu. maneno yao huwa ni muhimu sana katika kuimarisha imani za waumini wao hasa katika kipindi cha mkanganyiko hivyo kauli kama hizi zinaonyesha wao wenyewe wamechanganyikiwa na hawajui walisemalo.

Please ndugu zangu wachungaji yaeleweni maandiko na uwezo wa Mungu na eleweni wajibu wenu katika kuelekeza taifa la Mungu.
 
Ukitupa jiwe kwenye kundi la watu na ukasikia mtu analia basi ujue huyo ndiye limempata
Mbona mfano wako haufanani na chochote hapa, umeishia darasa la ngapi wewe? maana hapa watu wanajibishana kwa hoja sasa wewe unafananishaje hapo? pmbf
 
Bwana Yesu asifiwe,

Kwa kweli, Babu wa Loliondo na ndoto zake na dawa yake hakuna utukufu wowote anaopata Mungu aliye hai ambaye alijifunua kupitia neno lake Yesu Kristo. Kwa hiyo, watumishi wa Mungu kama Kakobe, Mwingira na wengine kupinga ni sahihi tu wala hawana kosa. Tatizo ni kwamba watu wamezama katika udunia na kusahau kabisa maisha ya utakatifu ndiyo maana wanatafuta ufumbuzi laini kwa matatizo magumu kitu ambacho hakiwezekani.

Cha kufanya ni kama mtu unaumwa dawa ni kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu; kama ukipona sawa na kama usipopona si unakufa na kwenda mbinguni. tusidanganyane hata ukinywa kikombe na kupona mwili je kesho ukifa utakwenda wapi? Na hata kama huumwi ugonjwa wowote kama mimi dawa ni kuishi maisha ya utakatifu wa kweli ndani ya Yesu tu.

Pia naomba tuwe wastaarabu tuache kuwatukana watumishi wa Mungu kwani tutavuna laana. Wao wanafanya kazi yao kwa kuangalia kila jambo kama linapingana na maandiko matakatifu ya biblia lazima walipinge tu kwani linatoka kwa yule mwovu.

Mwingira, Kakobe na wengine wanaopinga mambo ya Babu wa Loliondo mbarikiwe sana.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom