NYACHA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 273
- 65
Wadau, maafisa wetu wa halmashauri mbalimbali hapa nchini wanalia! yaani wanatia huruma jamani! ni miezi miwili tu tangu Mh Mwigulu Nchemba alipookoa zaidi ya bilion 40-50 za wafanyakazi hewa; ambapo zoezi hili lilifanyika mishahara yote ya wafanyakazi kuingiziwa kwenye akaunti zao moja kwa moja kutoka hazina! huu mchakato wa Mwigulu Nchemba maarufu kama mtoto wa mfugaji umewaathiri sana kiuchumi maafisa wengi wa halmashauri mbalimbali ambao ndio waliokua wanufaikaji wakubwa wa hizi billion 40; kwasasa hawana tofauti na walimu kwenda kwa mangi kukopa; kumbi za starehe hawaonekani tena kama ilivyozoeleka kwa baadhi yao; hawa maafisa kwa sasa wameanza kuheshimu ndoa zao tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya operation ya Mwigulu Nchemba. Wameanza kupaki magari yao nyumbani ; semina nazo zimepungua kwao. Jamani wanatia huruma maafisa wetu! Wafanyakazi wote wa serikali wanaanza kuwa sawa. Kwasasa wabunge ndo wamebaki wanasumbua mjini. Poleni sana maafisa, Mungu atawaidia. Ni maisha tu. MWIGULU NCHEMBA UMEKOMESHA.